Akiwa Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Daudi C. Pack husimamia tovuti ya kibiblia iliyo kubwa kuliko zote. Alihudhuria Chuo cha Mabalozi, aliingia katika huduma ya Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima mwaka 1971 na yeye mwenyewe alifundishw a na Herbert W. Armstrong. Ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, ameandika vitabu na vijitabu zaidi ya 80, makala nyingi mno, na alionekana kwenye Kituo cha Televisheni cha Historia. Akiwa Mchapishaji na Mhariri-Mkuu wa jarida la Ukweli Halisi na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, amewafikia mamilioni ulimwengu kote na kweli zenye nguvu za Biblia, zisizojulikana karibu kwa wote.
Akiwa amezaliwa mwaka 1948, Bwana. Pack alikulia Magharibi ya Kati ya Marekani, katika mji wa Lima, Ohio. Akiwa amebobea kwenye michezo na uogeleaji wa ushindani kwa miaka 14, na akiwa amehitimu shule ya upili heshima-yote ya Marekani, vile vile akiwa ameanza kufanya mafunzo kwa ajili ya Olimpiki ya mwaka 1968, Bwana Pack alipata hatua kuu ya kugeuza ambayo ilikuja kuwa yenye kubadili-mwelekeo—na inayobadili-maisha—tukio.
Alianza kusikiliza programu ya redio ya Ulimwengu wa Kesho, iliyodhaminiwa na Redio Kanisa la Mungu (baadaye lilikuja kuitwa Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima), na akamsikia Herbert W. Armstrong akitangaza injili ya kweli ya Biblia—habari njema ya kuja kwa ufalme wa Mungu.
Akikataa nafasi ya kujiunga na Chuo cha Dartmouth, vile vile uteuzi wa kujiunga na Chuo cha Jeshi la Majini la Marekani, na nafasi nyingine nyingi za kulipiwa gharama za masomo, Bwana Pack alichagua Chuo cha Mabalozi kilichokuwa Pasedena, Kalifonia, makao makuu ya Kanisa ulimwenguni. Baada ya kuhitimu mwaka 1971, alimwoa Shirley Ochs (aliyefariki mwaka 2007), mhitimu mwenza kutoka Chuo cha Mabalozi na aliyekuwa katibu muhtasi wa Bwana Armstrong, na akaingia katika huduma ya kichungaji. Alihudumia mikusanyiko katika Indiana, Illinois, Wisconsin, New York, New Jersey na Ohio, na alifunza na kusimamia wachungaji wengine katika eneo pana.
Akiwa ameanza kama mwandishi katika miaka ya 1970, vitabu, vijitabu na makala nyingi za Bwana Pack zimewasaidia mamilioni kujifunza kweli za Biblia kuliko hapo awali. Amesafiri duniani kote, amehudumia maelfu kama mchungaji, na ameendesha mihadhara mingi ya Biblia. Bwana Pack pia ameshikilia nafasi nyingi za uongozi ambazo zimempatia uzoefu mkubwa katika huduma ya kichungaji na kiutawala.
Panapo kifo cha Bwana Armstrong mwezi wa Januari, 1986, ujumbe wa injili ya kweli na karibu kila fundisho linalotiririka kutoka kwenye ukweli huu kiini ulikataliwa na walioshika madaraka baada yake. Akisimama katika uthibitivu, Bwana Pack aliachana na Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima mwaka 1993, akifundisha na kuongoza njia kwa maelfu ambao wangemfuata.
Akiwa amedhamiria kutokana yale aliyoyaamini, Bwana Pack alianzisha KMR mwaka 1999. Kanisa la Mungu Rejeshwa kweli ni shirika la pekee, lisilofanana na lolote Duniani. Chini ya uongozi wake, linatangaza ujumbe mzito na ulio chanya, akijibu swali kuu lililo kwenye fikira za mabilioni: Ni nini kusudi la kuwepo kwa mwandamu? Hili linahitaji uchunguzi maalumu juu ya majibu ya kiroho kwa matatizo mabaya, taabu, maovu na magonjwa ambayo mwanadamu amekabiliana nayo wakati wote, lakini ambao yamekuwa mabaya zaidi katika karne ya 21.
Bwana Pack na vifaa vya Kanisa anashughulikia mahitaji ya kila siku ya mwanaume na mwanamke wa kawaida—na hufanya hivyo bila kuomba fedha, kushawishi watu kubadili dini au kujihusisha na siasa. Vitabu vyote na programu vinatolewa bure na kwa faida ya umma. Bwana Pack amejitolea kufundisha njia pekee kuifikia amani ya ulimwengu—habari njema ng’ambo ya habari mbaya za leo. Kwa msingi huu, ametengeneza au kusimamia utengenezaji wa hifadhi kubwa ya vifaa vya elimu kwa ajili ya watu wa kila rika.
Jarida tambulishi la Kanisa, Ukweli Halisi, na programu ya Bwana Pack ya Ulimwengu Ujao vinafikia kila taifa na nchi za ulimwengu, ikiwa ni pamoja na wakuu wa nchi na viongozi wengine katika serikali, dini, elimu, tasinia na vyombo vya habari.
Kujifunza zaidi, soma Wasifu wa Daudi C. Pack Ulioidhinishwa (The Authorized Biography of David C. Pack).