Wengi wanaamini kwamba Mungu anajaribu kuokoa ulimwengu sasa! Mawazo haya yanaenda kama hivi: Mungu na ibilisi wako vitani juu ya hatima ya wanadamu. Hili linaonekana kama pambano kati ya wema na uovu—Mungu na Shetani. Hebu tuweke jambo hili kwa njia nyingine: Je, leo ndiyo fursa pekee kwa wanadamu wote kuchagua au kuukataa Ukristo? Je, ni lazima watu wote “waamue sasa hivi” kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi? Je, hivi ndivyo Biblia inafundisha?
Jibu ni HAPANA yenye msisitizo! Kama ilikuwa ndiyo, basi Mungu anashindwa vibaya sana katika vita vyake na shetani kwa ajili ya kudhibiti hatima ya watu wote. Kwa maneno mengine, Mungu “anawaita” wanadamu wote, lakini WENGI HAWAJIBU!
Fikiria! Mnamo 1920, baba yangu alipozaliwa, kulikuwa na watu wapatao bilioni 2 duniani. Sasa kuna takriban bilioni 7.5—na zaidi kila siku. Takriban bilioni 2.2, au thuluthi moja, wanaamini—kwa kiwango kimoja au kingine—katika jina la Yesu Kristo. Hii inawakilisha jumla ya kila aina inayoweza kuwaziwa ya zaidi ya aina 2,000 tofauti za wanaodai Ukristo. Takriban thuluthi nyingine ya wanadamu wamesikia habari za Kristo lakini hawajamkubali wala hawajadai kumfuata. Hatimaye, theluthi moja ya mwisho ya watu wote duniani hawajui lolote kuhusu Kristo. Wengi katika India, Afrika, Japan, China na sehemu za Amerika ya Kusini na Asia ya Kusini-Mashariki hawajawahi hata kumsikia. Je, wamehukumiwa kupotea, wakiwa hawajawahi pata fursa ya kuelewa walichokosa au kwa nini—kutokuwa na nafasi ya “kuitwa”?
Inapozungumza juu ya jina la Kristo, Biblia inasema waziwazi, “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Zaidi ya hayo, Warumi 10:13 inasema kwamba wanadamu lazima waliitie jina hili ili kuokolewa. Elewa! Ni dhahiri kwamba wote ambao hawajajisalimisha kwa Mungu wa Biblia na kumkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wao hakika hawajaokolewa! Mabilioni yasiyohesabika wamekufa katika hali hii. Wengi wamefikiri chaguo lingine la kipekee kwa hawa ni kwamba, walipotea na eti Mungu alipanga hilo zamani sana kwa ajili ya walio wengi ambao wamewahi kuishi.
Ikiwa vita vya kupata watu ni kama vile wahubirivyo wengi wanaodhaniwa kuwa wahudumu wa Kristo, basi shetani ana nguvu zaidi, na anafaulu zaidi katika jitihada zake kuliko Mungu. Huo ndio uwezekano mwingine—isipokuwa kuna kategoria ya tatu iliyo na idadi kubwa ya watu. Lakini ni lazima iwe kategoria ambayo haijatambuliwa. Kunayo kategoria hiyo!—Mungu hauiti umati wa wanadamu leo.
Lakini Anawaita wateule wachache!
Kuitwa na Kuchaguliwa na Mungu
Biblia inazungumza waziwazi juu ya wale ambao wameitwa na Mungu. Angalia kile Paulo aliwaambia ndugu wa Thesalonike: “Yeye [Mungu] anayewaita ni mwaminifu…” (1 Wathesalonike 5:24). Kama onyo kwa kusanyiko la Galatia, ambao walikuwa wakipoteza mwelekeo wa injili ya kweli, alisema hivi: “Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili nyingine” (1:6). na baadaye akaongeza, “Ushawishi huu hautoki kwake yeye anayewaita” (5:7-8). Kwa kusanyiko la Wakorintho aliandika, “Kwa maana angalieni mwito wenu, ya kuwa si wengi wenye hekima katika mwili, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa” (1Kor. 1:26).
Kristo mwenyewe alizungumza mara nyingi kuhusu wito wa Kikristo. Unaweza kuwa unafahamu kauli yake, “Kwa maana ni wengi waitwao, bali wateule ni wachache,” inayopatikana katika Mathayo 22:14 na 20:16. Baadaye, akiongeza maana kwa sehemu ya pili ya kifungu hiki cha maneno, Alieleza hili kwa wanafunzi Wake: “Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi” (Yohana 15:16), na kisha “Lakini mimi niliwachagua ninyi katika ulimwengu., kwa hiyo ulimwengu unawachukia ninyi” (fu. 19).
Mungu anawaita watu wachache—kwa kweli wachache sana—kutoka ulimwenguni kwa kusudi Lake kuu. Wale wanaoitikia wito Wake wanaweza kuendelea katika toba, ubatizo na wongofu.
Vipi Kuhusu Wewe?
Baada ya kusoma baadhi ya vitabu kutoka kwa Kanisa Rejeshwa la Mungu, wengi wametambua kwamba wamekutana na uelewa wa ajabu. Wengi wanashangaa kama wanaitwa na Mungu. Wanajikuta wakijifunza mambo ambayo hawajawahi kuyasikia. Wanatambua kwamba Biblia inaeleweka—kwamba si vigumu kuielewa kama walivyofikiri hapo awali. Kisha, wakihisi uhitaji unaoongezeka wa kutenda yale wanayojifunza, wengi hujiuliza, “Je, ninaitwa na Mungu?”
Wakati mwingine swali hili huwa katika mfumo wa “Je, ninapitia 'uongofu'?” au “Je, nibatizwe?” au hata “Je, nimekutana na Kanisa la Kweli la Mungu?” Bora zaidi, wengi hawana uhakika wa jinsi ya kujibu maswali haya ya msingi, na wengi hawajui kabisa jinsi ya kuyashughulikia vizuri.
Makala haya mafupi yataonyesha wazi, kutoka katika Neno la Mungu, jinsi ya kujua ikiwa Mungu anakuita. Ninakusudia kuiweka rahisi, kwa njia ambayo haiwezekani kuelewa vibaya. Kwa sababu, swali hili ni mojawapo ya maswali muhimu zaidi utakayokabiliana nayo maishani mwako. Kuelewa vizuri jibu lake Ni MUHIMU SANA kwa maisha yako!
Nilianza kujifunza kweli ya Mungu nilipokuwa na umri wa miaka 17. Kabla Mungu hajaniita, sikuwa nimejua hata fundisho moja la kweli la Biblia. Mchakato wa kuniita ulianza niliposikia sauti ya mtu anayeitwa Herbert W. Armstrong, ikitangazwa kutoka Pasadena, California. Hii ilikuwa 1966, na ilikuwa dhahiri kwangu mara moja kwamba nilikuwa nikisikia mambo kutoka kwa mtu huyu ambayo SIJAWAHI kuyasikia kabla—na UTHIBITISHO wazi wa kuyaunga mkono kutoka kwa Maandiko. Nakumbuka nilishangaa jinsi Biblia ilivyokuwa wazi—na jinsi ilivyokuwa jambo la kufurahisha kujifunza. Kabla ya hili—wakati wote nilipohudhuria dhehebu lililojulikana na kuheshimiwa sana la ujana wangu—sikuzote nilikuwa ninaona Biblia kuwa yenye kuchosha na ngumu kuelewa.
Kwa kweli, watu wa kila rika na asili zote hushangaa juu ya “mwito” ni nini. Wengi wanafanya mwito kuwa kidogo zaidi ya hisia fulani fulani inayowajia, ambayo wanadai kuwa ni ya Mungu. Mamilioni ya watu ulimwenguni wanahisi “wameitwa”—katika baadhi ya matukio kwa “kanisa,” au kwa “huduma,” au “kazi ya umishonari,” na katika visa vingine kuhudumia watoto, na pengine kutumika katika taaluma ya matibabu au hata katika jeshi. Kwa kutojua kile Mungu anasema, watu wengi sana wameachwa kutegemea hisia zao, wakidhani kwamba maisha yao—na njia wanazochagua—zimeongozwa na mungu. Wanahusisha “msukumo” huu kuwa wa kuitwa na Mungu. Kwa kusikitisha, wengi hawajifunzi kamwe kwamba “miito” hiyo haina uhusiano wowote na kumfuata Mungu wa kweli wa Biblia.
Kuitwa sahihi na Mungu ni zaidi ya aina ya hisia dhahania ambayo mawazo ya mwanadamu huhitimisha kuwa inatoka kwa Mungu!
Kufafanua Wito wa Kweli
Katika maelezo ya injili ya Yohana, Yesu alisema, “Hakuna mtu awezaye kuja Kwangu, asipovutwa na Baba aliyenituma …” (6:44). Mistari kumi na tisa baadaye, alirudia kwa wasikilizaji wake, “Kwa sababu hiyo naliwaambieni, ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja Kwangu, isipokuwa amejaliwa na Baba Yangu” (fu. 65). Katika mstari unaofuata, Yohana alirekodi kwamba “Tangu wakati huo wengi wa wanafunzi wake walirudi nyuma, wasiandamane naye tena.”
Wengi waliomsikia Kristo hawakuweza kuelewa kwamba ni lazima Mungu “awavute” watu na kwamba mwito ni kitu fulani “wanapewa”. Ingawa wengi leo-hii wanaonekana kuelewa kwamba lazima waitwe kwa namna fulani, hawatafuti kuelewa—kutoka katika Biblia—jinsi ya kujua kwa hakika kwamba ni Mungu anayewaita—akiwavuta—na kuwapatia kitu ambacho wanahitajika kukipokea.
Hebu tuchunguze maandiko machache yanayoweka wazi ni kitu gani Wakristo “wanapewa” wanapoitwa. Lazima tuondoe kabisa mkanganyiko wote.
Katika Mathayo, wanafunzi wa Kristo waliuliza, “Kwa nini unasema nao [makundi yaliyomsikia] kwa mifano?” (13:10). Jibu lake linatoa muhtasari wa jinsi na vile Mungu anavyoita: “Akajibu, akawaambia, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni [au ufalme wa Mungu], lakini wao hawakujaliwa” (fu. 11). Mistari kadhaa inayofuata inakuza kile Alichomaanisha, ikieleza ni wangapi ulimwenguni wanaweza kusikia kweli za Mungu (“siri za ufalme”) lakini wasizielewe. Kwa kuwa wanadamu wengi sana hawavutwi na nguvu za Roho wa Mungu, hawajapewa uwezo wa kulielewa Neno la Mungu.
Je, hii inakuhusu vipi? Jibu linaeleza moja kwa moja jinsi ya kujua kama Mungu anakuita: Kuitwa, kwa urahisi kabisa, ni kuzielewa kweli za Mungu unapoziona, unapozisoma au anapozisikia.
Jiulize: “Je, ninaelewa mafundisho na kweli za Biblia ninapozisikia?
Je, maandiko kuhusu injili ya Ufalme wa Mungu; mpango wa wokovu na kusudi la kuwepo kwa mwanadamu; matukio yaliyotabiriwa kutokea hivi karibuni; Ujumbe wa onyo la Mungu kwa watu wake; Sheria yake—pamoja na amri ya Sabato—Siku kuu Takatifu za Mungu; fungu la kumi; nyama-safi na nyama-najisi; Kanisa moja la kweli; na mafundisho mengine mengi, yanaeleweka wazi kwangu?”
Unaposoma au kusikia mambo haya katika magazeti, vitabu, vijitabu, makala na programu za Ulimwengu Ujao, je, yana maana kwako? Je, unayashika? Je, yako WAZI kwa uelewa wako? Je, unayaona kama UELEWA MAALUM ambao wengine hawana? Au Je, unahisi kujibana katika majaribu ya kutoamini kwamba unaweza kuonyeshwa mambo ambayo watu wengi hawayajui?
Kama majibu ya maswali haya ni “ndiyo,” basi Mungu anakuita—“anakuvuta”—wewe! Unapewa Siri za Ufalme wa Mungu!
“…Mungu anawaita watu wachache—hakika wachache sana—kutoka ulimwenguni kwa kusudi Lake kuu. Wale wanaoitikia kuitwa na Mungu wanaweza kuendelea na toba…”
Kuwajibika kwa Maarifa Yanayotolewa
Watoto huzaliwa wakiwa hawajui lolote. Hawajui hata misingi ya mema na mabaya. Wanapaswa kufundishwa karibu kila kitu. Vivyo hivyo, ulimwengu haujui mambo ya Mungu—kutofautisha kiroho kati ya mema na mabaya. Lakini kwa kupewa ujuzi wa mambo haya, tunawajibu wa kuyafanyia kazi.
Vifungu viwili vya Biblia vinaonyesha kwamba Mungu anawatoza watu hesabu kwa yale wanayoelewa. Angalia Yakobo 4:17: “Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.” Sasa soma Waebrania 10:26: “Kwa maana, kama tukifanya dhambi kusudi, baada ya kuupokea ujuzi wa Ile kwelI, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi.”
Hebu tuelewe. Kila wakati unapojifunza zaidi ukweli wa Mungu (ulio “mema”), na inaleta maana kwako—angalau kwa ujumla unaielewa—unapewa maarifa ya ajabu ya kiroho ambayo Mungu anakuchukulia kuwajibikia.
Hii ni sehemu ya mchakato wa kuitwa na Mungu—na kwa hakika ni muhimu kwake. Zaidi ya hayo, inafanya kuelewa jinsi Mungu anavyomwita mtu kuwa na uzito zaidi kuliko vile ambavyo wengi wameamini. Tambua kwamba Mungu atamwita kila mwanadamu mara moja tu. Kwa hivyo, unawajibika sasa kwa maarifa ambayo unapewa. Ikiwa mtu hatatenda kulingana na yale anayojifunza, Mungu ataondoa ufahamu huo (Rom. 2:13; Zab. 111:10), na mtu huyo yuko katika hali mbaya sana ya kiroho.
Uhuru Mkuu
Ukweli wa Mungu unasisimua sana zaidi ukiuelewa. Ni njia ya mambo yote ya ajabu, mambo mazuri maishani—mambo ambayo Mungu anataka uwe nayo. Pia ni njia ya ule uhuru mkuu uliopo! Kristo aliwaambia Wayahudi fulani waliodai kumwamini: “Ninyi mkikaa katika neno langu [kweli - Yohana 17:17], mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo KWELI ITAWAWEKA HURU” (Yohana 8:31-32). Ni lazima uwe tayari ‘kuendelea’ katika masomo yako ya Neno la Mungu, kujifunza zaidi kweli Yake, ambayo Kristo anaeleza ‘itawaweka ninyi huru’ kutoka kwa ulimwengu uliotengwa na Mungu na ukatekwa nyara na Shetani. Hata ufahamu huu ni uelewa wa thamani.
Labda wale mnashirikiana ulimwenguni hawaelewi hata moja ya mambo haya. Wala jamaa zako. Bila kuitwa na Mungu, hawana njia ya kufurahia wakati huu kile UNACHOPEWA—ikiwa unaelewa na kutenda ukweli wa Mungu.
Pia ni muhimu uhakikishe akilini mwako mambo unayojifunza. Unapaswa kujikuta unataka KUTHIBITISHA mafundisho ya Mungu. Paulo pia aliwaambia Wathesalonike “YAJARIBUNI mambo yote; lishikeni lililo jema” (1 Thes. 5:21). Ikiwa unajua Mungu anakuita, chukua muda kuthibitisha kwamba Mungu Yupo. Kisha thibitisha kwamba Biblia kwa kweli ni Neno Lake Lenye pumzi Yake kwa ajili ya wanadamu.
Hatimaye, thibitisha utambulisho wa Kanisa la Mungu. Ondoa shaka zote, na usiache nafasi ya kuchanganyikiwa. Kuna makanisa mengi ya uwongo—mengi ya kiroho “yanayofanana” ulimwenguni. Usidanganywe na yeyote kati yao. Kristo aliahidi, “Nitalijenga Kanisa Langu” (Mt. 16:18). Amua kujua kwa hakika kama kweli umekutana nalo. (Nakusihi usome kijitabu chetu Liko Wapi Kanisa la Mungu? na kitabu chetu Liko Wapi Kanisa La Mungu? – na Historia Yake ya Ajabu!)
Wakati huohuo unathibitisha mambo haya, omba kwa bidii kuhusu yale unayojifunza. Usipoelewa waziwazi jambo fulani, kumbuka kwamba Kristo alifundisha, “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa” (Mt. 7:7).
Yohana 14:17 inaeleza jinsi wale wanaoelekea kwenye uongofu wanavyoanza kupata kwamba wanaweza kuona waziwazi mambo ya Mungu. Tambua kile Kristo alisema alipozungumza na wanafunzi Wake kuhusu Roho Mtakatifu ambaye walikuwa watampokea hivi karibuni: “Yeye ndiye Roho wa kweli; [ambaye] ulimwengu hauwezi kuipokea, kwa sababu [hai] ioni, wala [hai] itambui: bali ninyi [mnai] itambua; kwa maana inakaa kwenu, nayo itakuwa ndani yenu.”
Katika hatua hii, wanafunzi walikuwa kama wengi walivyo leo hii—labda kama wewe pia. Walikuwa wanaona kweli nyingi za kiroho kwa sehemu, lakini bado hawakufahamu kikamilifu umuhimu mkubwa wa kujifunza Mpango wa Mungu na njia ya kuishi. Kupitia Roho Mtakatifu akifanya kazi pamoja nao, Mungu alikuwa akifichua mambo fulani ambayo wangeelewa tu kwa njia kubwa zaidi, Roho Mtakatifu inapokuwa ndani yao, kuanzia kwenye uongofu. Hatimaye, ili kuelewa kikamilifu mambo yote ya Mungu—mafumbo yote ya Ufalme wa Mungu—mtu lazima azaliwe na Roho Mtakatifu. Hii hutokea wakati inapoingia moja kwa moja kwenye akili! Bila ubatizo na muhimu-upokeaji wa Roho wa Mungu, haiwezekani kabisa kwa mtu yeyote kuelewa kwa kweli hata ukweli mmoja wa kibiblia!
Kabla ya kujadili jinsi hii inavyotokea, hebu tuangalie picha kuu.
Mpango Mkuu wa Mungu
Kuna sababu kubwa kwamba Mungu anawaita wachache tu sasa.
Msingi wa Mpango wa Mungu unajumuisha miaka 7,000. Wachache wame-elewa hili. Wengi wameelewa kwa usahihi angalau baadhi ya vifungu vinayoelezea utawala wa Mungu wa miaka 1,000 (Ufu. 20:4). Na ingawa wengi wanajua mengi zaidi ya haya, lakini hawajui lolote kuhusu ukweli kwamba Mungu ametenga miaka 6,000, au siku sita za milenia za “juma la siku saba,” kwa utawala wa mwanadamu, kabla ya “siku” ya saba ya miaka 1,000. “Siku” ya sita itakaribia mwisho na Shetani hatimaye atafungwa (Ufu. 20:2).
Hata hivyo, Shetani bado hajafungwa na kutolewa mahali pake pa “mungu wa ulimwengu huu.” Wakati Kristo, aliishinda dhambi, alifuzu kuchukua mahali pake (Mt. 4:1-11; Lk. 4:1-13) Alihakikisha kwamba siku moja Shetani hatakuwepo tena ili kuwadanganya na kuwavuruga wanadamu (1Kor. 14:33). Ni lazima tuelewe kwamba Shetani hutafuta kufanya kila kitu, katika uwezo alionao, akijitahidi daima kuzuia mpango wa Mungu. Hakika amewahadaa watumishi wake (2Kor. 11:13-15) kuamini kwamba Mungu ameshindwa kabisa katika mpango wake wa kuwaokoa wanadamu wengi, ambao Mungu hata bado hajawaitia wokovu. Lakini ni kwa ruhusa ya Mungu tu kwamba Shetani anamiliki juu ya “ulimwengu huu mbovu wa sasa” (Gal. 1:4).
Mungu hapotezi pambano lolote vile inalodhaniwa, bali ana udhibiti kamili juu yake. Anajua hasa kile Anachofanya, na uzuri wa mpango Wake unaweza kujulikana. Kuweni na uhakika kwamba hakuna Mungu wa kweli ambaye angechagua kuwashutumu watu wengi sana ambao wamewahi kuishi, bila kuwapa fursa kamili ya wokovu. Mungu wa namna hiyo hangestahili kufuatwa. Angekuwa zimwi asiye na haki ambaye lengo lake kuu ni kazi ya kuhukumu!
Lazima tuelewe! Biblia inasema, “Lakini wapenzi, msisahau neno hili moja, ya kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja” (2 Pet. 3:8). Bila shaka, watu wengi “hawajui” si “jambo hili moja” tu, bali karibu kila kitu ambacho Biblia inafundisha.
Walakini, hii ni aya ya kuvutia.
Mwanadamu amepewa siku sita, au miaka 6,000, kujaribu njia zake mwenyewe, serikali, dini, falsafa, mifumo ya maadili na aina za elimu. Chini ya ushawishi wa Shetani, amekuwa na mazoea ya dhambi—KUTOTII amri za Mungu—kwa karibu miaka 6,000. Mwanadamu amejaribu kutibu athari badala ya kutibu sababu ya kuwa amevunja sheria za Mungu. Hii ni pamoja na uvumbuzi wa dini nyingi zinazofundisha tu mawazo matupu ya wanadamu badala ya ajabu za UKWELI WA MUNGU.
Mungu anamruhusu mwanadamu kujifunza masomo machungu. Walio wengi sana, ambao hawajapata kamwe kujua thamani ya ukweli wa Mungu, wanapaswa kujifunza kwamba njia zao wenyewe hazifanyi kazi! Kabla tu ya ubinadamu kukaribia kujifuta kutoka kwa Dunia, kupitia mchanganyiko wa silaha za maangamizi makubwa na uchafuzi wa mazingira usioweza kutenduliwa, wa sayari ambayo ina mipaka ya kiasi inachoweza kuhimili, Kristo ataingilia kati na kuwaokoa wanadamu kutoka kwa kujiangamiza wenyewe!
Sasa endelea na waraka wa 2 Petro. Angalia mstari wa 9: “Bwana hakawii kuifikia ahadi yake… bali ni mvumilivu kwetu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Je, umeona kwamba Mungu anataka kuokoa kila mtu? Akizungumza kuhusu Mungu, Paulo asema, “Ambaye anataka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” (I Tim. 2:4). Huo ndio ukweli ulio wazi wa andiko hili. Mungu hayuko, wala hajawahi kuwa, katika shughuli ya “kuwahukumu wengi”.
Lakini Mungu anawaita na kuwafundisha wateule wachache ambao watatawala na Kristo na kusimamisha Ufalme Wake wa utukufu utakaotawala ulimwengu mzima. (Pia soma kitabu chetu muhimu kabisa Uwezekano Wa Kustaajabisha Wa Mwanadamu.)
Kumbuka. Shetani ameeneza aina nyingi za dini za uwongo katika dunia yote. Anaghushi ukweli kwa njia zisizo na mwisho, na hakubagua kuuacha mchakato wa wito wa Mungu. Ni MDANGANYIFU MKUU na mazao ya juhudi zake yapo kila mahali.
Njia Yako ya Uongofu
Biblia yako inasema, “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu” (Rum. 8:14). Mstari wa 9 unasema, “Basi mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” Vifungu hivi viwili vinafichua kwamba Mkristo ni—mtu ambaye yukona-na-anaongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu. Roho Mtakatifu hupokewa baada ya toba na ubatizo (Matendo 2:38).
Ikiwa ukweli unadhihirika—WAZI kabisa—kwako, weka lengo la toba, ubatizo, na kupokea Roho Mtakatifu wa Mungu—mwanzo wa UONGOFU WA KWELI!
Unapojitayarisha kwa ajili ya uongofu, zingatia kuchunguza tabia na mitazamo mibaya ambayo unaweza kukumbuka. Kuna mabadiliko fulani ya kimwili unaweza kufanya kabla ya ubatizo. Elewa. Uongofu unahusu kubadilika kabisa, kukua, kushinda—na kukuwa katika tabia ya Mungu. Hii inahusisha kuwa na mazoea ya kuomba mara kwa mara, kujifunza Biblia, kutafakari na hata kufunga mara kwa mara.
Kisha chukua muda kusoma vitabu vyetu vyote, vijitabu na makala zinazohusu imani, wongofu, ubatizo, uwezo wako wa kibinadamu, na uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu, Neno Lake na Kanisa Lake. Mengi—kwa kweli kila kitu—kiko hatarini kwako ikiwa Mungu anakuita sasa.
Chukua kila hatua kwa uangalifu. Fuata wakati unaofaa kwako. Hata hivyo, usicheleweshe isivyofaa, eti kwa sababu hujaomba kwa bidii au mara nyingi vya kutosha “kipawa” cha toba (2 Tim. 2:25; Mdo. 11:18). Kuwa mwangalifu ili usifuate mtindo wa ulimwengu, ukianguka katika kungoja hisia za kimiujiza kwamba “wakati ndio sasa.”
Biblia inafundisha kwamba “toba ni kwa Mungu” na kwamba “imani ni kwa… Yesu Kristo” (Matendo 20:21). Uongofu ni jambo la kibinafsi kati ya Baba na Kristo, na kila mtu binafsi. Ikiwa Mungu anakuita kweli, hakikisha wito wako (2 Pet. 1:10). Ni wa thamani zaidi!
Hii ndiyo njia pekee ya kukaribia hiki kipawa cha ajabu unachopewa!