JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.
Hifadhi ili kusoma baadaye
Inapatikana katika lugha hizi:
Liko Wapi Kanisa la Mungu Leo hii?
Photo of a CongregationNew York, Marekani Photo of a CongregationJamaika Photo of a CongregationPeru Photo of a CongregationIdaho, Marekani Photo of a CongregationIndia Photo of a CongregationUbelgiji Photo of a CongregationKenya Photo of a CongregationArkansas, Marekani Photo of a CongregationAfrika Kusini Photo of a CongregationUingereza Photo of a CongregationNigeria Photo of a CongregationOhio, Marekani

Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu.” Kuna shirika moja linalofundisha ukweli wote wa Biblia, na limeitwa kuishi kwa “kila neno la Mungu.” Je, unajua namna ya kulipata? Kristo alisema lita:

  • Fundisha “yote” Aliyoagiza
  • Kuwa na washiriki walioitwa na kuwekwa wakfu kwa ile kweli
  • Kuwa “kundi dogo”
Habari za Mwandishi
Photo of David C. PackDavid C. Pack 

Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Mhariri-Mkuu wa Jarida la Ukweli Halisi, na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, Daudi C. Pack amewafikia mamilioni wengi ulimwenguni na kweli za Biblia zilizo na nguvu sana—zisizojulikana karibu kwa wote. Ameandika vitabu na vijitabu 80, mwenyewe ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, na alionekana kama mgeni kwenye Kituo cha Historia (The History Channel). Bwana Pack alihudhuria Chuo cha Mabalozi huko Pasedena, Kalifonia, aliingia katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu Mzima mwaka 1971, na yeye binafsi alifundishwa na mwanzilishi wake, Herbert W. Armstrong.

Jinsi Ufalme wa Mungu Utakavyokuja

Kisa Ambacho Hakijawahisimuliwa!

na David C. Pack

Mabilioni wanasubiri Kurudi kwa Yesu Kristo kusimamisha Ufalme wa Mungu. Lakini wachache wanajua jinsi gani Atafanya hivi. Jambo hili halitatokea namna ambavyo wengi wanatarajia. Kijitabu hiki kina kisa cha ajabu, ambacho-kamwe-hakijawahisimuliwa cha jinsi ambavyo Ufalme wa Mungu utakavyosimamishwa juu ya mataifa yote!

Fikiria ulimwengu wa leo! Maendeleo katika teknolojia na viwanda kamwe hayajawahi kuwa makubwa kama hivi. Kile ambacho kilikuwa riwaya za kisayansi sasa ni mambo halisi ya kila siku. Utajiri wa vitu umezidi kwa mamilioni ya watu katika ulimwengu wa Magharibi. Lakini vipi kuhusu nusu ya wanadamu—mabilioni!—ambao wana vichache au hawana kitu? Na vipi kuhusu kupungua kwa mwanadamu kwa haraka katika maadili, unyofu na TABIA—ambavyo zamani viliaminika kuwa nguzo za kila jamii? Je, mwanadamu anao uwezo, na je, viongozi wake kwa pamoja wana utashi wa kutatua changamoto kuu za ustaarabu—au nguvu kuu isiyoonekana lazima iingilie kati?

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusali, “Ufalme Wako uje!” Kitu kilichofuata Alichoagiza kilihusiana moja kwa moja: “Mapenzi Yako yatimizwe hapa duniani kama ilivyo mbinguni.” Mungu mwenye upendo ni lazima atume Ufalme Wake hivi KARIBUNI ili KUHITIMISHA jaribio la mwanadamu lililoshindwa la sivyo hakutakuwa na ulimwengu wa kuupokea!

Kurudi kwa Yesu Kristo—Kuja Kwake “Mara ya Pili”—ni kiini cha Ukristo. Mabilioni wanakungojea. Wenye kudhihaki wanakanusha. Lakini wale wanaojua kitu chochote cha Neno la Mungu wanajua Yesu anarudi. Kila kiashiria kinapendekeza kuwa Kuja Kwake hakuwezi kuwa mbali. Biblia inaongelea kwa upana juu ya jinsi ambavyo Yesu atasimamisha Ufalme wa Mungu, wakati mwingine ukiitwa Ufalme wa Mbinguni. Vitu vichache vingeweza kuwa vya muhimu zaidi. Yesu Mwenyewe alieleza kwa wazi jinsi Ufalme wa Mungu utakavyoanza—na siyo kile ambacho umejifunza. Kijitabu hiki kina maarifa ambayo kamwe hayakuwahi kufafanuliwa kabla! Na yanawakilisha sehemu ndogo tu ya uthibitisho wote wa Biblia katika Agano la Kale na Jipya juu ya jinsi Ufalme wa Mungu utakavyowasili katika namna ambayo hakuna yeyote anayesikia juu yake!

Ufalme wa Mungu utaleta njia Yake ya ajabu ya maisha kwa wale wanaoishi ndani yake, ambayo siku moja itahusisha ulimwengu wote. Lakini siyo pale unapoanza…

Aina Nyingi za ”Ujio”

Imani inayoshikiliwa na wote ni kwamba Yesu Kristo atarudi Duniani katika Yerusalemu, na hii itafuatia miaka mitatu-na-nusu ya Dhiki Kuu—inayohusisha mihuri saba ya Ufunuo. Wanadamu wengi sana watakufa. Kisha mara hiyo atasimamisha serikali kuu ya ulimwengu. BIBLIA HAISEMI LOLOTE KATI YA HAYA! Ingawa haya yote yatatokea kwa wakati wake, na kwa kila namna yatakuwa mabaya zaidi kuliko mtu yeyote anavyofikiria, Neno la Mungu liko wazi kabisa kwamba Kurudi kwa Kristo kutakuja katika namna ambayo ni tofauti kabisa kuliko kile ambacho KILA MTU anatazamia!

Hebu tujiulize swali la kushangaza, swali ambalo hakuna anayeonekana kulifikiria. Biblia inaelezea aina ngapi za kurudi kwa Kristo? Mafungu yanayotofautiana yanashikilia jibu la kushangaza. Nabii Haggai aliandika juu ya Kurudi kwa Yesu, “Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na Kinachotamaniwa na mataifa yote [muda mrefu ilijulikana kuwa ni Yesu Kristo] kitakuja…” (2:6-7). Watu wengi sana leo-hii wanatafuta na kutamania kurudi kwa Kristo. Japokuwa wengi wanaelewa kidogo sana juu ya kuwasili Kwake, wengi wa Wakristo wanakutamani, na sababu kuu ya kuutumaini kila siku zaidi ya siku iliyopita ni vile kumekuwa na kuporomoka kwa maadili katika ulimwengu mzima!

Tatizo hili hapa—na ni kubwa! Kitabu cha Ufunuo kinaongelea mwitikio tofauti sana kufuatia kuonekana kwa Yesu: “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele…mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa…na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi” (11:15, 18). Picha ya mataifa yaliyokasirika haipatani na Haggai.

Aya hizi haziwezi kuwa zinarejelea wakati ule ule!

Wakiwa hawana maarifa ya Kristo kuja mara nyingi, wengi wanadai Anakuja na mara hiyo kuwafutilia mbali maadui Zake wote, akisimamisha Ufalme Wake. Ufunuo huonekana kusema hivyo, lakini fikiria 1 Wakorintho 15:25, ambayo inaonyesha kitu kingine tofauti kabisa, ikisema Kristo “sharti amiliki…, hata awaweke maadui Wake wote chini ya miguu Yake.” Wale ambao watapendekeza Anafika, anatawala kwa sehemu ya sekunde, kisha anawafutilia mbali maadui Zake wote, ni wazi wanapuuzia fungu hili, na mengine mengi.

Elewa. Mwanzo wa Ufalme wa Mungu hakuhusiani na imani potofu ya Kiprotestanti kwamba Kristo “anawanyakua mbinguni” kwa siri watumishi Wake. Hakuna mahali Neno la Mungu linasema Yesu anawachukua Wakristo na kurudi nao mbinguni. (Mafungu mengi huthibitisha hili.) Utaona aya zilizo wazi zikionyesha Anausimamisha Ufalme wa Mungu Duniani, akitumia watumishi ambao wako hapa. Hili litakuja kuwa wazi.

Kusimamishwa kwa Ufalme wa Mungu ni fokasi yetu. Hakuna Mkristo wa kweli anayetilia shaka kwamba Kristo anakuja. Lakini hakuna anayefafanua jinsi gani Atakuja—lini Atakuja (chini ya hali gani)—wapi Atakapowasili—kwa nini lazima aje—na namna gani hatimaye atasimika Ufalme Wake. Kwa urahisi hawajui.

Ufalme Kama Punje ya Haradali

Kila mmoja anajua Yesu aliongea kwa mifano mara nyingi. Katika Mathayo 13 pekee, Alitoa mifano saba­­—mingi ni mifupi sana. Kila mmoja unaelezea sura ya Ufalme, kwa pamoja ikichora picha kamili. Mahali pa kuanzia ni fungu la 31: “Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake” (fu. 31-32). Punje ya haradali iliyokuwa ikifahamika na wale waliokuwa wakimsikiliza Yesu ilikuwa ni ndogo sana—ambayo ni vigumu sana kuiona. Hii ndiyo sababu Aliziita “ndogo [ikimaanisha ndogo sana katika umbile] kuliko mbegu zingine zote.” Ufalme wa Mungu unafanana na kitu kisichoonekana kwa macho unapowasili! Hakuna yeyote anayefokasi kwa hili. Hatimaye unakua na kuwa SERIKALI YA ULIMWENGU, ukiwa “mkubwa kuliko mboga zote”—“mti”—lakini hauanzi namna ile. Mfano huu kamwe hautajwi kwa sababu hakika hakuna anayeufahamu.

Hivyo hapawezi kuwa na shaka juu ya mwanzo mdogo wa Ufalme, mfano unaofuata unathibitisha hili: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia” (fu. 33). Neno la Kigiriki “sitiri” ni egkrupto, likimaanisha fichwa ndani. Fikiria juu ya neno la kisasa linalofanana na hilo—iliyofichwa. Yesu anasema—kwa kumaanisha—analeta UFALME ULIOFICHWA. Awali utakuwa umefichwalakini unapanuka kwa sababu chachu muda wote husambaa.

Yesu anafunua zaidi hili katika mfano wa tatu: “ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile” (fu. 44). “Sitiri” hapa imetokana na krupto, ikimaanisha “kuficha kwa kufunika.” Ujumbe wa Yesu kwa mara nyingine umewekwa wazi: Ufalme wa Mungu unaanza kidogo, uliofichwa na uliofunikwa. Ni lazima mtu atoke na kuutafuta!

Bado mfano mwingine unathibisha hili: “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri” (fu. 45). Zikiwa ni nadra kupatikana na za thamani kubwa, lulu za asili ni vigumu kupatikana. “Naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa [ilikuwa imefichwa na alilazimika kuitafuta], alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua” (fu. 45-46). Kando na kuongezea nguvu mifano ya punje ya haradali na chachu, mifano ya hazina iliyositirika na lulu pia huongeza fokasi kwenye thamani ya kuuingia Ufalme.

Kabla ya kuingalia mifano mitatu iliyobaki ya Mathayo 13, tambua kwamba kila ufalme Duniani leo-hii una vitu vinne vya lazima: (1) Ardhi, mali au milki—bila kujali ukubwa au udogo wake. Lazima kuwe na mipaka halisi inayoonyesha ukubwa wa ufalme [saizi ya ufalme]. (2) Mtawala au mfalme anayeongoza serikali. (3) Watu—watawaliwa—wanaoishi katika milki inayotawaliwa. Na (4) mfumo wa sheria na kanuni pamoja na muundo msingi wa serikali.

Licha ya saizi yake, wakati ufalme kama punje ya haradali unapowasili, unakuwa na vitu vyote vinne. Wakati Kristo alipoongea mara kwa mara juu ya Ufalme kuwa “mdogo” na “ulifichika,” Alikuwa akirejelea kwenye idadi watawaliwa—ambayo itaongezeka haraka katika “kipimo cha pili na cha tatu cha chakula.” Uwezo wa Kristo na milki Atakayotawala itakuwa ndogo.

Ni Ufalme halisi.Usiufanye wa kiroho kama vile kanisa, au kitu “kilicho katika mioyo ya watu.”

Mifano Mitatu Zaidi

Mfano wa tano unaonyesha kupanuka kwa Ufalme wa Mungu kutoka mwanzo mdogo, vile vile kitu kingine ambacho hakuna anayeonekana kukiona: “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini...” (fu. 47). Juya linaanza likiwa tupu. Baada ya muda linajaa samaki wa “kila aina”—watu kutoka mataifa yote. Lakini siyo “samaki” wote wanastahili kuwepo: “hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia [au zama, wakati Kristo anahamia Yerusalemu]: malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki [angalia hii!], na kuwatupa katika tanuri [au oveni] ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” (fu. 48-50). (Mwisho wa waovu haupatani na moto wa milele baada ya maisha. Kwa mengi zaidi juu ya hili, msomaji atahitaji kusoma kijitabu chetu Ukweli Kuhusu Ahera (The Truth About Hell).)

Achana na mtazamo wowote kwamba Ufalme wa Mungu unaanza na roho za kiungu tu. Mfano huu unaondoa udhanifu huo usio sahihi. Waovu wanaweza kuingia katika Ufalme na wakati fulani lazima waondolewe!

Bado mfano mwingine wa Mathayo 13 unaelezea ngano na magugu yenye sumu awali vikikua pamoja katika Ufalme wa Mbinguni. Ni wazi kwamba Ufalme hauko mbinguni. Kristo anaagiza kwamba magugu lazima yabaki pamoja na ngano mpaka mavuno—wakati Anapohamia Yerusalemu. Anafafanua kwamba, katika wakati huu, kama wakati juya linapovutwa pwani—baada ya Ufalme kama punje ya haradali kuwepo Duniani kwa muda fulani—malaika wanakusanya “kutoka katika ufalme” magugu na “kila kitu kichukizacho na kutenda uovu,” akirudia kwamba hawa wanaunguzwa katika tanuri [oveni].

Hivyo basi, ni kana kwamba Ufalme, kadri unavyokua, aina mbaya ya watu wanaweza kuingia ndani yake. Kristo alisema hili mara mbili, akitumia vielelezo rahisi ili kwamba pointi isiweze kutoonekana. Fungu la 43 linaita mavuno wakati ambapo watakatifu katika Ufalme wa Baba yao “wanang’aa kama jua.” Kigiriki kinamaanisha “kung’aa kwa fahari.” Aya zingine zinaweka wazi ni katika kipindi hiki watakatifu wengine wengi zaidi, watu waliofuzu kwa utawala katika Ufalme wa Mungu, wanaungana na Kristo na Baba katika Yerusalemu mahali ambapo ataweka Ufalme Wake juu ya mataifa yote. Mpaka wakati huo utakuwa umechanua na kuwa mti mkubwa wa haradali ulioanza na punje ndogo.

Mfano wa kwanza kabisa katika Mathayo 13 bado unaleta mtazamo mwingine, ukionyesha wale ambao hatimaye wanafaulu kuingia katika Ufalme. Kristo aliongea juu ya mpanzi aliyekwenda kupanda mbegu, huku baadhi zikianguka katika udongo mzuri, zingine kwenye miamba, zingine kwenye miiba ambayo ilizisonga, na zingine zikianguka kando kando ya njia. Kama ilivyo kwa ngano na magugu, Kristo aliendelea kutafasiri mfano kwa faida yetu: “Basi ninyi sikilizeni [au eleweni] mfano wa mpanzi. Kila mtu alisikiapo neno la ufalme, asielewe nalo, huja yule mwovu [Shetani], akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno [la Ufalme], akalipokea...kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa” (fu. 18-21).

Angalia pia kuwa dhiki na udhia vimeambatana na wanaokuwepo katika Ufalme! Bado thawabu itakuwa ya kustaajabisha. Hakuna yeyote anayesikia kwamba kitu kama hicho kinawezekana.

Kuendeleza mfano, “Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno [lile lile]; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai” (fu. 22).

Hili ndilo kundi la mwisho: “Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno [la Ufalme], na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini” (fu. 23). Hii ndiyo aina pekee ya wanaosikia ambao wanadumu—na hawa wanasitawi.

Mathayo 13 pekee inatosha kuelewa kwamba maelezo yote ya Ufalme yanayopendwa na wengi hayajakamilika kwa kiwango cha kutisha—na mara nyingi ni makosa matupu! Kuwa mwangalifu usije ukakataa au kuyafanya ya kiroho MAFUNDISHO YALIYO WAZI kuhusu jinsi Ufalme wa Mungu utakavyokuja kwa sababu rahisi tu kwamba hukuwahi kuyasikia kabla—kwa sababu hakuna mwingine anayeyafundisha. Mungu analo Kanisa Lake na hapa ndipo Anapofunua Kweli Yake.

Lakini yako mengi zaidi ya kujifunza.

Lile “Kundi Dogo”

Yesu alitumia istilahi ya kushangaza kuelezea kundi ambalo litakuwa watawala wa awali katika Ufalme Wake mdogo. Kama Ufalme wenyewe ulivyo, kundi hili halitakuwa kubwa kwa kuanzia. Katika Luka 12, Yesu aliwaagiza watumwa Wake “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme” (fu. 32). “Dogo” ni mikros kwa Kigiriki. Ni kundi-dogo ambalo linachukua ufalme mdogo—ina mantiki na ni rahisi kuelewa jinsi gani!

Mfano mwingine katika Luka 19 unamwelezea kabaila (Kristo) aliyekwenda nchi ya mbali (mbinguni) ili “ajipatie ufalme” (fu. 12). Mfano huu unabeba habari ya pekee sana kwa ajili ya kila Mkristo wa kweli. Unaelezea hukumu, utoaji wa hesabu, unaokuja mara hiyo kwa kundi la “watumwa” wakati wa kuwasili kwa Kristo akileta Ufalme Wake mdogo. Angalia: “...Aliporudi [kutoka mbinguni], Ameupata ufalme Wake, Aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili Ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake” (fu. 15). Baadhi ya watumwa walifaulu jaribio la Mungu, wengine walishindwa.

Kusoma maelezo yote kunafunua kwamba wale wanaofaulu wanawekwa juu ya miji Duniani (siyo Dunia yote kwanza) katika awamu ya kwanza ya Ufalme. Mungu amekuwa akitenda kazi na watu ulimwenguni kote, akiwaandaa kwa ajili ya nafasi za uongozi katika awamu ya kwanza ya Ufalme. Ni baada tu ya kutoa hesabu ya utendaji wa nyuma mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo (Rum. 14:10; 2 Kor. 5:10) ndipo hawa watumwa walioitwa kipekee na kufunzwa wataruhusiwa kutawala.

Mathayo 25 ina maelezo yanayoelekeana, ambamo baadhi wanaambiwa, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako” (fu. 21). Ile “furaha ya Bwana” inahusisha kile ambacho ni awamu ya kwanza ya wokovu sambamba na kupokea sehemu katika kutawala kile ambacho kitakuwa ni Ufalme unaokua haraka—jukumu lililo na kusudi la kuwasaidia wengine waingie katika Ufalme wakati wa awamu yake fupi ya kwanza, ili kwamba pia wafuzu kutawala kitambo baadaye. Kila mmoja anayetamani kuja na kuwa chini ya Ufalme atapata fursa.

Kristo Kama Mfalme

Yesu Kristo, kama Mfalme wa Ufalme ulio kama punje ya haradali, Mwenyewe pia anaanza “kidogo” katika namna Anavyojifunua Mwenyewe na katika awamu ya kwanza inayopelekea kwenye utawala Wake. Maelezo ya Kristo akipaa mbinguni yameshikilia kifungua macho ambacho hakuna yeyote anayekiona. Mitume waliuliza swali: “Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” (Matendo 1:6). Baada ya jibu Lake inaongezea, “walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, Yeye alipokuwa akienda Zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe” (vs. 9-10). Wanaume hawa wawili, kwa hakika malaika, waliuliza, “...Mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Yesu huyu huyu [mtu, siyo Kiumbe Roho katika hali ya utukufu], aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona Akienda zake mbinguni” (fu. 11).

Usemi “Yesu huyu huyu” katika kumrejelea Yesu ni UFUNGUO muhimu sana. Kigiriki kwa hakika kinamaanisha “huyu huyu” Yesu, pamoja na neno la Kigiriki likiwa lile lile limerudiwa katika aya ya asili kwa ajili ya “huyu” na “huyu huyu.” Malaika walikuwa wakisisitiza kwamba Yesu atarudi katika mfanano wa umbile lile lile la kibinadamu Alilokuwa nalo Alipopaa.

Basi si ajabu kwamba mara nyingi Kristo ameitwa “Mwana wa Adam.” Hii ni kwa sababu Anakusudia kuendeleza (ya awali) umbile Lake la karne-ya-kwanza wakati atakaporudi. Hebu tuone uthibitisho zaidi.

Nabii Yeremia alimwelezea Kristo katika Ufalme Wake unaokua kwa jina lisilo la kawaida, wakati pia akimwita Mfalme wake: “Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki Mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku Zake [wakati fulani, lakini siyo mara ile] Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina Lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU” (23:5-6). Kwa Kiebrania “Chipukizi” ni kimea. Kama punje za haradali, vimea pia ni vidogo sana vinapoanza. Picha hii ya “kimea” haipatani kabisa na Yesu Kristo mwenye nguvu akirudi katika umbile lililotukuka.

Sura kumi baadaye Yeremia anaongeza zaidi, akithibitisha kitu nyeti kuhusu vimea: “Ni[ta]mchipushia Daudi Chipukizi la [kimea cha] haki; naye atafanya hukumu na haki...” (33:15). Kwa Kiebrania “chipushia” ni kitendo cha kuotesha. Mungu anasema, kwa hakika, atasababisha kimea kuchipuka. Tafakari uzito wa kile tunachoambiwa. Jukumu la Yesu litakua kutoka dogo kuwa kubwa.

Maelezo yote katika Yeremia yanafungamanisha “Chipukizi” kwa Mfalme Daudi. Angalia unabii mwingine kuhusu Kristo kutoka kwa malaika Gabriel kwenda kwa Mariamu: “Huyo [Kristo] atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba Yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na Ufalme Wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:32-33). Wakati wa kuja Kwake kama punje ya haradali—kwa hakika kufunuliwa Kwake katika Luka 17:30—Kristo anaketi juu ya kiti cha enzi cha Mfalme Daudi kabla ya baadaye kukalia kiti Chake mwenyewe katika Yerusalemu (wakati Daudi anapofufuka kupokea kiti kilichoachwa wazi alichokuwa amekalia Yesu).

Kutoka “Mahali Pake”

Ikithibitisha kwa nguvu Yeremia, Zakaria 6 pia inatoa picha ya ukuaji kuelekea utawala wa ulimwengu mzima. Fungu hili pengine ndilo lililo wazi sana miongoni mwa yale yanayoongelea juu ya Kristo kama Chipukizi: “Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, MTU [kwa mara nyingine, siyo Nafsi Roho katika umbile lenye utukufu] ambaye jina lake ni Chipukizi [kimea]; Naye atakua [chipuka] katika mahali Pake [mahali anapokaa mbali na Yerusalemu], naye Atalijenga hekalu la BWANA. Naam, yeye Atalijenga hekalu la BWANA; naye Atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti Chake cha enzi [wakati wa baadaye]; Naye Atakuwa kuhani katika kiti Chake cha enzi...” (fu. 12-13). Sehemu hii ya mwisho bila shaka inahusisha Kristo akitawala katika utukufu kutokea kwenye hekalu.

Zakaria 6:12 inatoa picha ya Kristo akikua kutokea mahali pasipojulikana—“mahali Pake”—kujenga mahekalu mawili.

Nusu ya kwanza ya fungu inaelezea ujenzi wa Hekalu la kiroho, ambalo tutakuja kuona ni Kanisa. Hii inawiana sawia na Malaki 3:1, ambayo inaelezea Kristo akirudi Duniani kwenye Hekalu Lake. Angalia: “Angalieni, Namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbeleYangu; naye BWANA mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; naam, yule Mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, Anakuja, asema BWANA wa majeshi.”

Hili haliwezi kuwa hekalu halisi katika Yerusalemu kwa sababu hakuna hekalu pale leo. Wayahudi hata hawamiliki Mlima wa Hekalu! Angalia kwamba Malaki anasema Kristo akija kwenye Hekalu Lake inamaanisha kwa watu wanaomtafuta na kumtamani.

Mtume Paulo alilifasili Hekalu hili kama Kanisa: “Hamjui ya kuwa ninyi [Kanisa—watu wa Mungu] mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho ya Mungu inakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi” (1 Kor. 3:16-17). (Pia ona 1 Wakorintho 6:19-20.) Hapa ni jinsi mtume Petro anavyowaelezea Wakristo wa kweli:

“Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai [ikimaanisha yanayoishi], mmejengwa mwe nyumba ya Roho, [u]kuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo” (1 Pet. 2:5). Ni mawe yanayoishi (binadamu) ambao kwa pamoja wanaunda “hekalu la Mungu” la kiroho.

Mahali Ufalme Unakoanzia

Aya fulani zinathibitisha Kristo anahamia Sayuni, na hizi zinatoa fununu juu ya taifa lipi Atakuja kwalo. Unabii kwa ajili ya wakati wetu—siku za mwisho—ambazo karibu hakuna mtu anayeuongelea unapatikana katika Hesabu 24. Nabii Balaam alitabiri, “Siku za mwishoNyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi [Mtawala] itainuka katika Israeli [siyo Yuda]…Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini [huu ni Yerusalemu]” (fu. 14, 17, 19).

Akiitwa “Nyota” hapa, aya zingine zinamweleza Kristo kama “Jua la Haki” (Mal. 4:2), “Nyota ya Asubuhi (2 Pet. 1:19) na ile “Nyota yenye Kung’aa ya Asubuhi” (Ufu. 22:16). Analeta milki Yake—utawala Wake!—pale Yerusalemu na Yuda kutoka taifa lingine la Yakobo wa leo (Israeli). Hii haiwezi kuwa inarejelea tu ukoo wa kuzaliwa kwa Yesu kwa sababu Alizaliwa katika Yuda, na katika Uyahudi. Maandiko mengi yameongelewa katika kitabu changu kamili Amerika na Uingereza katika Unabii (America and Britain in Prophecy) kinaweka wazi tofauti baina ya Yuda na makabila mengine 11 ya Israeli. Kwa hakika, rejeleo la kwanza kwa “Wayahudi” katika Biblia linawaonyesha wakiwa vitani na Israeli (2 Wafalme 16:1-16)! Taifa la leo katika Mashariki ya Kati linaloitwa Israeli kwa hakika ni Yuda, huku mataifa ya kidemokrasia ya Magharibi yanayoongea Kiingereza yakitambulika kama wazao wa makabila mengine ya Israeli wa kale. Yesu Kristo anakuja kwa moja ya nchi hizi, SIYO Yuda!

Mwanzo 49 inafafanua zaidi ni kwa kabila lipi miongoni mwa 11 yaliyosalia Kristo kwanza anarudi kwalo. Angalia mafungu ya 22-24, ambayo yote yanamwelezea Yusufu: “Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matawi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; (kutokea huko [Yusufu!] ni mchungaji, jiwe la Israeli).” Yesu Kristo, bila kupingwa aliye “mchungaji” na “jiwe la Israeli,” ametabiriwa kurudi kwa, na kuweka kambi katika, Yusufu—siyo Yuda. (Marekani na Uingereza katika Unabii – (America and Britain in Prophecy) kinaweka wazi utambulisho wa sasa wa kila kabila.)

Jiji Linalokuja

Tuliona awali kwamba Ufalme umeundwa na vitu vinne—ardhi, mfalme, watawaliwa na sheria. Bila shaka, himaya itakuwa pia na muundo wa kiutawala. Je! Kristo anayajenga haya yote pale anapowasili—au Anakuja nao?

Wanafunzi wale wale waliouliza juu ya Kurudi kwa Kristo katika Matendo 1 wangekuwa wamemsikia akifafanua jambo hili kutoka Yohana 14: “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na Mimi. Nyumbani mwa Baba yangu [Kigiriki: Makazi au makao] mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia…” (fu. 1-2). Kristo anatuambia tuamini chochote anachokaribia kusema—bila kujali kwamba kinaweza kuwa ni kitu kisichoweza kuaminika namna gani! Akiendelea, “…Naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, NITAKUJA TENA niwakaribishe Kwangu; ili Nilipo Mimi, nanyi mwepo” (fu. 2-3). Huyu ni Yesu Kristo akija kwa watu Wake kutokea mbinguni, na si vinginevyo.

Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “mahali” ni topos, kutoka kwalo linapatikana neno topografia (mandhari). Neno pia linaweza kutafasiriwa “mahali au mtaa.” Kristo aliongea juu ya kuleta mahali palipoandaliwa tayari.

Elewa! Kristo analeta majumba kutoka mbinguni. Lakini watakaa wapi?

Ufunuo 22 inaonyesha picha ya jiji linalokuja. Kurudi kwa Kristo ndio muktadha: “Tazama, Naja upesi, na ujira Wangu u pamoja Nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo [hii ni namna ya kutoa hesabu au hukumu iliyoelezwa awali]. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia jijini kwa milango yake.”

Kinachofuata ni maelezo ya kipekee ya mpangilio wa jiji: “Huko nje wako mbwa [manabii wa uongo na watumishi], na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya”. (fu. 12-15). Aya hii inaunganishwa na Kristo akiwa mzao [Chipukizi] la ukoo wa Mfalme Daudi: “Mimi Yesu Nimemtuma malaika Wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota yenye Kung'aa ya Asubuhi” (fu. 16).

“Jiji” hili haliwezi kuwa “Yerusalemu Mpya,” unaosimamishwa wakati wa kuanza kwa utawala wa Kristo wa miaka 1,000 baadaye. Wale wote wanaompinga Mungu—kila mtu Duniani aliyepokea Alama ya Mnyama—atakuwa ameuawa kabla ya kuwasili kwa jiji hilo. Kwa hiyo aina ya watu hapo juu hawawezi kuwa “nje”—ikimaanisha nje yake. Fikiria tu shetani atakuwa amefungwa wakati huu. Hii inafanya isiwezekane kwamba pangeweza kuwepo hata mchawi mmoja mahali popote Duniani. Vivyo hivyo kwa manabii wa uongo na waabudu sanamu. Pia, kwa kuwa Shetani ndiye “baba wa mauaji na uongo” (Yohana 8:44), hakutakuwa na mauaji au kupenda uongo.

Ufunuo 21 yote na sura ya 22 fungu la 5, Yohana anarekodi ujumbe wa Kristo juu ya Yerusalemu Mpya wa ajabu ambao utakuja Duniani mwanzoni mwa utawala wa Millenia wa Kristo baadaye. Mwishoni mwa Ufunuo 22, Mungu anarejelea kwa ufupi tena Yerusalemu Mpya, akiuita “Mji Mtakatifu.” Usiikose tofauti muhimu!

“Kazi ya Ajabu na Kushangaza”

Kabla ya Ufalme kama mbegu ya haradali, idadi kubwa sana watakuja kujua kweli hizi za Biblia katika kile ambacho Mungu kupitia nabii Habakkuki, anakiita “Kazi ya kustaajabisha” Angalia: “Angalieni, enyi mlio kati ya mataifa, katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda tendo siku zenu, ambalo hamtaliamini hata mkiambiwa” (1:5). Katika maandiko, “Kazi” huwakilisha watumishi wa Mungu wakifundisha na kuonya wale wote ambao watasikiliza. Je, utaamini ripoti tangulizi kwa Kazi hii?

Nabii Isaya anachambua kwa kina kile Habakkuki alichotabiri. “kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa”(29:14).

Paulo pia alimnukuu Haakkuki katika kitabu cha Matendo, akibadilisha kidogo: “Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii (Habakkuki). Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.

Hii ina maanisha lazima tutegemee kazi kubwa, yenye kutingisha-Dunia kuutangulia Ufalme wa Mungu—kazi ambao itafika mbali-sana itashangaza akili—kazi ambayo haiwezi kueleweka kikamilifu mpaka itakapoonekana—kiasi kwamba wengi watakapoisikia hawataiamini! Kijitabu hiki si tu kwamba kinaitangaza kwako, lakini kinaongeza kwamba inakuja upesi!

Mpinga Kristo

Wengi wanashangaa kujifunza kwamba Biblia inamwita Shetani “mungu wa ulimwengu huu” (II Kor. 4:4), ambaye katika historia yote “huyadanganya mataifa” (Ufu, 20:3). Katika Mathayo 4, mwovu alidai kuwa mmiliki wa “falme zote za ulimwengu” (fu. 8)—ukweli ambao Kristo hakuupinga.

Shetani anatafuta kupotosha kila kitu. Angalia kile kinachofuata “kazi ya ajabu na kushangaza” na inayotangulia Ufalme wa Mungu. Paulo anarekodi, “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana siku hiyo haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu” (fu. 3). Mtume Yohana alimwita mtu huyu “mpinga Kristo” (I Yoh. 2:18).

Aya ile ile inaendelea mbele kuonyesha chanzo—kiwango—cha uwezo huu: “...yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara” (II Thes. 2:9). Analeta uwezo wote wa mwovu kuwa nao—mfano wa kile ambacho Ayubu alikipitia, lakini kwamba ulimwengu kwa pamoja hata haujaanza kufikiria!

Mtu huyu atakuwa juu ya ulimwengu wote wakati wa kuja kwake. Anadai kuwa Mungu: “...hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu” (fu. 4). Uwezo wa mtu huyu (na mafungu mengi yanaonyesha kwamba kuna wanaume wengine wawili wanaofanyakazi sambamba na chini yake) unavuka ng’ambo ya Ukristo—yeye “ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa” (fu. 4)—kila dini Duniani!

Awamu ya kwanza ya Ufalme wa Mungu itaanza siku utawala wa mtu huyu unakoma. Tukirudi kwa II Wathesalonike, “...Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza (huyo) kwa mwangaza wa Kuja Kwake” (2:8).

Picha Isiyotatanisha

Muhtasari wa msingi. Kristo anakuja kwanza kwa watu Wake—Hekalu Lake. Ufalme wa Israeli awali unaongozwa na kundi dogo chini ya Kristo. Awali ataficha uwepo Wake kwa kuwa kama chipukizi. Ufalme utaongezeka katika idadi ya watawaliwa kabla Kristo hajahamishia Yerusalemu serikali ya ulimwengu mzima iliyo tayari kupanuliwa sana. Kutokea pale atatawala mataifa yote pamoja na kundi kubwa la watakatifu Wake likitoka kwenye kile ambacho kitakuwa kundi kubwa zaidi wakati huo.

Kama umeshangaa, hata kushtushwa, kutokana na kweli rahisi ndani ya mifano ya Yesu, na unashangaa kwa nini kamwe hujaambiwa maana zake, tambua kwamba aliiunda ili kuwakanganya wale ambao Alikuwa hawaiti. Hiki hapa ndicho Kristo alichosema: “Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba...” (Math. 13:13-15). Walio wengi huchagua kufumba macho yao kwa ukweli wa Biblia. Mifano huwazuia wasifahamu kile ambacho hawataki kusikia.

Lakini UNAWEZA kufahamu! Akiongea zaidi juu ya sababu za mifano, Mathayo aliongeza, “Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno... akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu misingi ya ulimwengu” (13:34-35).

Umepokea maarifa ya thamani kubwa—yaliyositirika kutoka kwa ulimwengu. Siyo tamaduni zinazofahamika na wengi—hadithi zilizotungwa—za Ukristo wa leo, lakini maneno ya wazi ya Kristo—ambayo yanajulikana sasa katika wakati wetu. Mungu amekuwa akingojea kwa miaka maelfu kusimamisha Ufalme Wake katika Dunia ambayo inauhitaji sana. Lakini hautakuja kama mabilioni wanavyotegemea. Fikiri. Umesikia neno la Ufalme kabla haujaja. Kuna faida kubwa katika hili! Leo Kristo anaandaa timu iliyochaguliwa maalumu ya watawala kabla ya kuwasili kwake waliofuzu kutawala chini.

Miaka elfu mbili iliyopita, Yesu Kristo alijenga Kanisa Lake—Kanisa la kweli—lile pekee Alilolijenga. Kanisa hili linaamini na kufundisha KWELI za Biblia—zote—siyo mawazo ya wanadamu—yoyote kati ya hayo! Watu wa Kanisa hili siku zote wamesimama katika UWAZI WA UHAKIKA wa kile ambacho Mungu anaahidi kwa ajili ya walio hai mwishoni—siyo matumaini ya uongo ya mavumbuzi ya wanadamu.

Sasa­—utang’ang’ania imani zilizoshikiliwa muda mrefu—au utashikilia UKWELI unaobadili-maisha?