Kituo cha Mabalozi (KM), kilianzishwa mwaka 2008 na Daudi C. Pack, Rais na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mungu Rejeshwa (KMR), kimejitoa kwa ajili ya maendeleo jumla ya mtu. KM kimejiweka wakfu kuwasaidia wanaume na wanawake kujiandaa kwa ajili ya majukumu yenye maana katika Kazi ya Mungu kwa kufundisha wanafunzi maadili ambayo hupelekea mafanikio maishani.
KM kinatafuta kufikia mafanikio katika ufundishaji huku kikitoa mpangilio wa kielimu ambao utasaidia kuendeleza tabia na maendeleo ya utu.
Azma ya Kituo cha Mabalozi ni marambili:
(1) Kuwa taasisi ya elimu-mchanganyiko kwa ajili ya kufunza wanafunzi, ikiwa ni pamoja na waajiriwa wa baadaye wa Makao Makuu ya Kanisa la Mungu Rejeshwa Ulimwenguni.
(2) Kuwa huduma iliyowekwa wakfu ya Kanisa la Mungu Rejeshwa kulingana na viwango vya juu vya kiroho, kiakili na ustaarabu, kuwahudumia wale ambao Mungu anawaita kwenye Kanisa Lake, na kwa ajili ya kuhubiri na kuchapisha injili ya ufalme wa Mungu kama ushuhuda kwa mataifa yote.
Kituo cha Mablozi kinatambua ulazima wa kuwawezesha wanafunzi sio tu kupitia maarifa na ufahamu makini wa Maandiko na theolojia, lakini pia katika masomo ya sanaa na sayansi za jamii, hivyo kutoa elimu iliyokamili, iliyosawasawa.
• Jiografia ya dunia
Utafiti wa kina wa jiografia ya dunia unaoshirikisha ardhi kuu, mito, bahari pamoja na maliasili nyinginezo na athari zake kwa dunia nzima. Wanafunzi husoma alamaardhi na ishara muhimu kwenye ardhi na mipaka ya mataifa.
• Uumbaji sayansi
Wanafunzi wanafunzwa sheria za kimsingi na nadharia za sayansi ya kisasa, jinsi ilivyokua tokea jadi hadi nyakati hizi. Uumbaji unathibitishwa kutokana na ushahidi wa sayansi, nadharia na uhalisia wa mambo, huku nadharia ya mageuzi ya binadamu ikikanushwa.
• Uthamini wa muziki na Sanaa Nzuri
Kuelekezwa kwenye mwanzo wa sanaa. Wanafunzi husoma jinsi nyakati za historia zilivyoikata nakshi na ushawishi wake ukapenya katika michoro iliyo maarufu, Sanaa na muziki. Hii huwasaidia wanafunzi kuthamini kazi hizi kwa mtazamo mpya na kuelewa utamaduni wa kisasa.
• Afya njema
Muhtasari wa afya njema kwa kujiendeleza maishani. Majadiliano ya maumbile ya mwanadamu na kazi za sehemu za mwili. Hushughulikia msingi wa utimamu wa mwili na mazoezi pamoja na kanuni za kufuata ili kufanya maamuzi muhimu kiafya.
Masomo mengine ni pamoja na:
• Utambuzi katika Kilimo na Historia yake
• Kufikiri kwa Makini na Uandishi
• Kilimo Cha Ufugaji
• Adabu na Itifaki
• Serikali ya Mungu
• Uchumi wa Nyumbani
Wanafunzi wanaosomea uchungaji hupokea mafunzo zaidi kuhusu huduma ya kichungaji, ushauri na nasaha pamoja na masomo ya juu ya kidini.