Mnamo mwaka 1966, Mungu alipoanza kuniita katika kweli yake, nilipata bahati ya kukutana na Mbunge wa Bunge la Marekani kutoka jimbo langu la Ohio. Nilikuwa nimeomba kujiunga na shule ya Jeshi la Majini la Marekani na waombaji wote walipaswa kukutana ana kwa ana na Mbunge wao katika hatua za mwisho kabla ya kuchaguliwa. Mwishoni mwa usaili, aliniuliza kama ningelipenda kumwuliza maswali yoyote. Huyu alikuwa ni mtu aliyeheshimiwa sana, Mbunge wa muda mrefu akinipa fursa ya kumwuliza swali lolote lililokuwa akilini mwangu.
Nilikuwa na swali moja tu.
Nilikuwa nikijifunza juu ya serikali isiyo ya kibinadamu, yenye kutawala dunia nzima, inayokuja hivi karibuni, itakayosimamishwa wakati wa Kurudi kwa Yesu Kristo. Nikiwa na jambo hili akilini mwangu, nilimwuliza Mbunge maoni yake juu ya serikali moja ya ulimwengu mzima, kama ingekuwa katika mikono ya wanadamu. Jibu lake lilikuwa la haraka na la msisitizo, “Siamini kwamba itafanikiwa, lakini kama ningekuwa naamini, ningepaaza sauti yangu kutoka juu ya mapaa ya nyumba.” Kisha akaendelea kutoa maoni mbalimbali.
Hili liliniachia ushawishi wa kudumu. Sijaweza kusahau mazungumzo yangu na mbunge huyu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka thelathini katika serikali ya muungano.
Tangu wakati huo, wengi wamependekeza kwamba serikali moja ya ulimwengu mzima ndiyo njia pekee ya kuuokoa ustaarabu. Lakini maswali mengi yanaibuka. Ni nani ataileta? Je, ni hatua gani zitafuatwa? Itasimamia sheria zipi? Sheria hizo zitatekelezwaje? Je, serikali za mataifa zitaachia madaraka yao kwa serikali hii? Je, itafanikiwa, au hatimaye itawagandamiza na kuwafanya watu wote watumwa? Maswali haya daima huwaacha wakikuna vichwa wenye kufikiria, wanamipango, viongozi na wanasayansi katika harakati za kutekeleza majukumu yao.
Injili ni Nini?
Yesu alisema, “Tubuni na kuiamini injili” (Marko 1:15). Lakini injili ni nini? Wengi hawajishughulishi na swali hili. Ukweli wa injili umefichwa mbali na upeo wa wengi wanaodai kuwa Wakristo. Tangu karne ya kwanza kumekuwepo na njama ya kuwadanganya Wakristo watarajiwa kuhusu maana ya injili. Jambo hili linatisha, lakini hivyo ndivyo ilivyotokea.
Wengi wanaamini kuwa injili ni juu ya habari za Yesu Kristo. Ni kweli kwamba jukumu la Kristo ni kubwa, lakini yeye siyo injili. Biblia inaonyesha kuwa Yesu Kristo huhubiriwa sambamba na injili.
Wengine hutangaza “injili ya wokovu” au “injili ya neema.” Bado wengine wanaamini “injili ya miujiza” au “injili ya mahusiano ya jamii” au “injili ya vyakula” au ya “uponyaji” au “imani.” Pia, wapo wengine ambao hufikiri juu ya “muziki wa injili” mara neno injili linapogonga akilini mwao. Hizi zote ni fikira za kibinadamu na si kile ambacho BIBLIA husema!
Angalia maelezo ya Marko kwa mara nyingine! “Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya akihubiri injili ya ufalme wa Mungu” (1:15). Hiyo ndiyo injili ambayo Yesu alihubiri. Ni katika muktadha huu alisema, “Tubuni na kuiamini injili,” Injili gani?—ya UFALME WA MUNGU.” Fungu la kwanza hurejelea ujumbe huu huu linaposema, “Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo.” Injili ya Yesu Kristo ilikuwa juu ya UFALME WA MUNGU—si kitu kingine! Ili mtu aokolewe ni lazima aamini na kuielewa injili hiyo—si ya bandia au mbadala.
Onyo Kali Kutoipotosha Injili
Ukweli wa somo hili ni wa muhimu mno kiasi kwamba Mungu alimvuvia Paulo kuwaonya Wagalatia kipindi kile—na sisi leo: “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini, ijapokuwa sisi au malaika kutoka mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe” (1:6-9).
Hii ni kauli nzito sana! Katika sura inayofuata (2:5), Paulo alienda mbele kusisitiza tumaini “kwamba kweli ya injili ikae pamoja nanyi.” Kwa hiyo ipo injili ya kweli, na zingine zote batili.
Ni wazi kwamba, Paulo hakufundisha injili nyingine tofauti au injili ya nyongeza, kama wengine wanavyodai. Kinyume chake, Mungu alimtumia kuonya dhidi ya kuruhusu fundisho hilo la uongo. Na hata alitamka laana (1:8) kwa mtu awaye yote, malaika au hata mtume—“Lakini, ijapokuwa sisi [mitume]…atawahubiri ninyi injili yoyote”—anayechagua kuvunja amri hii. Andiko lenye nguvu kiasi gani!
Paulo alieleza zaidi kuwa mitume waliaminiwa na Mungu kuihifadhi injili ya kweli. Angalia 1 Wathesalonike 2:4: “Bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.” Huu ni wajibu ambao hauwezi kuchukuliwa kirahisi. Watumishi wa kweli daima hufundisha kile ambacho Mungu anaamuru, si kile “kinachowapendeza wanadamu” au “wasomi” wa Biblia. Kwa hiyo fikira yoyote kwamba Paulo alifundisha injili nyingine (ambayo hudhaniwa kuwa juu ya Kristo) ni upuuzi. Kwa hakika angekuwa anatamka laana juu yake yeye mwenyewe!
Wale wote wanaohubiri injili ya uongo hutangaza laana juu yao wenyewe bila kufikiri. Kwa nini watu hawaogopi kufanya hivi? Makanisa mengi ya Kikiristo hayawezi kukubaliana juu ya nini ndiyo injili.
Kwa nini?
Kristo alisema injili ilikuwa juu ya ufalme wa Mungu, na kwa sababu watu hawajui ufalme wa Mungu ni nini, wamehitimisha kuwa ufalme unaweza kuwa ni kanisa fulani, dhehebu au Ukristo kwa jumla. Wengine huushusha chini hadi “hisia yenye kusisimua” katika “mioyo ya watu.” Bado wengine huamini kuwa ni “milenia” au hata “Himaya ya Uingereza.” Wengine hata wamefikia hitimisho kuwa ufalme wa Mungu si kwa ajili ya wanadamu leo!
Ujinga wa kushangaza kiasi gani!
Walio wengi wamedanganywa (Ufu. 12:9) na mungu wa dunia hii (2 Kor. 4:4), anayewatumia watumishi wake kusambaza injili ya uongo yenye kujulikana sana, kuhusu habari za Yesu, badala ya ujumbe juu ya ufalme wa Mungu, ambao Kristo aliuleta.
Angalia 2 Wakorintho 11:13-15, ambapo Paulo aliandika, “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki…”
Hili ni andiko la wazi, lenye kushtua. Bado ni kweli kwamba shetani anao watumishi wanaoonekana kama watumishi wa Mungu.
Mafungu yafuatayo yanaendeleza maelezo ya Paulo kuhusu kazi ya watumishi wa uongo. Angalia: “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, fikira zenu zisijezikaharibiwa, mkauacha urahisi au wepesi ulio katika Kristo. Maana yeye ajaye [akizungumzia wahubiri wa uongo] akihubiri Yesu mwingine…au mkipokea roho nyingine…au injili nyingine msiyoikubali…” (fungu 3-4). Kama Kristo NI injili, sasa kwa nini “Yesu mwingine” na “injili nyingine” yaliorodheshwa kama matatizo mawili tofauti?
Watu wanatakiwa waamke dhidi ya udanganyifu—madanganyo makuu—ya kile kinachodhaniwa ni Ukristo unaokataa karibu KWELI ZOTE ZILIZO WAZI za Biblia! Mpango wa Mungu kwa ajili ya wanadamu ni wa ajabu—usioweza kulinganishwa na kitu chochote ambacho wanadamu wamewahi kukibuni na kukiweka badala ya kile asemacho Mungu. Ulimwengu unapuuzia maandiko yaliyo wazi, bila kificho, yasiyoweza kukosewa, yanayopatikana katika Biblia nzima juu ya ufalme wa Mungu.
Kijitabu hiki kinaeleza ukweli wa kustaajabisha unaopuuziwa na wengi sana!
Ujumbe wa Kristo—Tangazo la Mbele
Akiwa mleta habari wa mbele, mbali sana kabla ya wakati wake, Kristo alikuja kutoa tangazo juu ya badiliko kamili kuhusu namna ambavyo siku moja ulimwengu utatawaliwa. Badiliko hili litaambatana na amani ya dunia isiyo kifani, furaha, umoja, afya kwa wote na mafanikio.
Kila mahali alikokwenda, Kristo aliongea juu ya ufalme wa Mungu. Lilikuwa ni somo kubwa katika mingi ya mifano yake. Alipowaagiza wale mitume kumi na wawili na kuwatuma kuhubiri, maelekezo yalikuwa ni kwenda kufundisha ufalme wa Mungu (Luka 9:1-2). Baadaye alipowatuma wanafunzi wake sabini (Luka 10:1), aliwaamuru pia kuhubiri ufalme wa Mungu (Fu. 9). Paulo alihubiri ujumbe huu huu juu ya ufalme wa Mungu kila mahali alikokwenda (Matendo 19:8; 20:25; 28:23, 31). Maneno ufalme na ufalme wa Mungu yanapatikana mara nyingi sana katika Agano Jipya lote. Lakini, inashtusha kuona namna gani karibu kila mmoja amepoteza maarifa na maana hasa ya ufalme huu.
Neno “injili” limetafsiriwa kutoka neno la Kiingereza cha zamani “gospel” lenye maana ya “god spell’ yaani habari njema. Neno “ufalme” pia limetafsiriwa kutoka neno la Kiingereza cha zamani “Kingdom” lenye maana rahisi ya serikali. Kwa usemi mwingine Kristo alihubiri “habari njema ya serikali ya Mungu.” Kuja kwa amani ya dunia, furaha, afya na vyakula tele kwa hakika itakuwa ni habari njema kwa wanadamu ambao hawajawahi kuijua kwa miaka 6,000.
Wanafunzi wa Kristo walimwuliza nini itakuwa ISHARA ya kuja kwake na ya mwisho wa zama (Mt. 24:3). Aliwaonya mitume dhidi ya udanganyifu kutoka kwa wengi ambao wangekuja “katika Jina Lake,” wakisema, “Kristo alikuwa Kristo” (fu. 5). Alimaanisha kuwa watatilia mkazo juu ya MAISHA yake Kristo badala ya UJUMBE aliouleta. Lakini, pia alitabiri kuwa “habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule MWISHO utakapokuja” (fu. 14).
Sasa tuko katika siku za mwisho. Kumbuka, kama ufalme wa Mungu ungekuwa umehubiriwa katika karne zote, kutoka wakati wa Kristo hadi leo, kuutangaza sasa kusingekuwa ishara kwamba ulimwengu umefikia zama za mwisho. Wazushi na viongozi wa uongo walihafifisha uhubiri wa injili ya kweli kwa ulimwengu hadi karne ya 20. Kuanzia mwaka 1934, Herbert W. Armstrong alianzisha utimilifu wa unabii huu. Unaendelea leo—Kanisa Rejeshwa la Mungu linahubiri injili hii.
Maisha Baada ya Kifo?
Lakini Kristo alipoongelea “ufalme,” alimaanisha nini? Injili ya ufalme wa Mungu ina vipengele viwili.
Wengi huzungumzia wokovu—imani katika kile kilichoko baada ya maisha. Baadhi wamedhani kwamba injili ni juu ya “kupokea uzima wa milele” pekee au fikira ya walio wengi ya “kwenda mbinguni” panapo kifo. Ni kweli, Biblia ina mengi ya kusema juu ya wokovu. Kwa hakika, wokovu unahusiana moja kwa moja na—ni kipengele kimoja cha—injili ya ufalme wa Mungu. (Soma vijitabu vyetu Kuna Maisha Baada ya Kifo? na Ni Nini Thawabu Yako Katika Maisha Yajayo?)
Wengi hudhani kuwa Mungu anajaribu kuuokoa ulimwengu sasa—kwamba leo ndiyo nafasi pekee ya wokovu kwa watu wote. (Kijitabu cha tatu, Je, Biblia Hufundisha Majaaliwa?, kinaelezea kuwa Mungu hajaribu kumwokoa kila mtu sasa na kwa nini. Kinatoa muhtasari wa mpango wake mzima na makusudi kwa ajili ya mwanadamu.) Watu wengi hawafahamu kwa nini walizaliwa—kwa nini waliwekwa duniani. Pia, hawaelewi kwa nini mwanadamu hawezi kupata amani, furaha, afya na vyakula tele kwa juhudi zake mwenyewe. Ulimwengu mzima umedanganywa kuhusu wokovu, pia maswali na majibu nyeti kuhusu maisha. Kijitabu hiki kinauliza na kujibu mengi ya maswali hayo.
Kipengele kingine cha ufalme wa Mungu ni SERIKALI. Kama ilivyosemwa hapo awali, neno ufalme lina maana ya serikali. Ufalme wa Mungu unapowasili utapanuka kutoka “punje ya haradali” (Math. 13:31-32) na kuwa SERIKALI BORA itawalayo-ulimwengu mzima. Biblia huichambua serikali hii kwa undani. (Kujifunza undani wa kushangaza wa ujio wa Ufalme, soma kijitabu chetu cha bure Jinsi Ufalme wa Mungu Utakavyokuja – Kisa Ambacho Hakijawahisimuliwa!)
Ujumbe Kuhusu Serikali
Sehemu ya kijitabu hiki iliyobaki itaelezea kipengele cha “serikali” cha ufalme. Vijitabu vilivyopendekezwa hapo juu vinajikita kuelezea kipengele cha “wokovu.”
Kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, malaika alimtokea mama yake, Mariamu. Mafungu haya yanachambua tukio hili na kile alichoambiwa: “…malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda…Nazareti, kwa mwanamwali bikra aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikra huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema…utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita YESU. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na UFALME Wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:26-33).
Katika Yohana 18:36, Yesu alisema mbele ya Pilato, “Ufalme wangu [serikali] sio wa ulimwengu huu.” Pilato alimwuliza, “Wewe u mfalme basi?” Kristo akajibu, “Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni” (fu. 37).
Yesu alizaliwa kuwa MFALME!
Hivi ndivyo ilivyotabiriwa katika Isaya juu ya Kristo: “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na UWEZA WA KIFALME utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya ENZI yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na UFALME WAKE; kuuthibisha na kuutegemeza; kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele” (9:6-7).
Wakati Kristo atakaposimamisha serikali ya Mungu duniani, ndipo hatimaye italeta amani kwa mataifa yote!
Manabii Wote wa Mungu Walihubiri Injili
Wakati akihubiri katika kitabu cha Matendo, mtume Petro alitamka jambo la kustajabisha katika historia ya Biblia, lakini undani wake ni kama haujulikani kabisa. Alizungumzia wakati “…zitakuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani: ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya [urejeshaji] vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu” (Matendo 3:19-21). Bila shaka, mbingu zimempokea Kristo “hata” urejeshaji wa vitu vyote. Lakini urejeshaji huu bado haujatokea—hivyo, neno “hata.”
Fikiria! Kila mmoja (“wote”) wa watumishi wa kweli wa Mungu amehubiri kwamba wakati unakuja ambapo Kristo atarudi na “vitu vyote” “vitarejeshwa.” Kabla ya uasi wa Shetani, Serikali ya Mungu ilikuwepo duniani. (Soma kijitabu chetu Mwovu Ni Nani? kujifunza kuhusu uasi huu.) Kwa miaka maefu, Watumishi wa Mungu wametangulia kunena undani wa kurejeshwa kwa serikali ya Mungu duniani. Huenda ungependa kuchunguza kuona kama manabii wote wa Agano la Kale kila mmoja wao kwa namna moja au nyingine alitangaza kuja kwa ufalme wa Mungu na kufanywa upya vitu vyote. Nimeyasoma mafungu haya mara nyingi, nawe utaona kwamba wote walifanya hivyo. (Kijitabu chetu Injili ya Kweli Ni Ipi? Kinachunguza jambo hili kwa undani.)
Haya hapa ni maelezo kutoka Agano Jipya, yanayomrejelea mmoja wa wasemaji wa Mungu katika Agano la Kale.
Kitabu cha Yuda kina kumbukumbu ya mahubiri ya babu-mkuu wa Nuhu, Henoko. Ni kumbukumbu ya kile kilichosemwa zaidi ya miaka 4,500 iliyopita—hata kabla ya Gharika. Tilia maanani upana wa mafungu haya ya kushangaza: “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda…na kwa ajili ya maneno magumu yote…wenye dhambi… wameyanena juu yake” (fu. 14-15). Elewa maana halisi ya aya hii. Inafunua kwamba watakatifu (Wakristo wa kweli) wanakuja na Kristo kuuhukumu ulimwengu—kuwahukumu “wote” sawa sawa na matendo yao.
Biblia inayo mengi mno ya kusema juu ya ufalme wa Mungu kuliko vile ulivyowahi kudhani. Kwa mara nyingine tena, ukweli unashangaza kabisa—hata kushtusha—na hupaswi kutoufahamu.
Danieli Alielewa
Kama vile Henoko alivyoelewa kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa ni serikali halisi ambayo siku moja itatawala juu ya watu halisi na mataifa halisi duniani, ndivyo alivyokuwa nabii Danieli. Hakushikilia fikira za uongo kwamba ufalme ulikuwa aina ya “hisia za kimakosa” au “hisia za kusisimua” zilizo ndani ya “mioyo ya watu.” Kupitia mfuatano wa ndoto na njozi (1:17), Mungu alimtumia kueleza ufahamu maalumu juu ya namna gani na lini ufalme wake ungekuja duniani.
Yale yote ambayo Danieli alionyeshwa “yalifungwa na kutiwa muhuri mpaka nyakati za mwisho” (12:9). SASA tupo kwenye nyakati za mwisho—na kuna ushahidi mwingi juu ya hili. (Soma kijitabu chetu Hizi ndizo Siku za Mwisho? kuelewa zaidi juu ya namna unabii wa Danieli ulivyoandikwa ili ueleweke katika WAKATI WETU.)
Ujumbe wake ni kwa ajili yetu, leo! Danieli alitoa ripoti ya habari kubwa—KUBWA MNO—zitakazokugusa wewe katika siku za maisha yako! Tutaona kuwa Danieli pia alielewa na kuinena injili ile ile ambayo Kristo alihubiri—na ni muhimu mno tuelewe kile alichosema.
Danieli alitambua kuwa yeye alikuwa kinywa tu ambacho kupitia kwake MUNGU alikuwa akifunua Mpango wake Mkuu. Katika sura ya pili, alikuwa akiongea na Mfalme wa Wakaldayo (Wababeli) Nebukadreza juu ya mambo ambayo yaliyomfika mfalme katika ndoto. Nebukadreza alikuwa mfalme wa himaya kubwa aliyoitawala karibu miaka mia sita kabla ya wakati wa Kristo.
Waganga katika mahakama ya mfalme hawakuweza kufunua kile ambacho Mungu aliweza kukifunua kupitia kwa nabii wake Danieli. Lilikuwa ni kusudi la Mungu kufunua, kupitia mfalme huyo mpagani, kuwa kuna Mungu Mkuu aliye hai atawalaye ulimwengu wote na wafalme wote, serikali na mataifa juu ya nchi hatimaye yatamtii. Mfalme Nebukadreza mwenye hekima ya kibinadamu hakuwa na maarifa kupita wafalme wengine wa hapo awali na miungu yao mingi ya uongo. Lilikuwa ni kusudi la Mungu wa kweli kufunua uwepo wa serikali YAKE inayotawala ulimwengu mzima. Pia, alikusudia kuweka wazi KUSUDI LAKE KUU la kuileta serikali hiyo duniani “katika siku za mwisho.”
Tumia muda kusoma kwa uangalifu Danieli 2:28-44. Unabii huu wa kushangaza ulioandikwa kwa mapana na marefu hufunua vitu vingi juu ya kusudi la Mungu la kurejesha serikali yake duniani—pamoja na mtiririko wa matukio katika kutimia kwa jambo hili.
Mafungu kadhaa ya mwanzo yanachambua sanamu ya jitu kubwa. Mafungu ya 32-33 husema, “Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.”
Ni wazi kwamba hii ni sanamu ya mtu, lakini iliyotengenezwa kwa sehemu nne tofauti. Mafungu ya 34-35 hatimaye huelezea “jiwe lisilokuwa la kawaida lililoipiga sananu [na] likawa mlima mkubwa, na kuijaza dunia yote” (fu. 35). Angalia kwamba fungu la 34 husema kwamba jiwe “likachongwa bila kazi ya mikono,” kwa sababu ni Mungu, na si mwanadamu, aliyekuwa amelitengeneza.
“Jiwe” liliiponda ponda sanamu ile na kuchukua mahali pake, likaenea na hatimaye kufunika mataifa yote—“dunia nzima.” Hiki si kingine bali ni maelezo juu ya SERIKALI YA MUNGU ikija duniani. Danieli anatangaza ujumbe ule ule wa injili ya ufalme ambayo Kristo alihubiri.
Huhitaji kuniamini mimi, kwa sababu hiki ndicho ambacho Biblia yako inakisema. Hakuna mtu mwenye kuhitajika kukufafanulia mafungu haya.
Wewe angalia tu fungu la 37. Linasema wazi, “Wewe, Ee Mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu.” Fungu la 38 linafafanua, “Wewe u kichwa kile cha dhahabu.” Ni lazima tuiache Biblia ijitafsiri yenyewe wakati wote.
Mafungu ya 39-40 yanaendelea kuchambua falme tatu zinazofuatana ambazo zingefuatia ufalme wa Nebukadreza na Babeli. Haya ni maarifa ya ajabu ambayo karibu kila mtu duniani leo hii haelewi.
Mafungu haya yanaonyesha mfuatano wa kihistoria wa MILKI ZA DUNIA zilivyowakilishwa na madini ya aina tofauti yaliyotengeneza sanamu ile kubwa. Hizi ni falme halisi: (1) Wakaldayo-Himaya ya Babeli ya dhahabu, (2) Himaya ya Wamedi na Waajemi ya fedha, (3) Himaya ya Ugiriki na Makedonia ya shaba, na (4) Himaya ya Rumi, iliyotengenezwa kwa chuma kilichochanganyika na udongo wa mfinyanzi inapoonekana mara ya mwisho. Ujumbe kutoka kwenye historia ni kwamba falme (himaya) hizi nne zilitawala, na ufalme wa nne utatawala tena na kuathiri ulimwengu, lakini hatimaye utahitimishwa na ufalme wa Mungu Duniani.
Kwa uwazi Mungu anatufunulia sasa kwamba ni yeye anayesimamisha na kuondoa—na husimamisha na kuondoa, tena na tena—serikali za dunia (falme).
Kufasili Ufalme
Wengi huuliza, “Lakini ni nini hasa fasili ya ufalme kibiblia?” Wahubiri na wanatheolojia wamejaribu kuifanya maana ya jambo hili kuwa ya kiroho, kwa sababu hawajachunguza kwa makini fasili ya Mungu.
Hii inapatikana mwishoni mwa fungu la 39, linalorejelea kwa falme hizi “zitakazoitawala dunia yote.” Hii haiwezi kuhusishwa na fikira isiyo wazi ya ufalme ndani ya “mioyo ya watu.” Vile vile hakuna namna ya kuifanya fasili hii iwe ni kanisa fulani au makanisa. Inaongelea utawala wa serikali zenye mamlaka juu ya mataifa halisi duniani—na juu ya watu halisi. Je, utamruhusu mtu fulani akuambie vinginevyo au utaiamini fasili ya Biblia kuhusu ufalme? Kumbuka, falme hizi “zitaitawala dunia yote”!
Tilia mkazo mambo mawili muhimu yahusuyo sanamu hii kubwa ya madini mbalimbali iliyoelezewa hapa. Kwanza, madini yanapungua THAMANI kadri tunavyoshuka kutoka kichwani kwenda miguuni na hatimaye nyayo za sanamu. Hii inamaanisha kuwa ubora wa kila ufalme/himaya ni hafifu kithamani kuliko ule ulioutangulia. Kwa maneno mengine, nguvu na upana wa kila ufalme/himaya unaofuata ni kubwa kuliko ule ulioutangulia.
Hatimaye angalia kwamba miguu miwili ya chuma inawakilisha ufalme uliogawanyika. Ni kweli Himaya ya Kirumi ilikuwa imegawanyika ikiwa na makao makuu mjini Roma na Konstantinopo. Nusu ya nyayo ni chuma na nusu ni udongo wa mfinyanzi. Chuma hakiwezi na wala haitatokea kuchangamana na udongo wa mfinyanzi, hii ni picha kwamba ufalme huu hautakuwa imara hapo mwishoni. Nyayo zinapovunjika, jitu hili kubwa litaanguka. Inatakiwa kujifunza kwa makini sura tatu ili kuelewa kikamilifu namna falme hizi nne zilivyofuatana.
Linganisha Ufunuo 13 na 17 na Danieli 7. Kwa pamoja, zinaelezea unabii wa kushangaza na wenye nguvu kuhusu matukio ya siku za mwisho—matukio ambayo yatatuathiri wewe na mimi katika siku za maisha yetu! Ufunuo 17:8 huelezea “mnyama” anayepanda kutoka “kuzimu” na anayeendeshwa na “mwanamke.” Fungu la 12 linaonyesha kuwa mnyama huyu anajumuisha WAFALME KUMI watakaopokea mamlaka na kuungana chini ya kiongozi mwenye haiba kubwa atakayetwaa jukumu la “mnyama.” Wengi wanafikiri kiongozi huyu ni yule ambaye ulimwengu unamsubiri. Lakini atakuwa ni wa nane, na kufufuka kwa mara ya mwisho kwa mfumo wa Kibabeli utakaodumu muda mfupi—unaotanguliwa na ule wa mara ya saba, ambao utaibuka huko Ulaya wakati wa kipindi cha Ufalme wa Mungu ulio kama punje ya haradali.
Nguvu hii kuu katika Ulaya inakuja na iko hapa karibu mbele yetu. Ni muhimu mno kwamba ufahamu unabii huu una maana gani! (Soma kijitabu chetu kipana Mnyama wa Ufunuo ni Nani au ni Nini?)
Kitu cha ajabu kinatokea “katika siku za wafalme hawa” (Dan. 2:44). Kuwasili kwa Kristo kunaondoa shaka yote juu ya NINI hasa ni ufalme wa Mungu. Danieli 2:44 inasema, “Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake [Mungu kamwe hataruhusu watu kuchukua utawala], bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele.” Bila shaka hii ni baada ya kipindi cha punje ya haradali kilichoelezewa kabla. Mabadiliko haya makubwa hayawezi kuwa sawa kama mwanzo wa Ufalme wa Mathayo 13.
Hiyo ni sawa! Mungu—siyo wanadamu—atasimamisha himaya ya mwisho iliyo kuu kuliko wakati wowote yenye kutawala dunia nzima. Na anatuambia kwamba hataruhusu mapendekezo ya wanadamu kuingilia na kuiharibu, maana “itasimama milele,” Ahadi hii ni AMINI. Itatokea—bila kujali wanadamu wanaiamini au hawaiamini!
Mathayo 6:33 inasema, “Bali utafuteni KWANZA ufalme wa Mungu na haki yake…” Ikiwa utatafuta kitu fulani kama lengo lako la kwanza na mtazamo wako katika maisha, ni lazima ujue kwa hakika ni kitu gani hicho!
Sura hii ina kile ambacho watu hukiita “Sala ya Bwana” (fu. 9-13). Kristo aliwaagiza Wakrtisto kusali “hivi,” na anaendelea kwa kuongeza usemi, “Ufalme wako uje.” Kujua kile unachokiomba kutafanya maombi yako yawe na maana zaidi!
Kuna Mambo manne ya lazima kwa ufalme wowote: (1) Ardhi, milki au nchi—japo iwe kubwa au ndogo. Kwa maneno mengine, ni lazima pawepo na mipaka halisi inayotambulisha eneo la ufalme, (2) mtawala, mfalme, mtawala mkuu au gavana anayeongoza serikali, (3) watu au wananchi wanaoishi katika eneo la utawala, na (4) mfumo wa sheria na muundo msingi wa serikali.
Hakuna ufalme uliokamilika bila kuwa na mambo yote haya ya msingi.
Mwanamke wa Ufunuo 17
Kwa kulinganisha Danieli 7 na Ufunuo 13 na 17, inakuwa wazi kwamba kuna kufufuka [uhuishaji] mara saba kwa Himaya Takatifu ya Rumi, pamoja na mara ya nane ambacho ni kichwa “tofauti” kitakachoinuka katika kipindi kilichotabiriwa katika Ufunuo. Sita vimekuja na kupita—na cha saba sasa kinajiunda! Kuhuishwa kwa mara ya nane kutadumu kwa miaka mitatu-na-nusu kamili (Ufu. 11:2, 3; 12:14; 13:5), pamoja na muhuri wa tano ukihusisha ile Dhiki na Ghadhabu ya Mungu.
Tambua kiungo kingine muhimu kwa hizi fufuko za mfumo wa Kirumi. Ufunuo 17 inaeleza kila mmoja ukiwa na “mwanamke a[nayeketi] juu ya MNYAMA mwekundu, aliyejaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi” (fu. 3). Vichwa saba ni kuibuka mara saba kulikotengana pamoja na kuibuka kwa mara ya mwisho kuliko na pembe kumi (kulikoundwa na wafalme kumi wakiwa na mmoja aliye mkuu—yule Mnyama) anayekuwa wa nane.
Kuhusu huyu mwanamke, mafungu ya 5-6 yanasema, “Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu”. Fungu la 1 linamwita “kahaba mkuu anayeketi juu ya maji mengi…”
Hebu tusimame na tujiulize: “Maji mengi” ni nini?
Huu ni mfano halisi wa kuiruhusu Biblia ijitafsiri yenyewe. Mafungu kumi-na-nne baadaye, istilahi imefafanuliwa: “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha” (fu. 15). Hii inaonyesha kwamba ushawishi wa kahaba unaikumba Dunia yote.
Katika hali hii, istilahi haikufafanuliwa mara moja, lakini kwa kuendelea kusoma tu ilifunua maana yake. Biblia ilijitafsiri yenyewe!
Mafungu ya 5-6 ni maelezo ya picha ya kile ambacho leo ni kanisa kubwa la Kipagani ambao ni mzao wa leo wa Babeli. Yeye ni “mama” wa mabinti “makahaba” wengi, waliotoka kwake katika upinzani kwa sababu hawakukubaliana na baadhi ya machukizo yake. Hili sio kanisa dogo, bali ni kanisa “kubwa” linalotawala watu wengi. Ufunuo 17 inaonyesha kurejea kwa mfumo huu lakini sio kanisa lile lile ambalo kwa hakika litakuwa limetoweka muda mrefu kabla Ufalme wa Mungu haujawasili. Fungu la 2 linaongelea juu ya “uzinzi” wake na “wafalme wa nchi.” Na fungu la 18 linamwongelea mwanamke kama “mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.” Huu ni mfumo mkubwa ambao umetafuta kuyaathiri mataifa na matukio ya ulimwengu. Ni mji mmoja tu unaolingana na maelezo haya kwa kipindi zaidi ya miaka 3,000 iliyopita—Yerusalemu—ijapokuwa mfumo huu kwa sasa uko kwenye mji mwingine.
Mwanamke wa tofauti kabisa, kama tulivyoona akielezewa katika Ufunuo12 kama Kanisa la Mungu, ameteswa na hili kanisa kuu la uongo kwa takriban miaka 2,000 (17:6).
Muda mchache umebaki kabla ya kuibuka kwa mara ya saba hakujatokea katika wakati wetu, huku Ufalme wa Mungu wa ajabu kuonekana ukianza kama punje ya haradali.
Kuuingia Ufalme
Biblia hufundisha kwamba ufalme wa Mungu hutawala JUU ya watu na mataifa ya
dunia. Kwa hakika mataifa siyo sehemu ya ufalme, kama ilivyo kwa wananchi wa kawaida wa nchi yoyote wasivyokuwa sehemu ya serikali inayotawala juu yao. Ni lazima mtu AUINGIE ufalme wa Mungu ili awe sehemu yake. Kwa hiyo, ni lazima tujiulize: Tofauti na wale wanaotawaliwa na serikali hii, ni nani hasa aliye KATIKA ufalme wa Mungu?
Katika 1Wakorintho 15:50-51, Paulo alisema, “Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika, angalieni nawaambia ninyi siri…” Bila shaka, hii ni siri karibu kwa kila mtu—kwamba mwanadamu wa nyama na damu hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Itasaidia zaidi kuisoma yote hii “sura ya ufufuo” ya 1 Wakorintho 15. Ni katika ufufuo tu wanadamu (Wakristo wa kweli) wanabadilishwa (wanazaliwa mara ya pili) kutoka nyama kuwa roho.
Je, unaona basi namna ambavyo hakuna kanisa lenye uwezekano wa kuwa ufalme wa Mungu? Makanisa ni vitu vilivyodhahiri. Wanadamu wa nyama na damu wanaweza kuingia ndani na kutoka nje ya jengo la kanisa. Hivyo, hii inayafungia nje makanisa yote (au, kwa mantiki hiyo, Dola ya Uingereza) yasiwe ufalme wa Mungu. Amini tu ukweli dhahiri wa Biblia!
Ufalme wa Mungu hauwezi kujumuisha watu wa nyama na damu!
Mfuatano wa mafungu katika Yohana 3 mara nyingi haueleweki kwa wale wanaoamini kwamba wanaweza “kuzaliwa mara ya pili” katika maisha haya (wakiwa wangali nyama na damu) na wakauona ufalme wa Mungu.
Katika maelezo haya, Nikodemo, Farisayo, alimwendea Kristo akikiri katika fungu la 2: “Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu.” Alikiri waziwazi kwamba walijua Kristo alikuwa nani na nani alimtuma duniani. Angalia kwamba Nikodemo aliongea kwa niaba ya wengi aliposema, “twajua.” Alikuwa akimaanisha yeye na mafarisayo wengine waliotambua ni nani na nini Kristo alikuwa. Hawakuweza kukana uweza wa Mungu uliodhihirika katika miujiza ambayo Kristo aliitenda.
Viongozi wa kidini, Mafarisayo, walielewa fika kwamba alikuwa “mwalimu aliyetoka kwa Mungu” akiileta kweli. Bado walimwita mjadhambi (mwenye kukufuru), mlevi, mzushi, haini, mwanaharamu, mwenye pepo, nabii wa uongo na zaidi—na wakamsulubisha!
Watu wengi huuona ukweli wa Biblia waziwazi, lakini bado huchagua kuupuuza wapate kuyashika mapokeo na fikira zao wenyewe (Marko 7:7)!
Kristo alimwambia Nikodemo, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (fu. 3). Alieleza kwamba ni kwa kuzaliwa mara ya pili tu ndipo yeyote ataweza “kuuona” ufalme wa Mungu. Kwa hiyo, kuna mpaka juu ya nani anaweza kuuona ufalme. Lakini hakuna mpaka kwa watu wenye mwili kuona kanisa au himaya. Mtu yeyote wa dini yoyote au imani anaweza kuona kitu kingine chochote.
Elewa mambo haya nyeti ambayo Kristo anayabainisha!
Katika fungu la 5, Kristo alisema kuwa isipokuwa mtu “amezaliwa kwa maji na kwa roho,” hawezi “kuingia katika ufalme wa Mungu.” Ndiyo, ufalme ni kitu ambacho kinaweza “kuingiwa”—lakini alielezea kauli yake ya “kuzaliwa kwa maji [ubatizo] na kwa Roho” katika fungu la 6: “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho NI roho.”
VITHIBITISHO SABA Ufalme wa Mungu Hauko Duniani Sasa!
Wengi wa wanaojidai kuwa Wakristo husoma kimakosa Luka 17:21 na Wakolosai 1:13 na kuhitimisha kwamba ufalme uko duniani sasa ama katika mfumo wa Kanisa au “katika mioyo ya watu.” Kisha wanahitimisha kuwa ni “wajibu wao wa Kikristo” kuueneza kwa njia ya upendano wa ndugu, kuvumiliana, n.k.
Japokuwa imani hii iwe inatoka kwenye moyo safi kiasi gani, si ya kibiblia. Ilikuwaje basi watu wakafikia hitimisho hili la uongo?
Hizi hapa ni sababu kubwa mbili:
Kwanza, hawaiachi Bibiblia iitafsiri Biblia. Badala ya kusikiza 2 Petro 1:20, “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu,” wanayapa mafungu ya Biblia maana walizozifikiria kabla. Pia, hawairuhusu Biblia kuwafundisha, kuwaonya, kuwasahihisha au kuwaelekeza (2 Tim. 3:16-17).
Pili, wanauwekea kikomo ufahamu wao katika kila mada kwa kusoma fungu moja au mawili, na kuyatoa nje ya muktadha. Pia, wanapuuzia mafungu mengine mengi ambayo yangeonyesha “taswira kubwa” ya kile ambacho hasa Biblia hufundisha. Ili kuilewa Biblia katika fundisho lolote, ni lazima mtu atafiti mafungu yote juu ya somo husika. Hakuna fungu moja linalobeba maana na uelewa wote kwa somo lolote.
Isaya 28:9-10 husema, “Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii?...Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.” Kwa busara yake, Mungu aliipangilia Biblia iwe kama mchezo-fumbo (wa kupanga vipande ili kupata picha kamili): Wakati wote, weka mafungu yote yanayohusiana katika Biblia nzima pamoja.
Hebu tuchunguze vithibitisho saba vinavyoonyesha kuwa ufalme wa Mungu hauko duniani sasa.
MOJA: Ufalme wa Mungu Umo Ndani Yenu?
Katika Luka 17:20-21 Kristo alisema, “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza: wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
Wengi husoma fungu hili na kuhitimisha, “Kumbe! Ufalme wa Mungu umo ndani yangu.” Lakini je! Hicho ndicho hasa fungu hilo husema?
Kristo alikuwa anaongea na akina nani? Sehemu ya kwanza ya fungu la 20 hutoa jibu. “Na alipoulizwa na Mafarisayo, ufalme wa Mungu utakuja lini, Aliwajibu akawaambia…” Kristo alikuwa anaongea na Mafarisayo—siyo wanafunzi wake! Walimwuliza, “Ufalme Wako utakuja lini?”
Hili hapa ni jibu la Kristo: “Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” Inawezekana Kristo alimaanisha kwamba ufalme wake ulikuwa ndani ya Mafarisayo—watu aliowaita “wanafiki” na “viongozi vipofu,” ambao “waliyaacha mambo makuu ya sheria, hukumu, rehema na imani,” waliokuwa wamejaa “unyang’anyi na kutokuwa na kiasi,” waliokuwa kama “[makaburi] yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana mazuri, bali ndani [yamejaa] mifupa ya wafu, na uchafu wote” (Mat. 23:21, 23-27)?
Kwa msisitizo, HAPANA! Uchunguzi zaidi unaonyesha kuwa usemi “ndani yenu” ni tafsiri isiyo sahihi. Maelezo ya pembeni kutoka tafsiri Mpya ya King James husema, “miongoni mwenu.” Tafsiri ya Kingereza Kipya husema, “uko kati yenu.” Tafsiri ya Biblia ya Revised Standard Version husema, “katikati yenu.” Kristo alikuwa akiwaambia hawa watu wa mwilini kwamba ufalme wake ulikuwa katika uwepo wao. Kwa namna gani?
Kristo alikuwa anajirejelea yeye Mwenyewe. Aliwakilisha ufalme wa Mungu. Ingawa Kristo alikuwa mwanadamu wa nyama na damu, pia alikuwa Masiha. Akiwa amezaliwa ili kuwa mfalme, hakutenda dhambi au kwenda kinyume na mapenzi ya Baba. Kwa hakika alikuwa mwakilishi kamili wa serikali ya Mungu.
MBILI: Kufasili Ufalme
Falme zote hujumuisha vitu vinne: Miliki, Mfalme (au mtawala), wananchi, na sheria.
Kama ufalme wa Mungu upo hapa tayari, iwe kama Kanisa au ndani ya “mioyo ya watu”, basi dunia nzima ingekuwa chini ya utawala wake (Zek. 14:9).
Kama ufalme wa Mungu upo hapa tayari, Mfalme wake, Kristo, angekuwa ameketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi (Isa. 9:6-7), na kisha, kutawala kutokea Yerusalemu (Zek. 8:3). Angalia: Yerusalemu maana yake ni “Jiji la Amani.” Lakini dunia ya leo imechafuka kuliko wakati wowote, ughaidi, miji iliyosambaratika kwa vita! Ni wazi Kristo hatawali kutokea pale sasa.
Kama ufalme wa Mungu upo hapa tayari, watawaliwa wake (wanadamu wote) wangeishi chini ya utawala wa Kristo. Hata nchi za Mataifa kama vile Misri wangetakiwa kumtii—la sivyo waadhibiwe (Zek. 14:16-19) mara ufalme unapohamia Sayuni (Mika 4:8). Hali sivyo ilivyo sasa.
Kama ufalme wa Mungu upo hapa tayari, sheria zake zingejulikana na kila mwanaume, mwanamke na mtoto katika dunia nzima. Karibu kila mtu angekuwa anaelekea kwenye utii. Hakuna yeyote ambaye angesema yeye hazifahamu sheria zake (Isa. 30:21; Yer. 31:34). Hili halijatokea bado.
TATU: Kuuona Ufalme
Katika Yohana 3:3, Kristo alimwambia Nikodemo, Farisayo, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Akiwa amechanganyikiwa, Nikodemo alijibu, “Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu…Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu” (fu. 4-5)
Ili kuuona na kuuingia ufalme wa Mungu, ni lazima uwe roho. Paulo aliandika, “Nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu” (1 Kor. 15:50)!
Kristo aliendelea kueleza kwamba Roho i kama upepo. Haionekani. Huwezi kuiona. Lakini wanadamu ni nyama na damu, na wanaweza kuonekana.
Wale ambao “wamezaliwa mara ya pili” watafanana na Kristo (1 Yohana 3:2). Hakuna mwanadamu mwenye mwili anayeonekana kama yeye alivyo mbinguni leo: “Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi… na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake” (Ufu. 1:13-17).
Je! Unamfahamu yeyote anayeonekana na kuongea namna hii sasa?
Pia tunapaswa kuzingatia kwamba ufufuo (wakati watumwa wa Mungu “wanapozaliwa mara ya pili”) hautatokea mpaka hapo Kristo atakaporudi
(1 Kor. 15:50-54). Kama ufufuo huu ungekuwa umeshatokea, ulimwengu mzima ungefahamu. Hakuna uwezekano wa yeyote kulikosa tukio hilo (Mat. 24:23-27).
NNE: Amani ya Dunia Sasa?
Isaya 9:6-7 linasema hivi juu ya Kristo, “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe.”
Angalia mitandao, soma majarida na magazeti ya habari za kitaifa. Je, ulimwengu huu unafaidi amani? Je! Unaamini Kristo angeruhusu mauaji, ubakaji, unyanyasaji wa watoto, migomo, ugaidi na vita chini ya utawala wake wa kiungu?
Hapana! Ni wazi, Kristo—Mfalme wa Amani—hajaanzisha utawala wa ufalme wake duniani.
TANO: Vipi Kuhusu Wakolosai 1:13?
Ili “kuthibitisha” kwamba ufalme wa Mungu upo hapa, wengi hudondoa fungu hili: Naye [Baba] alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.”
Hebu tuchunguze kwa uangalifu fungu hili na tuiache Biblia ijitafsiri yenyewe.
“Nguvu za giza” ni nini ambazo kutoka kwazo Mungu anawaokoa watu wake? Matendo 26:17-18 husema, “…nikikuokoa kutoka kwa watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao, uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu…” Shetani na Majini yake wanatawala mataifa leo. Hii ndiyo sababu Paulo aliandika kwamba Wakristo hawashindani “juu ya nyama na damu; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili” (Efe. 6:12), na ndiyo sababu Kristo pia alisema, “Ufalme Wangu [serikali] si wa ulimwengu huu: Kama…[unge]kuwa…watumishi wangu wangenipigania…Lakini ufalme wangu sio wa hapa” (Yohana 18:36).
Mungu anapowaokoa watu wake kutoka “nguvu za giza,” anawaita kutoka katika ulimwengu huu (Ufu. 18:4), nje ya mfumo na njia yake ya maisha vilivyovuviwa na Shetani (Efe. 2:2-3)—serikali zake. “Akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme [serikali] wa Mwana wa pendo lake.” Mungu huwaokoa watumishi wake kutoka serikali, sheria na njia za Shetani na kuwaingiza katika SERIKALI YAKE wanapoongoka.
Wakristo ni raia wa ufalme wa Mungu, japokuwa haupo hapa. Kwa mfano: Wewe ni Mmarekani anayesafiri nje ya nchi. Ingawa uko nje ya nchi ya Marekani, wewe bado ni raia wa Marekani. Uraia wako uko Marekani. Kwa namna iyo hiyo, uraia wa Mkristo uko mbinguni (Flp. 3:20), japokuwa haishi kule.
Sasa angalia Warumi 4:17 inapoongelea habari za Ibrahimu: “Mungu mwenye kuwahuisha [hutoa uhai kwa] wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako [hayapo] kana kwamba yamekuwako…” Mungu aliposema kwa Ibrahimu, “Nimekufanya uwe Baba wa mataifa mengi” (Mwa. 17:5), hata hivyo Isaka asingezaliwa mpaka mwaka mmoja baadaye (linganisha 17:1-5 na 21:5). Wazao wake hawakukua kuwa taifa moja mpaka miaka mamia baadaye katika nchi ya Misri! Mungu alijua kuwa wazao wao watakuja kuwa mataifa yaliyoendelea sana karne nyingi baadaye. Kwa kuwa hakuna chochote kinachoweza kumzuia Mungu kutimiza mipango yake, kwake yeye ni kana kwamba imekwisha kutendeka. Ingawa watu wake bado hawajazaliwa katika ufalme wake, anajua kuwa watakuwa. Hakuna kinachoweza kuzuia hili lisitokee. Moyoni mwake, ni hakika.
SITA: Ufalme Wako Uje
Kama ufalme uko hapa sasa, iwe kama Kanisa au “ndani ya mioyo ya watu,” kwa nini Kristo awaamuru watumishi wake kuomba bila kukoma, “ufalme wako UJE” (Mat. 6:9-10; Luka 11:2)? Kama angalau mianzo ya ufalme ingekuwa hapa, au kama Kanisa ndio ufalme, je, Kristo asingewaamuru wafuasi wake kuomba “ufalme wako ukue na kuenea”?
SABA: Kuutafuta Ufalme
Kama ufalme wa Mungu uko hapa sasa, kwa nini Kristo awaambie wafuasi wake, “Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu” (Mat. 6:33)? Kama washiriki wa kanisa wako kwenye ufalme tayari, kwa nini wautafute? Tena, Kristo si angewaambia waueneze kwanza ufalme”?
Madhara Makuu ya Kutisha
Biblia husema kuwa Shetani ni “mungu wa dunia hii” (2 Kor. 4:4). Kama anaweza kukushawishi kwamba ufalme wa Mungu upo hapa, basi utaamini kuwa “umezaliwa mara ya pili.” Na kama “umezaliwa mara ya pili,” Basi lazima utakuwa “umeokoka” “tayari.” Kama “umeshaokoka,” huwezi kutenda dhambi. Kama huwezi kutenda dhambi na kuvunja sheria ya Mungu (1 Yohana 3:4), kwa hakika huhitajiki kuishika sheria, kwa sababu haki inahesabiwa kwako na Kristo. Kama hushiki sheria ya Mungu—inayofasili njia yake ya maisha (Rum. 13:10)—usingeweza kuwa Mkristo (Yohana 15:4-10, 14). Hiki ndicho hasa Shetani, adui yako, hukitafuta.
Chunguza Biblia kwa uangalifu mambo yote inayosema juu ya kila somo. Iache ijitafisiri yenyewe. Hapo ndipo ufahamu wako katika ukweli wa kibiblia utakapoongezeka!
Nyama na damu haviwezi kuingia katika Ufalme wa Mungu—lakini roho inaweza! Kwa sababu Kristo hakutaka kuacha mwanya wa kuchanganyikiwa, aliifananisha roho na upepo. Upepo, kama roho, hauonekani. Roho haiwezi kuonekana. Kwa hiyo, wale walio katika ufalme lazima wawe roho.
Ufalme katika Mioyo ya Watu?
Wengi huchagua kuamini kwamba ufalme huingia ndani ya watu badala ya watu kuingia katika ufalme. Tumeona kuwa ili kufikia hitimisho hili, ni lazima watu wapuuzie kauli zilizo wazi za Kristo. Wanaugeuza ufalme halisi wa Mungu unaokuja kuwa jambo la kiroho, ili kuugeuza kuwa hisia za kufikirika katika mioyo ya watu. Waongo wamesema kwamba, kuwa na Roho wa Mungu ni kuwa na ufalme wa Mungu ndani yako. Karne nyingi za udanganyifu wa wazi zimewafanya wengi kuamini hadithi za kubuni—badala ya ukweli ulio wazi wa Biblia.
Kwa kuwa ni wazi kwa watu wengi ya kwamba wanaweza kuingia leo katika nyingi za nchi zilizokuwa sehemu ya Himaya ya Uingereza, na kwamba watu wanaweza kuingia ndani ya kanisa, washika dini waliodanganyika walibuni wazo kwamba ufalme wa Mungu hukaa katika “mioyo ya watu”
Mara nyingi nimewasikia watu wakieleza kitu kinachofanana kama hivi: “Ufalme wa Mungu unaweza kujengwa katika mioyo ya watu kama Wakristo wote kila mahali watafanya kazi pamoja kwa upendo ili walete amani duniani na watu wote wajenge tabia ya kuvumiliana.”
Wanalipata wapi wazo hili? Kutoka tafsiri potofu ya Luka 17:20-21! Katika aya hii, Kristo alionekana kuongea juu ya ufalme wa Mungu “ndani yenu.” Tunahitaji kuichunguza hii tafsiri potofu. Kama kweli fungu hili linasema ufalme wa Mungu uko “ndani” ya watu, basi linapingana na maandiko mengine yote tuliyokwisha kuyachunguza. Na kama Biblia inajipinga yenyewe kwa wazi namna hii, tunaweza kuitupilia mbali, maana haiwezi kuwa Neno la Mungu.
Ufalme Ndani ya Mioyo ya Mafarisayo?
Hebu sasa tuichunguze Luka 17:20-21: “Na alipoulizwa na Mafarisayo, lini ufalme wa Mungu utakuja, Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule! Kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
Kama huelewi kitu kingine chochote katika fungu hili, elewa neno hili moja kwa moja! Kristo alikuwa akiongea na watu wenye tabia ya mwilini, waongo, Mafarisayo wanafiki. Hata kama ile hisia ya kufikirika kwamba ufalme wa Mungu ni kitu ambacho kiko katika mioyo ya watu ingekuwa ya kweli, hakuna uwezekano kabisa kwamba Kristo alikuwa akimaanisha ufalme kuwa ndani ya mioyo ya watu hawa!
Mafarisayo walijihesabia haki na walikuwa hawajaongoka. Wakati wote walikuwa wakitafuta kumjaribu Kristo ili wapate kumshitaki. Ni jambo la kipumbavu kabisa na hata la mzaha kusema kwamba ufalme wa Mungu ulikuwa “ndani” yao. Usipoteze ukweli huu pale Kristo alipowajibu, inasema, “Aliwajibu.” Aliwahutubia—Mafarisayo. Elewa kwamba Mafarisayo hawakuwa Kanisani, na kwa hakika Kanisa la Mungu HALIKUWA ndani ya Mafarisayo. Kwa kweli, hata Kanisa la Agano Jipya lilikuwa halijakuwepo bado.
Angalia kile ambacho Kristo HAKUKISEMA katika fungu hili. Hakusema, “ufalme wa Mungu utasimamishwa katika mioyo ya watu” au “ndani ya mioyo yenu.” Alichokisema ni kuwa, “ufalme wa Mungu NI…” Ni muhimu tuelewe kwamba mara hii Kristo alikuwa haelezei, ufalme wa Mungu kama kitu cha wakati ujao, lakini badala yake aliutaja katika wakati uliopo.
Kwa nini?
Nimetangulia kusema kuwa hii ni tafsiri potofu ya Kigiriki asili. Maneno halisi ya Kigiriki aliyoyatumia Luka hapa hutafsiriwa vyema zaidi “kati yenu” au “miongoni mwenu.” Tafsiri zingine kadhaa zinasomeka namna hii, na Biblia nyingi zenye maelezo ya pembeni zinajumuisha semi hizi.
Tafsiri ya Revised Standard Version husema, “ufalme wa Mungu uko kati yenu,” na tafsiri ya Moffatt huenda ndani zaidi. Hutafsiri mafungu haya mawili kwamba
“Aliwajibu, UTAWALA wa Mungu hauji kama mnavyotumaini kuuona; hakuna mtu atakayesema, “Uko hapa” au “Uko kule,” kwa kuwa UTAWALA wa Mungu uko miongoni mwenu sasa,’”
Hebu tujiulize, nini—au nani—anaweza kuwa yule ambaye Kristo alikuwa akimzungumzia? Nini—au nani—yule aliyekuwa “kati yao” Mafarisayo? Nini—au nani—alikuwa “miongoni” mwao?
Mwana wa Mungu—Yesu Kristo mwenyewe—alikuwa amesimama katikati ya kundi hili la Mafarisayo. Fikiria hivi: Walikuwa mbele ya mwakilishi ambaye “atatawala” katika ufalme wa Mungu ujao. Ni Yesu aliyekuwa amesimama “miongoni mwao”. Ni wazi, Kristo alikuwa akiongea juu ya ufalme wa Mungu, kupitia yeye kama mwakilishi wake, akiwa pale pale waliposimama.
Hebu tuelewe! Mafarisayo walielewa unabii mwingi wa Agano la Kale na maandiko yaliyoelezea ufalme wa Mungu. Walikuwa na habari ya mafungu tuliyojifunza kutoka kitabu cha Daniel. Wangeliweza kuelewa kwa nini Petro baadaye angesema, “manabii wote watakatifu” walinena habari za “kufanywa upya vitu vyote.” Waliuelewa vizuri unabii wa Isaya, Yeremia, Ezekieli, Danieli na wengine wengi. Mafarisayo walipuuzia maandiko kuhusu kuja kwa Kristo mara ya kwanza kwa sababu walitaka zaidi kutazama mafungu mengi yanayoelezea kuja kwake Mara ya Pili.
Ni wazi, Mafarisayo hawakuamini ufalme wa Mungu ulikuwa kanisa. Kwa hakika hawakuamini ulikuwa Himaya ya Uingereza—ambayo ulimwengu usingeiona kwa karne nyingi. Na hawakuamini ulikuwa ni msisimko fulani ndani ya mioyo ya watu. Walielewa hakika kuwa ulihusika na serikali—UTAWALA!
Tatizo lilikuwa ni kwamba hawakuelewa ni LINI ufalme utakuja au kwamba lengo lake halikuwa kuyafagilia mbali majeshi ya Warumi kutoka Palestina. Kama wangeelewa madhumuni ya Kuja kwa Kristo Mara ya Kwanza, wangelielewa vyema “ni lini” kutakuwa kuja kwake Mara ya Pili—na kwa nini kutatokea baadaye sana. Kwa hiyo, walikuwa wanamtazamia Masihi shujaa ashindaye ambaye angewasaidia katika kiu yao ya kugeuza utawala wa Kirumi ili wao wachukue nafasi ya Warumi kama mabwana zao.
Yesu alielezea makosa ya kufikiri kwao. Aliweka wazi kuwa kuja kwa ufalme halikuwa tukio la mahali fulani, linaloishia eneo la utawala wa Wayahudi katika Palestina.
Wayahudi walikuwa wakitafuta serikali ya kibinadamu katika taifa moja—la kwao! Hii ndiyo sababu Kristo aliwaambia wasiufikirie ufalme kama upo “pale” au “hapa.”
Kumbuka, Katika Yohana 18:37, Kristo alikuwa amesema kwamba alizaliwa ili awe mfalme. Alijua kuwa hatimaye atakuwa mfalme juu ya Ufalme Wake. (Daniel 7:17-18 na 23 zinaonyesha kuwa maneno ufalme na mfalme hubadilishana katika Biblia.)
Kwa kuendelea kusoma muktadha katika Luka 17, tunaachwa bila shaka kuhusu kile ambacho Kristo alikuwa anarejelea. Soma fungu la 24, ambalo, kama Mathayo 24:27, linarejelea jambo hili, “Kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku Yake.” Yesu alikuwa anaelezea tukio la kutisha, litakalotikisa ulimwengu wote na litakaloonekana wazi kama umeme wakati Anapohamisha Ufalme Wake wa Mathayo 13 kwenda Sayuni (Mika 4). Lakini, angalia maneno “katika siku yake” yanayoonyesha kwamba bado ni tukio la wakati ujao. Chukua muda kusoma Mathayo 24:26-30 na jinsi inavyoelezea “siku ambayo Kristo atakapofunuliwa”
Huwezi kufikiri hata kidogo kwamba Kristo alisema ufalme wa Mungu ulikuwa ndani ya Mafarisayo wasio na haki, wa mwilini, wenye chuki—waliotafuta kumwua wakati wote—wala kwamba alisema ulikuwa kanisa.
Hapo awali, Kristo alikuwa amewakaripia Mafarisayo kwa onyo kali. Bila shaka hili liliwakasirisha, na liliwafanya wajaribu kumnasa kama atasema kitu chochote kinyume na aidha ufalme wa Mungu au jambo lingine lolote. Katika Luka 13:28-29, aliwaonya, “Ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini
na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.”
Kristo alikuwa akiwaambia wazi Mafarisayo kwamba hawatakuwepo katika ufalme wa Mungu. Hawataruhusiwa kuuingia, kama Ibrahimu, Isaka na Yakobo—ingawa watu hawa bado hawajauingia (Ebr. 11:13, 39-40)
Ufalme wa Mungu “Umekaribia”?
Hakika mtu atanukuu Marko 1:15, mahali Kristo alihubiri kwamba “ufalme wa Mungu umekaribia.” Hapo, kumbuka pia kuwa aliendelea mbele kuongeza, “Tubuni na kuiamini injili.” Kwa hiyo baadhi wamehitimisha kuwa watu wanapotubu na kuiamini injili, na kuwa sehemu ya kanisa—papo hapo pia wanauingia ufalme wa Mungu, ambao kana kwamba ulikuwa unawangojea—ulikuwa “umekaribia.”
Kama ilivyo kwa Luka 17:21, watu husoma katika fungu kile wanachotaka liseme. Kristo hakusema kwamba tayari ufalme wa Mungu umeundwa au kusimamishwa—au kwamba ulikuwa kanisa. Haya yote ni “mapokeo ya watu” ambayo watu huyashika badala ya Neno la Mungu lililo wazi (Marko 7:7).
Luka 16:16 huonyesha kwamba, kuanzia siku za Yohana Mbatizaji, ufalme wa Mungu ulikuwa ni kitu ambacho “kinahubiriwa”. Ufalme ulikuwa haujafika bado, lakini wakati huo ulikuwa unahubiriwa. Kuhubiri ufalme na kupata fursa ya kustahili kuuingia kipindi hicho (na hata sasa) hakika ulikuwa “umefika”.
Watakatifu Watawala Na Kristo
Kabla ya kurejea kwa Luka, hebu tuchunguze zaidi kile ambacho Danieli aliandika
kuhusu ufalme wa Mungu.
Kumbuka, baada ya ujio wake kama punje ya haradali, Kristo atahamia Sayuni kama vile umeme ung’aavyo kutoka mashariki hadi magharibi (Mat. 24:27). Hili litakuwa ni tukio litakaloitikisa dunia, ambalo hakuna mtu atakayelikosa. Lakini je, atakuja kuitawala dunia yeye tu—au kutakuwepo na wengine pamoja naye? Tungeweza kuuliza: Wakati Kristo anaposimamisha serikali yake itakayotawala ulimwengu mzima, ni akina nani wengine wanaweza kuwa sehemu ya mfumo anaousimamisha? Kama serikali za wanadamu zinahitaji nguvu za wengi, wanaomsaidia kiongozi mkuu, je, serikali ya Mungu ni tofauti? Hapana!
Danieli 7:13 humzungumzia Kristo akija katika “mawingu ya mbinguni.” Mungu anampa rasmi mamlaka ya kutawala ulimwengu wote. Fungu linalofuata linasema, “Naye AKAPEWA mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” (fu. 14)
Tunauliza tena, Kristo anatawala pekee yake, au wako wengine watakaotawala pamoja naye? Kwa hakika ni namna gani Mungu anakusudia kuwaongoza watu wote na mataifa ya dunia?
Mafungu mengine kadhaa katika Danieli 7 ni muhimu kuyafahamu. Kumbuka kwamba ufalme wa Mungu umetabiriwa kuziondoa falme nne zinazotawala dunia nzima zilizokwisha kujadiliwa huko nyuma, zilizoelezewa katika sura ya 2. Sasa angalia mafungu 17-18: “Wanyama hao wakubwa wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.”
Liamini fungu hili kwa kile linachosema! Hatima ya mwito wa Wakristo ni kuungana na Kristo ili kushiriki utawala katika ufalme wa Mungu juu ya mataifa yote na watu
wote. Hakika, Kristo ni “MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana.” Hawa wafalme na mabwana wengine wanaweza kuwa wewe au yeyote ambaye yuko tayari kukubali masharti ya Mungu katika kuuingia ufalme Wake.
Mafungu 19-20 yanafafanua zaidi kile kinachotokea wakati watakatifu wanarejea pamoja na Kristo. Pembe hii ndogo hapa ni UFALME WA KIDINI/MTAWALA wa mfumo ule ule ambao unatengeneza mwanamke anayemwendesha mnyama wa Ufunuo 17. Serikali hii ya kidini imetawala juu ya Himaya Takatifu ya Rumi katika vipindi vyote toka kuibuka kwake mwaka wa 554 BK.
Sasa soma mafungu 21-22: “Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.”
Mwisho, unabii mrefu wa Danieli unahitimishwa na fungu la 27 ukithibitisha zaidi tokeo la kipekee linalowangojea watakatifu wote wa Mungu huko mbele. Angalia: “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Kipi chaweza kuwa wazi zaidi? Si ajabu Kristo alisema, “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa: naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu” (Ufu. 2:26-27) na, mafungu machache baadaye, aliongeza, “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi…” (3:21).
Msemo “katika kiti Changu cha enzi” umetumika kwa sababu Kristo alielewa kwamba kiti chake cha enzi kiko duniani, tofauti na cha Baba, ambacho kiko mbinguni. Luka 1:32 inaonyesha kwamba Kristo kwanza ataketi juu ya Kiti cha Enzi cha Daudi kabla hajachukua kiti Chake Mwenyewe katika Yerusalemu. (Pia angalia Mathayo 5:5, Zaburi 25:12-13 na 37:11.) Hakuna shaka kwamba Kristo anaporejea, watakatifu watatawala pamoja naye—DUNIANI!
Hebu sasa tuchunguze mfano wa muhimu sana ambao Kristo aliutoa ili watu wapate kujua kuja kwa ufalme wa Mungu na wajibu wa Wakristo ili KUSTAHILI kuwa sehemu yake.
Mfano wa Talanta
Luka 19:11-27 ina mfano ulioandikwa kufafanua kitakachotokea wakati ufalme wa Mungu utakuja. Katika mfano huo, Kristo anajilinganisha na kabaila aliyesafiri kwenda “nchi ya mbali” (kivuli cha kwenda kuwa na Baba mbinguni) kwa takribani miaka 2,000, hadi kurudi kwake. Wanafunzi walidhani kwamba ufalme wa Mungu “ungetokea mara,” na Kristo alitaka kufafanua kwamba muda mrefu utapita kabla ufalme haujaja.
Katika mfano huu, Kristo anafutilia mbali wazo lolote kwamba ufalme utatokea mara, katika mwonekano wa Kanisa Lake. Na bila shaka bado hajarudi duniani.
“Kabaila” katika mfano “aliwaita” “watumwa wake kumi” (kivuli cha Wakristo wakiitwa na Mungu kutoka ulimwenguni) akawaagiza wafanye biashara ili kuongeza thamani ya “talanta” (fedha) aliyompa kila mmoja kwa ajili ya kuwekeza. Talanta hiyo kwa hakika iliwakilisha aina ya kipimo-mfano cha uthamani wa mambo ya kiroho. Kumbuka kwamba ulikuwa mfano, kwa hiyo Kristo alikuwa hamaanishi aina yoyote ya fedha halisi. Aliwaambia watumwa wake “Fanyeni biashara hata nitakapokuja”—au “kuizalisha” talanta hiyo iwe fedha nyingi. Wakati Kabaila akiwa amekwisha kwenda zake, baadhi ya watumwa wake wakasema, “Hatumtaki mtu huyu atutawale.” Ni muhimu kuelewa lengo la kauli hii.
Wenyeji hawa walielewa kwamba Kabaila (Kristo) alikuwa anakuja “kutawala” duniani. Hawakutaka sehemu yoyote katika hili na waliikataa serikali yake (utawala) juu yao—na, sehemu yao ndani yake katika wakati ujao (fu. 27). Walielewa kwamba ufalme wa Mungu ungekuwa ni SERIKALI inayotawala dunia. Kumbuka, mfano lianza na Kabaila (Kristo) kwenda mbinguni “ili ajipatie ufalme na kurudi.” (Tumekwisha kuona katika Danieli 7:14 kwamba Mungu anamvika Kristo mamlaka iliyo kuu muda mfupi kabla hajarudi kutawala na watakatifu.)
Kabaila anaporudi, anamwita kila mmoja wa watumwa wake kuja mbele yake apokee taarifa ya namna ambavyo kila mtu alizalisha talanta aliyopewa.
Wengine walikuwa wamezalisha talanta tano, wengine kumi, n.k., lakini mmoja alikuwa amezika talanta yake ardhini na hakuzalisha chochote. Kristo alitaka maelezo ya namna ambavyo “kila mmoja alivyozalisha” wakati akiwa amekwenda zake.
Mtumwa wa kwanza alikuwa amezalisha talanta kumi na Kristo alielezea thawabu yake kwa kusema, “Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi”. (fu. 17).
Mtumwa aliyekuwa amepata talanta tano aliwekwa “juu ya miji mitano.” Kwa sababu mtumwa wa pili alizalisha nusu, thawabu yake ilikuwa nusu pia. Kwa hiyo watu hawa walipewa “mamlaka”—waliwekwa katika nafasi za utawala “juu ya miji.” Thawabu yao ilikuwa ni “kutawala” pamoja na Kristo (Yuda 14) katika Ufalme wake unaotawala dunia nzima. Ni wazi namna gani!
Mtumwa aliyeweka talanta yake katika leso na kuizika alikuwa amepoteza fursa pekee ya kustahili kutawala katika ufalme wa Mungu. Inasema, “Naye [Kabaila, Yesu] akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe.”
Mtumwa huyu hakukua. Hakuzalisha chochote katika maisha yake na kwa hiyo akakosa sifa za kutawala juu ya miji katika ufalme wa Mungu. Kristo alimpatia yule aliyezalisha talanta kumi thawabu ya yule mtumwa mwovu—kiasi kwamba huyu akaishia kuwa na thawabu kubwa kuliko iliyompasa. Miji ambayo mtu huyu aliipoteza kwa sababu ya tabia yake italazimika kutawaliwa na mtu mwingine. La sivyo, itaachwa ukiwa, bila mtawala aliyepewa mamlaka juu yake.
Historia fupi inahitajika ili kuweza kuelewa mpangilio wa mfano huu. Kristo alikuwa Myahudi aliyekuwa akihubiri mfano huu katika ardhi ya Yuda.Yuda lilikuwa ni moja ya makabila kumi na mbili katika Israeli ya zamani. Makabila kumi kati ya hayo yalikuwa yameshapotea zaidi ya miaka 700 iliyokuwa imepita, kwa sababu walimwasi Mtoto wa Suleimani, Rehoboam. Walikuwa wamechukuliwa mateka na Waashuru wa zamani na baadaye walikuwa wamehamia pande za Ulaya ya Kaskazini-magharibi na kuwa nchi za kidemokrasia za watu wenye kuzungumza Kiingereza za Marekani, Uingereza, Kanada, Australia, New Zealand na baadhi ya mataifa ya Ulaya Magharibi. Ni baadhi ya makabila ya Benjamini na Lawi waliobaki na Wayahudi, makao makuu yao yakiwa Yerusalemu.
(Unahimizwa sana kusoma kitabu chetu kipana Marekani na Uingereza katika Unabii ili kuelewa picha kubwa ya kile ambacho kimeelezwa hapa kwa ufupi.)
Wakati mfano wa Talanta unazungumzia juu ya wenyeji wa mji wa yule Kabaila “kumchukia,” na kusema kwamba, “Hatutaki mtu huyu atutawale,” ni kielelezo cha Wayahudi. Historia inaandika wazi kwamba walikataa mamlaka ya Yesu Kristo. Hiki ndicho Yohana 1:11 inamaanisha inaposema kuwa “Alikuja kwa walio wake, na walio wake hawakumpokea.” Wale “watumwa kumi” (wale Wakristo wanaoitwa leo) ni kielelezo, katika kivuli, kwa MAKABILA KUMI ya Israeli yaliyopotea. Kristo aliwapa nafasi ya kutawala, kwa sababu Wayahudi walikataa mamlaka yake juu yao.
Kwa masikitiko, baadhi hawataki Yesu wa kweli wa Biblia awaambie nini cha kufanya. Hawataki atawale juu ya maisha na mienendo yao. Lakini wanataka wokovu—bila masharti.
Hakuna mtu atakayepewa utawala bila kuthibitisha kwamba anaweza kutawaliwa! Hakuna yeyote atakayekuwa sehemu ya serikali ya Mungu itawalayo ulimwengu mzima isipokuwa amejifunza kujisalimisha kwa serikali ya Mungu na kutawaliwa na Mungu na Yesu Kristo katika maisha haya. Hili ndilo fundisho kuu katika mfano wa talanta.
Wakati Kristo alipowaita watumwa wake kutoa hesabu, alikuwa anaonyesha kwamba siku moja watu wote watasimama na kutoa hesabu mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo. Kama ilivyo thawabu ya mitume kumi na wawili ambao watawekwa juu ya
makabila kumi na mbili ya Isreali (Mat. 19:27-28), wengine watapewa MAMLAKA makubwa sana kutawala juu ya miji pamoja na Yesu Kristo “katika kiti chake cha enzi cha utukufu.”
Ufalme Utakuja Lini?
Wote wanataka kujua Kristo atarudi lini. Wanafunzi walimwuliza, “Nayo ni nini dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia?” (Mat. 24:3.)
Mafungu yote 48 yanayofuata katika Mathayo 24 ni jibu la Kristo akieleza kwa kina matukio mengi, katika mfuatano ambayo yatatangulia Kuja Kwake Yerusalemu. Katika fungu la 36, akirejelea wakati hasa wa Kuja Kwake Duniani, Alisema, “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
Majuma machache tu baadaye, katika Matendo 1:6-7, kabla Kristo hajapaa kurudi mbinguni mara ya mwisho, wanafunzi walimuuliza swali linalohusiana kuhusu kipindi cha kwanza cha Mpango wa Mungu. Angalia: “…wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo UTAKAPOWARUDISHIA Israeli ufalme? Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.” Kristo aliwapa jibu lile lile kama kwenye Mathayo—“si juu yenu kujua nyakati au majira.”
Ni muhimu kuzingatia kuwa Kanisa la Agano Jipya lingesimamishwa siku kumi tu baada ya tukio hili (2:1). Kwa nini Kristo awajibu, “si juu yenu kujua nyakati na majira” kama ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja katika mfumo wa Kanisa, ambalo lingeanza baada ya muda mfupi? (katika siku ya Pentekoste)—siku kumi tu baadaye?
Hivyo ndivyo ilivyo kwetu leo. Hatuwezi kujua hasa ufalme wa Kristo utakuja lini, lakini tunaweza kujua ukaribu wake. Katika Luka 21:31, mwishoni mwa unabii mrefu ulio sambamba na Mathayo 24, Kristo alisema, “Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu [kwenda Yerusalemu].”
Aliwataka wafahamu kwamba “mtapokea NGUVU, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu” (Matendo 1:8), lakini siyo kujua lini ufalme utawasili. Vivyo hivyo ni kweli kwa wote wanaoongoka leo. Hatuwezi kujua hasa lini Kristo atarudi, lakini tunaweza kujua kuwa tutapokea nguvu sasa ili kukua na kushinda—na kuihubiri injili ya ufalme wa Mungu mpaka ajapo.
Juhudi za Watu Haziwezi Kuuleta Ufalme
Wakristo wa kweli siyo wanaharakati wakitafuta “kuufanya ulimwengu huu mahali pazuri”—na kwa namna hiyo kuuleta ufalme wa Mungu duniani. Wanayo “miguu iliyofungiwa utayari tupatao kwa Injili ya amani” (Efe. 6:15). Wanatembea maishani miguu yao ikiwa imefunikwa na maarifa ya namna ambavyo injili ya kweli inaonyesha njia pekee ya kuyaendea mambo mema ambayo mwanadamu anayatamani. Wanatambua kwa hakika kwamba ufalme wa Mungu unakuja. Wanajua kile kilicho mbele kwa ajili ya ulimwengu huu. Hawatoki na kwenda kutumika na kuua katika vita vya wanadamu visivyo na sababu, wala mwisho, au kushiriki katika masuala ya utawala wa serikali za wanadamu.
Hawachukui mambo katika mikono yao wenyewe, na kujaribu eti “kueneza ufalme,” na hivyo kujaribu kutangua kusudi la Mungu, la kumwonyesha mwanadamu kwamba hawezi kujitawala mwenyewe! (Chukua muda kusoma vijitabu vyetu viwili Vita, Mauaji na Mambo ya Kijeshi na Je! Wakristo Wapige Kura? ili kuelewa kwa nini.)
Angalia kile Paulo alichovuviwa kuandika: “Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo kuna amani na salama; ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi” (1Thes. 5:2-4).
Wale wote wanaoelewa ukweli wa kijitabu hiki hawahitaji tena kuwa “gizani” kuhusu Mpango wa Mungu au fursa ya kipekee ya wajibu wao ndani yake.
Akidondoa Isaya 52:7 Paulo naye aliandika, “Ni mizuri kama nini miguu yao waihubirio injili ya amani, na kuleta habari njema [habari njema ya injili] ya mambo mema” (Rum. 10:15). Katika fungu la 16, alidondoa andiko lingine kutoka Isaya: Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu?” (53:1).
Bila shaka, watu wengi hawataamini “Habari za Mungu” juu ya kile kilicho mbele ya ustaarabu. Hawataamini kwamba hawezi kuleta amani ya ulimwengu kwa juhudi za kibinadamu. Wengi watapaaza sauti “Amani, amani; wakati hakuna amani” (Yer. 6:14; 8:11, 14-15), na wengi wataendelea mbele kwa shauku wakiamini utabiri wao wa uongo, hata mbele ya kushindwa kuliko wazi wazi.
Wanaojidai kuwa Wakristo wa dunia hii wataendelea kung’ang’ana kwa nguvu kuuleta ufalme wa Mungu na amani ya ulimwengu kwa juhudi za kibinadamu. Viongozi wa dini waliodanganyika watawaambia kwamba huu ndio “wajibu wao wa Ukristo.” Wengi wataona huu ndio ujumbe pekee wa kanisa lao. Mamilioni wanatazamia furaha, wingi wa vyakula, amani na usalama kila mahali—lakini watakatishwa tamaa ajabu ndani ya muda mfupi. Hii ni kwa sababu hali ya mambo, inayoelekea kwenye kipindi kigumu cha majanga ya ulimwengu mzima, itakuwa mbaya mno kabla hatimaye kuwa bora.
“Ufalme Wako Uje”
Watu wengi wanafahamu kile kinachoitwa “Sala ya Bwana.” Wengi wanaweza kuikariri bila shida, wakiwa wameifanyia mazoezi kwa muda mrefu bila kujua kwamba huo ni mfano au kielelezo cha namna ya kusali. Nilijifunza kifungu hiki nikiwa na umri wa miaka minne. Inaanza, “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe. Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani…” (Mat. 6:9-10). Sala hii fupi inaendelea kwa mafungu matatu zaidi. Lakini, mamilioni ya wanaoijua na kuitumia, ni wangapi kati yao ambao hakika hufikiria juu ya kifungu “Ufalme wako uje”—au mapenzi ya Mungu [Mpango wake Mkuu] yatimie hapa duniani”? Kwa miaka 2,000, wengi wamedhani kufuata agizo la Kristo, katika kusali, “Ufalme wako uje” bila kutafakari kwa kina maana hasa ya kushangaza iliyo nyuma ya usemi huu mfupi.
Je! Wewe?
Mafungu machache tu baadaye, katika sura hiyo hiyo, Kristo alisema, “Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa” (fu. 33). Ni lazima Wakristo watafute ufalme wa Mungu KWANZA—juu ya kingine chochote—katika maisha yao! Watawezaje kufanya hivi kama hawajui ufalme ni kitu gani—au lini utakuja—au unaathiri vipi wokovu wao? Lakini sasa WEWE unajua!
Ufalme LAZIMA Uje
Nukuu ifuatayo inatoka kwenye kijitabu cha Herbert W. Armstrong Sasa Unamaanisha Nini…Ufalme wa Mungu? Ni muhtasari usiokuwa wa kawaida wa ukweli wa ajabu ulio katika jibu la swali, ufalme wa Mungu ni nini? Nukuu hii ilionekana chini ya kichwa kidogo “Aina Mbili za Majaliwa”:
“Matatizo ya ulimwengu huu yalianza mwaka 1914 wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kulikuwa na kuanguka kwa uchumi tokea 1918 hadi 1939. Sasa tuko katika anguko la pili… Lakini wakati huu hatimaye tuna nishati ya nyuklia. Tuna akiba ya mabomu ya Haidrojeni yaliyorundikwa kwa wingi yenye uwezo wa kuangamiza maisha ya wanadamu wote kutoka sayari hii mara kadhaa. Leo ziko aina nyingine mbili za silaha za maangamizi, ambazo kila moja inaweza kuwafuta wanadamu kutoka duniani.
“Wanasayansi mashuhuri ulimwenguni leo wanasema ni serikali moja bora ya ulimwengu mzima inayoweza kuuzuia ulimwengu usijiangamize. Bado WATU hawezi na hawataweza kuunda aina hiyo ya serikali itakayotawala ulimwengu mzima.
“Ni wakati mwafaka tuukabili UKWELI halisi, mgumu, baridi: ubinadamu una uchaguzi wa aina mbili: Ama yuko MUNGU Mwenyezi, mwenye uweza ambaye anaelekea kuingilia kati na kuusimamisha UFALME WA MUNGU kutawala mataifa yote kwa NGUVU isiyo ya kibinadamu wala kitaifa ili kutuletea AMANI—la sivyo maisha ya wanadamu wote yatatoweshwa (Mat. 24:22).
“Kama watu wa dini waliodanganyika, wanaodhani KANISA ni Ufalme wa Mungu, wangekuwa sahihi, na kwamba hapatakuwa na SERIKALI YA ULIMWENGU isiyokuwa ya kawaida yenye nguvu zote ambayo ni Ufalme wa Mungu, basi mwanadamu hana TUMAINI kabisa. Maisha ya wanadamu wote yamo katika hatari ya kutoweka.
“Lakini zingatia kile ambacho Kristo alisema!
“Unaweza KUMWAMINI Yesu Kristo?
“Tegemeo lako liko wapi—katika Neno la Mungu, au katika mafundisho ya kipagani, yaliyo tupu, yadanganyayo ambayo kwa uongo yamebandikwa jina ‘Ukristo’—yaliyorithiwa kama ‘mapokeo ya Ukristo’—yanayosema KANISA ni Ufalme wa Mungu; au, kwamba Ufalme ni hisia ya kusisimua ‘iliyowekwa mioyoni mwetu’? Ni muda mwafaka utambue ni akina nani ni manabii wa uongo, na NANI anayesema ukweli wa Neno la Mungu kwa uaminifu!”