JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.

Sikukuu ya Vibanda

Ikiwa imeelezewa katika Mambo ya Walawi 23:33-35, Sikukuu ya Vibanda (au “ile Sikukuu”) ni sherehe ya siku saba iliyoamuriwa inayoshikwa kila mwaka wakati wa majani kupukutika. Watu wa Mungu hutazamia kwa shauku kuu wakati huu maalumu wa mwaka, na hukusanyika mahali pazuri ulimwenguni mahali ambapo Mungu amepachagua “kuweka jina Lake” (Tora. 12:5). Wakati wa Sikukuu, ndugu huacha kazi zao za kila siku na kuja pamoja kufanya ushirika na kufurahi mbele za Mungu (Wal. 23:40) katika amani kamili, mapatano na umoja.

Watu wa Mungu wanapotunza sherehe hii wanakariri wakati ambapo wanadamu watakuwa wakiishi katika amani katika ulimwengu wa kusadikika, usio na ushawishi hasi wa mwovu Shetani. Sikukuu ni wakati wa kutafakari jukumu la watakatifu waliofufuliwa katika kumsaidia Yesu Kristo kuendesha serikali inayotawala ulimwengu mzima ambayo italeta kipindi hiki kisicho na kifani.

Kwa maelezo kuhusu sherehe hizi za mwaka, unaweza kusoma Siku Takatifu za Mungu au Sikukuu za Kipagani? na Somo la 28 la Kozi yetu ya Utambulisho wa Biblia, “Sikukuu ya Vibanda.”

2024 Maeneo ya Sikukuu ya Vibanda Ulimwenguni