Kampasi ya Makao Makuu ya Kanisa la Mungu Rejeshwa, iliyoko Wadsworth, Ohio, imekaa juu ya eneo zuri lililo zaidi ya ekari 100 zenye misitu na ardhi ya shamba. Eneo hili maridhawa lina Jengo la Utawala, Kituo cha Kuandaa Barua na Vifurushi Vinavyotumwa kwa Posta na Kituo cha Vyombo vya Habari. Ardhi inayozunguka Kampasi itatumika kwa ajili ya programu ya kilimo cha kibiblia inayoitwa Taasisi ya Elimu ya Kilimo na Utafiti - Agriculture Education and Research Institute (AEARI).
Jengo la Utawala lina ukubwa wa futi-za-mraba 40,000 ambalo lina ofisi kuu za utawala na utendaji wa Kanisa la Mungu Rejeshwa. Jengo hili zuri la kati linawakilisha mafanikio katika usanifu, ujenzi na teknolojia ambayo ni ya kipekee katika eneo.
Shughuli za Utendaji wa Kanisa, ambalo lina mikusanyiko katika nchi zaidi ya 70 zikiwa katika mabara sita, limesambaza bure vipengee zaidi ya milioni 180 (vitabu, vijitabu, makala, video na majarida) ulimwenguni kote kwenye mtandao—vingi kati ya hivyo vinapatikana katika lugha 12—na linaendesha tovuti kubwa zaidi ulimwenguni yenye msingi wa kibiblia.
Kazi kubwa ya Kanisa la Mungu Rejeshwa ni kutangaza ujumbe wa tumaini la mwisho kwa mataifa yote—habari njema ya ufalme wa Mungu unaokuja hivi-karibuni (Marko 16:15; Mathayo 24:14).
Kituo cha Kuandaa Barua na Vifurushi Vinavyotumwa kwa Posta ni jengo lenye futi-za- mraba 12,000 ambamo kunafanyika kazi za Kanisa za utumaji barua na kazi za ndani za uchapishaji, vile vile idara za Matengenezo na Ujenzi. Ukuaji mkubwa wa usambazaji wa vitabu na kampasi inayopanuka imelazimu kuwa na nafasi zaidi kwa ajili ya vifaa vya kazi na watumishi.
Mamia ya maelfu ya vitabu halisi na vijitabu vimetumwa ulimwenguni kote. Kanisa linazalisha vitabu, vijitabu, makala na kozi za masomo zinazojitosheleza zaidi ya 150 vinavyofafanua kikamilifu mafundisho ya Biblia, ambavyo vyote hutolewa bila gharama.
Kanisa pia linazalisha Jarida la Ukweli Halisi, chapisho la bure lenye matoleo-6-kwa-mwaka ambalo hutazama simulizi za habari kuu leo kupitia lenzi ya Maandiko. Zaidi ya milioni 23 za makala ya Ukweli Halisi zimesomwa kwenye mtandao, pamoja na maelefu ya matoleo ya nakala ngumu yakitumwa kwa njia ya posta ulimwenguni kote kila mwezi.
Kituo cha Vyombo vya Habari ni jengo la kisasa lenye ukubwa wa zaidi ya futi za mraba 4,000 ambalo lina studio nne na idara ya Kanisa ya huduma za Uzalishaji wa Habari. Programu ya televisheni ya Ulimwengu Ujao™ na Daudi C. Pack, ambayo inawafikia mamilioni ulimwenguni kote, huchukuliwa na kurekebishwa katika jengo hili sambamba na video zingine nyingi na uzalishaji wa matangazo ya sauti.
Mpaka leo, Kanisa limefikia nchi na majimbo zaidi ya 230 na programu na nyenzo zake. Zaidi ya video milioni ishirini zimetazamwa kwenye tovuti ya Ulimwengu Ujao na idhaa yake ya You Tube.
Pia katika kampasi kuna Kituo cha Mabalozi, program ya mafunzo maalumu ya kuandaa viongozi na huduma katika Kanisa na kutoa mafunzo ya lazima kwa wale wanaotoa huduma katika Kazi ya Mungu, pote Makao Makuu na katika mikusanyiko ulimwenguni kote. Kituo kinatenda kazi chini ya kauli mbiu “Kuteka Tena Tabia za Kweli”.
Kanisa pia huchapisha jarida la Vijana Mabalozi™, likijawa na makala zinazolenga kutatua matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo vijana wa leo. Vile vile, kila mwaka Kanisa hufadhili Kambi la Vijana Mabalozi, kambi la majuma mawili kipindi cha kiangazi likitoa fursa kwa vijana kati ya miaka 13 na 19 Kanisani, kutoka ulimwenguni kote, hulenga kuwafundisha kuishi Njia ya Mungu.
Kujifunza zaidi kuhusu Kanisa la Mungu Rejeshwa, nenda kwenye Kutazama Ndani ya Kanisa na ujionee mwenyewe matokeo ambayo Kanisa linayo ulimwenguni kote (Wanaoitenda Kazi).