Faragha yako kwenye mtandao ni kipengele muhimu sana cha tovuti zetu. Kauli hii ya faragha inaweka wazi ni taarifa zipi tunazokusanya na namna tunavyozitumia miongoni mwa mali zetu za Kimtandao.
Kanisa la Mungu Rejeshwa (rcg.org) na mali zake husika (Ulimwengu Ujao na Ukweli Halisi) hukusanya na kuchambua data kuhusu watumiaji wake. Kwa mfano: Takwimu za watumiaji, rejea za injini za utafutaji, masomo ya upendeleo, na habari na huduma zenye manufaa zaidi.
Watumiaji wanaoJisajili kwenye moja ya orodha ya usajili wetu wa barua pepe wanatakiwa kutoa baadhi au taarifa zote zifuatazo: (1) jina, (2) anwani ya barua pepe, (3) nchi na (4) ZIP/msimbo wa posta. Maeneo mengine ya nyongeza au maswali yanayoshabihiana pia yanaweza kuulizwa. Taarifa zote zinatuwezesha kutambua takwimu sahihi na kuboresha huduma tunazotoa.
Ziko njia mbalimbali ambazo kwazo tunaruhusiwa kupata taarifa juu yako kupitia utaratibu ufuatao:
Usajili wa Barua Pepe na Fomu: Watumiaji wanaweza kujisajili kwenye moja ya orodha zetu za barua pepe au kuomba vitabu kutoka kwenye tovuti zetu. Hizi huwajulisha watumiaji wetu sasisho mbalimbali na mabadiliko kwenye tovuti zetu au zinasaidia ufanisi katika kushughulikia maombi ya vitabu.
Cookies: Cookie ni faili dogo la data ambalo tovuti huliandika kwenye kwenye diski ngumu ya komputa yako unapozitembelea. Mara nyingi linakuwa na taarifa kama vile Utambulisho wa Mtumiaji ambazo tovuti zinatumia kuchagua mwonekano wa taarifa au kufuatilia kurasa zilizotembelewa. Tunatumia taarifa hii ili kufanya kuwa bora kabisa utembeleaji, kubuni na utendaji wa tovuti zetu. Wakati wote una uhuru wa kuzikataa “cookies” zetu kama kisakuzi chako kinaruhusu, lakini hii inaweza kuzuia utendaji wa baadhi ya vipengele vya tovuti zetu.
Anwani za IP: Tunakusanya taarifa za anwani za IP kwa ajili ya lengo la kusimamia mfumo, kuripoti taarifa za jumla (za pamoja), na kukagua matumizi ya huduma zetu na vifaa. Kwa sababu tunakusanya na kuhifadhi takwimu moja kwa moja juu ya shughuli zako mtandaoni kwa msingi wa kiujumla, mara nyingi taarifa hizi hazitambuliki kibinafsi. Hatuunganishi anwani ya IP kwa utambulisho wa binafsi, isipokuwa ridhaa imetolewa kabla au inapolazimu kutatua tatizo.
Rcg.org hutumia taarifa yoyote iliyotolewa kwa hiari na watumiaji kuimarisha uzoefu wao mtandaoni, ama kwa kutoa vipengele tendani au vilivyobinafisishwa kwenye tovuti au kuandaa kwa uzuri maudhui ya baadaye kulingana na utashi wa watumiaji.
Wakati mwingine, tunatumia taarifa zako zinazojulikana kibinafsi kukupatia taarifa, kama vile, lakini haziishii kwenye, vijarida mtandao na vitu vinavyotolewa kwa barua pepe.
Hatutatoa kwa umma habari yoyote tunayokusanya kutoka kwa watumiaji wa mtandao bila kibali kwa maandishi kilichotolewa kabla na mtumiaji isipokwa: (a) habari hiyo tayari inajulikana kwa umma, au (b) utoaji wa namna hiyo unatakiwa kisheria, agizo la mahakama, au unatakiwa na serikali nyingine au mamlaka ya kusimamia sheria.
Kanisa la Mungu Rejeshwa (na rasilimali husika) hutumia taratibu za viwango vya usalama viwandani kulinda dhidi ya upotevu, matumizi yasiyo sahihi au mabadiliko yasiyoruhusiwa habari zote za kibinafsi zilizo chini ya uwezo wake zinazoweza kutambuliwa. Aina hii ya itifaki inajumuisha, kuta za moto, vificho, ulinzi kwa neno la siri na ulinzi halisi mahali pa kazi.
PAMOJA NA HATUA HIZI ZA KIUSALAMA, HATUWEZI KUKUHAKIKISHIA KWAMBA MAWASILIANO YAKO YOTE YA BINAFSI AU HABARI BINAFSI HAZITAWEZA KUTOLEWA AU KUFIKIWA KINYUME CHA SHERIA NA UPANDE WA TATU USIORUHUSIWA.
Mtumiaji anaweza kujitoa wakati wowote kutoka katika orodha yetu ya watu waliosajili barua pepe. Tutatuma ujumbe wa kuthibitisha uamuzi wa kutaka kutoa data kwenye anwani ya barua pepe inayotumika sasa iliyosajiliwa kwa ajili ya mtumiaji huyo. Mtumiaji lazima ajibu ujumbe wa uthibitisho huo ndani ya siku tatu (3) za kazi. Pindi unapojibu, habari zako zinaondolewa kabisa kutoka kwenye kanzidata yetu. Kama ujumbe wa kuthibitisha hautapokewa, tutaendelea kumhifadhi mtu aliyekwisha jisajili pamoja na data zake husika.
Ingawa faragha yako ni ya muhimu mno kwetu, kwa sababu ya kuwepo mazingira ya kisheria na kikanuni, hatuwezi kuhakikisha bila shaka kwamba mawasiliano yako binafsi na habari zingine za kibinafsi zinazoweza kutambulika hazitaweza kutolewa kwa upande wa tatu. Kwa mfano, tunaweza kulazimishwa kutoa habari kwa serikali au pande za tatu katika nyakati fulani, au pande za tatu zinaweza kuingilia au kufikia upitishaji au mawasiliano binafsi kinyume cha sheria. Vilevile, tunaweza (na unatupatia mamlaka) kutoa habari yoyote juu yako kwa vyombo binafsi, kama vile vya usimamizi wa sheria au maafisa wengine wa serikali, na ikiwa, kwa busara yetu tutaamini ni lazima au inafaa kuchunguza au kutatua matatizo yanayoweza kutokea au maulizo.
Mahali hapa ni chanzo na msingi rasmi wa habari za kimtandao za Kanisa la Mungu Rejeshwa. Tukitambua kwamba kuna watu ambao wanapenda kuhamasisha juhudi zetu kwenye Mtandao kwa kudumisha kurasa za mtandao zinazorandana na tovuti hii, tumechukua sera ifuatayo kuhakikisha uthabiti na kulinda dhidi ya makosa.
Maudhui yote na michoro iliyo katika tovuti hii yamekatiwa hati miliki 2000-2024 na yanamilikiwa na Kanisa la Mungu Rejeshwa. Baadhi ya vipengele pia vinalindwa kama lebo ya biashara au lebo ya biashara iliyosajiliwa ya Kanisa la Mungu Rejeshwa. Kanisa la Mungu Rejeshwa linadumisha na kuhifadhi haki pekee kwenye leseni na matumizi ya maudhui hayo.
Tunaomba kwamba maudhui yoyote au yote na michoro yanayorejelea au kuhusiana na Kanisa la Mungu Rejeshwa au tovuti hii yawasilishwe kwetu kwa ajili ya kupitiwa na kuthibitishwa kabla hayajaonyeshwa wazi kwenye mtandao.
Malalamiko ya mtumiaji kuhusu utunzaji wa faragha yapeleke kwenye Huduma za Tovuti.