JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.

Herbert W. Armstrong Alikuwa Nani?

Herbert W. Armstrong aliliongoza Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima (Worldwide Church of God) [ambalo hapo kabla liliitwa Redio Kanisa la Mungu (Radio Church of God) hadi 1968] mpaka kifo chake mwaka 1986. Mamia ya mamilioni waliisikia sauti yake na kusoma vitabu vyake. Mungu alimwita katika kipindi cha kipupwe cha 1926 na aliongoka katika majira ya machipuko ya 1927. Kwa kipindi cha miaka 52 ya utumishi wake, Mungu alifunua kupitia kwake mamia ya mafundisho ya kweli yaliyokuwa yamepotea kadri karne zilivyokuwa zinapita; Bwana Armstrong mwenyewe alilisema hili mara nyingi. Katika miaka ile baada ya kifo chake, waliorithi uongozi wake walikoma kuamini na kufundisha mafundisho haya. Ingawa haki ya kunakili inalizuia Kanisa la Mungu Rejeshwa (The Restored Church of God) kuzalisha na kusambaza vitabu vyake vilivyoandaliwa wakati akiongoza Kanisa la Mungu la Ulimwengu Mzima, Kanisa la Mungu Rejeshwa limejizatiti kuhifadhi na kufundisha kweli zote alizozifundisha!