JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.
Hifadhi ili kusoma baadaye
Inapatikana katika lugha hizi:
Liko Wapi Kanisa la Mungu Leo hii?
Photo of a CongregationNew York, Marekani Photo of a CongregationJamaika Photo of a CongregationPeru Photo of a CongregationIdaho, Marekani Photo of a CongregationIndia Photo of a CongregationUbelgiji Photo of a CongregationKenya Photo of a CongregationArkansas, Marekani Photo of a CongregationAfrika Kusini Photo of a CongregationUingereza Photo of a CongregationNigeria Photo of a CongregationOhio, Marekani

Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu.” Kuna shirika moja linalofundisha ukweli wote wa Biblia, na limeitwa kuishi kwa “kila neno la Mungu.” Je, unajua namna ya kulipata? Kristo alisema lita:

  • Fundisha “yote” Aliyoagiza
  • Kuwa na washiriki walioitwa na kuwekwa wakfu kwa ile kweli
  • Kuwa “kundi dogo”
Habari za Mwandishi
Photo of David C. PackDavid C. Pack 

Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Mhariri-Mkuu wa Jarida la Ukweli Halisi, na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, Daudi C. Pack amewafikia mamilioni wengi ulimwenguni na kweli za Biblia zilizo na nguvu sana—zisizojulikana karibu kwa wote. Ameandika vitabu na vijitabu 80, mwenyewe ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, na alionekana kama mgeni kwenye Kituo cha Historia (The History Channel). Bwana Pack alihudhuria Chuo cha Mabalozi huko Pasedena, Kalifonia, aliingia katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu Mzima mwaka 1971, na yeye binafsi alifundishwa na mwanzilishi wake, Herbert W. Armstrong.

Nini Thawabu Yako Katika Maisha Yajayo?

na David C. Pack

Hakuna kitu kisichoeleweka zaidi kuliko wokovu. Kwa nini watu wengi wamechanganyikiwa—wamedanganyika—kuhusu kile watakachofanya baada ya maisha haya? Je, wokovu huja kwa neema au kwa njia ya matendo—na tofauti yake ni nini? Kwa namna gani—kwa vigezo vipi—watu hulipwa katika maisha yajayo? Kijitabu hiki cha muhimu sana kinaondoa mkanganyiko wote!

Wengi wanategemea kupata wokovu mwishoni mwa maisha haya. Lakini hii ina maana gani? Wengi mno hawaelewi kile isemacho Biblia kitakuwa thawabu yao ya mwisho. Wengi kwa hakika hawana wazo watakuwa wanafanya nini milele yote.

Je, wewe?

Mwinjilisti maarufu aliwahi kuulizwa mbinguni kutakuwa kwa namna gani. Alijibu, “Sijui lakini itakuwa ni ajabu na wote tutakuwepo pale.” Akakwepa swali.

Tanzia nyingi husema kuwa “waliofariki” “huenda nyumbani kuwa na Bwana.” Wengine huandika kwamba ndugu zao wapendwa waliofariki “waliungana na malaika” na kwamba “sasa hivi wanatuangalia.”

Baadhi wanaamini kwamba “wanaelekea kwenye utukufu.” Wanapoulizwa hii ina maana gani, wengi hawana uhakika. Lakini fikira za kawaida sana ni kwamba kila mmoja “atapaa mawinguni,” “kupiga vinubi,” “kutembea katika mitaa ya dhahabu mbele ya lango la lulu,” “kukaa katika viti vya kunesanesa” ama tu “kuzunguka mbinguni siku nzima.”

Mamia ya mamilioni wengine wamefundishwa kuamini kwamba wokovu ni kuutazama uso wa Yesu milele. Si tu kwamba wazo hili limejengwa katika uelewa potofu wa maandiko, lakini pia linafundisha kwamba hakuna atakayeweza kuuona uso wake moja kwa moja.

Ni kitu gani kinaweza kuwa cha kuchosha zaidi ya kutimiza mojawapo ya fikira hizi? Sitamani kufanya lolote la mambo haya kwa muda kitambo—achilia mbali kwa MILELE YOTE! Mtu fulani alipotafakari juu ya fikira hizi, alipendekeza kwamba ni “bora akaenda ahera, kwa sababu huko kunaonekana kuvutia zaidi.”

Mkanganyiko mwingi ajabu! Ujinga mwingi sana! Walio wengi wamedanganywa katika kuamini wokovu wa uongo.

Ni kitu gani umekisadiki bila kukithibitisha? Ni fikira gani maarufu uliyoifyonza bila kuchunguza ili kuona kile ambacho hasa Biblia hufundisha?

Wokovu ni Zawadi

Je, matendo yana sehemu yoyote katika wokovu wako? Liweke swali hili kwa namna nyingine, je, “haki” yako inahusiana na kuokoka? Kama ndivyo, je, vitu hivi huhakikisha wokovu moja kwa moja? Je wokovu hupatikana “kwa matendo?” Je, unaweza kuchuma wokovu kwa kitu chochote unachofanya?

Baadhi wanaamini kwamba wanaweza kuchuma wokovu wao. Tumeshutumiwa kwamba tunafundisha “wokovu kwa matendo,” kirahisi tu kwa sababu tunaamini Wakristo wana wajibu wa kutenda mambo fulani.

Biblia hufundisha kuwa kuna kitu ambacho watu “huchuma” kwa matendo yao. Inasema, “Wote wametenda dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Rum. 3:23). Warumi 6:23 huongeza, “mshahara wa dhambi ni mauti”—“bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

Lakini dhambi ni nini? 1 Yohana 3:4 husema, “kwa kuwa dhambi ni uasi wa sheria.”

Isaya 59:1-2 inaeleza kwamba dhambi huwatenga watu na Mungu. Ni hakika mdhambi ambaye hajasamehewa dhambi za nyuma na kuoshwa hawezi “kumfikia". Isaya 55:6-7 inawaagiza wale wanaotamani kuja kwa Mungu, “Mtu mbaya na aache njia yake.”

Mafungu mengi yanaeleza kwamba dhambi inaweza kusamehewa tu kwa njia ya kafara ya Kristo. Mtume Yohana alivuviwa kuandika, “Na Huu ndio ushuhuda, ya kwamba, Mungu ametupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima” (1 Yoh. 5:11-12)

Isipokuwa tunaye mwokozi—Yeye aliyelipa adhabu ya dhambi zetu—tunaelekea kwenye kifo! Mafungu mengi zaidi yanaweza kunukuliwa kuthibitisha kauli hii. Chunguza Yohana 5:26 ili kuona kwamba ni Mungu peke yake aliye na uwezo wa kutoa uzima wa milele. Habari njema ni kwamba Mungu anao uwezo wa kutoa karama ya uzima wa milele. Usifanye makosa! Wokovu hauwezi kuchumwa—Ni zawadi ya bure. Lakini ni zawadi inayotolewa kwa masharti kwa wale wanaostahili.

Wakristo walio wengi wanaamini kuwa “wanaokolewa kwa damu ya Kristo.” Hii siyo kweli! Biblia inasema kwamba “tunaokolewa KWA MAISHA YAKE” (Rum. 5:10), ili hali “tunapatanishwa na Mungu na “kuhesabiwa haki kwa damu Yake” (5:9). Pata ufahamu wa jambo hili. Hatuhesabiwi haki kwa matendo, lakini kwa damu ya Yesu Kristo.

Toba—kumrudia Mungu na kumtii—hutambulisha utii ujao wa Mkristo. Utii huo haufanyi chochote kufunika dhambi ZILIZOPITA. Damu ya Kristo huhesabia haki—husafisha, hufanya nyeupe, yenye haki—uasi wote wa zamani, dhambi. Angalia pia 1 Wakorintho 15:17-18. Lakini, “kuokolewa KWA MAISHA YAKE” ni muhimu ikaeleweka na inahitaji maelezo.

Zingatia! Kama Kristo hakufufuka kutoka kwa wafu, basi Roho wake hawezi kuongoza na kuwatia nguvu waongofu wapya, maana ni Roho Mtakatifu anayewaongoza Wakristo. Paulo aliandika, “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rum. 8:14). Ni Roho hii hii ambayo Mungu ataitumia kuwabadilisha waongofu kuwa wana wa Mungu wenye miili ya roho—Nafsi Roho zilizofufuliwa. Wanapobadilishwa, Roho hii iliyo ndani yao, hufanya uzima wa milele—wokovu—uwezekane. Imeeleweka? Kama Kristo angekuwa hajafufuka, basi asingeenda mbinguni mahali ambapo Baba na Yeye wanaweza kutuma Roho wao kwa wafuasi wao. Pasipo kuwa na Roho hii ikiishi akilini mwa Mkristo, hakuna tumaini la uzima wa milele.

Wanadamu hawana maisha wenyewe ndani yao. Hawazaliwi na nafsi isiyokufa. Mwanzo 2:7 hutamka kuwa watu NI nafsi hai—HAWANA roho isiyoweza kufa. Na Ezekieli 18:4, 20 husema, “Nafsi ile itendayo dhambi, itakufa.” Mathayo 10:28 huthibitisha hili. Wewe si kiumbe asiyeweza kufa. Maisha yako ni ya kipindi fulani kilichoamuliwa, baada ya hapo utakufa. Kama Mungu hataingilia kati, hauna maisha

ng’ambo ya ukomo wa kipindi cha takribani miaka 70-80. Kristo pekee ndiye aliye na kutokufa pamoja na Baba (1 Tim. 6:16; 1:17).

Hebu tuelewe kitu hiki moja kwa moja! Lazima tumalize mashaka yote kuhusu nini hasa kinacholeta wokovu. Ni karama au zawadi ya bure kutoka kwa Mungu. Kwa hakika hakuna kitu chochote ambacho Mkristo anaweza kufanya kustahili au kuuchuma. Malipo pekee ambayo wanadamu wanaweza kuchuma ni mauti. Kabla ya kujifunza somo la matendo ya Mkristo, tambua kuwa hakuna mtu anayeweza kupata uzima wa milele kwa matendo.

Wokovu ni kwa neema ya Mungu. Lakini neema ni nini? Ni msamaha kwa dhambi za mtu usiostahiliwa kabisa. Hii ndiyo maana ya neema. Wokovu maana yake ni kwamba mtu ameokolewa kutoka mautini. Bila ya Mungu kuingilia kati kwa kutumia damu ya Yesu Kristo kufunika maisha yaliyopita ya mtu anayetubu, hapawezi kuwa na wokovu.

Imani ina jukumu gani? Baadhi wanaamini kuwa “kuhesabiwa haki kwa imani” ndiyo kitu pekee ambacho Wakristo wanapaswa kushughulika nacho. Wanaamini kuwa yeyote anayefundisha kwamba aina yoyote ya matendo ni lazima, basi anakataa zawadi ya Mungu ya wokovu. (Hili tutalichambua zaidi baadaye.) Imani ina sehemu yake, lakini ni ipi?

Waefeso 2:8-9 hupanua zaidi fungu la Warumi 6:23: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo [imani] haikutokana na nafsi zenu, ni [imani] kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” Wokovu huja kama karama ya bure, kwa neemakwa njia ya imani! Hata hivyo, Paulo anaelezea kuwa imani nayo lazima iwe ni karama. La sivyo, ingekuwa “matendo” yaliyopatikana kwa nguvu za kibinadamu. Kama Mungu angetoa wokovu kwa kigezo hiki, ingemaanisha kuwa Mkristo ameupata kupitia imani iliyotokana na mwanadamu. (Soma kijitabu chetu Imani Halisi ni Nini? ili uelewe hakika somo hili.)

Swali lingine linaibuka. Je, Mkristo anapaswa kuwa katika maandalizi—mafunzo kwa ajili ya kitu chochote ambacho atakuwa anakifanya katika maisha yajayo? Na hii inahusiana vipi na karama ya wokovu? Maswali haya yanalenga kwenye kiini cha swali lingine kubwa: Mkristo ni nani?

Wengi sana hawajui majibu ya maswali haya ya msingi—lakini unaweza kujua!

Mkristo ni Nani?

Kabla ya kueleza kama Mkristo analazimika au halazimiki kutenda matendo mema katika maisha yake, tunalazimika kuchunguza swali lingine la msingi.

Mkristo halisi ni nani? Je, ni yule “anayehudhuria kanisani”—“anayemkiri Yesu”—“anayemjua Kristo”—“aliyebatizwa?” Je, lipo fungu moja linalotoa fasili ya Biblia ya Mkristo na kuondoa mkanganyiko wote?

Paulo aliandika, “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rum. 8:14). Mkristo ni yule aliye na Roho Mtakatifu akimwongoza. Lakini je, ni lazima sana kuwa na Roho wa Mungu ili kuwa Mkristo? Hapo awali, Paulo alikuwa amesema, “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake!” (fu. 9).

Ndivyo ilivyo rahisi! Ama mtu ana Roho wa Mungu na ni Mkristo, au hana na siyo Mkristo—si “wake.” Wale ambao wameongoka halisi lazima wawe na Roho Mtakatifu ndani yao.

Mtume Petro alifundisha, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha [Roho] Mtakatifu” (Matendo 2:38).

Kama ilivyo kwa wokovu na imani, Roho Mtakatifu ni kipawa! Kama Mungu hatakitoa, hakuna mtu anayeweza kuwa nacho. Lakini angalia! Kuna MASHARTI ya kutimiza kabla ya kukipokea. Toba na ubatizo hutangulia kupokea Roho wa Mungu. Hakuna chochote kati ya hivi kinachomstahilisha mtu kupata Roho wa Mungu lakini ni

vigezo—MASHARTI—ambavyo lazima vitimizwe ili Roho Mtakatifu aweze kutolewa!

Sasa angalia maana ya kupokea Roho wa Mungu, katika mantiki ya uzima wa milele, utakaotolewa baadaye, kwenye ufufuo: “Kristo...katika huyo pia baada ya kuwa mmeamini, mlitiwa muhuri na Roho Mtakatifu wa ahadi, aliye arabuni ya urithi wetu, hadi ukombozi wa milki iliyonunuliwa” (Efe. 1:12-14). Roho wa Mungu, ndani ya mtu ni malipo ya awali—“arabuni”—ya urithi wetu hapo baadaye pamoja na Kristo katika ufalme wa Mungu. Sisi ni “warithi sawa sawa na ahadi” ya wokovu (Gal.3:29)!

Kupokea Roho wa Mungu huanzisha mchakato unaoishia katika urithi pamoja na Kristo. Je, hiki ndicho kilichopo tu kwenye Ukristo na uongofu, au kuna mengine mengi zaidi?

Kuna mengine mengi zaidi!

Kristo alipofanya kumbukumbu ya Pasaka katika usiku ule kabla hajasulubiwa, alifundisha kanuni muhimu kwa wanafunzi wake kwa njia ya ombi: “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.Uwatakase kwa ile kweli; NENO LAKO NDIYO KWELI” (Yohana 17:15-17)

Mkristo huamini na kuifuata kweli. Kweli humtenga (humtakasa) kutoka kwa wote wanaomzunguka. Yeye si wa ulimwengu na njia zake, mila, na desturi. Hii ina maana gani tena? Vile vile, ukweli ni nini kuhusu uhusiano baina ya namna ambavyo maisha ya Mkristo sasa na kile atakachokuwa anafanya milele yote?

Unatakiwa Kufanya Kitu Chochote?

Wakristo wanatakiwa kutii sheria za Mungu? Jibu ni nini—ukweli—kutoka Neno la Mungu?

Yesu kamwe hakuwahi kufundisha kwamba watu wamwamini ili kupata wokovu. Kijana mmoja tajiri alipomwuliza afanye nini kuupata uzima wa milele—kupata wokovu—Kristo hakumwambia, “wewe niamini tu mimi.” Badala yake alimwambia, “Kama utaingia katika uzima, ZISHIKE AMRI.” Wanafunzi waliposikia hili waliduwaa. (Ndivyo ilivyo kwa wahubiri na waumini walio wengi.) Hawakuelewa namna gani hili linawezekana na wakauliza, “Nani basi atakayeokolewa?

Kristo alijibu, “Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana” (Math. 19:17, 25-26). Inawezekana kumwamini Mungu.

Ni lazima Wakristo wasiendelee katika dhambi baada ya ubatizo na uongofu. Paulo aliandika “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? HASHA! Sisi tulioifia dhambi [Kristo alishalipa adhabu kwa ajili yetu], tutaishije tena katika dhambi?” (Rum. 6:1-2).

Fungu la 12 hueleza zaidi jambo hili: “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake.” Mafungu ya 14-16 huendelea, “Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. Ni nini basi? Tufanye dhambi [uasi wa sheria, 1 Yohana 3:4], kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? HASHA! Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki?”

Wakristo wako chini ya neema. Lakini, japokuwa hawako tena “chini ya sheria”—chini ya adhabu ya mauti ambayo huletwa na uasi wa zamani—sasa wanamwamini Mungu. Msamaha kwa dhambi zilizotangulia kutendwa siyo leseni ya kutenda dhambi za mbele kwa uhuru.

Katika Marko 7:7-8, Kristo alisema, “Nao WANIABUDU BURE, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.” Inawezekana kumwabudu Kristo bure. Inawezekana kumfikiria, kumwongelea na kumrejelea mara kwa mara kama Bwana—YOTE BURE!

Sasa angalia, “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni [“wa” siyo “huko” mbinguni]; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Math. 7:21). Paulo aliandika, “WAITENDAO sheria [ya Mungu]

watakaohesabiwa haki” (Rum. 2:13).

Kwa hakika Mkristo ni yule anayetenda mambo fulani. Wajibu wake ni zaidi ya kuamini tu. Katika muktadha wa kuelezea tofauti baina ya wale wanaojenga nyumba zao juu ya mwamba na wale wanaojenga juu ya mchanga, Kristo alisema, “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?” (Luka 6:46). Mkristo hutenda yale ambayo Mungu anasema kutenda! Pia, soma kwa uangalifu Yakobo 1:22-25; 2:8-12, 14, 17-20. Mafungu haya huthibitisha maelekezo ya Kristo akiwaamuru Wakristo kushika amri za Mungu, akivifunga pamoja matendo na imani. Wanaonyesha siyo imani AU matendo lakini imani NA matendo.

Biblia huongea juu ya “[Roho] Mtakatifu, [ambaye] Mungu amewapa [NI KIPAWA] wote wamtiio” (Matendo 5:32). Kupokea Roho wa Mungu hutanguliwa na toba (kwa kuvunja amri za Mungu) na ubatizo (Matendo 2:38). Ni katika hatua hii ambapo maisha ya kiumbe-roho kipya huanza. Mtoto huyu mpya wa Mungu aliyetungwa sasa ni “mrithi pamoja na Kristo” (Rumi 8:17). Anakuwa sehemu ya kanisa ambalo Kristo aliahidi kulijenga na kuliongoza (Math. 16:18; Efe. 1:22-23; Kol. 1:18), analolilisha kupitia huduma ya watumishi wake wa kweli (Efe. 4:11-15)

Lakini vipi habari ya “kuwa na upendo”? Je, Wakristo si wale tu ambao “huonyesha upendo”? Kama ndivyo, upendo ni nini? Na tuchunguze mafungu kadhaa zaidi. Tuondoe mkanganyiko wote!

Paulo aliandika, “…kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na [Roho] Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Rumi. 5:5). Mkristo anapopokea Roho Mtakatifu, anapokea sehemu (ndogo sana hapo awali) ya upendo wa Mungu. Kiwango na kina cha upendo huu huendelea kuongezeka kadri mhusika navyoudhihirisha kwa bidii.

Kuna njia mbili tofauti za maisha. Moja ni ya njia ya “KUTOA”—njia ya upendo na kufikiria wengine—njia ya Mungu. Nyingine ni njia ya “KUPATA”—njia ya ubinafsi na kujifikiria mwenyewe—njia ya mwanadamu. Baadhi hulenga kwenye “kupata” wokovu kwa ajili yao tu, wakati huo wakitenda kitu kidogo sana kadri inavyowezekana. Kristo alifundisha kwamba ni “heri KUTOA kuliko kupokea” (Matendo 20:35)

Tukiwa na hili akilini tujiulize, ni nini fasili ya Biblia kuhusu upendo? Yohana aliandika, “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE; wala amri zake si nzito” (1 Yohana 5:3). Wengi wanaodai kuwa na upendo wanaamini kuwa amri ni nzito. Mungu anasema si nzito. Anaitaja sheria yake “takatifu, na ya haki, na njema” (Rumi 7:12, 14).

Biblia hueleza, kupitia Paulo, kwamba amri na sheria ziko sawa: “Pendo halimfanyii jirani neno baya; BASI PENDO NDILO UTIMILIFU WA SHERIA” (Rumi 13:10). Biblia hufasili upendo kama “utimilifu wa sheria.”

Maelezo ya kina juu ya upendo yanapatikana katika 1 Wakorintho 13. Chukua muda kusoma sura hii kwa uangalifu. Kudhihirisha upendo wa Mungu kunajumuisha Nyanja nyingi za tabia—vitendo—matendo—yanayofanywa na Mkristo!

Watu wote wanaweza kutembea kwa uhuru katika jamii zao pale tu wanapofuata sheria za wanadamu. Raia wa kila taifa wanaelewa kuwa uhuru ni fursa ambayo inaweza kupotezwa kwa uvunjaji wa sheria. Kwa hakika wanadamu hawana busara zaidi kuliko Mungu. Watu wako huru katika Kristo pale tu wanapomtii.

Kwa hiyo, Mkristo ni “mtendaji” si tu “muumini” au “msikiaji.” Wokovu ni kipawa, lakini kuna masharti ya kutimiza—mwenendo, tabia, matendo—ambavyo ni lazima vitekelezwe, ama sivyo imani katika Kristo ni bure! Na yeyote anayedai kuwa na upendo lazima atekeleze “matendo” ya utii wa sheria, yanayoithibisha imani hiyo.

Kwa Nini Kijitabu Hiki?

Kijitabu hiki kimeandikwa kuelezea thawabu ambayo Mkristo anaweza kutegemea katika maisha yajayo. Lengo lake ni kuunganisha matendo ya mtu katika MAISHA HAYA na kiwango cha thawabu itakayotolewa katika MAISHA YAJAYO. Biblia ina mengi ya kuse-

ma na hauna budi kutambua namna ufahamu huu ulivyo wa muhimu kwa maisha yako yajayo. “Kuokolewa kwa neema” na “kulipwa sawa sawa na matendo” ni mambo mawili tofauti kabisa. Wachache wanaelewa kwamba si kimoja au kingine—NI VYOTE VIWILI

Usishindwe kuelewa umuhimu wa kipekee wa kinachoelezewa hapa. Kwa hakika hakuna kingine kitakachokuwa cha muhimu zaidi utakachosoma kutoka Kanisa Rejeshwa la Mungu (RCG) kuliko jibu la swali lililoibuliwa katika kichwa cha kijitabu hiki. Lengo hapa ni kuelezea uhusiano kati ya matendo yako katika maisha haya na thawabu yako katika maisha yajayo.

“Matendo” Si Matambiko ya Sheria ya Musa

Biblia husema tena na tena kwamba Wakristo watalipwa baadaye sawa sawa na matendo wayafanyayo sasa. Tutakuja kuona kwamba jambo hili ni fundisho la maandiko lililo WAZI—PEUPE. Lakini, ni aina gani ya matendo yanayorejelewa hapa? Kwa hakika Biblia hurejelea matendo kwa maana mbili zilizokusudiwa. Kijitabu hiki kitajikita kwenye maana moja kati ya hizi.

Nyaraka za Paulo kwa Warumi na Wagalatia zina kumbukumbu ya “matendo ya sheria.” Neno la Kigiriki kwa haya, ergon, humaanisha kazi za kutaabisha za sherehe, matambiko, na makafara ambayo Waisraeli wa zamani walitakiwa kufanya katika nyakati fulani. Kitabu cha Mambo ya Walawi na sehemu zingine huyajadili kwa undani. Mara nyingi walitakiwa kuyafanya sambamba na kutii Amri Kumi.

Lakini, hii siyo maana ambayo tutajikita kwayo. Ergon pia inaweza kuhusisha “kazi za kimwili, vitendo, kazi au matendo ya kiroho ya haki.” Mara zote, wakati maana hii inakusudiwa, neno “matendo” husimama pekee yake, bila kuwa na usemi “ya sheria” (sheria ya Mungu, Amri Kumi). Neno la Kigiriki linalotumika mara kwa mara praxis, ambalo nalo mara nyingi limetafsiriwa “matendo” karibu lina maana sawa.

Huwezi kuishi maisha yako bila kufanya mambo mengi kila siku. Mambo yote unayoyafanya ama huwa ni mema au ni mabaya. Ni “matendo yako.” Yanakutambulisha wewe namna ulivyo. Sulemani aliandika, “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake” (Mith. 20:11). Kama hii ni kweli kuhusu mtoto, ni zaidi kiasi gani kwa watu wazima?

Wakati wokovu ni karama, thawabu yako katika ufalme wa Mungu itaamuliwa na matendo yako sasa, katika maisha haya. Elewa hili!

Kabla ya kuchunguza maandiko yanayothibitisha hili, lazima kwanza uelewe japo kidogo wokovu kimsingi unajumuisha nini.

Watakatifu Kutawala

Wakristo husali, “Ufalme wako uje.” Maandiko mengi yanafunua kwamba Kristo atasimamisha ufalme wa Mungu wakati wa Kurudi Kwake. Atatawala mwenyewe—au wengine watatawala pamoja naye? Atakaposimamisha serikali yake itawalayo ulimwengu mzima, je, itakuwa na muundo wa namna gani?

Chunguza kile Danieli alichoandika kuhusu huu ufalme. Danieli 7:13 huongelea kuja kwa Kristo. Kabla hajarudi, Mungu atampa rasmi mamlaka ya kutawala ulimwengu. Fungu la 14 husema, “Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.”

Kwa hakika ni namna gani Mungu anakusudia kuwaongoza watu wa mataifa yote duniani? Tena, Kristo atatawala pekee yake, au pamoja na wengine?

Mafungu kadhaa zaidi katika Daniel 7 ni ya lazima mno kuyafahamu. Angalia fungu la 18: “Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.” Hiyo ni sahihi! Hatima ya mwito wa Wakristo wa kweli ni ku-

ungana na Kristo na kushirikiana utawala katika ufalme wa Mungu juu ya mataifa yote na watu. Hakika, Kristo ni “MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana.”

Sasa soma fungu la 22: “…nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.”

Fungu la 27 linadhihirisha mategemeo ya kushangaza yaliyo mbele kwa watakatifu wote wa kweli wa Mungu: “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.”

Kristo anasema, “Na yeye ASHINDAYE, na KUYATUNZA MATENDO YANGU hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye ATAWACHUNGA kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu” (Ufu. 2:26-27) na baada ya mafungu machache baadaye anaongeza, “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi…(3:21).

Wakristo ni washindaji. Wanaelewa kuwa ni lazima “watunze” “matendo” ya Kristo.” Hawakai kivivu, “wakiamini tu” katika Yesu. Wanatambua kuwa wako katika mafunzo ya kuwa waalimu na watawala!

Ufunuo 5:10 inaongeza, “ukawafanya [Mungu] kuwa ufalme [watawala] na makuhani [waalimu] kwa Mungu wetu; nao WANAMILIKI juu ya nchi.” Si ajabu Kristo alisema, katika Hubiri la Mlimani, “wenye upole…watairithi nchi” (Math. 5:5). Pia angalia Yuda 14-15.

Usemi “katika kiti changu cha enzi” (Ufu. 3:21) unatumika kwa sababu Kristo anatambua kwamba kiti chake cha enzi kiko duniani—tofauti na kiti cha enzi cha Baba, ambacho kiko mbinguni. Luka 1:32 inaonyesha kwamba Kristo ataketi Yerusalemu katika kiti cha enzi cha Daudi.

Ufunuo 20:4, 6 husema, “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu…nao wakawa hai, WAKATAWALA pamoja na Kristo miaka elfu…Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa MAKUHANI wa Mungu na wa Kristo, nao WATATAWALA pamoja naye hiyo miaka elfu.”

Kitu gani chaweza kuwa wazi kama mafungu haya? Kristo anaporudi, watakatifu wanatawala pamoja naye! Watatawala ulimwengu wote pamoja naye!

Sasa, inawezekana mtu yeyote akadhani kwamba Mungu atampa mtu yeyote madaraka makubwa namna hii bila kwanza kufuzu na kujifunza namna ya kuyatumia? Inawezekana mfalme yeyote wa kibinadamu kutawala nchi kwa ufanisi bila kupitia mafunzo yoyote? Bila shaka hapana!

Baadhi Hukataa Mamlaka ya Mungu Juu Yao

Kristo alinena mfano muhimu sana kwa lengo la kuwafanya Wakristo waweze kuelewa utawala ujao wa ufalme wa Mungu na wajibu wao KUFUZU na kuwa sehemu yake. Tumia muda kuusoma.

Katika Luka 19:11-27, Kristo alijilinganisha na Kabaila aliyesafiri kwenda “nchi ya mbali” (kielelezo cha yeye kurudi mbinguni kwa takribani miaka 2,000) hadi Kurudi Kwake. Wanafunzi waliamini kwamba ufalme wa Mungu “ungetokea mara” na Kristo alitaka kufafanua kuwa muda mrefu ungepita kabla ufalme haujatokea. Yule “Kabaila” katika mfano “aliwaita” “watumwa wake kumi” (Kivuli cha Wakristo wakiitwa na Mungu kutoka ulimwenguni) na kuwaagiza kuzalisha thamani ya “talanta” (fedha) aliyompa kila mmoja kwa ajili ya kuwekeza. Talanta iliwakilisha kipimo-msingi cha uthamani wa mambo ya kiroho. Kumbuka huu ni mfano, kwa hiyo Kristo alikuwa hamaanishi fedha halisi. Aliwaambia watumwa wake “Fanyeni biashara hata nitakapokuja”—au kuizalisha talanta iwe fedha nyingi zaidi. Kabaila alipokwenda zake, inasemekana, wakiongelewa watumwa wake, “Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu ATUTAWALE. Ni muhimu kuelewa lengo la kauli hii!

Historia fupi inahitajika ili kuelewa mazingira ya mfano huu. Kristo alikuwa Mya- hudi akihubiri mfano huu katika nchi ya Yuda. Yuda lilikuwa ni moja ya makabila ku-

mi na mbili ya Israeli wa zamani. Makabila kumi kati ya hayo yalikuwa yameshapotea miaka 700 iliyopita kwa sababu walimwasi Rehoboam mtoto wa Sulemani. Walikuwa wamechukuliwa utumwa na Waashuru wa zamani (Wajerumani wa leo) na baadaye wakahamia Ulaya ya kaskazini-magharibi. Hatimaye wakawa nchi za kidemokrasia zenye kuongea Kiingereza za Marekani, Uingereza, Kanada, Australia, New Zealand na baadhi ya mataifa ya Ulaya magharibi. Vile vile, baadhi ya watu wa makabila ya Benyamini na Lawi walibaki na Wayahudi, ambao makao makuu yao yalikuwa Yerusalemu.

Mfano huu unapoongelea wakazi wa mji wa Kabaila “kumchukia” na kusema, “Hatumtaki mtu huyu atutawale,” ni kielelezo cha Wayahudi, ambao historia inaandika kwamba walikataa mamlaka ya Kristo. Hiki ndicho Yohana 1:11 inachomaanisha inaposema kwamba “Alikuja kwa walio wake, na walio wake hawakumpokea.” Wale “watumwa kumi” (Wakristo wanaoitwa leo) ni kivuli cha kiroho cha MAKABILA KUMI YALIYOPOTEA ya Israeli. Kristo aliwatuma wanafunzi wake (Math. 10:6) “kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Math. 15:24). Alitoa fursa kwa makabila haya kutawala kwa sababu Wayahudi walikataa mamlaka yake juu yao.

Wengi hawataki Kristo awaambie cha kufanya. Hawamtaki awatawale. Wanataka wokovu, lakini pasipo masharti.

Hawa “wenyeji wa mji” walielewa kuwa Kabaila (Kristo) alikuwa anakuja “kutawala” duniani. Walidhihirisha kwamba hawakutaka sehemu katika hili na wakakataa serikali yake (utawala) juu yao—na hivyo sehemu yao ndani yake katika wakati ujao (Luka 19:27). Walitambua kuwa ufalme wa Mungu utakuwa ni serikali itawalayo. Elewa! Mfano ulianza na Kabaila (Kristo) kwenda mbinguni “kupokea ufalme kwa ajili yake na kurudi.”

Kabaila aliporudi, alimwita kila mtumwa kuja mbele yake kutoa hesabu ya namna ambavyo alizalisha talata aliyokuwa amepewa. Kristo alitaka kujua kiasi gani “kila mmoja alikuwa amezalisha” (fu. 15) alipokuwa amekwenda zake. Baadhi walikuwa wamezalisha talanta tano, wengine kumi, n.k., lakini mtumwa mmoja alikuwa amezika talanta yake ardhini na hakuitumia kuzalisha chochote.

Sasa hii ni muhimu sana. Ipate vizuri hii, kwa sababu inarahisisha uelewa wa namna gani matendo yako sasa yanachangia kiwango cha thawabu yako baadaye. Usielewe isivyo.

Mtumwa wa kwanza aliongeza talanta kumi. Kristo alielezea thawabu yake, akisema, “Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na MAMLAKA JUU ya majiji kumi” (fu. 17). Kazi zake zilimletea malipo haya.

Mtumwa aliyeongeza talanta tano aliwekwa “JUU ya majiji matano.” Kwa sababu mtumwa wa pili alizalisha nusu ya yule wa kwanza, malipo yake yalikuwa nusu yake pia. Hivyo, watu hawa walipewa MAMLAKA—walipewa nafasi za uongozi wa juu kwenye majiji. Thawabu yao ilikuwa ni KUTAWALA pamoja na Kristo kwenye ufalme wake utawalao ulimwengu mzima. Na ilihusisha moja kwa moja kazi au matendo yao katika maisha haya!

Mtumwa aliyezika talanta yake kwenye kitambaa alikuwa amepoteza fursa kuu ya kufuzu kwa ajili ya utawala katika ufalme wa Mungu. Hakuzalisha chochote wakati wa uhai wake. Fungu la 22 husema “Akamwambia [Kabaila, Yesu], Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe.” Mtumwa huyu hakukua na hivyo hakufuzu kwa utawala juu ya majiji. Kristo aligawa thawabu ya mtumwa huyo mwovu kwa yule aliyekuwa ameongeza talanta kumi—kiasi kwamba huyu akawa na zaidi ya hata thawabu yake mwenyewe. Inawezekana yule mtumwa mwovu alidhani kwamba alikuwa na wokovu, lakini alikuwa amejidanganya mwenyewe. Alikuwa “mtumwa asiyekuwa na faida” na “alitupwa…katika giza la nje” (Math. 25:30).

Hakuna yeyote atakayepewa utawala kama hatakuwa amethibitisha kuwa anaweza kutawalika! Hakuna yeyote atakayeweza kuwa sehemu ya serikali ya Mungu kama hatakuwa amejifunza kujisalimisha chini ya serikali ya Mungu—kutawaliwa na Mungu na Kristo katika maisha haya. Hili ndilo somo muhimu la mfano huu! Wakristo wanapaswa “kukua katika neema na…maarifa” (1 Petro 3:18). Hata neema haiji yote mara moja.

Kristo alipowaita watumwa wake kutoa hesabu, alikuwa anaonyesha kuwa siku moja watu wote watasimama mbele ya kiti cha cha hukumu cha Kristo kutoa hesabu. Kama ilivyothawabu ya mitume ambao wata“keti katika viti kumi na viwili, mkiwa- hukumu kabila kumi na mbili za Israeli” (Math. 19:27-28), baadhi watapewa MAM- LAKA makubwa kutawala juu ya majiji pamoja na Kristo “katika kiti cha enzi chau tukufu wake”

Kumbuka, wale “wenyeji” walisema, “Hatumtaki mtu huyu atutawale.” Ni wewe pekee yako unayeweza kuamua kama utamruhusu Yesu Kristo atawale juu yako sasa, na kama utajiandaa mwenyewe kutawala juu ya wengine hapo baadaye!

“Kuokoka” Maana Yake Nini?

Marudio ya namna fulani yanahitajika katika kuelezea ni lini Mkristo anapookoka. Hili ni somo lenye mkanganyiko mkubwa. Kulielewa ni jambo nyeti katika mchakato wa wokovu.

Kwa hakika mtu anaokoa katika hatua tatu tofauti. Kumbuka kwamba Warumi 6:23 ilielezea kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. Katika kutubu, kubatizwa na kuongoka, Mkristo husamehewa kwa damu ya Kristo na mara hiyo anaokoka kutoka adhabu ya dhambi ZILIZOPITA. Kwa hiyo kwa namna moja, mtu ameokoka katika saa hiyo, kutoka mautini. Mpaka sasa umegundua kuwa hii siyo habari yote.

Kuna matakwa mengine mawili kuhusu lini na kwa namna gani mtu anaokoka. Neno wokovu limetokana na neno kuokoka. Kwa hiyo, hatua ya pili ndiyo iliyo wazi zaidi—wokovu kwenye ufufuo panapo Marejeo ya Kristo (1 Kor. 15:50-55; 1 Thes. 4:13-18)

Lakini hakuna mtu apokeaye wokovu bila kupitia maisha ya dhiki, majaribu, kujifunza, kukua na kushinda. Njia ya tatu mtu anayookoka ni kwamba “anaokoka kila siku”—mchakato unaoendelea—maisha yake yote. Mafungu mengi yanaonyesha kwamba hakuna kitu kinachotokea chenyewe baada ya kuongoka. Kuamini kwamba kuna kitu kama hicho ni kumdhihaki Mungu. Tumeona mafungu mengi yakitamka masharti fulani kabla ya ubatizo, na mahitaji mengine zaidi, baada ya ubatizo, kwa wale wanaopokea wokovu.

“Kuokoka Mara Moja”, Si “Kuokoka Moja Kwa Moja”

Zingatia kuwa Kristo alisema, Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka” (Math. 24:13; 10:22). Ukristo ni jaribio la uvumilivu, pasipokuwa na chochote kinachotokea chenyewe. Mkristo anaweza kuvia (mfano wa mimba iliyoharibika) katika maisha haya, kama hataendelea katika njia sahihi. Hakuna hata mmoja anayeokoka moja kwa moja anapoongoka. Kristo alisema (mara mbili) kwamba watumwa wake lazima “wavumilie mpaka mwisho” wa maisha yao. Kauli hii ina mantiki gani kama wokovu unahakikishwa tu pale mtu anapompokea Kristo?

Kitabu cha Waebrania kina maonyo—ILANI—kwa wale ambao wataishi njia ya Ukristo kwa namna ya kizembe! Paulo aliandika, “Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa [Kigiriki: Kuvuja kama kwenye chombo chenye matundu]. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! Tutapataje kupona, TUSIPOJALI wokovu mkuu namna hii…” (Heb. 2:1-3).

Kuwa mwangalifu! Hii ni tahadhari kwa wote. Wokovu si lelemama. Unaweza kutuponyoka kama tutaruhusu ufahamu wa muhimu na hitaji la kutenda vivuje kutoka kwenye vyombo vyetu.

Paulo aliendelea mbele kuelezea hatari kubwa ya dhambi ya makusudi: “Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; (maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;) tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na KAZI NZURI; wala tusiache kukusanyika pamoja [Washiriki wa Kanisa la Mungu la kweli hukutana pamoja kila Sabato]…Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi

wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi” (Ebr. 10:23-26).

Hii ni nzito! Wahubiri wa dunia hii huwafundisha watu kwamba wako chini ya neema—wameshaokoka katika maisha haya—kwamba hawawezi kuanguka au kuvia kwa sababu ya mwenendo mbaya, dhambi. Usikanganyishwe kwa maneno malaini ya wale wanaodai kumwakilisha Kristo. Mungu ana viwango na ni lazima vifikiwe. (Soma pia Yakobo 4:17.)

Katika Waebrania 6, Paulo alimwelezea yule ambaye “ameanguka.” Anachora picha inayopasa kutafakariwa sana: “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, WAKAANGUKA baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri” (fu. 4-6). Kwa hao “haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi.”

Mafungu haya hayaachi shaka kwamba inawezekana ukawa Mkristo na ukaanguka kutoka njia ya kuuendea wokovu. Nimewafahamu wengi ambao”walilionja neno zuri la Mungu” na kufanywa “washirika wa Roho Mtakatifu” waliokoma kuwa “wenye nuru”—na wameanguka kutoka kwa Mungu na wokovu. Paulo anatamka kwamba HAIWEZEKANI watu hao kupona!

Haya ni maneno ya wazi ya Biblia. Kila fungu lililonukuliwa hapa ni la umuhimu wa kipekee na inapasa lisomwe kwa uangalifu, ili kutambua wajibu ambao Mungu anauweka kwa watumwa wake. Usiwe miongoni mwa wengi wanaoyapuuzia, wakijidanganya kwamba wana “Yesu mioyoni mwao”

Wale wanaojidai Watumishi wa “Kikristo” katika dunia hii hufundisha wokovu wa uongo, wa kipagani wa kwenda mbinguni, usiokuwa kwenye maandiko, badala ya ukweli—kwamba maisha haya ni kutuandaa kwa ajili ya utawala. Wanapuuzia mafungu ambayo tumeyachunguza muda mfupi uliopita kwa sababu hawataki kuwajibika kwa kufanya kitu chochote. Ni kwa namna gani “kuokoka tayari” kunaendana na maisha ya mateso, kukua, utii kwa Mungu na mateso makali (Yohana 15:20; 2 Tim. 3:12; Zab. 34:19; n.k.)?

Kama wokovu unatokea hapo hapo, wakati ule uzoefu wa kidini uliobandikwa jina la “uongofu,” unatokea, pasipo kulazimika kutenda matendo mema, kwa nini Mungu asiyaruke maisha haya na kuwachukua watu mara moja kwenda kwenye chochote ambacho kinatakiwa kuwa thawabu yao? Watumishi wa kidini wa dunia hii hawajibu wala hawawezi kulijibu swali hili!

Usianguke kwenye hatari ya wimbo “wewe amini tu.” Ndio uongo mkuu kabisa ambao wanatheolojia wa Kikristo vipofu wa mambo ya kiroho wameughilibu umma wa Ukristo wa kawaida usiotilia shaka!

“Kulipwa…Sawa Sawa na Matendo”

Tumesoma Waefeso 2:8-9 kuhusu wokovu “kwa neema, kwa njia ya imani” na kwamba hata imani ni kipawa. Wanatheolojia, wanadini na watu wa makanisa karibu wote kwa pamoja huishia kusoma hapa. Kwa nini karibu kabisa hakuna anayeendelea kusoma fungu la 10 lililo la muhimu sana?

Angalia: “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” Hiyo ni sahihi! Wakristo lazima “waenende…katika matendo mema” kama “kazi yake [Mungu].”

Sasa soma na kuelewa fungu nyeti. Mathayo 16:27 husema, “Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo ATAKAPOMLIPA kila mtu kwa kadiri ya MATENDO yake.” Angalia haisemi, “kuokolewa kwa matendo” (kwa kuwa wokovu ni kipawa) lakini kwamba kila mtu “HULIPWA…kadri ya matendo yake.” Kristo huleta malipo ya kila mtu anapokuja.

Alipokuwa chini ya mashambulizi ya matendo maovu ya Iskanda mfua shaba, Paulo alisema, “Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake” (2 Tim. 4:14). Katika hali hii matendo maovu ya Iskanda yalikuwa yamemchumia “malipo.”

Fikiria hili: Malipo yako ni kile unachochuma—baada ya kuwa umeshapokea ki-

pawa cha wokovu kwa neema! Unaweza kuchuma “ujira” wenye malipo makubwa au madogo katika ufalme wa Mungu kadri ya kiwango cha matendo yako mema. Angalia kile ambacho Paulo aliandika kwa Warumi: “Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni DENI (4:4). Wokovu ni kwa neema, lakini malipo ni deni linalolipwa na Mungu kwa kila mtu kwa ajili ya matendo yake.

Lifikirie kwa njia hii. Hakuna chochote ufanyacho kitakuingiza katika ufalme wa Mungu. Hii ni kwa neema. Kila kitu ufanyacho kitaamua kiwango cha malipo yako baada ya wewe kufika pale. Kwa maneno mengine, wokovu si neema AU matendo, lakini neema NA matendo!

Pambano la Maisha Yote

Tunasoma, “Mwenye kuvumilia mpaka mwisho ndiye ATAKAYEOKOKA.” Kuishi maisha ya kukua na kushinda siyo rahisi. Ni mapambano ya kila siku dhidi ya mivuto ya kimwili na majaribu ya dhambi. Hii ndiyo sababu Kristo pia alisema, “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba [ngumu]; maana mlango ni mpana, na njia ni pana [rahisi] iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba [ngumu], na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache” (Math. 7:13-14). Kawaida wengi hutafuta njia rahisi, “pana”.

Lakini Petro aliandika, “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? (1 Pet. 4:17-18)

Wakristo wanahukumiwa sasa. Ulimwengu hauhukumiwi. (Soma kijitabu chetu Ulimwengu Matekani kujifunza kwa nini.) Hukumu hii ingekuwa na maana gani kama matendo yetu—mienendo yetu—haileti tofauti yoyote kwa Mungu? Matendo yetu huleta tofauti kwake.

Paulo alilielewa hili. Angalia: “Nami nafanya…ili kuishiriki pamoja na wengine. Je! Hamjui [wengi hawajui], ya kuwa wale washindanao kwa kupiga MBIO, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate [shinda]. Na kila ashindanaye katika michezo [ubingwa au ushindi] hujizuia katika yote; basi hao [wasio Wakristo] hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi [Wakristo] tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi NAPIGA MBIO vivyo hivyo, si kama asitaye; NAPIGANA…isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa [shindwa, poteza]” (1 Kor. 9:23-27) na “Basi…na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na TUPIGE MBIO kwa saburi katika yale MASHINDANO yaliyowekwa mbele yetu” (Ebr. 12:1)

Paulo alijua kwamba mbio zake zilikuwa ndefu, siyo fupi. Na ndivyo ilivyo kwako pia.

Pia aliuelezea Ukristo kama “kupiga mieleka” (Waefeso 6:11-12) dhidi ya “hila za shetani.” Na aliwaagiza Wafilipi “NAKAZA MWENDO, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu” (3:14). Alitambua kuwa inahitajika juhudi kubwa kukimbia na kushinda mbio ndefu.

Mfano wa Mpanzi

Mathayo 13:1-9, 18-23 ina mfano wa mpanzi. Usome kwa uangalifu. Unaelezea “mpanzi” aliyetawanya mbegu shambani. Aina nne tofauti za matokeo zinaelezewa katika mfano huu mpana.

Aina ya kwanza walisikia injili na ukweli na hawakufanya chochote—hawakuongoka. Aina ya pili waliipokea kweli ya Mungu kwa furaha kubwa wakadumu kwa muda mfupi, mpaka masumbufu na majaribu vilipowakatisha tamaa na kuacha. Aina ya tatu “walisongwa” na “masumbufu ya ulimwengu huu na madanganyo ya utajiri” na “wakashindwa kuzaa matunda.” Wakaukosa wokovu. Waliruhusu mivuto na masumbufu ya ulimwengu huu kuwaharibu.

Aina ya nne waliongoka na “wakazaa matunda, wengine MIA, wengine SITINI, wengine THELATHINI” Kitabu cha Luka huielezea aina ya nne kama wale “ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia (8:15).

Kauli ya Kristo kuhusu “Mia…sitini…thelathini” ni kielelezo wazi juu ya viwango vya malipo vinavyotofautiana watakavyopokea Wakristo katika ufalme wa Mungu, kwa kuzingatia kile wanachofanya katika maisha haya. Cheo, ofisi, daraja ukubwa wa nafasi au kiwango cha utukufu wa kila mmoja utategemea na namna gani anaweka katika matendo kile alicho nacho katika muda wa mwito wake aliotengewa.

Mito ya Maji—na Matunda

Kristo alielezea Roho Mtakatifu kama “mito ya maji ya uzima” (Yohana 7:37-39). Aliwafafanulia wanafunzi wake kwamba atatiririka kutoka ndani yao kama mto. Warumi 5:5 inafafanua kwamba “pendo la Mungu limekwisha kumiminwa” katika moyo wa Mkristo “na Roho Mtakatifu.” Wagalatia 5:22-23 huelezea “matunda ya roho,” ambayo hutiririka kutoka kwa Roho wa Mungu katika moyo ulioongoka. Matunda (matendo mema) siku zote hudhihirika katika maisha ya Mkristo. Kuwa Mkristo, ni lazima udhihirishe matunda katika maisha yako.

Usiku ule wa kusalitiwa kwake, Kristo alifanya Pasaka pamoja na wanafunzi wake. Aliwapa maagizo mengi kuhusu wajibu wao wa siku za usoni kama Wakristo. Yohana 15:1-8, 16 ina fundisho kuu juu ya umuhimu wa kuzaa matunda.

Sura inaanza na Kristo akisema, “Mimi ndimi MZABIBU wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi [Mkristo] ndani yangu lisilozaa MATUNDA huliondoa; na kila tawi LIZAALO MATUNDA hulisafisha, ili lizidi kuzaa” (fu. 1-2). Mara nne tofauti katika kifungu hiki Kristo anawaambia wanafunzi wake “kuzaa matunda mengi” au “zaeni matunda.” Hapa kuna agizo nyeti. Baba (Mkulima au Mtunza mizabibu) huondoa (kupunguza) matawi (Wakristo mmoja mmoja) ambao lazima wawe wameungana (fu. 4) na mzabibu (Kristo). Angalia kwamba wale wasiozaa matunda Mungu “huwaondoa.” Hawa wanapata hasara ya kuukosa wokovu na “wanatupwa…motoni, na…kuteketea” (fu. 6). Wengine watakumbana na ziwa la moto—jehanamu—kwa kutokuzaa chochote katika maisha yao.

SI Matendo “Yetu” au Haki

Ni jambo lenye umuhimu wa juu kuelewa kwamba Wakristo wameunganishwa kwa Kristo. Mara nyingi Biblia huzungumzia “Kristo ndani yetu” (Gal. 2:20; 4:19; Kol. 1:27; Efe. 3:17; 2 Kor. 13:5). Sisi hatutendi matendo badala yake “Kristo ndani yetu,” pamoja na Roho wake akitiririka kutoka kwenye Mzabibu, kama maji yakibeba viini lishe kwa ajili ya kila tawi, ndiye atendaye. Elewa. Baba huongoza mchakato wa kuzaa matunda kadri Mkristo anavyobaki ameunganishwa na yeye kwa njia ya Roho wa Kristo (na Mungu) ndani yake.

Weka jambo hili wazi, Si chochote unachokifanya, wewe kwa nguvu zako, kinachozalisha matendo ya haki. Kumbuka kwamba Warumi 5:5 ilisema pendo la Mungu “limemiminwa mioyoni mwetu na Roho Mtakatifu.” Kila Mkristo anapaswa kudhihirisha “tunda” la upendo lakini hii inawezekana tu kwa Mungu kwanza kutoa Roho wake akibeba uwezekano wa kuzalishwa kwa mojawapo ya matunda ya Roho ndani ya kila mtu.

Warumi 10 inawaonya wale ambao hawaelewi jukumu la Mungu katika kujenga tabia, matendo mema na haki: “Kwa maana, wakiwa hawaijui HAKI ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya HAKI YA MUNGU” (fu. 3) Ni kupoteza nguvu bure kutengeneza tabia yako mwenyewe, matendo yako ya haki. Hayakupi chochote kutoka kwa Mungu!

Mungu anajieleza mwenyewe kama “Mfinyanzi’ afanyavyo kazi na udongo, pale

anapofanya kazi na wanadamu. Anamuunda na kumchonga kila mtu ili kuwa chombo kizuri kilichokamilika. Paulo anawaelezea wale ambao wako “katika Yesu Kristo” kama “kiumbe KIPYA.” Mungu, kama Muumbaji, anafanyiza uumbaji mpya ndani ya wale walio na Roho wake Mtakatifu akitenda kazi ndani yao.

Petro anawaelezea Wakristo kama “washiriki wa asili ya uungu”—asili ya Mungu. Mungu anaunda upya asili ya mwilini ya manadamu iliyopotoka, iwe tabia takatifu ya kiroho, ya ajabu, tukufu na kamilifu.

Ukuaji wote wa kiroho hutoka kwa Mungu!

Waumini wa Korintho waliteseka kwa kuwa na “roho za ufuasi,” baadhi wakipendelea mtumishi mmoja zaidi ya mwingine, na hivyo kuligawa kanisa. Paulo aliwaelimisha: “Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa?” (I Kor. 3:5). Fungu la 6 linaendelea na “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali MWENYE KUKUZA NI MUNGU.” Waumini makanisani walikuwa wanajichagulia watumishi wakati uongezekaji wowote kiroho (Revised Standard Version husema “ukuaji”) hakika ulitoka kwa Roho wa Mungu akiwa kazini (kwa sehemu kupitia watumishi wake). Baada ya kueleza kwamba watumishi wa kibinadamu si kitu, fungu 7 husisitizia kitu hicho hicho.

Fungu la 8 linavutia zaidi. Angalia kile linachofunua: “Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata THAWABU YAKE mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.” Hii inamaanisha kuwa kila mtu anawajibika na atalipwa kwa kazi yake mwenyewe—juhudi yake! Rahisi kabisa—wazi kiasi gani!

Neema hutuweka katika ufalme wa Mungu lakini matendo yetu huamua thawabu yetu tukishakuwa pale.

Paulo anaendelea, “Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu” (fu. 9). Mungu anajenga familia yake. Ni mkulima. Sisi wote ni mazao ya “ukulima” wake.

Kanisa hili, Kanisa Rejeshwa la Mungu, linafanya kazi ya Mungu. “Tunatenda kazi pamoja” ulimwenguni kadri Mungu anavyoita watenda kazi kwenda kuvuna (Math. 9:36-38). Tuna makumi ya vijitabu na rasilimali zingine zenye kweli za Mungu zikisambazwa kwa maelfu. Tunawashauri na kuwabatiza wale wanaotubu na kuongoka. Washiriki wengi na watenda-kazi wenza, zaidi na zaidi wanasaidia kwa njia ya maombi ya kila siku na msaada wa fedha katika kazi hii inayopanuka!

Watumishi wetu wa makao makuu wanasaidia katika juhidi hizi zote, kadri injili ya ufalme wa Mungu inavyoenea ulimwenguni kote. Ni jukumu letu kuwasaidia watu wakue na kushinda ili waje kuwa na kiwango kikubwa cha thawabu wakati Mungu, kwa neema yake atakapowaokoa. Kazi yetu ni kutimiza kile ambacho Paulo anakielezea kwenye fungu la 10: “Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.”

Ni jambo nyeti kuelewa hili. Kumbuka, Mungu anajenga Kanisa lake. Kristo alisema, kwenye Mathayo 16:18, “NITALIJENGA Kanisa langu.” Hii ndiyo maana Paulo aliandika, “ninyi ni JENGO LA MUNGU.” Kila jengo imara lina msingi ulio mathubuti. Na ndivyo lilivyo Kanisa la Mungu. Fungu la 11 husema, “Maana MSINGI mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.”

Kanisa la Mungu linasimama kwenye njia ya uzima na mafundisho ya Yesu Kristo. Luka 4:4 husema Wakristo “huishi…kila neno la Mungu.” Kumbuka vile Kristo alivyoonya namna ambavyo wengi “hamyatendi nisemayo” (Luka 6:46). Kile Kristo asemacho ni maneno yake. Wale wote ambao “hujenga nyumba juu ya mwamba” (Math. 7:24-29) wameelezewa kama wale ambao “huyasikia maneno yangu na KUYAFANYA.”

Kujifunza Biblia na maombi ya dhati ni sehemu ya ratiba ya Mkristo kila siku. Ameipata “lulu ya thamani kuu” na amekusudia kujenga tabia ya kiroho na asili ya Mungu katika maisha yake. Kwa kufanya hivi anajenga moja kwa moja kiwango cha thawabu atakayoifurahia milele yote. Ingawa hakuna chochote kati ya haya kitakachomfikisha pale, uzito wa tabia yake unaamua thawabu yake.

Sasa turudi kwenye 1 Wakorintho 3. Paulo anaitengeneza dhana nyeti ya kujenga juu ya Kristo kwa wazi kabisa akitumia kielelezo ambacho kila mtu atakielewa. Angalia namna anavyoelezea maana ya kufanya hivi” Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata THAWABU” (1 Kor. 3:12-14).

Mafungu haya yanaongelea kile tunachojenga katika maisha yetu. Vitu vitatu vya mwanzo, “dhahabu au fedha au mawe ya thamani,” ni vya thamani kubwa. Vile vile, vinahimili moto ulioelezewa kwenye fungu la 15: “Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.” Moto hauna madhara ya kikemikali kwa metali hizi za thamani au vito. Lakini fungu linaonya juu ya wale ambao wanaweza “kupata hasara” kwa sababu kazi zao zilikuwa “miti au majani au manyasi” kithamani. Moto huteketeza vitu hivi vitatu vya mwisho, ambavyo thamani yake ni ndogo sana. Watu hawa wanaokolewa lakini wanapoteza baadhi ya thawabu.

Vitu vyote sita vinaonyenyesha mfuatano wa kupungua kwa thamani katika ubora. Kwa kweli majani hayana thamani—ni ya hali ya chini kithamani. Manyasi ndio kabisa, hayana thamani yoyote.

Kila Mkristo yapasa afanye uchunguzi kamili wa namna gani anavyojenga!

Moto ni Nini?

Mafungu mawili ya msingi huelezea namna ambavyo Mungu hutumia “moto” kuwasafisha wale ambao ndani yao anajenga tabia yake. Yanaongelea wakati wa Kurudi kwa Kristo, wakati ambao watu wote watajifunza ukweli wa Neno la Mungu. Anasema kwamba atawapitisha “kati ya moto, nami nitawasafisha kama FEDHA isafishwavyo, nami nitawajaribu kama DHAHABU ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu” (Zak. 13:9).

Malaki 3, huelezea kuja kwa Kristo mara ya pili, huongezea maelezo ya Zakaria: “… naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa MOTO wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye FEDHA na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama DHAHABU na FEDHA; nao watamtolea Bwana dhabihu KATIKA HAKI” (fu. 1-3)

Angalia kwamba ni moto wa majaribu (1 Pet. 4:12) unaoleta ubora kamili wa dhahabu na fedha katika tabia ya mtu. Fungu la 2 hapo juu kwa hakika linasema kwamba Kristo mwenyewe ndiye “moto wa mtu asafishaye fedha” na wale wote waliojenga juu ya miti, majani na manyasi watayaona yakiteketea. Ndiyo, baadhi wataingia katika ufalme kwa kunusurika na watapokea thawabu kidogo sana kulingana na kiasi kidogo cha mawe ya thamani au vito walivyomruhusu Mungu kujenga katika tabia zao. Itakuwa ni kwa sababu ya kipawa chake cha neema kwamba wameokoka. Lakini kwa sababu walitenda kidogo, watapokea kiwango kidogo cha thawabu—cheo, ofisi, daraja na utukufu katika serikali ya Mungu itawalayo ulimwengu mzima inayokuja hivi karibuni. Ingawa watakuwepo pale, watapewa mamlaka juu ya majiji machache.

Wengine wataonyesha juhudi na kumtafuta Mungu kwa mioyo yao yote katika maisha haya. Watajitahidi kukua na kushinda mwili na mapungufu, dhambi na udhaifu wake bila kuchoka. Lengo lao kuu ni ufalme wa Mungu (Math. 6:33), na hukaza macho yao pale—na thawabu utakaokuja nayo!

Kristo anawauliza wale wanaojidai kuwa Wakristo, “Kwa nini kuniiita Bwana, Bwana, na HAMFANYI yale nisemayo?” Wale wanaochagua kufanya yale Kristo asemayo ya-

tendwe katika MAISHA HAYA na hatimaye kuzawadiwa sawa sawa na matendo yao katika MAISHA YAJAYO. Hiyo ni ahadi ya hakika ya Mungu katika Maandiko. Hakuna chochote kinachoweza kuitengua!

Thawabu yako katika maisha yajayo itakuwa nini?

Kwa Muhtasari

Katika kijitabu chake Utakuwa Unafanya Nini Katika Maisha Yajayo?, Herbert W. Armstrong alihitimisha kama ifuatavyo chini ya kichwa kidogo “Sehemu Yako Katika KAZI YA MUNGU”:

“Katika miaka yangu zaidi ya hamsini ya uzoefu mwingi wa kila siku, tangu Mungu alipobadilisha mwelekeo WANGU kuingia katika NJIA YAKE, nimeona kwamba hitaji la kwanza kabisa la kila Mkristo, anayetaka KUKUA na kujenga tabia hii ya kiroho, ni kuweka moyo wake wote katika KAZI YA MUNGU, ambayo Kristo aliye hai amewaita watumishi wake kuifanya, kama vitendea kazi vyake! “MATENDO” yetu ni sehemu ya KAZI YA MUNGU—kuifikisha Injili yake ulimwenguni kote kuwa ushuhuda—kuandaa njia kwa marejeo ya Kristo. Sisi ni VITENDEA KAZI Vyake tu. Ni KAZI YA MUNGU! Wale wanaopinga “MATENDO”, wanampinga MUNGU Mkuu aliye MTENDAJI halisi kupitia sisi kama vitendea kazi na Watendakazi-wenza! Hata hivyo, si matendo yetu!

“Wale wanaojiangalia wenyewe, wasiojali chochote kwa ajili ya KAZI YA MUNGU, wasiokuwa na mtazamo mpana wa kutaka kusaidia KUUPELEKA UJUMBE WA KRISTO kwa huu ulimwengu unaoangamia, uliopofushwa, kudanganyika, huanguka. Wale wanaoelekeza maisha ya Kikiristo na shughuli zao zote katika kujijenga wao wenyewe kiroho, ambao miyo yao haiko katika au hawajali KAZI hii kubwa ya MUNGU INAYOKWENDA ulimwenguni kote, ambayo kwa hakika inaoongozwa na KRISTO aliye hai, hujengeka KUELEKEA NDANI tu, mpaka wanyauke kiroho na kuanguka pembeni mwa njia! Wale ambao mioyo yao, MAOMBI yao ya dhati, yasiyokoma na zaka na sadaka zao viko katika KAZI YA MUNGU huendelea KUPANUKA kiroho—huwa wenye FURAHA—WANABARIKIWA sana—maisha yao yananeemeka na kuwa makamilifu—na nyuso zao hujaa tabasamu. WANANG’AA! WANAFANIKIWA!”

“Agano Jipya limejaa maagizo juu ya maisha ya Mkristo kihalisia—kuwa na maisha mapya, tofauti, maangavu, yenye furaha—au, pengine kwa usahihi zaidi, kumruhusu Yesu Kristo kuishi aina hii ya maisha—NJIA YA MUNGU ndani yao!

“Njia ya Mungu ni ya AJABU namna gani!

“WOKOVU huja—kama tunataka—ukiwa ni KIPAWA cha Mungu—kwa NEEMA!

“Lakini ni lazima tubadilike. Kuna KUTENDA, si kusikia tu (Rum. 2:13). Kuna kujengeka kwa TABIA mpya ya haki. Bado, hata hiyo ni KRISTO NDANI YENU akitenda! Ama kwa hakika hata “matendo” kimsingi yanafanywa na yeye! Lakini ni AJABU namna gani kwamba kuna “MATENDO” ya haki katika maisha ya Mkristo wa kweli—fursa ya kupata zaidi ya wokovu, japo huo hauna kipimo—fursa kwa cheo cha juu, daraja, fursa ya KUTUMIKIA, UTUKUFU wa juu!”

Pengine ungependa kusoma: