JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.

Kambi la Vijana Mabalozi

Kambi la Vijana Mabalozi (KVM) linafanywa kila mwaka na Kanisa la Mungu Rejeshwa (KMR).

Kila majira ya joto, vijana wa KMR kutoka ulimwenguni hukusanyika pamoja nchini Marekani kwa muda wa majuma mawili ya uzoefu wa kipekee. Kwenye KVM, wanakambi hufaidika kutokana na mihadhara ya kila siku na mafundisho ya Biblia, wanajifunza njia ya Mungu ya kuishi, wanashiriki kwenye michezo ya aina mbalimbali na kazi zingine za nje zenye changamoto, kujenga urafiki wa kudumu kwenye msingi sahihi, na kutengeneza kumbukumbu ambazo zitadumu maisha yote—kwenye mazingira yaliyo mbali na mivuto na majaribu mengi ya ulimwengu.

Video iliyo hapo juu inaonyesha baadhi ya michezo, hali ya utendaji mbalimbali, mihadhara, urafiki, na kumbukumbu za uzoefu za wakati wa kambi. Jionee mwenyewe kinachoifanya kambi hii maalum ya majira ya joto, uzoefu unaobadilisha maisha!