JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.

Kutazama Ndani ya Kanisa la Mungu Rejeshwa

Yesu Kristo alijenga Kanisa ambalo linatenda Kazi katika ulimwengu mzima. Kanisa la Mungu Rejeshwa limejizatiti kutoa bure ufahamu dhahiri kwenye karibu kila fundisho la Biblia, likitoa ujumbe unaobadilisha maisha ya mamilioni usiopatikana mahali pengine popote.

Makao Makuu ya Kanisa Ulimwenguni yako Wadsworth, Ohio, Marekani, likiwa na mikusanyiko ya waumini wanaokutana kila juma katika nchi na himaya zaidi ya 70 ulimwenguni. Soma zaidi hapa chini na jisikie huru kuwasiliana na sisi.

Kanisa la Mungu Rejeshwa, likiongozwa na Mchungaji Kiongozi Daudi C. Pack, limeagizwa na Yesu Kristo kufanya yafuatayo:

 1. Kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu kwa mataifa yote (Math. 24:14), ikiwa ni pamoja na kuyaonya mataifa ya leo yaliyotokana na Israeli ya kale juu ya adhabu ya kitaifa inayowangoja (Isa. 58:1-2; Ekek. 33:1-19)
 2. Kulilisha kundi la Mungu lililoitwa kutoka ulimwenguni na kuingia ndani ya Kanisa Lake (Yoh. 21:15-17; I Pet. 5:1-2)

Bofya kwenye viungo hivi kwa ajili ya kutazama Kazi ya Mungu iliyo kubwa mno na inayoongezeka haraka sana:

 • Ulimwengu Ujao na Daudi C. Pack: programu inayowafikia mamilioni ulimwenguni kote ambayo inafafanua visababishi vilivyo nyuma ya matatizo makuu ya mwanadamu—na suluhisho la pekee
 • Ukweli Halisi: jarida maarufu la kila mwezi—mwendelezo wa Ukweli Dhahiri
 • Mamia ya vitabu na vijitabu, makala, masomo na majalida bila malipo (pia katika Kiafikaani, Kijerumani, Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kiitaliano, Kiholanzi, Kipolandi, Kisabia, Kifini, na Kitahiti)
 • Kibunda cha Ufafanuzi wa Genge la Uasi: vitabu nane, ongeza mahubiri, kwa ajili ya wote wenye chimbuko la Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima, kikifafanua uasi wa karine ya 20
 • Kituo cha Mabalozi: taasisi ya juu ya miaka-miwili kufunza watumisi na viongozi wa baadaye
 • Sikukuu ya Vibanda: mahali pa kukusanyikia ulimwenguni kote
 • Nguzo: jarida litokalo kila baada ya miezi miwili kwa ajili ya washiriki
 • Vijana Mabalozi: jarida litokalo kila baada ya miezi miwili kwa ajili ya vijana
 • Kambi la Vijana Mabalozi: hufanyika kila mwaka kwa ajili ya vijana wa Kanisa
 • Taasisi ya Elimu ya Kilimo na Utafiti (AERI): ikiongozwa na mtaalamu wa kwanza kabisa katika kilimo cha kibiblia na ukulima endelevu, AEARI inaonyesha kanuni sahihi za kilimo kwenye-shamba na kupitia programu za ughani ulimwenguni kote
 • Uendelezaji wa Kampasi: ikiwa chini kidogo ya ekari 100 za viwanja inatoa mpangilio mzuri kwa ajili ya Ukumbi wa Utawala, jengo zuri lenye futi za mraba 40,000 ambalo lina ofisi za utawala wa Kanisa na utendaji; Kituo cha Kuandaa Barua na Vifurushi Vinavyotumwa kwa Posta, ambamo kunafanyika kazi za uandaaji na utumaji wa barua na vifurushi na uchapishaji wa ndani; na Kituo cha Vyombo vya Habari, chenye studio-nyingi za kisasa ambamo programu ya Ulimwengu Ujao na video zingine huzalishwa

Kanisa la Mungu Rejeshwa linapitia ukuaji wa haraka ulimwenguni kote! Tunaendelea kufundisha na kuajiri wachungaji na tunafungua mikusanyiko mipya mara kwa mara.

Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.