JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.
Hifadhi ili kusoma baadaye
Inapatikana katika lugha hizi:
Liko Wapi Kanisa la Mungu Leo hii?
Photo of a CongregationNew York, Marekani Photo of a CongregationJamaika Photo of a CongregationPeru Photo of a CongregationIdaho, Marekani Photo of a CongregationIndia Photo of a CongregationUbelgiji Photo of a CongregationKenya Photo of a CongregationArkansas, Marekani Photo of a CongregationAfrika Kusini Photo of a CongregationUingereza Photo of a CongregationNigeria Photo of a CongregationOhio, Marekani

Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu.” Kuna shirika moja linalofundisha ukweli wote wa Biblia, na limeitwa kuishi kwa “kila neno la Mungu.” Je, unajua namna ya kulipata? Kristo alisema lita:

  • Fundisha “yote” Aliyoagiza
  • Kuwa na washiriki walioitwa na kuwekwa wakfu kwa ile kweli
  • Kuwa “kundi dogo”
Habari za Mwandishi
Photo of David C. PackDavid C. Pack 

Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Mhariri-Mkuu wa Jarida la Ukweli Halisi, na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, Daudi C. Pack amewafikia mamilioni wengi ulimwenguni na kweli za Biblia zilizo na nguvu sana—zisizojulikana karibu kwa wote. Ameandika vitabu na vijitabu 80, mwenyewe ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, na alionekana kama mgeni kwenye Kituo cha Historia (The History Channel). Bwana Pack alihudhuria Chuo cha Mabalozi huko Pasedena, Kalifonia, aliingia katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu Mzima mwaka 1971, na yeye binafsi alifundishwa na mwanzilishi wake, Herbert W. Armstrong.

Jinsi Dini Inavyokudanganya Kuhusu Mustakabali Wako wa Kustaajabisha

na David C. Pack

Ukweli wa injili—kusudi la Mungu la kustaajabisha kwa ajili ya mwanadamu—umefichwa. Hufafanua kwa nini ulizaliwa. Ni maarifa ya kushangaza! Yatakuacha umepigwa bumbuazi. Maarifa haya ya ajabu yamefunuliwa sasa—sambamba na njama ya kuyazuia!

Mabilioni hivi sasa wamedanganywa. Mabilioni huko nyuma vivyo hivyo. Hata wewe umedanganywa. Upotoshaji kamili umetokea, na dini zote ulimwenguni zimeshiriki. Maarifa juu ya uwezekano wako wa kustaajabisha—mustakabali wako wa ajabu—yamefichwa kutoka machoni pako!

Wengi hushangaa na kuwa na wasiwasi kuhusu yasiyojulikana—na nini kitakuwa mustakabali wao. Wengine wana hofu kwamba hata hawana mustakabali. Bado wengine wana hofu kwamba ustaarabu hauna mustakabali. Huhitaji kuwa na shaka kuhusu mustakabali wako tena—au wa ubinadamu.

Laiti kama ubinadamu ungejua kile ambacho Mungu ameuandalia! Ila uzuiaji wa makusudi wa ukweli umeficha maarifa haya kutoka machoni pa wote isipokuwa kwa wachache. Unaweza kuwa wa kipekee. Unaweza kuwa miongoni mwa wachache ambao hawajadanganywa!

Ulimwengu umeamini injili ya uongo kwa miaka 2,000. Kwa ujumla umechukulia kwamba Yesu Kristo ndiye injili badala ya Mjumbe wake. Ujumbe—kiini—cha injili siyo Kristo. Kwa kusisitiza [kufokasi] juu Yake—Mjumbe—wadanganyifu wa kidini wamefaulu kuuzuia na kuufunika Ujumbe Aliouleta!

Maarifa muhimu ya namna ambavyo mwanadamu angeweza kutatua matatizo yake na kuufahamu Mpango Mkuu wa Mungu yamefichwa kutoka kwa ulimwengu, yakiuacha gizani. Mwanadamu hajui yeye ni nini au sababu ya kuwepo kwake. Hajui njia ya kuleta mafanikio tele, amani na mambo yote mema ya maisha. Injili ingekuwa imemwonyesha mwanadamu suluhisho la matatizo yake yasiyotatulika.

Na bado, ukiacha mtume Yohana, mitume wengine wote wa awali waliuawa kwa ajili ya kufundisha ukweli wa kusudi la Mungu la kustaajabisha. Yesu alisulubishwa kwa sababu watu hawakutaka kusikia Ujumbe Wake!

Ufahamu sahihi wa injili ya kweli hufunua maarifa ya muhimu sana. Hujumuisha upana wa uelewa ambao hauwezi kugunduliwa kwa majaribio ya kisayansi. Dini za ulimwengu huu zimeuzuia. Wanateolojia wake hawaelewi wala hawako tayari kuyafundisha. Tutaona ya kwamba wamezuilia ufunguo mkuu unaofungua kusudi la kuwepo kwako—MUSTAKABALI WAKO WA KUSTAAJABISHA!

Namna gani hii ilitokea? Na ni nani aliye nyuma ya uzuiaji huu wa maarifa?

Mdanganyifu Mkuu

Kwa wasioelewa, Biblia ni kitabu chenye kauli za kushtua. Hufunua ukweli wa kushtusha, usioeleweka kabisa hata kwa wale wanaodai kuifahamu. Lakini kuna kauli chache zinazoduwaza zaidi ya ile inayopatikana katika Ufunuo 12:9. Fungu hili husema moja kwa moja kwamba mwovu Shetani—ambaye yuko—“audanganyaye ulimwengu WOTE.”

Akiwa “mfalme wa UWEZO wa anga” (Efe. 2:2), Shetani ameshawishi, kaongoza, katawala na kawadanganya kabisa makutano wasiotilia shaka.

Kwa hakika huu ni ufunuo wenye kuduwaza—kiasi kwamba wengi kirahisi tu huupuuzia au kuukataa, wakiamini kwamba haiwezekani kuwa kweli. Lakini fungu hili liko ndani ya Biblia yako. Na ulimwengu mzima unabaki umedanganyika kuhusu ukweli kwamba umedanganywa!

Chimbuko la Ibilisi

Tuangazie historia kidogo sasa. Shetani alitoka wapi? Namna gani alikuja kuwa vile alivyo?

Mwanzoni Mungu aliumba malaika wakuu watatu Lusifa (aliyegeuka kuwa Shetani), Mikaeli na Gabrieli. Kila mmoja alitawala theluthi ya mamia ya mamilioni ya malaika (Ufu. 5:11). Lusifa na theluthi yake walitawala ulimwengu uliokuwa kabla ya Adamu. Pamoja na malaika zake waliasi serikali ya Mungu. Aya nyingi sana hufafanua hili.

Hebu tusome juu ya Lusifa baada ya kuwa Shetani. Isaya 14:12-15 husimulia kisa cha kushangaza. Ina viashiria vingi kuhusu mahali ambapo Lusifa alishawahi kuwa, alichokifanya na kilichomtokea. Soma kwa uangalifu, ukiangalia msisitizo kwenye semi za msingi: “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe Lusifa, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu [“kaburi”—ona fungu la 9 na 11]; Mpaka pande za mwisho za shimo.” (Jifunze mengi zaidi kwa kusoma kijitabu chetu Shetani ni Nani?)

Tangu kuasi kwake kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu, kwa kiwango kikubwa Shetani “ameyaangusha mataifa” katika ufahamu na maarifa ya muhimu sana yanayofafanua kusudi la Mungu. Udanganyifu wake umekuwa kamili.

Mungu wa Ulimwengu Huu

Biblia pia inamwita ibilisi “mungu wa ulimwengu huu”—ufunuo mwingine wa kushtusha! Hiki ndicho 2 Wakorintho 4:4 inasema: “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili…”

Shetani huupofusha ulimwengu usiione injili ya kweli kwa sababu binafsi. Injili inauelezea ufalme wa Mungu unaokuja hivi karibuni—Serikali ya Mungu itawalayo ulimwengu mzima. Bila shaka, Shetani anatafuta kuwazuia watu wasiuelewe ukweli huu wa ajabu, akiwa hataki “nuru” iangazie kusudi la Mungu la kustaajabisha kwa ajili ya mwandamu. Anataka ubinadamu, kwa pamoja na kila mmoja mmoja, ufikiri kwamba hauna mustakabali! Kwa hakika, ibilisi anatambua kwamba kuwasili kwa ufalme wa Mungu inamaanisha yeye atafukuzwa kutoka kwenye nafasi yake ya sasa (Ufu. 20:2-3) ya kuushawishi ulimwengu mzima akiwa mungu ambaye ubinadamu huabudu bila kukusudia. Hataruhusiwa tena kuyadanganya ama kuyadhoofisha mataifa. Pia anatambua kwamba kamwe hawezi kupata kile ambacho Mungu amewaahidia watu.

Katika Yohana 12:31, 14:30 na 16:11, Kristo alimrejelea Shetani kama “mkuu wa ulimwengu huu.” Mafungu haya yanasema kuwa siku moja ibilisi atahukumiwa. Yohana 12:31 huziweka sambamba hukumu ya ulimwengu huu na hukumu ya Shetani. Kwa nini? Kwa sababu ulimwengu huu ni wake! Kauli ya Paulo iliyovuviwa hufunua kwa hakika kwamba yeye ni “mungu” wake halisi.

Huu ni ukweli dhahiri kutoka ndani ya Biblia yako! Ustaarabu wa mwanadamu pamoja na tamaduni zake, njia na mifumo, viko chini ya uongozi wa ibilisi!

Fikiria. Ikiwa Shetani ameudanganya ulimwengu wote, basi huu hauwezi kuwa ulimwengu wa Mungu. (Pia angalia 1 Yohana 5:19) Na kwa kuwa ulimwengu wote umedanganywa, umekatwa kutoka kwa Mungu. Watu waliodanganyika hawajui kusudi la kuwepo kwao, na wanaendesha maisha yanayoakisi ujinga huu (Isa. 59:1-2; Yer. 5:25).

Tunaweza kuuliza: Jinsi gani kiumbe mmoja anaweza kudanganya zaidi ya watu bilioni sita? Ziko njia mbili za msingi.

Kwanza, Ufunuo 12:9 inahitimisha na, “akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Angalia inasema kwamba, “malaika zake.” Viumbe hawa, anaowaongoza, wanajulikana kama pepo wabaya (au malaika walioanguka), na wanamsaidia Shetani katika jukumu lake kama mdanganyifu mkuu. Kwa hiyo, Shetani hafanyi kazi peke yake—ana mamilioni ya viumbe roho waliodanganyika wanaomsaidia.

Lakini kuna mengi zaidi ya kuelewa. Iko njia ya pili, iliyo na umuhimu sawa ambayo kwayo Shetani amefaulu sana kuwadanganya watu wengi hivyo—na kuficha uwezekano wao wa ajabu kutoka machoni pao.

Shetani Ana Watumishi

Jamii ya Kikristo inawakilishwa na mamia ya madhehebu na vikundi tofauti vinavyoshindana na kupingana. Kinachodhaniwa kuwa Ukristo huonekana katika kila mwonekano wa kufikirika wa “sura, ladha, rangi na umbile asili” vya imani na tamaduni. Wengi wamedhania kuwa hii ndiyo hali halisi ya mambo katika ulimwengu wa “Kikristo”—kwamba hii ndiyo njia ambayo Mungu ameitaka.

Jinsi gani wamekosea!

Weka namna nyingine, hii inamaanisha kwamba wako mamia ya maelfu, na pengine mamilioni, ya waalimu wa dini wanaowakilisha na kufundisha imani za aina hizi za Ukristo zinazotofautiana na zisizokubaliana. Wengi wanaohudhuria makanisa haya tofauti tofauti wamedhania kwamba hawa wote kwa ujumla lazima wawe ni watumishi wa Mungu—kwamba wanawakilisha na kufundisha kile ambacho Mungu anataka kifundishwe. Hakuna hatari zaidi ya hii—au MAKOSA ya dhahiri—udhanifu!

Sasa hapa bado kuna kauli moja zaidi ya kushtusha!

Akiwa ndiye mungu wa ulimwengu uliodanganyika kabisa, ambao ni lazima ujumuishe aina zote za Ukristo zinazotofautiana na dini zingine, Shetani anao mawakala wake mwenyewe. Anawatumia mawakala hawa kueneza mafundisho yake ya uongo bila kujulikana. Ndiyo, ameweza kupata mafanikio haya makubwa kwa sababu anao WATUMISHI WAKE MWENYEWE! Bila shaka, mawakala wake—watumishi wake—wao wenyewe wamedanganyika wakiamini kwamba ni watumishi wa Mungu. Baadhi hufundisha vipengele vichache vya ukweli wa Mungu, lakini kwa hakika hakuna chochote cha kweli Zake muhimu zaidi!

Sasa angalia 2 Wakorintho 11:13-15. Mtume Paulo alionya dhidi ya werevu ambao watumishi wa Shetani huutumia kudanganya kwa mafanikio: “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.”

Hili ni andiko la wazi, linaloshtua sana. Bado, ni kweli kwamba watumishi wa Shetani huonekana kuwa watumishi wa Mungu. Elewa hili! Shetani haneni moja kwa moja na wanadamu. Hutenda kazi kupitia watumwa wake—watumishi wake!

Na huu hapa ndio uongo mkuu wa watumishi hawa wa uongo: Ibilisi anawatumia kama vyombo vyake kwa ajili ya kueneza injili ya uongo kuhusu Nafsi ya Yesu Kristo—badala ya Ujumbe Wake wa ufalme wa Mungu, ule ambao Kristo aliuleta. Ukweli mkuu ambao watumishi, wanateolojia na wanadini wa ulimwengu huu huukataa ndio uwezekano wa kustaajabisha ambao kila mwanadamu anao.

Mafungu yafuatayo yanaendeleza maelezo ya Paulo kuhusu kazi za watumishi wa uongo. Yanaonyesha hatari inayoendelea ya mawakala wa Shetani wakitafuta kujipenyeza ndani ya Kanisa la kweli kuwapofusha watumishi wa kweli wa Mungu mara ya pili wasiuelewe ukweli wa ajabu wa injili ili wawarudishe gizani. Angalia: “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikra zenu [ndugu wa Korintho], mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye [akiongelea wahubiri wa uongo] akihubiri Yesu mwingine… au mkipokea roho nyingine… au injili nyingine msiyoikubali…” (11:3-4).

Paulo alionya dhidi ya roho “nyingine” ambayo hata iliweza kuingia katika Kanisa la kweli. Roho hii hii nyingine ilipotosha ukweli kuhusu injili na Kristo halisi wa Biblia. Kihistoria, Ukristo bandia wa leo ulionekana mara ya kwanza mara tu baada ya kufa na kufufuka kwa Kristo.

Pia, jiulize mwenyewe: Kama Kristo ni injili, basi kwa nini kunukuu “Yesu mwingine” na “injili nyingine” kama makosa mawili tofauti ya mafundisho?

Tutarudi kwa hili.

Maonyo ya Agano Jipya

Agano Jipya lina maonyo mengi dhidi ya walaghai, wadanganyifu na matapeli ambao wangejaribu kuingia katika Kanisa la kweli wajipatie wafuasi na kuwaongoza katika mafundisho ya uongo. Wengi miongoni mwa mitume, kwa namna moja au nyingine, kwa hakika walilionya kila kusanyiko dhidi ya hatari hii. Ni mfumo huu huu wa Ukristo wa uongo ambamo watu wengi wamezaliwa na kutumikia maisha yao ndani yake.

Mtume Petro alionya dhidi ya waalimu wa uongo “miongoni mwenu (Kanisa).”

Angalia: “Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako WAALIMU WA UONGO, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na WENGI watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa” (2 Pet. 2:1-3).

Haya ni maneno makali. Kama vile manabii wa uongo walivyosumbua Israeli ya zamani, vivyo hivyo Kanisa limeshambuliwa na “waalimu wa uongo” katika karne zote ambao, kwa “maneno yaliyotungwa,” waliwashawishi “wengi” wawafuate. Lengo lilikuwa ni kuwavuta watu watoke kwenye “njia ya UKWELI.”

Mtume Yuda, ndugu mdogo wa Kristo, yeye naye alitoa onyo lake moja kwa moja: “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu…ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu WALIOJIINGIZA kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi [leseni ya kuvunja Amri za Mungu]…” (fu. 3-4).

Shtaka hili rasmi lililoandikwa kwa uzito huwaelezea wale ambao “walijiingiza” na kuwasababisha baadhi kutoipigania “imani ambayo ilikabidhiwa mara moja tu.” Angalia inasema kwamba baadhi ya hawa wazushi walikuwa “wameandikiwa tangu zamani.” Kwa sababu walikuwa makafiri, waliwafundisha wengine wavunje amri za Mungu pia. Tutachunguza Matendo 8 hivi punde ili kuelewa vizuri watu hawa walitoka wapi. Mfumo na mafundisho yao si mapya kabisa.

Yohana alirekodi karibu sura nzima ya maneno ya onyo la Kristo mwenyewe. Kristo habakizi kitu chochote anapoelezea asili ya kweli ya viongozi na waalimu wa uongo. Hizi hapa ni dondoo kutoka sura hiyo: “Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo [Kanisa]… huyo ni MWIVI naye ni MNYANG'ANYI…mchungaji wa kondoo [Kristo na watumishi wake waaminifu]... kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. MGENI hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za WAGENI…Basi Yesu aliwaambia tena…Mimi ndimi mlango wa kondoo. Wote walionitangulia ni WEVI na WANYANG'ANYI; lakini kondoo hawakuwasikia. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. MWIVI haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa MSHAHARA…humwona MBWA-MWITU...na kukimbia; na MBWA-MWITU huwakamata na kuwatawanya. YULE hukimbia kwa kuwa ni mtu wa MSHAHARA; wala mambo ya kondoo si kitu kwake” (10:1-13).

Tumia muda kuisoma sura hii yote. Angalia kujirudiarudia kwa maneno “mbwa-mwitu”, “mgeni”, “mwivi”, “mnyang’anyi” na “mtu wa mshahara”—hawa wa mwisho ni wale ambao huliacha kundi, wakitafuta matakwa binafsi. Katika historia yote ya Kanisa, wakati maadui walipowatishia watu wa Mungu, watumishi wengi walilitelekeza kundi, na kondoo wengi walidanganywa na kufagiliwa mbali kutoka Kanisa la Mungu na ukweli.

Pamoja na Wakorintho, Paulo pia aliyaonya makusanyiko mengine. Hiki hapa ndicho alichowaambia Wagalatia walipokuwa wametumbukia kwenye mafudisho ya uongo: “Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii KWELI? Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. Chachu kidogo huchachua donge zima” (5:7-9).

Wagalatia walikuwa wameiacha njia. Hawakuelewa kwamba mafundisho kidogo ya uongo (“chachu”) hatimaye huenea (kama chachu kwenye unga uliokandwa) kwenye “donge zima” la kweli nyingi za Mungu. Tutakuja kuona kwamba Wagalatia hawa walikuwa wanapoteza uelewa wao wa injili.

Siri ya Kuasi

Sasa geukia onyo alilolitoa Paulo kwa Wathesalonike, ambamo aliongelea juu ya “siri ya kuasi” iliyokuwa tayari inatenda kazi katika Kanisa la karne ya kwanza. Muktadha wa pale (fu. 3) pia una maelezo ya matukio ambayo hutangulia muda mfupi kabla ya Kurudi kwa Kristo. “Ukengeufu” na kufunuliwa kwa “mtu wa kuasi…mwana wa uharibifu” vitatokea kwanza kabla ya Kuja kwa Kristo Mara ya Pili. Aliandika, “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi” (2 Thes. 2:7). Paulo alielewa kwamba matukio fulani yalikuwa “tayari” yanatokea Kanisani wakati huo, vile vile kama ambavyo yatakuja kutokea, mara nyingine tena, mwishoni mwa zama.

Kitabu cha Matendo huelezea matukio katika Samaria na hutoa mambo ya muhimu yanayopaswa kufikiriwa: “Siku zile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume… Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria… Ikawa furaha kubwa katika mji ule” (8:1, 4-5, 8).

Wakati ukweli dhahiri wa Neno la Mungu unapohubiriwa kwa wale ambao akili zao zimefunguliwa, hakika huleta “furaha kubwa” (8:1, 4-5, 8).

Baadaye, mafungu kadhaa humrejelea mtu mmoja aitwaye Simoni Mchawi—ambaye mara nyingi huitwa Simoni Magusi na wanahistoria mbalimbali wa kanisa. Mtu huyu alikuwa na mvuto mkubwa katika eneo la Samaria ambalo wakazi wake wengi walikuwa watu wa Mataifa. Alikuwa sehemu ya mfumo wa siri ambao Paulo aliwaonya Wathesalonike dhidi yake (ona pia Ufu. 17:5, kisha baadaye kwenye kijitabu hiki). Mfumo huu huu wenye nguvu, ambao hapo awali uliongozwa na Simoni, umeendelea kutafuta kuingia ndani ya Kanisa la kweli.

Sasa angalia: “Na mtu mmoja, jina lake SIMONI, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa: Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake” (fu. 9-11).

Biblia hufafanua ni “neno” gani ambalo Filipo alikuwa anahubiri: “Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za UFALME WA MUNGU, na jina lake YESU KRISTO, wakabatizwa, wanaume na wanawake” (fu. 12). Angalia kwamba hawa watu wa Samaria walibatizwa tu pale “walipoamini” ujumbe huu—ufalme wa Mungu—si fikira zingine. Bila shaka, pia walipaswa kuelewa jukumu la Kristo kama Mwokozi.

Hiki hapa ndicho Paulo alichowaandikia Waefeso. Ujumbe huu huelezea ofisi mbalimbali ambazo Kristo alizianzisha ndani ya huduma Yake ya Agano Jipya. Hufafanua makusudi ya ofisi hizo katika kuwajenga, kuwaunganisha na kuwakamilisha ndugu wa Kanisa la Mungu. Angalia: “Naye alitoa wengine kuwa MITUME, na wengine kuwa MANABII; na wengine kuwa WAINJILISTI na wengine kuwa WACHUNGAJI na WAALIMU; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike KWELI katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo” (4:11-15).

Huu ni mfululizo mwingine wa maonyo makali yenye kuwaelekeza watu wa Mungu. Kristo alikusudia kwamba kondoo Wake wawasikilize watumishi wa kweli na wagundue “upepo wa elimu” ya uongo ambayo inaweza kuja ikiwa imefungwa katika njia za “ujanja” na “hila.”

Karibu na mwisho wa huduma ya Paulo, muda mfupi kabla hajaenda kushitakiwa kwa ajili ya maisha yake, alikutana na wazee wote waliokuwa wamekusanyika huko Efeso. Ulikuwa ni mkutano wenye hisia [mhemuko] kali, kwa sababu alijua kuwa asingewaona tena. Alitumia muda kuwakumbusha wajibu wao na kile ambacho alikuwa amewaagiza mara kwa mara kwa kipindi zaidi ya miaka mitatu! Wajibu ambao Paulo aliuelezea unabaki kuwa jukumu la watumishi wa kweli wa Mungu leo.

Kwa uangalifu angalia jinsi Paulo alivyosisitizia umuhimu wa kwamba alikuwa amehubiri ufalme wa Mungu: “Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria UFALME WA MUNGU… hamtaniona uso tena. Jitunzeni… na lile kundi lote…kulilisha kanisa lake Mungu…Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu MBWA-MWITU WAKALI wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Kwa hiyo KESHENI, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi” (Matendo 20:25, 28-31).

Kile ambacho Paulo alionya dhidi yake kilitokea. Wazushi waliingia si tu katika kusanyiko la Efeso lakini katika maeneo mengine mengi ya Kanisa la Mungu na kuwachochea wafuate uelewa na vitendo vya udanganyifu. Wanahistoria wa Kanisa kwa pamoja hurejelea kipindi kuanzia katikati ya karne ya kwanza BK hadi katikati ya karne ya pili BK kama “karne iliyopotea.”

Katika kipindi hiki, Kanisa lenye kuonekana lilibadilisha mwonekano wake kabisa, likawa vigumu kutambulika. Waumini wa kweli, waliokuwa miongoni mwa wachache wa hali ya chini, walilazimika kukimbia na kuwaacha wengi waliokuwa wanaonekana, waliokuwa wamegeukia makosa. Maarifa juu ya kusudi la Mungu la ajabu kwa ajili ya uwepo wa mwanadamu yakapotea miongoni mwa walio wengi ambao walifagiliwa mbali kwenye wokovu wa uongo.

Tangu hapo karne ya kwanza, wakati Kristo alipoanzisha Kanisa Lake, lililazimika kuupigania ukweli. Watu wa Mungu walipaswa kuwa waangalifu wakati wote—wenye kujihadhari sana—kuhusu hatari ya watumishi wa uongo wakijipenyeza miongoni mwao na kupotosha baadhi au mafundisho yote ya Mungu. Na hawa walaghai wakati wote huhubiri injili ya uongo. Kumbuka, Paulo aliwaonya Wakorintho kwamba walikuwa “wamedanganywa” kwa kukubali “injili nyingine” (2 Kor. 11:4). (Kitabu chetu Liko Wapi Kanisa la Kweli? – na Historia Yake ya Ajabu! huchambua somo hili la kusisimua kwa undani.)

Injili—Moja ya Kweli, Nyingi za Uongo

Fundisho moja kuu kabisa katika Biblia ni maarifa ya injili ya kweli. Elewa. Iko injili moja tu iliyo sahihi. Zingine zote ni upotoshaji, uliobuniwa na Shetani kuubadili ukweli wa Ujumbe wake wa ajabu. Ni ufahamu huu wa muhimu sana ambao mara nyingi watumishi wa Shetani huonekana kuupotosha kwanza.

Pale mwanzoni kabisa mwa huduma Yake, Kristo alifundisha, “Tubuni na kuiamini INJILI” (Marko 1:15). Lakini injili ya kweli ni nini? Je ziko zaidi ya moja ambazo Mungu anaziridhia? Majibu kwa hili na maswali mengine yanapatikana ndani ya Biblia—na kwa hakika ni MUHIMU kwako kuyaelewa. Lakini majibu yamebaki mafichoni kwa walio wengi sana.

Maelfu ya vitabu vipya vya kidini huchapishwa kila mwaka nchini Marekani! Vile vile kuna madhehebu na vikundi tofauti zaidi ya elfu mbili nchini Marekani! Ila, mkanganyiko na kutokukubaliana kuhusu majibu kwa maswali makuu ya maisha miongoni mwa wanaodai kuwa Wakristo, au katika ulimwengu mzima, umeongezeka zaidi kuliko wakati wowote. KWA NINI? Kwa nini yako maarifa mengi, na kwa wakati huo huo kuna ujinga mwingi juu ya ukweli kuhusu maswali MAKUU ya maisha? Majibu kwa maswali haya yanahusiana moja kwa moja na INJILI!

Walio wengi sana wamefundishwa—na wanaamini—kwamba injili ni kuhusu Nafsi ya Yesu Kristo. Hakika, jukumu la Kristo ni somo la muhimu mno, lakini Yeye si injili. Biblia huonyesha kwamba Kristo huhubiriwa sambamba na injili. Kwa mara nyingine, jukumu Lake ni la muhimu sana kwa Ukristo na ni lazima lieleweke, lakini Yeye si injili!

Baadhi hutangaza “injili ya wokovu” au “injili ya neema.” Wengine huamini “injili ya miujiza” au “injili ya ujamaa” au “injili ya vyakula” au “uponyaji” au “imani.” Bado wengine tu hufikiria “muziki wa injili” wanaposikia neno hili. Haya yote ni mawazo ya kibinadamu ambayo hupuuza ukweli wa Biblia!

Hebu turudi kwenye Marko 1, na tuangalie fungu la 14: “Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya UFALME WA MUNGU.” [injili ya ufalme wa Mungu] Hii ndiyo injili aliyohubiri Yesu. Na ni katika muktadha huo huo alisema, “Tubuni, na KUIAMINI INJILI.” Lakini, injili gani? Injili ya “ufalme wa Mungu.” Fungu la kwanza hurejelea ujumbe huu linaposema, “Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Injili ya Kristo ilikuwa juu ya UFALME WA MUNGU—si kitu kingine! Mtu awaye yote hana budi kuiamini injili hiyo, si bandia au mbadala. Ulimwengu kwa-njia-rahisi hauijui injili hii!

Wachache wanatambua. Lakini kwa nini? Kwa nini ni wachache sana leo-hii wanaoelewa vizuri mustakabali wa kustaajabisha wa mwito wa Kikristo? Paulo alivuviwa kufafanua: “Lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu” (1 Kor. 2:9-10). Pasipo Mungu kuifungua akili, haiwezekani kuelewa mambo ya Mungu. Vile vile haiwezekani hata kuja kwa Mungu (Yohana 6:44, 65). Kwa hakika, fungu hili linasema kwamba kusudi la Mungu halijawahi kuingia katika fikra za mwanadamu!

Mungu, kwa kusudi Lake la ajabu sana, amefunua ukweli wa injili kwa wachache sana kwa wakati huu—na amewaweka ndani ya Kanisa Lake. Walimwengu waliosalia wamepofushwa. Elewa hili! Ibilisi hataki wanadamu wafurahie kile ambacho yeye amenyimwa milele—uanakaya [kuwa memba] katika Familia ya Mungu.

Wengi hawataamka dhidi ya udanganyifu—madanganyo kwa halaiki—wa “Ukristo” uliopotoshwa unaokataa kweli dhahiri za Mungu! Mpango wa Mungu kwa ajili ya wanadamu unaduwaza­­—usioweza kulinganishwa na chochote ambacho mwanadamu amekiunda kichukue mahali pake. Ulimwengu unapuuza maandiko yaliyo wazi, na dhahiri yapatikanayo kote katika Neno la Mungu kuhusu ufalme wa Mungu. Kijitabu hiki kinafafanua ukweli wa kustaajabisha ambao wengi huupuuza—na kinafunua kile ambacho chaweza kuwa mustakabali wako!

Onyo Kali Kutoipotosha

Somo hii ni muhimu mno kiasi kwamba Mungu alimvuvia mtume Paulo kutoa onyo hili kwa Wagalatia kipindi kile na kwetu sasa: “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kugeukia INJILI YA NAMNA NYINGINE. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini, ijapokuwa sisi au malaika kutoka mbinguni atawahubiri NINYI INJILI YOYOTE isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe” (1:6-9).

Hii ni kauli nzito! Baadaye kidogo, Paulo alisisitizia tumaini lake kwamba “kweli ya INJILI ikae pamoja nanyi” (2:5). Kwa hiyo iko injili moja ya kweli—na zingine zote za uongo.

Sasa unaweza kuelewa vyema onyo la Paulo katika Wagalatia 5:7-9, lililorejelewa hapo awali.

Ingawa baadhi hudai kuwa Paulo alifundisha injili tofauti au injili ya nyongeza, ni wazi kwamba hakufanya hivyo. Kinyume na hilo, Mungu alimtumia Paulo kuonya dhidi ya kuruhusu fundisho la uongo kama hilo kwa kutangaza laana kwa mtu awaye yote, malaika au hata mtume yeyote—“Lakini, ijapokuwa sisi [mitume]… atawahubiri ninyi injili nyingine yoyote…na alaaniwe”—anayechagua kukiuka amri hii (1:8).

Andiko zito kiasi gani—na ONYO!

Paulo alieleza kwamba mitume waliaminiwa na Mungu kuhifadhi injili ya kweli. Angalia 1 Wathesalonike 2:4: “Bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.” Huo ni wajibu usioweza kuchukuliwa kirahisi. Watumishi wa kweli daima watafundisha kile ambacho Mungu ameamuru, si kile kinachowafurahisha wanadamu (ikiwa ni pamoja na “wasomi” wa Biblia). Hivyo, dai lolote kwamba Paulo alifundisha injili tofauti au ya pili (inayodhaniwa kuwa ni juu ya Kristo au ya “amani”) haiwezekani. Kwa hakika angekuwa anatangaza laana juu yake yeye mwenyewe!

Yesu Alitabiriwa Kuleta Injili

Yesu alikuja kama mtangazaji akibeba tangazo. Kila mahali alikokwenda Alitoa tangazo hilo hilo kuhusu kuja kwa SERIKALI BORA itawalayo-ulimwengu itakayosimamishwa wakati wa Kurudi Kwake.

Alipokuwa akizungumza na kundi la wasikilizaji jangwani, Kristo alifafanua kusudi Lake—wajibu Wake. Angalia jinsi Alivyofafanua utume Wake: “Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya UFALME WA MUNGU katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa” (Luke 4:43).

Mathayo anaangazia zaidi suala hili: “Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri HABARI NJEMA YA UFALME, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu” (Math. 4:23). Kazi ya Kristo ilikuwa ni kupeleka ujumbe wa ufalme wa Mungu katika miji yote ya Israeli. “Alitumwa” kwa kusudi hili.

Katika Agano la Kale, Yesu alitabiriwa kuwa angekuja kama MJUMBE. Angalia Malaki 3:1: “Angalieni, namtuma mjumbe wangu [Yohana Mbatizaji], naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana, mnayemtafuta, atalijilia hekalu lake ghafla; naam, yule MJUMBE [Kristo] wa agano, mnayemfurahia.” Kristo alikuwa “MJUMBE”, si ujumbe wenyewe. Ujumbe Wake kuhusu ufalme wa Mungu ndiyo kiini hasa—KITOVU!—cha Biblia nzima.

Sasa linganisha aya katika Malaki na nyingine: “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana [maandiko ya Agano la Kale pekee ndiyo yaliyohubiriwa kabla ya Yohana Mbatizaji]; tangu wakati huo habari njema ya UFALME WA MUNGU hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu” (Luka 16:16). Kumbuka kwamba, katika Marko, Kristo alihubiri “ufalme wa Mungu” na akauita injili.

Shetani, aliyejua kwamba Kristo alitabiriwa kuhubiri Ujumbe ambao anauchukia, kupitia Mfalme Herode, alitafuta kumuua akiwa angali mtoto mchanga. Hii pia ndiyo sababu ibilisi alitafuta kumjaribu kule nyikani (Math. 4:1-11). Alijua kuwa kama angefaulu katika jaribu moja wapo, basi angevuruga Mpango wa Mungu na kubaki na mamlaka juu ya mataifa ya ulimwengu.

Maana ya “Injili”

Neno “injili” ni neno la Kiingereza cha zamani “god spell” lenye maana ya habari njema. Neno “ufalme” pia ni neno la Kiingereza cha zamani, lenye maana rahisi ya serikali. Tunaweza kusema kwa usahihi kwamba Kristo alihubiri “habari njema ya serikali ya Mungu.” Tutajifunza juu ya nani, nini, wapi, lini, kwa nini na jinsi gani HABARI NJEMA hii inahusiana na unabii mkuu wa Biblia.

Neno injili linapatikana mara 101 katika Biblia. Wakati mwingine linapatikana peke yake, na wakati mwingine “ya ufalme” hulifuatia. Wakati mwingine hujumuisha “ya ufalme wa Mungu” au usemi unaolingana na huo “ya ufalme wa mbinguni.”

Angalia kwamba inasema, “wa mbinguni,” siyo “huko mbinguni.” Ni ufalme wa mbinguni na kuna tofauti kubwa. Kama ilivyo kwa ufalme wa Mungu, si ufalme katika Mungu, vivyo hivyo ni kweli kuhusu ufalme wa mbinguni au ufalme wa mbingu. Hili ni jambo muhimu kulielewa.

Kote katika Agano Jipya, neno “ufalme” hupatikana mara 27, “ufalme wa Mungu” mara 75 na “ufalme wa mbinguni” mara 34. Yote haya yako wazi na ni kitu kimoja na yanafanana.

Sasa elewa pointi hii. Somo la ufalme wa Mungu si tu ndiyo mada kuu katika Agano Jipya, lakini pia ndiyo mada kuu katika Biblia NZIMA. Lakini, ajabu ni kwamba, wengi wanaelewa kidogo au hawajui kabisa habari zake. Watumishi wa makanisa ya ulimwengu huu hawaijui injili ya kweli na kamwe hawahubiri juu yake. Kwa hiyo, karibu ulimwengu mzima unasimama katika ujinga kamili kuhusu moja ya ukweli mkuu katika Neno la Mungu. Na-wale WOTE ambao wakati mmoja walijifunza ukweli huu lazima wawe makini wakati wote, usije ukawaponyoka (Ebr. 2:1).

Mitume Walihubiri Injili ya Kweli

Kuna ushahidi gani kwamba waandishi wengine wa Agano Jipya walihubiri ujumbe huu huu? Ni mwingi sana!

Petro alihubiri ufalme. Angalia: “Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika UFALME wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo” (2 Pet. 1:11).

Ndivyo alivyofanya mtume Yakobo: “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa UFALME aliowaahidia wampendao?” (2:5).

Maelezo ya Mathayo hutaja usemi “injili ya ufalme” mara tatu tofauti. Huu hapa ni mfano mwingine ambao ni karibu sawa na 4:23, iliyokwisha kunukuliwa: “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri HABARI NJEMA YA UFALME, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina” (9:35)

Katika mingi ya mifano Yake, Kristo alifundisha mambo ya msingi ya ufalme wa Mungu. Mathayo peke yake, hasa kwa njia ya mifano, hufanya rejea zaidi ya hamsini kwa ufalme wa Mungu unaokuja.

Luka anarekodi kuwa Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi Wake kuhubiri ujumbe huu huu: Angalia “Akawaita wale Thenashara...Akawatuma wautangaze UFALME WA MUNGU” (9:1-2). Baadaye kidogo, aliwatuma wengine sabini waende kuhubiri, nao pia walibeba ujumbe wa “UFALME WA MUNGU” (10:1, 9)

Yohana anarekodi maneno ya Kristo mbele ya Pontio Pilato usiku ule aliposalitiwa. Hiki ni kiashiria muhimu kukielewa. Kristo alisema, “UFALME WANGU si wa dunia hii [jamii hii ya sasa]” (Yohana 18:36). Baadaye tutagundua undani wa jinsi ambavyo serikali ya Mungu itasimamishwa duniani.

Kumbuka kwamba Filipo, shemasi, alihubiri ufalme kwa Wasamaria (Matendo 8:12). Angalia kwamba katika kuhubiri alitenganisha ufalme na Kristo: “Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri… ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.”

Filipo hakuhubiri injili ya ufalme pekee, lakini pia aliitofautisha na fudisho juu ya Yesu Kristo. Tumia muda kusoma habari hii yote. Kumbuka mjumbe siyo ujumbe. Kristo si injili. Hata hivyo, Husimama kando yake moja kwa moja na atatawala dunia nzima wakati ufalme unasimamishwa.

Hivyo basi Luka, mwandishi wa Matendo, hutofautisha zaidi kati ya kuhubiri juu ya ufalme wa Mungu na kuhubiri juu ya Yesu Kristo! Wakati yote ni ya muhimu sana, ni wazi kwamba ni masomo mawili tofauti!

Tumetatua tatizo ambalo baadhi hudai Paulo alihubiri “injili toauti.” Kwa hakika hawa hawana habari kwamba ni Paulo ambaye Mungu alimtumia kutamka laana kwa yeyote aliyefanya hivyo (Gal. 1:8-9). Tumeona kwamba Paulo alihubiri ufalme wa Mungu. Hata hivyo, tutaona mafungu mawili katika Matendo, ambayo huonyesha kwamba hakupuuzia somo la pili juu ya jukumu la Kristo katika mchakato wa wokovu.

Kwanza, hebu tuthibitishe kwamba Paulo alihubiri ufalme wa Mungu kwa watu wa Mataifa. Matendo 19:8 inasema: “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya UFALME WA MUNGU.” Yako maeneo mengi katika nyaraka zake ambapo Paulo alifundisha ufalme kwa makanisa mbalimbali ya watu wa Mataifa. Ujumbe wake ulikuwa huo huo wakati wote, akiendelea kuhubiri na kurejelea ufalme wa Mungu.

Chunguza hili kutoka Matendo 20:25: “Niliowahubiria UFALME WA MUNGU…wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo” (fu. 21). Maelezo haya yanaweka wazi kwamba Paulo alihubiri injili hiyo hiyo—pia kando yake jukumu la Kristo—kwa Wayahudi na watu wa Mataifa. (Kimsingi Waefeso walikuwa waongofu kutoka kwa watu wa Mataifa.)

Kisha, angalia sura ya 28:30-31: “Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za UFALME WA MUNGU, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo.” Kama Filipo, Paulo alielewa kuwa injili na Kristo yalikuwa masomo mawili tofauti.

Mwisho, angalia aya moja zaidi mahali ambapo Paulo alibainisha tofauti kati ya injili na Nafsi ya Kristo, kwa kurejelea tena kwa ufupi 2 Wakorintho 11:4:

“Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri… au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye” (maelezo ya pembeni kwa usahihi hutamka usemi wa mwisho “na mimi”). Paulo aliwahimiza Wakorintho kuwakataa waalimu wa uongo na kushikilia kile alichokuwa amewafundisha. Kwa wazi alitofautisha mafundisho ya Yesu wa uongo na injili ya uongo kama makosa mawili tofauti.

Jiulize mwenyewe tena: Kama Kristo ni injili, basi kwa nini Paulo (mara nne) na Filipo huyaongelea kama mambo mawili tofauti?

Kila Nabii wa Agano la Kale Alihubiri Ufalme

Wengi wamedhani kwamba injili ni ujumbe wa Agano Jipya peke yake. Hakuna kitu ambacho kinaweza kuwa mbali na ukweli kama hiki! Kwa hakika Biblia imejaa maeneo, katika Agano la Kale na Jipya, yanayoelezea vipengele mbalimbali na unabii kuhusu ufalme wa Mungu.

Hebu tuchunguze kauli ya kushangaza ya Petro inayopatikana katika Matendo 3:19-21: “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.”

Angalia kwamba Petro anarejelea Kuja kwa Kristo—“kuwako kwake Bwana” (fu. 19), na fungu la 20 likisema kwamba Mungu “apate kumtuma Kristo Yesu.” Fungu la 21 huelezea ufalme wa Mungu kama “kufanywa upya vitu vyote.” Petro alitamka kwamba huku “kufanywa upya” (Kristo akisimamisha ufalme Wake) ni zamani ambazo “zilizonenwa na Mungu kwa… manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.”

Hii ni kauli ya kushangaza! Lakini je, ni kweli?

Inawezekana kweli Mungu alimtumia kila mmoja wa manabii Wake kutangaza ufalme Wake? Kwa nini wasomi wa Biblia na watu wa dini hupuuzia hili—au hata kulikataa hapo hapo? Hebu kwa ufupi tuchunguze Agano la Kale.

Wahubiri Kabla ya Gharika

Yuda aliandika, “Henoko [Babu-mkuu wa Nuhu]…alitoa maneno ya unabii…akisema, Angalia Bwana YUAJA na watakatifu Wake, maelfu maelfu ili afanye hukumu juu ya watu WOTE” (fu. 14-15). Ni wazi hii humrejelea Kristo akija kusimamisha serikali, inayotawala mataifa YOTE, akisaidiwa na watakatifu.

Katika 2 Petro 2:5 Nuhu hurejelewa kama “mhubiri wa haki wa nane”. Yuda aliandika kuwa Henoko alikuwa wa “saba kutoka Adamu.” Hivyo, Nuhu aliyemfuatia, anarejelewa kama wa “nane.” Ukianza na Habili, ukimjumlisha na Henoko, kulikuwa na watu wengine saba ambao walibeba jukumu hili hapo kabla. Maisha ya watu hawa wanane yalienea kipindi chote kati ya Adamu na gharika na wote walihubiri ujumbe huo huo.

Uchunguzi makini wa Yuda hufunua kuwa Henoko alihubiri kuhusu dhambi na haki. Wakati mengi yanaweza kusemwa kuhusu kipindi hiki cha karne kumi-na-sita-na-nusu, inatosha kusema, watu hawa wote walizungumzia ujumbe ule ule. Kumbuka Petro alisema, “…tokea mwanzo wa ulimwengu.”

Nani mwingine alihubiri ufalme wa Mungu?

Ibrahimu, Musa, Samweli na Daudi

Je, kuna ushahidi kwamba injili ilihubiriwa katika kipindi kilichofuata baada ya Gharika?

Katika Mwanzo 12:3, Mungu alimwambia Ibrahimu, “Katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.” Fungu hili pia hurejelewa katika Wagalatia 3:8, lakini limesemwa tofauti kidogo. Hapo linasema, “…Katika wewe [Ibrahimu] mataifa yote watabarikiwa.” Fungu hili hili husema kwamba injili “ilihubiriwa zamani kwa Ibrahimu.”

Hii inavutia! Si tu kwamba Ibrahimu alihubiriwa injili (bila shaka na Melkizedeki—Kristo), lakini pia ilihubiriwa katika Mwanzo, kupitia maandiko ya Musa, kuhusu Ibrahimu! Sasa fikiria. Inawezekanaje mataifa yote ya dunia kubarikiwa isipokuwa Kristo atakuwa amesimamisha serikali Yake duniani?

Ingawa Musa hakuwa “mhubiri wa haki” au mtume, alikuwa nabii na mwamuzi, na mtu wa kwanza ambaye Mungu alimwinua kuwaongoza Israeli. Pengine hujawahi kumfikiria Musa kama mmoja wa waliohubiri injili. Bado, Biblia hufunua kwamba alihubiri, kwa Israeli wa zamani, walipokuwa jangwani. Kama ilivyo Mwanzo 12:3, vivyo hivyo Hesabu 24:17-19 hurejelea injili, ambavyo vyote viliandikwa na Musa.

Matendo 3:22 kwa wazi inasema Musa alitangulia kunena kwamba Mungu atamwinua Yesu Kristo kama Nabii mkuu (Torati 18:15) ahubiri kwa ulimwengu wote mzima (Matendo 3:23) wakati wa Kurudi Kwake! Wengi wanaelewa tu juu ya Musa kuwaongoza Israeli kutoka Misri, na hawajui kabisa jinsi Mungu alivyomtumia katika njia hii.

Waebrania 3:9 na 4:2 pia huonyesha kwamba Musa alihubiri injili kwa Israeli wa zamani. “Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao [Israeli wa zamani]” (4:2). Mafungu haya, pamoja na Matendo 3, huonyesha kwamba hii ilijumuisha kipindi chote mpaka—na cha—Samweli!

Matendo 3:24 humrejelea Samweli pia kama aliyehubiri injili. Angalia: “Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena [ikimaanisha kila mmoja], walihubiri habari za siku hizi [Kuja kwa Kristo na ufalme wa Mungu].” Hizi ni kauli nzito na za wazi. Haziwezi kufunikwa. Tumia muda kutafakari juu ya kile ulichokisoma. Fungu hili linatamka, “manabii WOTE wa Mungu…wote walionena, walihubiri habari za siku hizi.”

Hatimaye, ingawa kila mtu anajua kuwa Daudi alikuwa mfalme, karibu hakuna anayefahamu kwamba alihubiri ufalme wa Mungu. Katika Zaburi 67:4, aliandika, “… Maana kwa haki Wewe [Bwana] utawahukumu watu, na kuwaongoza mataifa walioko duniani.” Kauli hii ni kielelezo dhahiri kwa serikali ya Mungu inayokuja.

Isaya, Yeremia, Ezekieli na Danieli

Nabii Isaya alitoa kauli za wazi kuhusu ufalme wa Mungu, kuhusu vile utakavyotokea na kuleta amani kwa mataifa yote duniani. Vile vile aliweka wazi kwamba ufalme wa Mungu huhusisha serikali. Angalia “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na UWEZA WA KIFALME utakuwa begani mwake; Naye ataitwa Jina Lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Maongezo ya ENZI Yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na UFALME wake; Kuuthibisha na kuutegemeza; Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele” (9:6-7).

Unabii huu uko wazi mno kiasi kwamba hauhitaji ufafanuzi zaidi!

Nabii Yeremia alitangulia kusema, “Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la Haki [Kristo]; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama: na Jina Lake Atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU”(23:5-6; pia soma fu. 7-8).

Kama ilivyo kwa Isaya, mafungu haya hayahitaji ufafanuzi zaidi. Yeremia anatoa maelezo ya wazi ya matukio ambayo yanaweza kuelezewa tu kama kipindi baada ya ufalme wa Mungu kuwa umekwisha kuja duniani. Hivyo, alihubiri injili kwa Nyumba ya Yuda.

Kitabu cha Ezekieli huelezea wakati ambapo Mungu atawakusanya watu Wake kutoka matekani watakakochukuliwa siku zijazo. Hiki ni kipindi kinachofuata mara tu baada ya Dhiki Kuu (Math. 24:21-22)—kipindi cha maafa kwa wazao wa leo wa Israeli wa zamani. Sasa angalia: “Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe” (36:24).

Mafungu kumi yanayofuata huelezea kipindi cha ujenzi mpya na mafanikio ambayo yanaweza kutokea tu baada ya Kurudi kwa Kristo. Chukua muda uyasome.

Danieli aliandika hivi: “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha UFALME ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa ENZI yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele” (2:44).

Je, nabii huyu alihubiri ufalme wa Mungu? Biblia inajibu ndiyo—na tutakuja kuona baadaye kuwa alifanya hivyo katika maeneo mengine mengi!

Manabii Wadogo Wote

Pengine kuacha Yona (ambaye bila shaka alihubiri injili nje ya kitabu chake), inaweza kuonyeshwa kwamba, kwa njia moja au nyingine, wale wote ambao hujulikana kama “Manabii Wadogo” walihubiri injili ya ufalme wa Mungu. Kumbuka, kuuona usemi “injili ya ufalme wa Mungu” si njia pekee ya kuielezea injili! Mwanzo 12:3 na Wagalatia 3:8 yamekwisha kudhihirisha hili.

Yapitie tena mafungu yafuatayo. Katika kila fungu, utaona kuwa yanarejelea ufalme wa Mungu, moja kwa moja au kwa namna nyingine: Hosea 2:16, 19; 3:5; Yoeli 2:21-27; Amosi 9:11-15; Obadia 21; Mika 4:1-3; Habakuki 2:14; Zefania 3:14-20; Zakaria 14:1-3, 8-9; Malaki 3:1-3.

Baada ya kusoma maandiko haya, ni wazi kwamba Petro alikuwa sahihi, na kwamba “...zije zamani za kufanywa [urejeshaji] upya vitu vyote zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu,” ambazo zaweza kutokea tu pale serikali ya Mungu itakapokuja duniani.

Ni muhimu sana kusema jambo moja la mwisho. Matendo 3:21 husema, “Mungu amenena kwa kinywa cha…” Ufalme wa Mungu ni ujumbe kutoka kwa Mungu.

Ni lazima iwe wazi kwamba ni MUNGU anayenena kupitia kwa aina yoyote ya mtumishi Anayemtumia—nabii, mzee, mwamuzi, shemasi, mhubiri wa haki, mfalme, mwinjilisti au mtume! Kama kweli mtu alikuwa mtumishi Wake, wakati wote Mungu alinena ujumbe huu huu kupitia kwake—“tokea mwanzo wa ulimwengu”!

Je, Kuna Injili Iliyojitenga ya Yesu Kristo?

Kama ilivyotajwa, Marko 1:1 huzungumzia “Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo.” Hebu tuulize: Je, “injili ya Yesu Kristo” ni tofauti—injili—ya pili? Je, Paulo alisahau kwamba kulikuwa na injili nyingine kando ya ile inayohusu ufalme?

Jibu ni “Hapana” ya msisitizo! Lakini wahubiri wengi hufundisha kwamba injili ya Yesu Kristo ni kuhusu Kristo, pia wakidai kwamba Yeye ndiye Ufalme wa Mungu na kwamba injili ya ufalme ni Kristo. Tumekwisha kuona kwamba huu ni uongo, na hautokani na Biblia kabisa! Injili ya Yesu Kristo ni injili Yake—ujumbe Wake kuhusu ufalme wa Mungu!

Tumeona kwamba Yesu alikuwa Mjumbe aliyetumwa kutoka kwa Mungu akiwa na TANGAZO! Haikuwa kuhusu Yeye Mwenyewe—ilihusu ufalme wa Mungu ukija kutawala juu ya dunia yote. Katika Yohana 12:49-50, Yesu alisema, “Kwa sababu Mimi sikunena kwa nafsi Yangu tu; bali Baba Aliyenipeleka, Yeye mwenyewe Ameniagiza Nitakayonena na Nitakayosema. Nami najua ya kuwa agizo Lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo Mimi, kama Baba Alivyoniambia, ndivyo Ninenavyo.” Lazima iwe wazi sasa kwamba Kristo Alitenda kama mjumbe—kama MSEMAJI kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

Katika Yohana 14:24, Yesu alisema, “nalo neno mnalolisikia silo Langu, ila ni Lake Baba Aliyenipeleka.” Kristo alileta ujumbe wa Baba—sio Wake Mwenyewe. Jambo hili sasa lazima liwe limekuwa wazi kabisa. Kumbuka, Alisema katika Luka 16:16 kwamba “Torati na manabii vilikuwapo [hubiriwa] mpaka Yohana: tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa.”

Hicho ndicho Kazi hii inafanya leo. Kupitia kijitabu hiki, ukweli wa ufalme wa Mungu unahubiriwa kwako na kwa maelfu wengine.

Kufasili Ufalme

Wengi huuliza, “Lakini ni nini hasa fasili ya Biblia ya ufalme?” Wahubiri na wanateolojia wamejaribu kuifanya maana ya jambo hili kuwa ya kiroho kwa sababu hawajachunguza kwa makini fasili ya Mungu mwenyewe iliyo wazi.

Fungua Danieli 2. Sura hii kwa hakika ni unabii mrefu unaowakilishwa na sanamu kubwa ya mtu mwenye sehemu nne (elementi nne) zilizoundwa kwa madini, ambazo huwakilisha falme nne halisi. Chukua muda kuusoma unabii huu wote. Sura hii ndiyo ina kile ambacho Biblia humaanisha kuhusu neno “ufalme.” Ufafanuzi huu unapatikana mwishoni mwa fungu la 39, ambalo hurejelea falme hizi “zitakazotawala dunia yote.” Hizi zinaweza kuelezewa tu kama serikali halisi zenye nguvu halisi juu ya watu halisi.

Baadhi huamini ufalme wa Mungu ni wazo tu katika “mioyo ya watu.” Fungu hili haliwezi kufafanuliwa kama kielelezo cha wazo lisilowazi, kuhusu “ufalme katika mioyo ya wanadamu.” Vile vile hakuna namna ya kuifanya fasili ya Mungu ikubaliane na kanisa fulani au makanisa. Huongelea utawala wa kiserikali wenye mamlaka juu ya mataifa halisi duniani—na juu ya watu halisi. Je, utaruhusu mtu awaye yote akuambie vinginevyo au utaliamini neno la Mungu? Kumbuka, falme hizo hapo juu “zilitawala dunia yote.

Tilia maanani vipengele viwili muhimu vya sanamu kubwa ya madini iliyoelezewa katika Danieli 2. Vinatoa mwanga katika matukio yaliyotabiriwa kutokea muda mfupi kabla ya Kurudi kwa Kristo. Kwanza, madini hupungua thamani kadri tunavyotelemka kutoka kichwani kwenda miguuni na nyayo za sanamu. Ubora wa kila ufalme/himaya unaofuata hupungua thamani kuliko ulioutangulia. Pili, madini huongezeka katika uimara kadri tunavyotelemka kwenye mwili wa sanamu hii. Kwa maneno mengine, nguvu na upana wa kila ufalme/himaya ni kubwa kuliko ule uliotangulia.

Mwisho angalia kwamba ile miguu miwili ya chuma (fu. 32-33, 40-42) huwakilisha ufalme uliogawanyika. Hii inaonyesha himaya ya Kirumi, ambayo ilikuwa imegawanyika, ikiwa na makao makuu sehemu mbili yaani Roma na Konstantinopo. Vidole kumi vya nyayo za miguu nusu yake ni chuma na nusu nyingine ni udongo wa mfinyanzi. Chuma hakiwezi kuchanganyika na udongo wa mfinyanzi, kwa hiyo hii ni picha ya hali isiyokuwa thabiti hapo mwishoni. Wakati miguu inavunjika, mtu huyu ataanguka.

Usomaji wa makini lazima ufanywe kwa sura tatu ili kuelewa kikamilifu mfuatano wa hizi falme nne na kuona wazi zaidi kwamba vile vidole kumi kwa hakika ni wafalme kumi tofauti watakaoungana kwa muda katika siku za mwisho.

Kisha, linganisha Ufunuo 13 na 17 pamoja na Danieli 7. Huu ni unabii wenye kutafakarisha na wenye nguvu kuhusu matukio ya siku za mwisho—matukio ambayo yatatuathiri wewe na mimi katika siku za maisha yetu! Ufunuo 17:8 huelezea “mnyama” anayetoka “kuzimu” na amepandwa na “mwanamke.” Fungu la 12 huonyesha kwamba mnyama huyu hujumuisha wafalme kumi watakaochukua madaraka na kuungana chini ya kiongozi mmoja mashuhuri atakayechukua jukumu la mnyama. Tukio hili litakuwa ni kufufuka kwa mara ya saba na ya mwisho kwa Himaya Takatifu ya Kirumiinayoibuka SASA HIVI katikati ya Ulaya. Muungano wa Nchi za Ulaya unakuja na uko hapa karibu mbele yetu. Ni muhimu kwamba uelewe unabii huu una maana gani! (Soma kijitabu chetu kipana Nani au Ni Nini Mnyama wa Ufunuo? ili ujifunze zaidi.)

Kitu cha kushangaza hutokea “katika siku za wafalme hawa” (vidole kumi vya miguu, ikimaanisha wafalme kumi wa mwisho wa Ufunuo 17:12). Tukio kubwa kuliko yote linalokuja huondoa shaka yote kuhusu NINI hasa ni ufalme wa Mungu. Pia, kwa kuwa hilo hutokea “katika siku za wafalme hawa” ni Mungu anatuambia LINI litatokea. Tulisoma hapo awali. Danieli 2:44 husema, “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake [Mungu kamwe hataruhusu watu kushika uongozi]; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.”

Ni Mungu, siyo watu, atakayesimamisha himaya ya mwisho iliyo kuu kuliko zote yenye kutawala ulimwengu mzima. Naye anatuambia kuwa Hataruhusu wanadamu kuingilia na kuikatisha—kwamba “itasimama milele na milele.” Ahadi hii ni HAKIKA. Lakini ulimwengu hauna habari kabisa kuhusu gari moshi la mizigo linalokuja hivi karibuni, lililosheheni matukio ya siku za mwisho tayari kuugonga—iwe watu wanaamini au hawaamini!

Mwanamke wa Ufunuo 17

Kabla hatujaendelea, tunahitaji kuchunguza zaidi kuhusu sura nzima za unabii, zinazoeleza zaidi Danieli 2.

Kwa kulinganisha Danieli 7 pamoja na Ufunuo 13 na 17 hufunua kuwa kuna kuibuka mara saba kwa Himaya Takatifu ya Kirumi. Mara sita imeibuka na kupita—na imebaki mara moja ambayo sasa inajiunda! Itakaa kwa muda wa miaka 3 ½, na ni katika kipindi kile kile kigumu cha Dhiki Kuu (Math. 24:21-22). Mara tu baada ya kufufuka huku kwa mara ya mwisho, ufalme wa Mungu utakuja.

Ni muhimu kuelewa kiunganishi kingine kwenye uibukaji mara saba (au kufufuka) kwa mfumo wa Kirumi. Ufunuo 17 inaelezea kila moja ya uibukaji kama una “mwanamke [ana]keti juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi” (fu. 3). Vichwa saba ni kuibuka mara saba tofauti, pamoja na uibukaji wa mwisho wa pembe kumi unaojumuisha wafalme kumi. Ni huyu mwanamke anayeeneza “siri ya kuasi” iliyoongelewa na Paulo (2 Thes. 2:7).

Kuhusu mwanamke, mafungu ya 5-6 husema, “Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.” Fungu la 1 humwita “kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi…” pamoja na fungu la 15 likifafanua kwamba “maji” ni “jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha.”

Hii ni lugha ya picha inayoelezea kanisa la watu wa Mataifa lililo kubwa na lenye nguvu ambalo ni mzao wa leo wa Babeli. Ni “mama” wa mabinti wengi “makahaba” waliotoka kwake kiupinzani kwa sababu hawakukubaliana na baadhi ya machukizo yake. Hili si kanisa dogo, bali ni kanisa “kuu” linalotawala watu “wengi”. Fungu la 2 huongelea juu ya “uzinzi” wake na “wafalme wa dunia.” Na fungu la 18 humwongelea yule mwanamke kama “ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.”

Huyu ni mwanamke tofauti kabisa na yule wa Ufunuo 12, ambaye ataolewa na Kristo (Ufu. 19:7; Math. 25:1-10; Efe. 5:23) wakati wa Kurudi Kwake. Sura hii huelezea Kanisa la Mungu la kweli ambalo kanisa kuu la watu wa Mataifa limelitesa kwa takribani miaka 2,000 (17:6). Ni watumishi wa hili kanisa kubwa “waliojiingiza kwa siri ndani” ya Kanisa la Mungu (Yuda 3-4) kama “mbwa mwitu” wakinena “mambo ya ufisadi” wakitafuta kuwavuta watu warudi kwenye siri ya Ukristo wa uongo.

Danieli 7:19-20 hutoa mwanga zaidi juu ya nini hutokea wakati watakatifu wanaporudi na Kristo. Wajibu wao wa kwanza ni kuchukua mahali pa kile Danieli alichokiita “mnyama wa nne” (himaya ya mwisho ya ulimwengu anayoiondoa Kristo wakati wa Kurudi Kwake), atawalaye kwa msaada wa “pembe ndogo.” Hii pembe ndogo ni ufalme wa kidini ambao ni sawa na yule mwanamke anayempanda mnyama wa Ufunuo 17. Ufalme huu wa kidini umetawala juu ya kila ufufuo, au uhuishwaji, wa Himaya ya Kirumi.

Watakatifu watakuwa wamevumilia mateso makali kwenye mikono ya huyu mwanamke “pembe ndogo.” Lakini hatimaye watakatifu waaminifu watazawadiwa kwa namna ya ajabu. Fikiria: “Nikatazama, na pembe iyo hiyo [mfumo wa Kibabeli wa Ufu. 17:5-6] ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; Hata akaja huyo Mzee wa Siku, nao watakatifu wake Aliye Juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki UFALME.” (Dan. 7:21-22).

Hatimaye, Mungu atamharibu kabisa kahaba huyu mkuu na mabinti zake makahaba, kwa kumgeuza mnyama anayempanda kinyume chake (Ufu. 17:16). Lakini kwanza lazima “aendeshe” ufufuo wa mwisho wa Himaya Takatifu ya Kirumi (mfumo wa Kibabeli)!

Hakuna muda mwingi uliobaki hadi kufikia uhuisho huu wa mwisho kutokea—unajiunda hata sasa—na ufalme wa ajabu wa Mungu kutokea muda mfupi baada ya hapo (19:11-16). Serikali zote za wanadamu—ikiwa ni pamoja na zile za kila nchi kubwa na ndogo duniani leo—zitavunjwa na mahala pake kuchukuliwa na SERIKALI BORA ya Mungu inayokuja.

Ufalme wa Mungu Unakuja

Usifanye kosa lolote! Pamoja na hali ya ulimwengu kukaribia mgogoro wa mwisho, kamwe hakuna mwanadamu anayeweza kuleta serikali moja yenye kutawala dunia nzima ambayo ingeweza kufanikiwa. Yesu Kristo atarudi hivi karibuni na kusimamisha ufalme WAKE.

Wanafunzi hawakuelewa ni lini Kristo angefanya hili. Ilimlazimu kuwaeleza kwa kutumia mfano. “Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa UFALME WA MUNGU utaonekana mara” (Luka 19:11). Mfano huu mrefu hufafanua kwamba muda mrefu ungepita kabla ufalme haujaja.

Kabla ya kupaa Kwake mbinguni, katika Matendo 1, baada ya kukutana mara kadhaa na wanafunzi Wake, Kristo alikutana nao kwa mara moja ya mwisho. Mpaka mwisho kabisa, Aliendelea kuwafafanulia zaidi ufalme wa Mungu. Lakini walibaki wakiwa wamekanganyikiwa kuhusu ni lini utasimamishwa: “Hata siku ile alipochukuliwa juu... [alikuwa] akiyanena mambo yaliyouhusu UFALME WA MUNGU… Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli UFALME?” (fu. 2-3, 6). Kristo alifafanua, “Si kazi yenu kujua nyakati wala majira…” (fu. 7). Hata leo hatuwezi kujua hasa ni lini utakuja, lakini tunaweza kujua kuwa uko karibu.

Sasa angalia Danieli 7:18: “Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.” Kisha fungu la 22 linasema, “Hata akaja huyo Mzee wa Siku [hapa ni Kristo, na Baba ametajwa kwenye fungu la 13], nao watakatifu wake Aliye Juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.”

Mwisho, angalia fungu la 27: “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu Wake Aliye Juu, ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka [watawala] watamtumikia na kumtii.”

Danieli alijua kwamba siku moja watakatifu watatawala na Kristo duniani!

Hubiri la kwanza la Kristo lililorekodiwa, linaitwa “Hubiri la Mlima [wa Mizeituni],” husema kwamba “wapole watairithi nchi” (Math. 5:5). Kwa hakika, Kristo alikuwa anamnukuu Daudi, aliyerekodi hili katika Zaburi 37:11—ni mahali pengine Daudi alipoitangaza injili. Maneno yaliyotumika hapo ni yale yale. Unabii mwingine pia huonyesha kwamba siku moja Daudi mwenyewe atatawala juu ya makabila yote ya Israeli, ndani ya ufalme wa Mungu.

Angalia mafungu matatu tofauti katika Ufunuo. Kristo amenukuliwa kupitia kwa Yohana akisema, “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja Nami katika kiti Changu cha enzi, kama Mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba Yangu katika kiti Chake cha enzi” (3:21). Pia 2:26-27: “Na yeye ashindaye…Nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.” Mwisho, “ukawafanya kuwa UFALME na MAKUHANI kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi” (5:10).

Je, dini yoyote iliyoundwa imekuambia kuhusu mojawapo ya mafungu haya? Bila shaka hakuna kabisa. Japokuwa yamekuwepo ndani ya Biblia kwa maelfu ya miaka.

Si ajabu kwamba Kristo alipokuwa akishtakiwa kwa ajili ya maisha Yake, Alisema, “UFALME Wangu si wa ulimwengu huu. Kama UFALME Wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi Wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini UFALME Wangu si wa hapa” (Yohana 18:36). Katika majibizano haya, Pilato alikuwa amemuuliza, “Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni…” (fu. 37).

Yesu alielewa kikamilifu kwamba Alizaliwa kuwa Mfalme.

Kristo Kuwa Mfalme

Kuja kwa Kristo Mara ya Kwanza lilipaswa kuwa tukio kubwa. Isaya alitabiri kuzaliwa Kwake na bikra: “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli (7:14).

Kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, malaika alimtokea Mariamu kumfafanulia kusudi la Mungu na kile kilichokuwa kinaenda kumtokea: “Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali…Mariamu” (Luka 1:26-27).

Kuanzia fungu la 30, Gabrieli anaelezea zaidi jinsi ambavyo hatimaye Kristo atatawala kutoka kwenye kiti cha enzi cha Daudi. Angalia: “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto Mwanamume; na jina Lake utamwita YESU. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa KITI CHA ENZI cha Daudi, baba yake. ATAIMILIKI nyumba ya Yakobo hata milele, na UFALME Wake utakuwa hauna mwisho” (fu. 30-33).

Kristo kamwe hakuwa na shaka kuhusu wito wake maalumu na kusudi la maisha Yake. Hii ndiyo sababu aliendelea kuhubiri ufalme wa Mungu popote alipokwenda.

Isaya aliongelea kwa undani zaidi kuhusu jinsi ambavyo ufalme wa Mungu utaenea duniani, hatimaye kuyafunika mataifa yote: “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye Atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe” (2:2-4).

Unabii ulio sawa na huu unapatikana katika Mika 4:1-3. Aya hizi hutabiri kwamba ufalme wa Mungu utaenea ulimwenguni. Hii ndiyo sababu mfano mmoja wa Kristo unaulinganisha na chachu (Luka 13:20-21), ambayo daima husambaa na kujaa ilimowekwa. Kusudi kuu la maisha yako ni kushiriki kuieneza SERIKALI ya Mungu wakati ujao.

Mbele ya jengo la Umoja wa Mataifa kuna sanamu ya mtu mkubwa akifua panga kuwa jembe. Nimeiona mara nyingi sana, kwa sababu niliendesha huduma za kanisa mtaani hapo mkabala na mahali ilipo kwa miaka kadhaa. Lakini hakuna mtu anayeonekana kutilia maanani tena, au hata kuamini, unabii wa kushangaza unaoelezewa na sanamu hili maarufu.

Yesu Kristo alikuja kuwa MFALME ambaye siku moja ATATAWALA duniani. Atakaporudi, mateso, masikitiko, huzuni na matatizo yote ya dunia na maovu vitatoweka—na amani ya dunia “itajitokeza” halisi, sambamba na furaha kuu, mapatano na mafanikio tele kwa mataifa yote. Hakuna serikali ya mwanadamu iliyoweza kuleta mambo haya hata kwa nchi moja duniani. Hiki ndicho kiini cha injili ambayo Kristo aliileta.

Je, unaiamini? Utaiamini?

Ufalme wa Mungu Lazima Uendelee Kuhubiriwa Leo

Katika unabii wa Mlima wa Mizeituni kwenye Mathayo 24 (na 25), Kristo aliulizwa kuhusu matukio ambayo yangekuwa ishara ya Kuja Kwake Mara ya Pili na mwisho wa ulimwengu (zama). Alijibu kwamba matukio na hali mbalimbali tofauti vitatokea kwanza.

Tukio moja linalotangulia Kurudi kwa Kristo limeelezewa katika fungu la 14: “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Injili ya kweli ilitabiriwa kuhubiriwa mpaka “mwisho utakapokuja.” Hii inamaanisha wazi kwamba mtu fulani atakuwa anaihubiri sasa, katika zama yetu, kwa sababu mwisho bado haujaja.

Historia kidogo: Maarifa ya injili ya kweli yalirejeshwa na Herbert W. Armstrong (1892-1986). Injili ilikuwa haijahubiriwa kwa ulimwengu kwa takribani karne 19 mpaka bwana Armstrong alipoanza kuihubiri mwezi Januari 1934, wakati unabii wa Mathayo 24:14 ulipoanza kufunuliwa. Elewa! Tangu karne ya kwanza ulimwengu wote haukuwahi kusikia ujumbe huu. Kwa kipindi chote cha huduma ya miaka 52, mpaka kifo chake mwaka 1986, Mungu alimtumia bwana Armstrong kuwafikishia ufahamu huu mamia ya mamilioni. Huyu ndiye mtu aliyenifundisha mimi injili ya kweli na ambaye chini yake nilifunzwa kuweza kuupeleka ujumbe huu huu kwa ulimwengu.

Kumbuka, mwisho bado haujaja. Kwa hiyo, Kanisa la Mungu Rejeshwa linaendeleza utume huu, kwa ujasiri likihubiri ukweli huu mkuu kati ya kweli za kiunabii. Kuwasili kwa ufalme wa Mungu ni hakika—hakuna shaka! Utakapofika, wewe pia unaweza kuwa sehemu yake.

Mpango wa Miaka 7,000

Ukiwa umetengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi (Isa. 59:1-2), ubinadamu umeamini uongo wa mungu wa dunia hii kwa miaka 6,000. Muhula wa Mpango wa Mungu kwa wanadamu utachukua miaka 7,000. Wachache wameelewa hili. Wengi wameelewa kwa usahihi angalau machache ya baadhi ya mafungu yanayoelezea Utawala wa Kristo wa miaka 1,000 unaokuja, utakaoanza wakati wa Kurudi Kwake (Ufu. 20:4-6). Lakini hawajui chochote kuhusu Mungu kutenga miaka 6,000, au siku-milenia sita za “juma la siku-saba,” kwa ajili ya utawala wa mwanadamu, chini ya Shetani, kabla ya miaka 1000 ya “siku” ya saba. Tuko karibu sana na mwisho wa “siku ya sita.”

Hebu tuelewe! Biblia inasema, “Lakini, wapenzi, MSILISAHAU neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja” (2 Pet. 3:8; Zab. 90:4). Kwa hakika wengi “wamepuuza” karibu KILA KITU ambacho Biblia inafundisha.

Je, utatambua?

Mwanadamu (chini ya utawala wa Shetani usioonekana) amepewa “siku” sita, au miaka 6,000, kujaribu njia zake, serikali, dini, falsafa, mifumo ya maadili na mitindo ya elimu. Chini ya ushawishi wa Shetani ameendelea kutenda dhambi na uasi kwa maagizo ya Mungu wakati huu wote. Na ameshajaribu kutibu athari zote mbaya zilizojitokeza, badala ya chanzo, ambacho ni uvunjaji wa amri za Mungu. Mungu anauruhusu ubinadamu kujifunza masomo magumu, machungu. Walio wengi ambao kamwe hawakuwahi kujua thamani ya ukweli wa Mungu, lazima wajifunze kwamba njia zao hazifai kitu!

Muda mfupi ujao, ulimwengu utashuhudia kutimia kwa Ufunuo 11:15: “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo Wake, Naye atamiliki hata milele na milele.” Kama vile hakuna shaka leo-hii kwamba nchi huwakilisha, falme (mataifa na serikali) halisi, vivyo hivyo hapawezi kuwa na shaka kutoka kwenye fungu hili, kwamba serikali ya Mungu inayokuja pia ni halisi, itawalayo mataifa halisi duniani.

Yesu Kristo alizaliwa kuwa Mfalme ambaye atatawala mataifa ya dunia milele akisaidiwa na wafalme wengine walio roho: “Na upanga mkali hutoka kinywani Mwake ili Awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma…ana jina limeandikwa katika vazi Lake na paja Lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA” (Ufu. 19:15-16).

Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kukuambia juu ya aya hizi? Sikuwahi kujifunza habari zake au hata kuzisikia katika kanisa la ujana wangu—na bado, ndizo hizi hapa, zimeandikwa zikiwa na maana iliyowazi kwa wote ambao watasikia.

Ufalme wa Mungu Wafafanuliwa

Mathayo 6:33 inasema, “Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki Yake…” Kama unatafuta kitu fulani kwanza katika maisha, ingekuwa vyema ukaelewa ni nini unachotafuta. Sura hii ina kile ambacho wengi hukiita “Sala ya Bwana” (fu. 10). Kristo anawaelekeza Wakristo kusali, “Ufalme wako uje.” Ili kufanya hivyo kiusahihi, ni lazima ujue kile unachokiomba.

Lengo kuu hapa si kufafanua kwa undani ufalme wa Mungu. Ni kufafanua fasili ya injili ya kweli na mustakabali wa ajabu wa mwanadamu. (Kujifunza mengi zaidi, soma kijitabu chetu Ufalme wa Mungu ni Nini?)

Hivyo hebu tuelewe. Neno “ufalme” kwa urahisi humaanisha serikali. Kwa hakika, huwezi kuwa na serikali bila taifa la kutawala. Kwa hivyo, ufalme kwa uchache ni taifa moja pamoja na serikali yake.

Kuna vipengele vinne vya lazima ili pawe na ufalme wowote: (1) Ardhi, mali au eneo—liwe kubwa ama dogo. Kwa maneno mengine, ni lazima pawepo na mipaka halisi inayotambulisha ukubwa wa ufalme; (2) mtawala, mfalme, mtawala mkuu au gavana anayeongoza serikali, (3) watu au wananchi wanaoishi katika eneo la utawala, na (4) mfumo wa sheria na kanuni sambamba na muundo msingi wa serikali. Hakuna ufalme uliokamilika bila kuwa na mambo haya yote ya msingi.

Lakini mambo haya yanahusika vipi na ufalme wa Mungu? Wengi hawajui mambo ya msingi ya ufalme wa Mungu. Je ni ufalme halisi wenye mahali halisi duniani, wenye watu na sheria, zikisimamiwa na mtawala? Baadhi huamini kuwa ufalme ni kitu fulani kilichomo katika mioyo ya watu. Wengine wanaamini kuwa uko mahali popote utakapoona kanisa fulani. Bado wengine wanaamini kuwa ni Yesu Kristo mwenyewe. Wengi wanaamini kuwa uko hapa sasa na wengine wanaamini kwamba haujaja bado, lakini hawajui jinsi ambavyo utatokea.

Tunaweza kuuliza: Jinsi gani mtu anauingia ufalme wa Mungu?

Ni Lazima Mtu Azaliwe Mara ya Pili Kuuingia Ufalme

Paulo aliandika kwamba Kristo ni “mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu” (Kol. 1:18), na pia “mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi” (Rum. 8:29). Yakiunganishwa, mafungu haya yanaonyesha kwamba Yesu ni mzaliwa wa kwanza tu kutoka kwa wafu, na wengine wengi watafuatia. Lakini ni lini, na katika nini, watazaliwa?

Katika Yohana 3:3, Kristo alimwambia Nikodemo, “Amin, amin [hii humanisha kweli, kweli], nakuambia, Mtu ASIPOZALIWA MARA YA PILI, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Katika fungu la 6, Kristo aliendelea, “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Kwa urahisi tu amini maana dhahiri ya fungu hili. Ni lazima mtu afanyike roho ili aweze KUUONA ufalme wa Mungu. (Soma kijitabu chetu “Kuzaliwa Mara ya Pili”Kuna Maana Gani?

Paulo alifundisha, “nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu” (1 Kor. 15:50). Mafungu mawili yanayofuata yanafafanua kuwa ufufuo utatokea wakati wa Parapanda ya Saba (mwisho), wakati “wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.”

Kristo atarudi wakati Parapanda ya Saba (ya Ufunuo 11) italia. Huu ndio wakati ambao ufufuo wa wafu utatokea. Usilielewe vibaya tukio hili la upeo wa juu kabisa. Watu ambao hapo kabla walikuwa wanadamu wa nyama watabadilishwa wawe roho—watazaliwa mara ya pili—na kuingia katika ufalme wa Mungu. Hakuna watu halisi wanaoweza kuuingia ufalme huu.

Yohana 4:24 inasema, “Mungu ni Roho.” Chini ya Baba, Kristo anaongoza ufalme Wake, ambao unaundwa na viumbe roho. Wakati wa Kurudi Kwake, Kristo, kama mwanakaya [memba] wa Familia ya Mungu, atakuwa na wadogo wengi “ndugu wakiume na wakike,” watakaokuwa wamefuzu kutawala pamoja Naye.

Lifikirie jambo hili kwa njia hii: Uko ufalme wa mimea, ufalme wa wanyama, falme za wanadamu na ufalme wa malaika. Vile vile kuna ufalme wa Mungu.

Sasa angalia Mwanzo 1:26: “Na tumfanye mtu kwa mfano WETU, kwa sura YETU.” Wakijirejelea wao wenyewe, yule anayeongea anasema, “Sisi,” “Wetu” na “Yetu.” Huu ni uthibitisho kwamba katika Uungu wako zaidi ya mmoja—kwa sasa wako wawili! Katika andiko hili, neno la Kiebrania kwa ajili ya Mungu ni Elohim. Neno hili ni la wingi katika umoja kama kundi, timu, kamati au familia. Maneno haya yote huwakilisha kitu kimoja, chenye washiriki kadhaa au watu.

Kwa hivyo, Biblia inafundisha kwamba yuko Mungu mmoja, anayeundwa na nafsi mbili—Baba na Kristo—na wengine wengi zaidi kuongezewa baadaye. Mara ya kwanza Mungu atakapoongeza wana wengi katika Familia Yake ni pale ufalme wa Kristo unaposimamishwa. Lakini kuuingia ufalme wa Mungu halitakuwa jambo la moja kwa moja kwa mtu yeyote.

Yako Masharti Kuuingia Ufalme

Tunasoma mahali kadhaa ambapo Kristo alisema ni wale tu wanaoshinda ndio watakaourithi ufalme na kutawala pamoja Naye. Kuna zaidi ya kuwepo katika ufalme wa Mungu kuliko kuutamani tu. Kuna MASHARTI ya kufuzu ambayo lazima yatimizwe.

Yesu alimwaambia kijana tajiri aliyeuliza kuhusu uzima wa milele, “…ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri” (Math. 19:17). Alifafanua mtu ni sharti azishike Amri Kumi ili aweze kuokolewa, na kwa dhahiri akanukuu tano kati yake.

Sasa dhambi ni nini? Kwa kuwa kuitenda huleta mauti (Rumi 6:23), si ni vyema ukajua ni nini? 1 Yohana 3:4 imerekodi, “Dhambi ni uvunjaji wa sheria.” Hii ni sheria ile ile ambayo kijana tajiri aliambiwa ni sharti aitii ili aweze kuurithi uzima wa milele.

Wengi wanadai kuwa Wakristo—kuwa wafuasi wa Kristo. Wanadai “kumwamini Kristo” na wanadai kuwa “watafutaji wa ukweli,” wakati hawataki ukweli halisi wa Biblia kabisa. Angalia majibizano haya marefu yaliyotokea kati ya Kristo na Mafarisayo: “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika NENO LANGU, mmekuwa wanafunzi Wangu kweli kweli; tena mtaifahamu KWELI, nayo hiyo KWELI itawaweka huru... Lakini sasa mnatafuta kuniua Mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, Niliyoisikia kwa Mungu...Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda Mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja...Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia NENO LANGU...Nami, kwa sababu nasema ILIYO KWELI, hamnisadiki [lakini bado inasema “waliomwamini”]...Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?” (Yohana 8:31-32, 37, 40, 42-46). Katika maelezo hayo Kristo anaendelea kuwashitaki kwa wazi wale ambao wangedai kuwa Wakristo wakati kwa hakika wao ni “wa baba (yao) ibilisi.”

Wengi wanadai kwamba “wanamjua Yesu” wakati kwa hakika hawajui chochote juu ya Kristo wa Kweli wa Biblia. Kama alivyosema, kwa hakika “hawawezi kusikia” maneno ya Kristo—ile KWELI—ingawa wanaweza kudhani kwamba wanasikia: “Yeye asemaye, NIMEMJUA, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala KWELI haimo ndani yake” (1 Yohana 2:4). Ulimwengu umejawa na mamia ya mamilioni ya “Wakristo” wa aina hii, wakimkiri Yesu fulani, lakini hawaijui kweli.

Wengi wasiouishi Ukristo, hujiingiza katika Kanisa la kweli. Lakini hatimaye wote huondoka. Yohana aliendelea, “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (fu. 19). Nimeliona hili mara nyingi. Wengi wanaonekana kuamini “juu” ya Kristo tu, si kumwamini Yeye hakika—yaani kuamini kile alichokisema, na akasema KUTENDA!

Kumbuka maneno ya Kristo katika Marko 1:15: “TUBUNI, na kuiamini injili.” Toba ni kutoka dhambini (Matendo 3:19). Mkristo ni yule aliyegeuka kutoka—ametubu—dhambi zake, na amebatizwa (2:38) na kuongoka (3:19). Kwa maisha ya kushinda dhambi, Mkristo hufuzu kwa (ingawa hawezi kuchuma) wokovu na kuzaliwa katika roho kuingia ufalme wa Mungu.

Mustakabali Wako wa Kustaajabisha

Kumbuka Mungu alisema kwamba Aliwaumba wanadamu katika “sura” na “mfano” Wake. Fungu hili linamaanisha kile linachosema. Mungu alikuumba wewe ili uwe “kama” Yeye kwa kila namna. Kwa njia ya Roho Yake kuingia katika fikra za kila mtoto Wake mpya aliyeongoka, maisha mapya kabisa ya roho yametungwa. Wakati huo, “kiini tete-roho” kidogo kinapata kuwepo. Kama vile watoto wadogo wanavyokua na kuonekana kama wazazi wao, vivyo hivyo pia watoto wa Mungu taratibu huchukua mfano wa KIROHO wa Mungu (Mzazi wao), katika asili na tabia, kadhalika katika sura na umbile (2 Pet. 1:4).

Agano la Kale na Jipya kwa pamoja huweka pointi hii dhahiri kabisa! Wakati wengi wana ufahamu hafifu kwamba Wakristo wanaweza, kwa namna fulani, kuwa “wana wa Mungu,” hakuna aliyewahi kufikiria jambo hili: “Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa Atakapodhihirishwa, TUTAFANANA Naye; kwa maana tutamwona kama Alivyo” (1 Yohana 3:2). Tafakari maarifa haya ya kuduwaza! Siku moja tutakuwa na mwonekano halisi wa Yesu. Warumi 8:16 inasema sisi ni “watoto” wa Mungu na “warithi” pamoja na Kristo.

Mfalme Daudi pia alielewa jambo hili miaka elfu moja mapema alipoandika, “Bali mimi nikutazame uso Wako katika haki, nitashibishwa, wakati nitakapoamka, na SURA YAKO” (Zab. 17:15). Bila kutegemea, fungu hili huondolea mbali wazo la “njozi nzuri” ya kufikirika iliyosambazwa na kanisa la ulimwengu—kwamba watu hawatauona uso wa Mungu katika maisha yajayo. Daudi alielewa kwamba tutamwona Mungu—na uso kwa uso. Vivyo hivyo Yohana. Wote walielewa kuwa, kwenye Ufufuo—“tutakapoamka”—tutakuwa kamili kama Mungu, katika umbo na tabia.

Kwa hivyo, kwa hakika Mungu anazaliana Mwenyewe ndani ya watu waliopokea Roho Yake Takatifu. Anaumba watoto ambao wataonekana na kuwa kama Yeye Mwenyewe!

Ni Roho ya Mungu yenyewe iliyo ndani yetu ambayo itatuwezesha kuamuka katika Ufufuo. Angalia Warumi 8:11: “Lakini, ikiwa Roho yake Yeye aliyemfufua Yesu katika wafu inakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, KWA Roho Yake inayokaa ndani yenu” (pia 1 Kor. 15 na 1 Thes. 4:13-18). Kristo aliinuliwa na kurudi kwenye nafasi Yake kando ya Mungu Baba. Alikuwa ametimiliza jukumu Lake la kuwa Mwokozi.

Sasa, elewa! Roho ile ile, inayokaa ndani yetu tangu wakati wa kuongoka, itatufufua (wale wote waliotungwa na Mungu) kuungana na Mungu katika ufalme Wake.

Kama vile kitoto kipya kilichotungwa kinavyokua katika tumbo la mama yake, Mkristo pia lazima akue kabla hajaweza kutoka nje ya tumbo. Petro aliandika, “Lakini, KUENI katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo” (2 Pet. 3:18). Wakristo wanapaswa kukua katika kipindi hiki cha maisha. Ili kupewa mamlaka ya kiungu na uwezo, kama warithi-pamoja na Kristo, lazima wafuzu, kupitia kujenga tabia ya Mungu iliyo takatifu, na ya haki katika maisha yao.

Paulo alifafanua kwamba jukumu la watumishi waaminifu katika Kanisa ni kulilisha kundi. Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu” (Math. 16:18). Ni Kanisa—Kanisa LILE—ambalo ni “Yerusalemu wa juu...mama yetu sisi” (Gal. 4:26; Ebr. 12:22-23). Kama alivyo mama yeyote, Kanisa linawatunza na kuwalisha watoto wake—na amekuwa akifanya hivyo kwa miaka 2,000.

Andiko la Kustaajabisha

Kitabu cha Waebrania kinafunua Kusudi la Mungu la kustaajabisha kwa uwazi kama kioo. Muktadha huanza katika Sura ya 1. Tazama picha ya wokovu ikifunuka.

Kwanza, elewa kwamba Mungu aliumba malaika wawe “roho watumikao” wakitumwa kuwahudumu “wale watakaourithi wokovu” (fu. 14). Hili ndilo jukumu lao katika Mpango wa Mungu. Malaika hawajapewa nafasi ya kuwa wanakaya [memba] katika Familia ya Mungu. Hii ndiyo sababu Shetani (kama malaika aliyeanguka) anachukia sana wazo kwamba wanadamu wa nyama, wadhaifu, wa hali ya chini wanaweza kupokea kile ambacho hakikutolewa kwake wala hawezi kukipata.

Paulo ananukuu sehemu mbili katika Zaburi: “Kwa maana Alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe Mwanangu, Mimi leo Nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake Baba, Na Yeye atakuwa Kwangu Mwana?...” (fu. 5). Kamwe Mungu hajawahi kusema hili kwa malaika yeyote!

Kisha Paulo ananukuu Zaburi nyingine, akifafanua kile ambacho wakati wote kimekuwa kusudi la Mungu: “Kiti chako CHA ENZI, Mungu, ni cha milele na milele: Na fimbo ya UFALME Wako ni fimbo ya adili...” (fu. 8). Fimbo hutumika kama alama ya utawala au mamlaka—na katika ufalme Wake ni Mungu aliye na nguvu zote.

Mwisho, Paulo analiuliza swali lile lile kwa namna nyingine kuhusu malaika: “Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono Wangu wa kuume hata Nitakapoweka adui Zako chini ya Miguu Yako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” (vs. 13-14).

Hii inaweka jukwaa kwa ajili ya kile ambacho lazima tukifahamu! Hebu tutafakari vilivyo mustakabali wa kustaajabisha ambao Mungu ameandaa kwa ajili ya wale wote wanaomtumikia.

Mfululizo wa mafungu ya kushangaza unaendelea katika sura ya 2. Paulo alimnukuu Daudi (kutoka Zaburi 8:4-6) alipouliza swali hilo la muhimu-kuliko yote, “Mwanadamu ni nini hata Umkumbuke?” (Ebr. 2:6). Kwa kuwa Mungu ni wa milele, na huketi juu ya ulimwengu wote na ndiye mwenye uweza wote chini Yake, sio ajabu Daudi aliuliza, na Paulo akarudia, swali hili lilio kiini cha maisha.

Jibu la kushangaza linaanza katika fungu linalofuata: “Umemfanya [mwanadamu] mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono Yako.”

Hatimaye Mungu atashiriki utawala wa uumbaji Wake wote na Wana Wake. Kwa mara nyingine, Kristo ni wa kwanza tu wa Wana wengi. Kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza hakuzuii kuzaliwa kwa wana wengine (na mabinti) kwa familia hiyo. Ninao wana wawili na mimi ni mzaliwa wa kwanza wa kiume nikiwa na ndugu mdogo. Baba yangu alikuwa kijana wa pili, akiwa na kaka yake na kuendelea. Unaiona pointi.

Paulo anaendelea kufafanua kwamba Mungu anapanga kuwapa Wana Wake nguvu nyingi ajabu na mamlaka: “Umeweka VITU VYOTE chini ya miguu yake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza KITU kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake” (fu. 8). Bado hili halijatokea—lakini litatokea hivi karibuni.

Mungu anaposema kwamba “vitu vyote” vitawekwa chini ya miguu ya mwanadamu, hicho ndicho Anachomaanisha! Ulimwengu usiopimika, pamoja na mamilioni kwa kipawa cha nne cha nyota na trilioni moja ya galaksi, vitawekwa chini ya mamlaka ya wanadamu watakaokuwa wamezaliwa katika Familia ya Mungu. Kwa hakika, tafsiri ya Biblia ya Moffatt hulitafsiri neno la Kigiriki “vitu vyote” kama “ULIMWENGU.”

Kwa kweli haya ni maarifa ya kuduwaza! Tumia muda kuyashika. Furahia kile ambacho kinaweza kuwa mustakabali WAKO!

Kabla ya kuendelea, angalia fungu la kushangaza kuhusu kipengele kingine kinachohusiana cha wokovu ambacho hakikueleweka kabla. Tumeona kwamba Wakristo wanasubiri wokovu wa kustaajabisha. Lakini uumbaji kwa ujumla nao unasubiri kwa hamu kubwa kufunuliwa kwa wale wana wapya watakaoongezwa kwenye Familia ya Mungu. Soma mafungu yafuatayo kwa uangalifu kutoka Biblia ya Revised Standard Version:

“Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana uumbaji [vitu vyote katika ulimwengu unaojulikana] wote ulitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari Yake, ila kwa sababu Yake Yeye aliyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa uumbaji wenyewe utawekwa huru kutoka katika utumwa wa uharibifu, hata uingie katika uhuru wa utukufu wa WATOTO WA MUNGU. Twajua ya kuwa uumbaji wote [kila kitu] umekuwa ukiugua pamoja nao una utungu pamoja hata sasa; wala si uumbaji tu, ila na sisi wenyewe [Wakristo] tulio na malimbuko ya Roho [wale WACHACHE wanaoitwa sasa], sisi pia tunaugua katika nafsi zetu kadri tunavyongoja [kuzaliwa] kama wana” (Rum. 8:19-23).

“Wana wote wa Mungu” wajao hatimaye watauweka huru uumbaji ambao sasa uko utumwani, na uliotabiriwa kuendelea kuwa mbaya zaidi. Dunia iliyooza na kujeruhiwa, jua, mwezi na nyota—ulimwengu!—utafanywa upya hivi karibuni na kurudishwa kwenye hali ya uzuri, usawa na utulivu chini ya uongozi wa Kristo na watakatifu waliofufuliwa.

“Kuleta Wana Wengi Kwenye Utukufu”

Sasa tunaweza kuendelea na maelezo ya muhimu sana katika Waebrania 2: “Ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu Aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. Kwa kuwa ilimpasa Yeye, ambaye kwa ajili Yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta WANA WENGI WAUFIKILIE UTUKUFU, kumkamilisha Kiongozi Mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso” (fu. 9-10).

Aya hii inafunua uwezekano wa kushangaza uliopangwa kwa ajili ya Wakristo wote. Wakati Kristo atakaporudi, Paulo anafunua kwamba watakuwepo “WANA WENGI” watakaoufikilia “utukufu” kwa njia ya “Kiongozi Mkuu wa wokovu wetu.”

Fungu la 11 husema kwamba Kristo “haoni haya kuwaita [wale wana wengine wengi—sisi] ndugu.” Hawa ndio wale ambao kwao Kristo huitwa “mzaliwa wa kwanza.” Kwa kweli, mtu aliyetungwa ameitwa kuufikilia “utukufu” na kuwa mmoja wa “wana wengi.” Mateso na dhabihu ya Kristo ndivyo vinavyomfanya kuwa “Kiongozi Mkuu wa wokovu wao”—na awezekanaye kabisa kuwa wako!

Ni uwezekano wa kustaajabisha namna gani kwa wale ambao Kristo “anawaita…ndugu.” Sasa angalia fungu hili la mwisho: “Maana Yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii Haoni haya kuwaita ndugu” (fu. 11). Kristo na watakatifu wanashiriki wokovu ule ule.

Fungu hili linaonyesha kwamba Wakristo “wametakaswa” (tengwa). Kwa namna gani? Yohana anasema, “Uwatakase [Wakristo waliotungwa] kwa ile kweli; NENO LAKO NDIYO KWELI” (Yohana 17:17).

Tamaduni na hadithi zinazoshabikiwa na wanadamu, kuhusu maisha baada ya kifo au kitu kingine chochote, huanguka vinapochunguzwa. Wakristo, wakiwa wametoka kwenye ulimwengu uliodanganyika na kukanganyikiwa, wametengwa kutoka ulimwenguni kwa ile KWELI!

Kama Kristo “haoni haya kuwaita (sisi) ndugu,” hivyo basi sisi, wana wa Mungu waliotungwa, lazima tusione haya kuitetea ile kweli inayotutakasa—na kweli ya injili (Fil. 1:17). Ni lazima “tukue” kwa Kristo (Efe. 4:13) na tuyashike mafundisho ya kweli ya Mungu. Ni lazima TUFUZU ili siku moja tusimame kando ya Kristo juu ya “vitu vyote.”

Je, unakiona kilichoelezwa hapa? Lengo la kushangaza la Mkristo ni kuzaliwa katika ufalme wa Mungu—kufanyika nafsi roho AKITAWALA chini ya Kristo, kama Mwana halisi wa Mungu. Kitu gani chaweza kuwa cha ajabu zaidi—cha UTUKUFU zaidi!—kwa ajili ya Mkristo kukitazamia?

Kristo Anarudi

Mathayo 24:27 inasema kwamba Kristo atakaporudi, Kuja Kwake kutakuwa kama umeme uking’aa kutoka mashariki hata magharibi. Hili litakuwa ni tukio litikisalo dunia yote, isiwezekane kulikosa.

Danieli aliongea juu ya Kristo kuja katika “mawingu ya mbinguni” (7:13). Kabla ya Kurudi Kwake, Mungu anampa rasmi MAMLAKA kutawala ulimwengu. Watakatifu hawawezi kupewa mamlaka na Kristo mpaka Yeye atakapopewa mamlaka kwanza. Hapo ndipo atakapoweza kuwapa nguvu wengine. Angalia: “Naye AKAPEWA [Kristo] mamlaka, na utukufu, na UFALME, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka Yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na UFALME Wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” (fu. 14).

Si ajabu Kristo alisema, “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo Yangu hata mwisho, Nitampa mamlaka juu ya mataifa: naye atawachunga kwa fimbo ya chuma... kama mimi nami Nilivyopokea kwa Baba Yangu” (Ufu. 2:26-27) na mafungu machache baadaye, “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja Nami katika kiti Changu cha enzi... (3:21). Kristo atakaporudi, watakatifu watatawala pamoja Naye!

Lakini wajibu wa Mkristo katika maisha haya ni KUFUZU kuwa sehemu ya ufalme wa Mungu.

Je, wewe utakuwa sehemu yake?

Mustakabali Wako wa Kustaajabisha

Lifuatalo ni hitimisho la Herbert W. Armstrong kwa kijitabu chake Mustakabali Wako wa KustaajabishaJinsi Dini Inavyokudanganya:

“Wakati wa Kurudi Kwake duniani katika nguvu na utukufu wale walioongoka na walipokea Roho Takatifu ya Mungu watazaliwa katika Familia ya Mungu kwa ufufuo. Kisha ulimwengu wote utawekwa [utatiishwa] CHINI yao!

“Kisha, kutoka Warumi 8, ikiwa tunayo na tunaongozwa na Roho Takatifu ya Mungu, tutafufuliwa na kuwa waliofanyizwa kwa Roho na kutokufa katika Familia ya Mungu kama vile Kristo alivyokuwa mwaka 31 B.K. baada ya kufufuka Kwake.

“Kwa mara nyingine tena kutoka fungu la 19, ‘Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu’ (RSV). Jambo hili litatokea wakati wa ufufuo, wakati wale walio wanadamu hasa wanakuwa—kwa ufufuo au badiliko la kufumba na kufumbua kutoka kwa nyama yenye kufa na kuwa Roho isiyokufa—wana wa Mungu.

“Sasa elewa tafadhali. Kwa nini ulimwengu wote—uumbaji—uwe unasubiri kwa shauku nyingi kwa ajili ya kuzaliwa halisi na kuonekana kwa hawa wana wote wa Mungu, kuzaliwa katika Familia ya Mungu? Mafungu yafuatayo yanaonyesha ulimwengu uliojawa na sayari zikiwa katika kuharibika na ubatili—bado kana kwamba sasa zimewekwa katika hali ya kufa kwa tumaini! ‘Kwa maana uumbaji wenyewe [ulimwengu ambao sasa hauwezi kuhimili maisha] utawekwa huru kutoka utumwa wake wa uharibifu na kuufikia uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu...

“Aya hii inaonyesha kwa ufanisi kile ambacho wanaanga wote na uthibitisho wa kisayansi unaonyesha—ma-jua ni matufe ya moto, yakitoa mwanga na joto; lakini sayari ziko katika hali ya kufa, kuoza na ubatili, isipokuwa hii dunia—lakini si milele—zikingoja mpaka wanadamu walioongoka WANAZALIWA watoto wa Mungu; wakizaliwa katika ile Familia ya Mungu ya Kiungu, wakiuunda Ufalme wa Mungu.

“Injili ya Yesu” ilikuwa ni Ufalme wa Mungu. Injili ya Kristo ya Ufalme hakika inajumuisha maarifa yote yaliyofunuliwa hapa—hata ulimwengu mzima utatawaliwa na sisi, ambao, pamoja na Mungu Baba na Kristo, tunakuwa Ufalme wa Mungu.

“Mungu kwanza ni Muumbaji, lakini Mungu pia ni Mtawala. Na ni Mwelimishaji, anayefunua maarifa yaliyo ng’ambo ya pili na nje ya uwezo wa fikira za mwanadamu kwa zenyewe kutambua!

“Yaweke pamoja maandiko haya yote katika kijitabu hiki, na utaanza kuelewa uwezekano wa kushangaza wa mwanadamu. Uwezekano wetu ni kuzaliwa katika Familia ya Mungu, tukipokea nguvu kamili! Lazima tupewe mamlaka juu ya ulimwengu wote!

“Tutakwenda kufanya nini basi? Maandiko haya yanaonyesha tutatoa [gawa] maisha kwa mabilioni ya sayari zilizokufa, kama maisha yalivyotolewa kwenye dunia hii. Tutaumba, kama Mungu atakavyoongoza na kuagiza. Tutatawala milele yote! Ufunuo 21 na 22 zinaonyesha hakutakuwa na maumivu tena, hakuna mateso, hakuna maovu, kwa sababu tutakuwa tumejifunza kuchagua njia ya Mungu ya mema. Yatakuwa ni maisha ya milele ya mafanikio, wakati wote tukitazamia kwa furaha isiyo kifani tukitegemea mradi mpya wa uumbaji, na bado tukiangalia nyuma pia kwenye yaliyofanikishwa pamoja na furaha juu ya kile tutakachokuwa tumekamilisha tayari.

“Kamwe hatutachoka na kudhoofika. Wakati wote tutakuwa hai—tukijawa na nguvu ya furaha tele, afya, maisha yenye kuchangamka sana na uimara na nguvu!

“Uwezakano wa jinsi gani!”

Pengine ungependa kusoma: