Kila mwaka baada ya Kutoa shukurani, mawazo ya watu wengi hugeukia kwenye Krismasi. Ni wakati ambao wale wanaodai kuwa Wakristo wanadhaniwa kufokasi juu ya Yesu Kristo. Hata hivyo, ni majira ya “Kristo-masi”!
Rudofu Kulungu wa nchi za baridi mwenye Pua-nyekundu, Mashada ya mholi (mti wenye majani yaliyo na ncha kali), miti iliyopambwa, mlimbo (mmea ambao matunda yake hutoa ulimbo), salamu za majira, muziki wa majira, “njugu zinazokaangwa kwenye moto hadharani” na Baba Krismasi vyote hivi vinaenda pamoja na sikukuu hii. Vyote hivi huleta hisia nzuri kwa wale wanaoisherehekea.
Nilikulia kwenye familia ambayo ilitunza Krismasi, na lilikuwa tukio kubwa sana kwenye familia yetu kila mwaka. Hatukubakisha chochote kilichostahili kufanywa kwenye tukio hili. Siku ya 24 Desemba, msisimko ulizidi kila dakika iliyokuwa inapita. Wazazi wangu hata waliandaa kahawa nyeusi kwa ajili ya Baba Krismasi muda mfupi kabla ya kutupeleka kulala. Mimi sikuzote nilikuwa nashangaa ni kwa jinsi gani walijua kwamba Baba Krismasi alipenda kahawa nyeusi—namna ile ile wazazi wangu walivyopenda kahawa yao iwe. Baada ya kwenda kulala usiku wa mkesha wa Krismasi, sikuweza kulala wala kusubiri kuamka asubuhi ili kuona yale yote ambayo “Baba Krismasi” alikuwa ameniletea.
Krismasi inafikiriwa na wengi kuwa ni wakati wa ajabu sana, ukiwaelekeza wahusika kwenye utoaji, umoja wa familia, muziki mzuri na mapambo, kusherehekea kwa kula vyakula maalumu na kuimba vibwagizo vya Krismasi katika ujirani wote (ndivyo familia yangu ilivyofanya kila mwaka). Yote haya yakidhaniwa kuwa yamejengwa katika kumwabudu Kristo. Bila shaka, Biblia inatuagiza kufanya haya yote—sawa?
Majibu yatakushtua!
Kwa nini watu wanafikiri kwamba Krismasi ni ya ajabu sana? Kwa hakika ilionekana kuwa ya ajabu kwangu. Niliamini kile wazazi wangu walichoniambia. Sikuwa na sababu ya kuwatilia shaka. Walikuwa wakinifundisha tu kile ambacho walifundishwa na wazazi wao. Kamwe sikuhoji asili ya kweli ya Krismasi—au kile Mungu anachosema juu yake!
Wengi huwa hawafikiri kwa nini wanaamini kile wanachoamini au kufanya kile wanachofanya. Tunaishi katika ulimwengu uliojawa desturi, lakini wachache wanatafuta kuelewa asili zake. Kwa ujumla huwa tunazikubali bila swali. Watu wengi kimsingi wanafanya kile ambacho kila mmoja anafanya—wanafuata umati kwa sababu ni rahisi!
Hebu tuchunguze kwa makini mizizi ya Krismasi. Hebu tuangalie kwa nini watu wanafuata desturi zinazoambatana nayo. Kwa nini inatunzwa siku ya 25 Desemba? Je, Kanisa la mwanzo la Agano Jipya liliitunza? Kijitabu hiki kimejawa na ukweli wa historia na Maandiko ambayo, yakiwekwa pamoja, huchora picha kamili. Hebu tuachane na kudhani na tukubali tu kile kinachoweza KUTHIBITISHWA!
Asili ya Kipagani
Katika mwaka 1990, bodi ya shule ya Soloni, Ohio (kitongoji cha Cleveland) ilipiga marufuku uzaliwa wote na mionekano mingine ya Krismasi kwenye mali yote ya shule yoyote kwa sababu walihisi kwamba inakiuka utengano wa kanisa na serikali. Walipelekwa mahakamani wakati wazazi wenye hasira nyingi walipowapinga, wakihisi kwamba Krismasi ilikuwa inaibwa kutoka kwa watoto wao na kwa jamii. Bodi ilishindwa katika kesi hii! Wananchi walikuwa wamedai kwamba Krismasi ni desturi ya ulimwengu mzima ambayo haikuwa sehemu ya, na ilizidi, dini. Ilionekana kuwa ya ki-dunia—karibu sehemu ya tamaduni zote ulimwenguni.
Uamuzi wa mahakama ulikazia kwamba Krismasi haina mizizi ya Ukristo! Hata hivyo, mtazamo wa mahakama pia ulitoa angalizo kwamba usomaji wa Biblia na maombi ni wazi vina-ambatana na Ukristo—kukiri kunakoshangaza! Mahakama ilihitimisha kwamba utunzaji wa Krismasi na mazingira ya zizi yanaweza kubaki kwa sababu siyo sehemu hasa ya ama Ukristo au dini—ila maombi na kusoma Biblia, ambavyo ni [vya Ukristo au dini], lazima viondolewe kutoka mashuleni!
Karibu kila kipengele cha utunzaji wa Krismasi kina mizizi katika mila na dini za Kirumi. Fikiria kukiri kufuatako kutoka kwenye gazeti kubwa la Amerika (The Buffalo News, Nov. 22, 1984): “Kielelezo cha mapema kabisa kuhusu Krismasi kushikwa siku ya 25 Des. kinapatikana kutoka karne ya pili baada ya kuzaliwa kwa Yesu. Huu ndio unaofikiriwa kuwa wakati wa sherehe za kwanza kabisa za Krismasi zilizofanyika kwa kuheshimu Satanalia ya Kirumi, sikukuu ya mavuno iliyoashiria kilele cha majira ya baridi kali—kurudi kwa jua—na ilimwadhimisha Zohali, mungu wa kupanda. Satanalia ulikuwa wakati wa fujo, uliopingwa sana na viongozi wenye kushikilia maadili miongoni mwa kilichokuwa bado kikundi kidogo cha Kikristo. Krismasi ilikuwa, mwanazuoni mmoja alisema, kama njia ya kubadilisha kutoka kuabudu jua na kumwabudu Mwana. Hadi kufikia mwaka 529 B.K., baada ya Ukristo kuwa dini rasmi ya serikali ya Himaya ya Rumi, Mfalme mkuu Justinian aliifanya Krismasi kuwa sikukuu ya kitaifa. Sherehe za Krismasi zilifikia kilele chake—baadhi wanaweza kusema wakati wake mbaya kabisa—katika kipindi cha zama za kati ulipofikia wakati wa utumiaji mkubwa wa wazi na sherehe makelele na vifijo.”
Fikiria nukuu hizi kutoka Ensaiklopidia ya Kikatoliki, toleo 1911, chini ya “Krismasi”: “Krismasi haikuwa miongoni mwa sikukuu za mwanzo za Kanisa…Ushahidi wa kwanza wa sikukuu ni kutoka Misri.” Zaidi, “Mila za kipagani zilizojikita kuzunguka kalenda ya Januari zilipelekea kwenye Krismasi.” Chini ya “Siku ya Natali,” Origen, mwandishi wa awali wa Kikatoliki, alikiri, “…Katika Maandiko, hakuna mtu aliyerekodiwa kuwa aliwahi kutunza sikukuu au kufanya karamu kubwa kwenye siku ya kuzaliwa kwake. Ni wenye dhambi pekee (kama Farao na Herode) wanaofanya shangwe kuu juu ya siku zao za kuzaliwa katika ulimwengu huu” (msisitizo wa kwangu).
Ensaiklopidia Amerikana, toleo 1956, inaongeza, “Krismasi…haikutunzwa kwenye karne za kwanza za kanisa la Kikristo, kwa kuwa kawaida ya Wakristo ilikuwa ni kusherehekea kifo cha watu maarufu badala ya kuzaliwa kwao…sikukuu ilianzishwa kwa kukumbuka tukio hili [kuzaliwa kwa Kristo] katika karne ya 4. Katika karne ya 5 kanisa la Magharibi liliagiza sikukuu isherehekewe kwenye siku ya matambiko ya Mithireiki ya kuzaliwa kwa jua na kwenye kufunga Satanalia, maana hapakuwa na maarifa ya uhakika wa siku ya kuzaliwa kwa Kristo.”
Hakuna kukosea ASILI ya sherehe za kisasa za Krismasi. Vyanzo vingine vingi vingeweza kunukuliwa na tutarudi kwa hili baadaye. Hebu tuanze kuweka pamoja mambo mengine yaliyotendeka.
Ilikuwa miaka 300 baada ya Kristo kabla ya kanisa la Rumi kutunza Krismasi, na haikutokea mpaka karne ya tano ilipoamuriwa kutunzwa katika himaya yote kama sikukuu rasmi inayomwadhimisha “Kristo.”
Je Kristo Anaweza Kuadhimishwa kwa Krismasi?
Uhalalishaji wa kawaida ambao mtu atausikia kuhusiana na Krismasi ni kwamba watu wamebadilisha mila za zamani za kipagani na dhamira kwa kudai kwamba sasa “wanafokasi juu ya Kristo.” Nimewasikia wengi wakisema kwamba “wanamwadhimisha Kristo” katika utunzaji wao wa Krismasi. Tatizo ni kwamba Mungu hasemi kwamba hii inakubalika Kwake! Kwa kweli, ni dhahiri Anaamurisha kinyume chake! Kutunza Krismasi kunamfedhehesha Kristo! Anachukulia kila kitu kinachohusiana na hili kuwa ni machukizo! Hivi karibuni tutaona kwa nini.
Kristo alisema, “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Math. 15:9). Krismasi si amri ya Mungu—ni mapokeo ya wanadamu. Kristo aliendelea, “Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu” (Marko 7:9). Kila mwaka, ulimwenguni kote, siku ya 25 Desemba, mamia ya mamilioni wanafanya hivyo!
Tutaona kwamba Mungu anaamuru dhahiri kwamba, “Msifuate njia ya mataifa.” Lakini watu wengi hawamwogopi Mungu, na Anawaruhusu kufanya maamuzi yao wenyewe. Wanadamu ni viumbe huru—huru kumtii au kumwasi Mungu! Lakini ole wao wasiojali Neno dhahiri la Mungu!
Je Kristo Alizaliwa Siku ya 25 Desemba?
Kristo alizaliwa majira ya majani kupukutika ya mwaka. Wengi wameamini kimakosa Alizaliwa mnamo kipindi cha mwanzo wa majira ya baridi—25 Desemba! Hawako sahihi! Angalia Maoni ya Adam Clarke, kitabu cha 5, ukurasa 370, toleo la New York: “Ilikuwa kawaida miongoni mwa Wayahudi kuwapeleka nje jangwani kondoo wao mnamo kipindi cha Pasaka [mapema majira ya machipuko], na kuwarudisha nyumbani mara mvua za kwanza zinapoanza.” Mvua za kwanza zilianza mwazoni hadi katikati ya majira ya majani kupukutika. Tukiendelea na nukuu hii: “Wakati walipokuwa nje, wachungaji waliwaangalia kondoo usiku na mchana. Mara…mvua ya kwanza ilipoanza mapema mwezi wa Machi-esvan, ambayo inatoa jibu kwa sehemu juu ya mtazamo wetu wa Oktoba na Novemba [huanza wakati fulani Oktoba], tunakuta kwamba kondoo walifugwa nje katika nchi ya wazi wakati wote wa majira ya joto. Na kwa kuwa wachungaji hawa walikuwa bado hawajarudisha nyumbani makundi yao, ni ukweli unaodhaniwa kwamba Oktoba ilikuwa bado haijaanza na kwamba, kwa mantiki hiyo, Bwana wetu hakuzaliwa siku ya 25 Desemba, wakati ambao hapakuwa na makundi yoyote nje makondeni; wala isingeweza kuwa alizaliwa baada ya Septemba, kwa kuwa makundi ya kondoo bado yalikuwa makondeni wakati wa usiku. Kwa msingi huu, kuzaliwa kwa Yesu Kristo Desemba lazima kutupiliwe mbali. Ulishaji wa makundi ya kondoo makondeni wakati wa usiku ni tukio la hakika lililokuwa katika utaratibu wa matukio yaliyopangika kwa mwaka [wendo wa hakika]… Angalia nukuu kutoka Talmudists katika Lightfoot.”
Luka 2:8 inafafanua kwamba wakati Kristo alipozaliwa, “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Angalia kwamba walikuwa “wakikaa” makondeni. Jambo hili kamwe halikutokea Desemba. Ezra 10:9-13 na Wimbo Uliobora 2:11 zinaonyesha kwamba majira ya baridi ulikuwa ni wakati wa mvua na wachungaji hawangeweza kukaa kwenye makonde ya wazi yenye baridi usiku.
Ensaiklopidia nyingi hutamka dhahiri kwamba Kristo hakuzaliwa siku ya 25 Desemba! Ensaiklopidia ya Katoliki inathibitisha hili moja kwa moja. Kuna uwezekano mkubwa, Kristo alizaliwa wakati wa majira ya majani kupukutika! Ufafanuzi mrefu wa kitaalam utathibitisha jambo hili.
Kwa kuwa sasa tunajua kwamba 25 Desemba kwa vyovyote haikuwa karibu na tarehe hasa ya kuzaliwa kwa Kristo, sikukuu inayoambatana na tarehe hii ilitoka wapi?
Sasa soma nukuu hii chini ya “Krismasi”: “Katika ulimwengu wa Kirumi Satanalia (17 Desemba) ulikuwa wakati wa kuwa na furaha na kupeana zawadi. 25 Desemba pia iliheshimiwa kama tarehe ya kuzaliwa mungu-siri Mithra wa Irani, aliye Jua la Haki. Panapo mwaka mpya wa Kirumi (Januari 1), nyumba zilipambwa kwa kijani na mianga, na zawadi zilitolewa kwa watoto na masikini. Matambiko ya Ujerumani na Seltiki Yuli yaliongezwa kwenye maadhimisho haya wakati makabila ya Teutonic yalipojipenyeza na kuingia Gaul, Uingereza na Ulaya ya kati. Chakula na ushirika mzuri, kigogo kinachochomwa mkesha wa Yuli, na keki za siku ya Yuli, mapambo ya kijani na miti ya misonobari, zawadi na salamu vyote viliadhimisha nyanja tofauti za majira haya ya sikukuu. Moto na mianga ishara za joto na maisha ya milele, wakati wote zimehusishwa na sikukuu ya majira ya baridi, ya kipagani na Kikristo” (Ensaiklopidia Britannika, Toleo 15, Kit. II, uk. 903).
Nukuu ya mwisho juu ya uchaguzi wa 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa Kristo ni ya lazima. Angalia makala katika The Toronto Star, Desemba 1984, na Alan Edmonds, yenye kichwa, “Tunawiwa mengi na Wadruidi, Wadachi”: “Mageuzo hayo yalitia doa kwenye Krismasi. Wakati huo, bila shaka, wanasiasa wa kidini wajanja walikuwa wamekubali sikukuu ya kipagani ya katikati ya majira ya baridi kama ilivyodaiwa kuwa tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu, wa Nazareti, na wakatumbukiza humo mengine machache mazuri ya kipagani ili kufanya utwaaji madaraka wao ukubalike zaidi.”
25 Desemba haikuchaguliwa kwa sababu ilikuwa ni kuzaliwa kwa Kristo au kwa sababu eti ilikuwa karibu na hapo. Ilichaguliwa kwa sababu iligongana na sikukuu ya kipagani ya ibada ya sanamu ya Satanalia—na sherehe hii ni lazima ichunguzwe kwa makini. Katika tukio lolote, hatujui hasa tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo. Ingawa Mungu bila shaka angeweza kuiweka wazi, Alichagua kuificha kutoka macho ya ulimwengu!
Zohali Alikuwa Nani
Nukuu zilizotangulia zilianzilisha somo la Satanalia. Hebu kwa uangalifu tujifunze Zohali alikuwa nani hasa. Fikiria nukuu ifuatayo kutoka kwenye gazeti lingine kubwa la Kiamerika, The Democrat and Chronicle, Rochester, New York, Desemba 1984: “Sikukuu ya Kirumi ya Satanalia, 17-24 Des. iliwavuta raia kupamba nyumba zao na mapambo ya kijani na mianga na utoaji wa zawadi kwa watoto na maskini. Sikukuu ya 25 Des. ya natalis solis invicti, kuzaliwa kwa jua lisiloshindwa, iliamuriwa na mfalme mkuu Aurelian katika mwaka 274 B.K. kama sherehe za Kilele cha Majira ya Baridi, na wakati fulani (baadaye)… ilifanywa-ya-Kikristo kama tarehe ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mwana wa Nuru.”
Dkt. William Gutsch, mwenyekiti wa Makumbusho ya Historia Asili ya Kiamerika—Hayden Planetarium, alithibitisha zaidi jina la asili [kwanza] la Krismasi kwa nukuu hii siku ya 18 Desemba, 1989, kwenye gazeti la The Reporter Dispatch, la Westchester, NewYork:
“Warumi wa awali walikuwa hawasherehekei Krismasi isipokuwa sikukuu ya kipagani iliyoitwa Satanalia. Ilitokea kila mwaka mnamo mwanzoni mwa majira ya baridi, au kilele cha majira ya baridi. Huu ulikuwa wakati ambapo jua lilikuwa limefikia kimo chake cha chini angani na mchana ulikuwa unaanza kuwa mrefu, hivyo kuhakikisha majira mengine ya ukuaji.
“Ikiwa matandiko mengi ya Satanalia, hata hivyo, yanaonekana kwenda sambamba na kile wengi wetu tunafanya leo, tunaweza kuona wapi tuliazima…mapokeo yetu ya sikukuu. Na kwa hakika, imependekezwa kwamba wakati inawezekana Kristo hakuzaliwa mwishoni mwa Desemba, Wakristo wa mwanzoni—wakati huo kikiwa kikundi kisichotambulika kisheria—waliihamishia Krismasi kwenye wakati wa Satanalia ili kujificha wasijulikane wakati wakisherehekea sikukuu yao wenyewe.”
Satanalia, kwa hakika, ilimsherehekea Satuni (Zohali)—mungu wa moto. Saturday (Jumamosi) ilipata jina lake kutokana na mungu huyu, kama yalivyo majina ya siku zingine za juma (katika kiingereza) yalitokana na miungu ya kipagani—siku ya Jua (Jumapili), siku ya Mwezi (Jumatatu), siku ya Twisi (Jumanne), siku ya Woden (Jumatano), siku ya Thor (Alhamisi), siku ya Frigga (Ijumaa) na siku ya Satuni (Zohali) (Jumamosi). Lakini Zohali alikuwa nani? Alikuwa mungu wa upandaji (upanzi) kwa sababu joto la jua lilikuwa linahitajika ili kuruhusu upanzi na ukuaji wa mimea ya mazao. Alikuwa pia akiabudiwa katika sikukuu ya kipindi hiki cha majira ya baridi kali ili apate kurejea (alikuwa “jua”) na kutia joto dunia tena ili upanzi wa majira ya machipuko uweze kutokea. Sayari Zohali baadaye iliitwa kwa jina lake kwa sababu, miongoni mwa sayari zote, pamoja-na zile pete zake na rangi ya wekundu mwangavu, ilimwakilisha vizuri zaidi mungu wa moto!
Karibu kila jamii iliyostaarabika ina mungu wa moto/jua. Wamisri (na wakati mwingine Warumi) walimwita Vulcan. Wagiriki walimwita Kronos, vile vile kama Wafoenike—lakini pia walimwita Zohali. Wababeli walimwita Tammuzi, Moleki au Baali, kama walivyofanya Wadruidi. Haya yote yalikuwa ni majina mbalimbali ya Nimrodi, mwasi wa kibiblia anayejulikana sana kwa ubaya wa Mwanzo 10. Nimrodi alifikiriwa kuwa baba wa miungu yote ya Kibabeli.
Kafara za Watoto
Angalia kitendo hiki cha kutisha kilichoambatana na ibada ya mungu moto (Nimrodi, Zohali, Kronos, Moleki na Baali) katika nukuu ifuatayo kutoka The Two Babylons [Babeli Mbili], Alexander Hislop, ukurasa wa 231:
“Sasa, hii inaenda sawa na tabia ya Kiongozi Mkuu wa mfumo wa kuabudu-moto. Nimrodi, kama mwakilishi wa moto ulao ambao kwao waathiriwa wa kibinadamu, hasa watoto, walitolewa kama kafara, alitazamwa kama mraruaji mkuu wa watoto…alikuwa, hakika, baba halisi wa miungu yote ya Kibabeli; na, kwa hiyo, kwa tabia hiyo alikuja kujulikana hivyo duniani kote. Kama Baba wa miungu, alikuwa, kama tulivyoona, akiitwa Kronos; na kila mmoja anajua kwamba simulizi ya kipekee ya Kronos ilikuwa hii, kwamba, ‘alirarua watoto wake mara tu walipozaliwa.’ (Lempriere Classical Dictionary, ‘Satuni.’)…Hadithi hii ina maana zaidi yenye kina; lakini pale inapotumiwa kwa Nimrodi, au ‘Mwenye Pembe,’ inarejelea ukweli, kwamba, kama mwakilishi wa Moleki au Baali, watoto wachanga ndio walikuwa kafara inayokubalika zaidi katika madhabahu yake. Tunao ushahidi wa kutosha na wa kusikitisha juu ya somo hili kutoka kumbukumbu za zamani za kale. ‘Wafoenike,’ anasema Eusebius, ‘kila mwaka waliwatoa kafara kwa Kronos au Zohali wapendwa wao na wazaliwa wao pekee.’”
Lakini kwa nini kafara ya binadamu ilikuwa kitu muhimu sana kwa ibada ya mungu huyu wa kutisha? Kitu gani kizuri ambacho wanadamu waliweza kufikiri walikiona katika kuchinja watoto wao? Ikiendelea: “…yeye aliyeukaribia moto angepokea nuru kutoka kwa uungu” na “kupitia moto wa kiungu madoa yote yaliyotokana na vizazi yangeweza kufutiliwa mbali.” Kwa hiyo, “watoto walipitishwa motoni kwa Moleki” (Yer. 32:35).
Ikiwa inashangaza kama inavyoonekana, wanadamu waliodanganywa hakika waliamini walikuwa wanampendeza “mungu” wao kwa kuwatoa kafara kwake watoto wao wadogo wasio na hatia. Waliamini moto uliwasafisha kutoka dhambi ya asili. Fundisho la kipagani la kukaa pagatori kwa muda kusafisha nafsi kutoka dhambi zote lilitokana na imani hii!
Nimrodi Alikuwa Nani?
Sasa lazima tuangalie kwa karibu zaidi kwamba alikuwa nani huyu mtu mashuhuri wa kibiblia, Nimrodi. Tumekwisha kumwona kama mmoja wa miungu ya uongo ya awali katika historia, lakini nini zaidi chaweza kueleweka?
Mwanzo 10:9 inasema kuhusu Nimrodi, “Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za [mahali pa] Bwana.” Kwa hakika alijaribu kuchukua mahali pa Mungu.
Mwanahistoria mashuhuri wa Kiyahudi, Josephus, anarekodi katika Jewish Antiquities ushahidi muhimu wa jukumu la Nimrodi katika ulimwengu baada ya gharika. Angalia: “Pia pole pole alibadilisha serikali na kuwa udikteta…vile vile [Nimrodi] alisema angejilipiza kisasi kwa Mungu, kama angekuwa na mawazo ya kuugharikisha tena ulimwengu; maana angejenga mnara mrefu sana ambao maji yasingeufikia…Sasa makutano walikuwa tayari sana kufuata dhamira ya Nimrodi, na kukienzi kama unyonge kitendo cha kujisalimisha kwa Mungu” (Kt. I, Su. IV, seh. 2, 3).
Chini ya majina mengi, mwasi wa awali zaidi wa kibinadamu na pengine mkuu kuliko wote amekuwa akiabudiwa katika dini zote za uongo. Israeli ya kale iliendelea kuangukia katika kuwatumikia miungu mingi ya uongo ambayo iliwakilishwa na Nimrodi.
Ezekieli 18:13-14 inarekodi picha ya wanawake wa Israeli “wakimlilia Tammuzi.” Huyu Tammuzi (mungu wa moto) alifikiriwa kuwa Nimrodi na etimolojia (elimu ya asili na historia ya neno) ya neno lenyewe inashangaza. Tam inamaanisha “kufanya kamilifu” na muzi “moto.” Maana iko wazi katika mwanga wa kile tulichokwisha kujifunza. Bila kutegemea, katika Vita vya Tufani ya Jangwani baina ya Iraki na Kuweiti, Saddam Hussein aliita moja ya makombora yake “Tammuzi.” Bila shaka alielewa kwamba maana yake ilihusisha moto.
Kuchomwa moto kwa ajili ya Moleki
Hebu tuangalie jinsi ambavyo watu wa Mungu, Israeli, walimwabudu Baali/Moleki mara walipomwacha Mungu wa kweli: “Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni Mwangu kwamba walitende chukizo hilo...” (Yer. 32:35)
Angalia kwamba Mungu Mwenyewe anasema kwamba machukizo makubwa kama hayo kamwe hata hayakuingia moyoni Mwake: “Nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni Mwangu; basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo” (Yer. 19:5). Fungu la 6 linaunganisha bonde la Tofethi au Hinomu na tendo hili. Yeremia 7:31 inaunganisha Tofethi na Hinomu kwa kafara za watoto. Tofethi inamaanisha “ngoma.” Ngoma zilipigwa ili kuzamisha vilio vya waathiriwa katika miali ya moto.
Angalia nukuu hii kutoka Paradise Lost (Paradiso Yapotea), na John Milton, juu ya mungu wa kutisha Moleki: “Kwanza, Moloki, mfalme katili aliyejipaka damu ya kafara za wanadamu, na machozi ya wazazi, Ingawa kwa kelele za Ngoma na milio ya Matari Vilio vya watoto wao havikusikiwa, ambao walipitishwa motoni Kwa ajili ya Sanamu yake katili.” Bila shaka, kila mmoja atasema kwamba leo watu hawawatoi kafara watoto wao kwa Moleki, lakini endelea kusoma.
Katika Agano Jipya, mfia dini Stefano alipigwa mawe hadi kufa, angalau kwa sehemu, kwa sababu aliwashitaki wasikilizaji wake kuabudu sanamu hii ya uovu (Matendo 7:43).
Wakati mfalme mwenye haki Josia lipoketi katika kiti cha enzi, kama mfalme wa Yuda, aliharibu madhabahu katika Bonde la Tofethi (au Hinomu—bonde lile lile ambalo Kristo alilifananisha na moto wa “jehanamu” katika Marko 9:43-49) mara baada ya kuingia madarakani. Aligundua uovu mkuu wa matendo yaliyokuwa yakitendeka pale.
Wadruidi na Kafara za Wanadamu
Watu wengi wamewasikia Wadruidi. Wachache wanawajua kuwa ni akina nani na walikuwa nini.Tutawarejelea baadaye na kuwaunganisha na matendo ya Krismasi yanayojulikana vyema. Lazima kwanza tuainishe umuhimu wao kihistoria kuhusiana na kafara za wanadamu.
Julius Caesar ni chanzo cha habari kinachofahamika sana kuhusiana na Wadruidi. Hii inapatikana kutoka Ensaiklopidia Britannika. Nukuu hii chini ya “Wadruidi,” inaeleza kwa wazi walikuwa akina nani: “Wadruidi, daraja la wasomi miongoni mwa Waseltiki wa zamani, ambao jina lao linamaanisha Kujua (au Kupata) Mti wa Mwaloni. Walionekana kuingia mara kwa mara kwenye misitu ya mialoni na walitenda kama makuhani, waalimu na mahakimu. Rekodi za awali zinazojulikana za Wadruidi zinatokea karne ya 3 [K.K.]…Wadruidi walisimamia kafara za umma na binafsi, na vijana wengi waliwaendea kupata maelekezo. Walitolea hukumu matata yote ya umma na ya watu binafsi na kutangaza adhabu…Kanuni ya msingi ya Wadruidi ilikuwa kwamba nafsi haifi…(walitoa) sadaka waathiriwa wa binadamu kwa ajili ya wale waliokuwa mahututi au katika hatari ya kifo vitani. Maboma makubwa yaliyojengwa kwa fito yalijazwa watu walio hai na kisha kuchomwa moto; ingawa Wadruidi walichagua wahalifu kwa kupendelea, walitoa kafara waathiriwa wasio na hatia kama ililazimu.”
Agano la Kale limejaa hukumu za Mungu kwa Waisraeli kwa ajili ya kufuata mila za mataifa yaliyowazunguka—na tunakusanya mambo muhimu yaliyotendeka yanayofunua picha inayoshtua. (Kwa kujifunza zaidi juu ya somo hili, soma kijitabu chetu Siku Takatifu za Mungu au Sikukuu za Wapagani?)
Dhima ya Ulaji wa Nyama ya Watu
Ukweli mwingine juu ya asili ya Krismasi unachipuka kutoka neno la kisasa la Kiingereza cannibal. Kitendo hiki kina mizizi yake katika utendaji mkuu wa makuhani wote wa Baali. Weka akilini kwamba neno la Kiebrania kwa ajili ya kuhani ni Cahn.
Fikiria nukuu ifuatayo kutoka The Two Babylons (Babeli Mbili), na Alexander Hislop, ukurasa 232: “Na ilikuwa kanuni ya Sheria ya Musa, kanuni ambayo bila shaka ilitokana na imani ya wazee, kwamba kuhani ni lazima ale sehemu ya chochote kilichotolewa kama sadaka ya dhambi (Hesabu xviii. 9, 10). Hivyo basi, makuhani wa Nimrodi au Baali walilazimika kula sehemu ya kafara za binadamu; na hivyo imekuja kuwa kwamba ‘Cahn-Bal,’ ‘Kuhani wa Baali,’ ni neno lililojulikana katika lugha yetu kwa ajili ya walao kwa ulafi nyama ya binadamu.”
Mtu yeyote hawezi kushindwa kuuona ukweli wa jambo hili! Pia ni kweli kwamba jamii nyingi zilizostaarabika zina mapokeo ambayo yanahusisha ulaji nyama za watu. Angalia kauli hii kutoka gazeti la The New York Times, “Nini Maana ya Ulaji Nyama za Watu?” na Erik Eckholm: “Ulaji nyama za watu umewahi kushangaza na kuchukiza karibu kila jamii inayojulikana, ikijumuisha zile zilizosemekana kutenda kitendo hicho.”
Makala hii iliendelea kuonyesha kwamba jamii nyingi zilizostaarabika pia ziliambatanisha umuhimu wa kiungu katika utendaji wake.
Vipi Kuhusu Hadithi Inayoeleza Asili ya Baba Krismasi?
Umeshawahi kufikiri kwamba hata wewe unaweza kuwa unawapitisha motoni, hata kuwatoa kafara watoto wako leo (japokuwa kwa njia tofauti) katika kutekeleza Krismasi, wakati unajitahidi kwa dhati “kufokasi kwa Kristo”?
Wazazi huwaza kwamba wanawiwa hadithi yote inayoelezea asili ya Krismasi kwa watoto wao! Mapokeo ya Krismasi yanawalenga hasa watoto, na bila shaka ndio kiini cha mengi ya yanayotokea. Najua kwa sababu nilitunza Krismasi kumi na saba. Dada yangu mkubwa na mdogo wangu wa kiume na mimi tulipokea vitu vingi na tulitoa kidogo sana siku hiyo—na yote ilianza na uongo wa Baba Krismasi.
Miaka kadhaa iliyopita, padri mmoja huko New Jersey aliliambia darasa lake la shule ya Jumapili kwamba Baba Krismasi alikuwa hadithi ya kubuni. Hasira iliyotoka kwa wazazi na wasimamizi wake ilikuwa ni ya haraka. Alikuwa “amemuua Baba Krismasi!” Alikuwa “ameharibu mapokeo ya familia!” Alikuwa “amenyang’anya mamlaka ya familia,” makala iliendelea. Alionywa rasmi na wakubwa wake kwa “kuvuka mipaka na kutojali hisia.”
Uhalifu wake? Alisema ukweli!
Kulingana na Ensaiklopidia ya Historia ya Ulimwengu ya Langer, (makala “Santa”—“Baba Krismasi”), “Santa” (Baba Krismasi) lilikuwa ni jina la kawaida la Nimrodi kote katika Asia Ndogo. Huyu alikuwa ni yule yule mungu moto aliyekuja chini kwenye dohani za wapagani wa kale na mungu moto yule yule ambaye kwake watoto walichomwa moto na kuliwa katika kafara za wanadamu miongoni mwa hao waliowahi kuwa watu wa Mungu.
Wakati huu Baba Krismasi linatokana na “Mtakatifu Nikolai.” Washington Irving, katika mwaka 1809, ndiye anayehusika kulibadilisha jina la askofu mkali wa awali na wa kale kuwa jipya la “mchangamfu sana Mt. Niko” katika kitabu chake kiitwacho Knickerbocker History of New York (Historia ya Nikaboka ya New York). (Mengi ya mapokeo ya Krismasi ya Amerika ni ya hivi karibuni kuliko hili.) “Niko wa Kale” kwa muda mrefu limetambulika kama neno kwa ajili ya ibilisi.
Katika Ufunuo 2:6 na 15, tunasoma kuhusu “mafundisho ya Wanikolai,” ambayo mara mbili Kristo analiambia Kanisa Lake “Anayachukia.” Hebu tulichambue neno Mnikolai. Linamaanisha “mfuasi wa Nikolai.” Nikos inamaanisha “mshindi, mharabu (mwangamizi).” Laos inamaanisha, “watu.” Wanikolai, basi, ni watu wanaomfuata mshindi au mharabu (mwangamizi)—Nimrodi. Kama uliamini kwamba kufuata Krismasi ni desturi ya Kikristo isiyo na hatia, hebu ukweli huu uzame ndani yako!
Je ni Jambo la Kimaandiko Kupeana Zawadi?
Wafanyabiashara wanatoa taarifa kila mara kwamba zaidi ya 60% ya mauzo yao ya rejareja kwa mwaka hupatikana msimu wa manunuzi ya Krismasi. Hii inawakilisha manunuzi makubwa sana ya zawadi. Wengi leo wanaamini kwamba utoaji wa zawadi unatokana na mfano wa Biblia wa “mamajusi watatu” (Biblia haitoi idadi) wakitoa zawadi kwa Kristo. Je hii ni kweli? Je kupeana zawadi kulitoka wapi, na Neno la Mungu linasema nini kuhusu jambo hili?
Bibliotheca Sacra inasema, “Kitendo cha kubadilishana zawadi baina ya marafiki ni kitendo kinachofanana kwa Krismasi na Satanalia, na lazima Wakristo walikichukua kutoka kwa wapagani, kama onyo la Tertullian linavyoonyesha wazi” (Kit. 12, uk. 153-155).
Kama kilivyo kila kipengele cha Krismasi, ukweli unaoshtua ni kwamba hata hii inayodhaniwa kuwa desturi ya Kikristo haitoki kwenye Biblia. Ni jambo la kushangaza kwamba watu wanapenda kuamini kuwa wanafuata desturi ya mamajusi ya kutoa kwa Kristo, wakati kwa hakika karibu wanapeana wao kwa wao tu! Unafiki kiasi gani! Kristo amesahauliwa kabisa.
Kwa hakika Biblia inafundisha kwamba Wakristo wasishike siku za kuzaliwa. Maandiko mengi yanaiweka wazi kanuni hii. (Makala yetu “Je Sherehe za Siku za Kuzaliwa ni za Kikristo?” inaelezea zaidi juu ya somo hili.) Hata hivyo, ingekuwaje kama ungeenda kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa iliyoandaliwa kwa ajili yako na kila mtu akatoa zawadi kwa kila mtu mwingine na wewe kuachwa bila zawadi? Wazo hili ni mzaha! Kama jambo hili lingetokea, ungesema kwamba watu hao wamekuwa wabinafsi na kukusahau wewe. Ukweli, watu wengi wanawapa wengine siku ya Krismasi kwa sababu tu wao wenyewe wanategemea kupokea zawadi!
Hebu kwa ufupi turudi kwa “mamajusi” waliompa zawadi Kristo. Andiko linaloelezea habari hii ni Mathayo 2:1-11: “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi?...Wakaingia nyumbani, wakamwona Mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.”
Kwa kawaida imedhaniwa kwamba hizi zilikuwa zawadi za siku ya kuzaliwa kwa ajili ya “mtoto Yesu.” Lakini je, hiki ndicho hasa Biblia inachosema? Hakika ni hapana! Kwanza ni muhimu kutambua kwamba walitoa tunu kwa Yesu. Hawakusimama mbele yake na kubadilishana tunu wao kwa wao au kuwapatia wengine. Tunu “zilitolewa Kwake.” Pia, walifika baada ya “siku ya kuzaliwa” Kwake. Hii ni sababu nyingine kwamba tunu hizi zisingekuwa “zawadi za siku ya kuzaliwa.”
Desturi ya kale, iliyodumu ya Mashariki ilikuwa ni kutoa tunu unapokuja mbele za mfalme. Hawa wanaume walijua kwamba walikuwa wamesimama mbele za “Mfalme wa Wayahudi.” Biblia ina mifano mingi ya watu wakituma zawadi kwa wafalme au wakizitoa baada ya kufika mbele zao. Desturi hii ni ya kawaida leo wakati mabalozi au watu wengine wanapofika mbele za kiongozi wa dunia.
Mwisho, angalia kile ambacho Maelezo ya Adam Clarke, kitabu 5, ukurasa 46, yanavyosema kuhusu kile kilichotokea hasa juu ya tukio hili: “Fungu la 11. Wakamtolea tunu. Watu wa mashariki kamwe hawafiki mbele za wafalme na watu wakubwa, bila zawadi mikononi mwao. Desturi hii mara nyingi inaonekana katika Agano la Kale, na bado inaenea mashariki, na katika baadhi ya Visiwa vya Bahari za Kusini vilivyogunduliwa hivi karibuni.” Kidesturi tunu zilitolewa kwa wafalme.
Nini kingekuwa dhahiri zaidi?
Asili ya Mkrismasi
Hakuna kijitabu kuhusu Krismasi kitakachokamilika bila ufafanuzi kidogo wa “Mkrismasi.” Tumeugusia bila kufokasi kwake moja kwa moja. Mkrismasi wa siku hizi ulianzia Ujerumani. Lakini Wajerumani waliupata kutoka kwa Warumi, walioupata kutoka kwa Wababeli na Wamisri.
Nukuu ifuatayo inadhihirisha kile ambacho Wababeli wanaamini kuhusu asili ya Mkrismasi: “Hadithi ya kale ya kubuni ya Kibabeli ilisimulia juu ya mti uliokuwa wa kijani wakati wote uliochipuka kutoka kisiki cha mti uliokufa. Kisiki cha kale kilimwashiria Nimrodi aliyekufa, mti mpya wa kijani wakati wote uliashiria kwamba Nimrodi alikuwa amefufuka tena katika Tammuzi! Miongoni mwa Wadruidi mwaloni ulikuwa mtakatifu, miongoni mwa Wamisri ulikuwa ni mtende, na katika Rumi ulikuwa ni msonobari, ambao ulipambwa kwa matunda madogo madogo mekundu wakati wa Satanalia!” (Walsh, Curiosity of Popular Customs—Uchunguzi wa Desturi Mashuhuri—uk. 242).
Kitabu cha Frederick J. Haskin Answers to Questions (Majibu kwa Maswali) kinasema, “Mkrismasi unatoka Misri, na tarehe za asili yake ni kutoka kipindi kirefu kabla ya Zama ya Kikristo.” Je ulifahamu hili—kwamba mkrismasi ulitangulia muda mrefu kabla ya Ukristo?
Vipengele vingi vya Krismasi havirejelewi katika Biblia. Hakika, sababu ni kwamba havijatoka kwa Mungu—siyo sehemu ya njia ambayo Anawataka watu wamwabudu Yeye. Mkrismasi, hata hivyo, umetajwa moja kwa moja katika Biblia! Fungua Yeremia 10:2-5, “BWANA asema hivi, Msijifunze njia ya watu wa mataifa…Maana DESTURI za watu hao ni UBATILI, maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi na shoka. Huupamba kwa fedha na dhahabu; huukaza kwa misumari na nyundo, usitikisike. Mfano wao ni mfano wa mtende, kazi ya cherehani, hawasemi; hawana budi kuchukuliwa, kwa sababu hawawezi kwenda. Usiwaogope; kwa maana hawawezi kutenda uovu, wala hawana uwezo wa kutenda mema.”
Maelezo haya ya mkrismasi wa kisasa ni dhahiri. Moja kwa moja Mungu huurejelea kama “njia ya watu wa mataifa,” akiziita desturi hizi “UBATILI.” Fungu la 23 linaongezea kauli ya ajabu na nzito: “Ee BWANA, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua [zake] si katika uwezo wa mwanadamu atembeaye. Ni lazima Mungu awafundishe watu jinsi ya kuishi. Ni rahisi tu kwamba mwanadamu hawezi kung’amua njia za Mungu yeye mwenyewe.
Hakuna nafasi katika Yeremia 10 kuamini, kama baadhi walivyojaribu kupendekeza, eti kwa sababu miti hii yenyewe haina uwezo wowote, hivyo haijakatazwa kabisa kuwa na Mkrismasi. Mungu analaani uwekaji wa mikrismasi ya upagani kwa amri hii dhahiri ya Biblia!
Chanzo cha Mashada ya Mholi, Vigogo Yuli (Vinavyochomwa Mkesha wa Krismasi) na Mlimbo (Mmea ambao Matunda Yake Hutoa Ulimbo)
Ensaiklopidia Amerikana inasema, “Mholi, mlimbo, kigogo Yuli…ni masalio ya yaliyokuwepo nyakati kabla ya Ukristo.” Kwa maneno mengine, upagani! Kigogo kinachochomwa mkesha wa Krismasi kilitumika kwenye matambiko ya Kitutoni ya kuabudu viumbe.
Frederick Haskin anaendelea kusema, “Mamlaka zinaamini kuwa matumizi ya mashada ya Krismasi yanaweza kufuatiliwa hadi kwenye desturi za kipagani za kupamba majengo na mahali pa ibada kwenye sikukuu hiyo ambayo ilifanyika wakati sawa na Krismasi.”
Ensaiklopidia ya Britannika, chini ya “Celastrales,” ambayo ni mimea ya maua, inafunua asili ya mashada ya mholi: “Wapagani wa Ulaya walileta vitawi majumbani mwao, wakiwapatia watu wasenge wa mistuni waliokuwa wakimbizi kutoka hali ya hewa mbaya ya baridi kali. Wakati wa Satanalia, sikukuu ya Warumi ya wakati wa majira ya baridi, matawi ya mholi (mti wenye majani yaliyo na ncha kali) yalitumiwa kupeana kama ishara ya urafiki. Wakristo wa awali wa Rumi ni dhahiri walitumia mholi kama mapambo kwenye majira ya Krismasi.”
Kuna dazeni (fungu la vitu kumi na viwili) nyingi za aina ya mholi. Binafsi nimepanda makumi yake. Miti hii kweli hujitokeza katika aina za madume na majike—kama vile “Mwana Mfalme wa Buluu na Binti Mfalme wa Buluu” au “Mvulana wa Buluu na Msichana wa Buluu” au “Mvulana wa China na Msichana wa China.” Miti ya mholi ya jinsia ya kike haitaweza kuzaa matunda mpaka hapo mmea jirani wa jinsia ya kiume iichavushe. Ni rahisi kuona kwa nini shada la mholi lilipata nafasi kwenye matambiko ya kipagani kama ishara ya urafiki na UZAZI!
Krismasi itakuwa haijakamilika kwa wengi isipohusisha “kupigana busu chini ya mlimbo.” Desturi hii ya kipagani pia ilikuwa kawaida kwenye usiku ambao ulijumuisha sherehe nyingi wakati ambapo kulikuwa na karamu za ulevi, ulafi na uasherati. Kama vile ilivyo Krismasi leo, “kupiga busu” huku kwa kawaida kulitokea mwanzoni mwa sherehe za Satanalia. Mlimbo ulifikiriwa kuwa na nguvu maalumu za uponyaji kwa ajili ya wale “walioshereheka” chini yake.
Ensaiklopidia Britannika, chini ya kichwa “Santalales,” inasema, “mlimbo wa Ulaya unafikiriwa kuwa ulikuwa na umuhimu wa pekee kimatambiko katika sherehe za Kidruidi na maisha katika desturi, mila na hadithi za kitamaduni leo, heshima yake ya kipekee kama mlimbo wa Krismasi ukiwa umekuja kutoka nyakati za Anglo-Sakzoni.” Mlimbo ni kimelea kinachoishi kwenye miti ya mialoni. (Kumbuka kwamba Wadruidi waliabudu kwenye vijisitu vya miti ya mialoni.) Waseltiki wa kale (wenye uhusiano na Wadruidi) walikuwa na kawaida ya kutoa mlimbo kama tiba ya mitishamba kwa wanyama tasa ili kuwafanya wazae. Dawa hii ya mitishamba bado inarejelewa kama “mponyaji mkuu” katika Seltiki.
Kama ulivyo mlimbo, matunda ya mholi pia yalifikiriwa kuwa matakatifu kwa mungu wa-jua. “Gogo jua” la asili likaja kujulikana kama gogo yuli (krismasi) (kigogo kinachochomwa mkesha wa Krismasi). “Yuli” kwa urahisi humaanisha “gurudumu,” ambalo kwa muda mrefu limekuwa kiwakilishi cha jua kwa wapagani. Si ajabu leo watu huongelea juu ya “wimbi la majira ya yuli takatifu.” Hii pia inafafanua maandazi ya mviringo ambayo yamekuwa yakitolewa kwenye misa kwa mabilioni vizazi na vizazi.
Jinsi gani ulivyo wa kuvutia—na kufikirisha—ukweli wa historia.
Ibada ya Mungu wa Kweli Kuchanganywa na Mazoezi ya Uongo
Neno la kisasa kwa ajili ya kuunganisha desturi za kipagani za uongo pamoja na ibada ya Mungu wa kweli katika lugha ya Kiingereza linaitwa syncretism. Mtu yeyote aliyefanya hivi katika Israeli ya kale aliuawa (Law. 18:21, 29)! Ilikuwa hatari kiasi hicho!
Uchunguzi wa kuvutia sana kuhusu jinsi Israeli walivyofikiri na kuamini, katika mioyo yao wenyewe, kwamba walikuwa wanamwabudu Mungu kama taifa lote, unatoka 2 Wafalme 17:33: “Wakamcha Bwana, na kuitumikia miungu yao wenyewe, sawasawa na kawaida za mataifa ambao wao walihamishwa kutoka kwao.”
Je uliipata hii? Ndiyo, walimcha Mungu wa kweli huku wakitumikia miungu mingine. Si ajabu fungu linalofuata (34) linasema kwamba kwa hakika, “HAWAMWOGOPI BWANA” kulingana na namna Mungu alivyoamuru. Hivi ndivyo Mungu anavyotazama kile watu wanachokifanya leo—bila kujali kile ambacho watu wanakifikiri juu ya vitendo vyao wanaponakili mazoezi ya kipagani!
Fungu la 30 linasema kwamba yote haya walipata kujifunza kutokana na kuwa pamoja na “watu wa Babeli” (miongoni mwa wengine), ambao mungu wao mkuu, tutakumbuka, alikuwa Nimrodi (Baali au Moleki)—ambao sasa tunajua walikuwa yule yule mmoja.
Angalia jinsi onyo la Mungu lilivyokuwa bayana katika Kumbukumbu la Torati 12:29-31, na kwa nini Aliwaonya! “BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa mbele yako… nawe ukawatwaa, na kuketi katika nchi yao; ujiangalie, usije ukanaswa ukawafuata…wala usije ukauliza habari za miungu yao, ukisema, Mataifa haya waitumikiaje miungu yao? Nami nifanye vivyo. Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani KILA YALIYO MACHUKIZO kwa BWANA, AYACHUKIAYO YEYE, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.”
Mafungu mengi, yenye kufanana na Kumbukumbu la Torati 12, yapasa yasomwe kwa makini. (Ona Kutoka 34:10-17; 23:23-33; Mambo ya Walawi 20:22-26; Kumbukumbu la Torati 20:13-18, nk.) Mungu wa kweli alijua ya kwamba kuitumikia miungu mingine kulielekeza kutoa kafara za watoto kwao!
Kumbukumbu la Torati 12:32 liliweka wazi kwamba Mungu hataki tuchanganye njia Zake pamoja na njia za uongo: “Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.” Kwa maneno mengine, fanya sawa sawa na kile Ninachosema—hakuna zaidi, hakuna pungufu!
Haya ni MANENO DHAHIRI ya Mungu kwa wote wasemao kwamba wanaweza kuchanganya desturi za kutisha za upagani kabisa pamoja na kinachodhaniwa “kufokasi kwa Kristo.”
Mazoezi ya Kipagani ya Israeli ya Kale Katika Desturi za Kisasa
Kumbukumbu la Torati 12:2-4 inajenga muktadha wa muhimu. Mungu anasema dhahiri, “Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi [kila mti wa kijani]; nanyi zivunjeni madhabahu zao…na maashera yao yateketezeni kwa moto…Wala msimfanyie hivyo BWANA, Mungu wenu.”
Angalia kielelezo cha Mungu kwa “kila mti wa kijani” na “maashera (vijisitu) yao.” Kuna mafungu kama kumi kwa uchache katika Agano la Kale lote yanayorejelea “miti ya kijani” na uhusiano wake na ibada ya sanamu. Wanahistoria wanashikilia kwamba kielelezo cha neno “kijani” hurejelea kwa kijani mwaka-wote—miti ya kijani wakati wote!
Kwa mara nyingine tena, hebu tuchunguze kwa ukaribu zaidi historia halisi na asili ya baadhi ya desturi za Satanalia ambazo bado zinafanywa leo. Angalia nukuu ifuatayo inayozizimisha kutoka Dictionary of Greek and Roman Antiquities [Kamusi ya Kigiriki na Mambo ya Kale ya Kirumi] “Oscilla” toleo 3, kitabu II: “…watu wa tabaka zote walijitoa wenyewe kusherehekea na kufurahi, zawadi zilitolewa kwa kila mmoja miongoni mwa marafiki, na makundi makubwa yakafurika mitaani, wakisema kwa sauti kubwa ‘Lo Satanalia.’ Sadaka ilitolewa chini ya mti wa kijani uliopambwa, kulingana na mwanamashairi wa kipagani, Virgil. Sanamu ndogo na vinyago—viitwavyo ‘oscilla’—vilining’inizwa mtini, kama yalivyo mapambo ya Krismasi leo. Historia inakubali…hapawezi kuwa na shaka kwamba katika hizi ‘oscilla’ tuna ukumbusho wa kafara za binadamu…”
Je haya yote hayaonekani kufahamika? Zawadi, kuimba mitaani, miti ya kijani, mapambo, sadaka chini ya miti, kufurahi, kusherehekea? Yanaweza kusikika ya kipekee, lakini yanawakilisha mambo ambayo kwa kweli ni machukizo.
Oscilla wa kisasa wanaonekana kama “malaika” wadogo wanene wanapokuwa wakining’inia juu ya mti. Niliwaweka hawa “malaika watoto” wadogo juu ya miti yetu, mimi mwenyewe, kama mtoto mdogo. Kwa uchache nilifikiria walikuwa watoto wa malaika. Nilikuwa nimekosea kiasi gani! Unafikiri yeyote kati ya marafiki zako wanatambua nini hasa wanachowakilisha? Kwa hakika hapana—lakini hiyo haifanyi kuwa hatari ndogo au makosa kidogo mbele za macho ya Mungu!
Upagani Halisi Uliochanganywa Kanisani
Chanzo kimoja zaidi kinadhihirisha jinsi haya yote yalivyokuja kuwa urithi uliofanywa na mamilioni “bila kujisikia kuwa na hatia”—lakini wako mbali na kutokuwa na hatia machoni pa Mungu. Sasa soma nukuu ifuatayo kutoka Ensaiklopidia Britannika, toleo 15, kitabu 10, kurasa 1062-3: “Ukristo…kwa mchakato changamani na wa pole pole…ukawa dini rasmi ya himaya ya [Kirumi.]
“Kwa muda, sarafu na sanamu zingine za ukumbusho ziliendelea kuunganisha maandiko pamoja na ibada ya jua, ambayo kwa hiyo Konstantini alikuwa amezoea hapo kabla. Lakini hata awamu hii ilipofika mwisho, upagani wa Kirumi uliendelea kuwa na ushawishi [wa namna zingine] wa kudumu, mkubwa na mdogo…Kalenda ya kidini imebakiza masalio mengi ya sikukuu zilizokuwepo kabla-ya-Ukristo, kubwa zaidi Krismasi, inayounganisha sifa za lazima au muhimu zinazojumuisha sikukuu za Satanalia na kuzaliwa kwa Mithra. Lakini, zaidi ya yote, mwelekeo tawala wa Ukristo wa Magharibi unawiwa na Rumi ya kale ile nidhamu imara ambayo uliupatia uthabiti na sura.”
Mamlaka inayoaminika kama Ensaiklopidia Britannika kwa hakika inatambua, kwa yeyote anayetaka kuona, kwamba Satanalia na Rumi ya kale ndivyo vilivyofasili ile “nidhamu…uthabiti na sura” ya Ukristo wa Magharibi!
Kweli huku ni kukiri kunakoduwaza!
Nukuu nyingine nzito ifuatayo inafunua jinsi ibada hii ya sanamu, sikukuu za kipagani, zilivyotelezea ndani ya ulimwengu wa “Kikristo”. Inatoka kwenye New Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge (Ensaiklopidia Mpya ya Schaff-Herzog ya Maarifa ya Kidini), chini ya “Krismasi”:
“Jinsi gani tarehe ya sikukuu ilitegemea juu ya Brumalia ya kipagani (25 Desemba) inayofuatia Satanalia (17-24 Desemba), na kusherehekea siku fupi kuliko zote ya mwaka na ‘jua jipya’…haiwezi kutambuliwa kwa usahihi. Satanalia na Brumalia za kipagani zilikuwa zimezama katika, desturi maarufu ambazo haingewezekana ziwekwe kando kwa ushawishi wa Kikristo…Sikukuu ya kipagani pamoja na shangwe zake ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba Wakristo walifurahia kisingizio cha kuendelea kuisherehekea huku kukiwa na badiliko dogo rohoni na katika mwenendo. Wahubiri wa Kikristo wa Magharibi na Mashariki ya Karibu walipinga upuuzi usiosemeka ambao kwa huo siku ya kuzaliwa kwa Kristo ilisherehekewa, wakati Wakristo wa Mesopotamia waliwashutumu ndugu zao wa Magharibi kwa ibada ya sanamu na kuabudu jua kwa kuikubali sikukuu hii ya kipagani kama ya Kikristo.”
Chanzo kimoja zaidi kinafunua jinsi kanisa la Kirumi lilivyoichukua Krismasi na kuifanya sherehe rasmi. Ensaiklopidia Britannika, toleo 1946, inasema, “Krismasi haikuwa miongoni mwa sikukuu za mwanzo zaidi za kanisa…Walatini fulani, mapema kama mwaka 354, huenda walihamisha siku ya kuzaliwa kutoka 6 Januari hadi 25 Desemba, ambayo ilikuwa sikukuu ya Kimithraiki…au siku ya kuzaliwa JUA lisiloshindwa…Wasiria na Waarmenia, waliong’ang’ania 6 Januari, waliwashutumu Warumi kwa kuabudu jua na ibada ya sanamu, wakishikilia kauli…kwamba sikukuu ya 25 Desemba, ilikuwa imebuniwa na wanafunzi wa Serinthasi…”
Hivyo, sikukuu ya kipagani, iliyosherehekewa muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, ikaingia ndani ya Ukristo uliotambuliwa.
Je uliwahi kujua kwamba hata Wapyuritani wa karne ya kumi-na-saba wa New England walielewa jinsi gani Krismasi ilivyokuwa makosa? Kwa hakika walipiga marufuku utunzaji wake kwa sheria, katika mwaka 1659, kote katika koloni la Massachusetts Bay. Faini na kifungo vingeweza kutolewa kwa yeyote aliyekutwa akiitunza. Ilikuwa karibu miaka 200 (1856) baadaye kabla ya watu kuacha kufanya kazi siku ya Krismasi katika Boston. Wapyuritani walijua mizizi yake na kuibandika jina “ya kipagani, ibada ya sanamu ya kipapa.”
Wale “Wanaobadili Majira na Sheria”
Nabii Danieli (7:8) anazungumzia juu ya “pembe ndogo,” ambayo (7:25) “inanena maneno makuu kinyume chake Aliye Juu…na kuazimu kubadili majira na sheria.” Hii pembe ndogo ni mamlaka kuu ya kidini ambayo inajaribu kuweka juu mtazamo wake yenyewe wa tarehe na sherehe, kwa ulimwengu usio na habari, mahali pa maagizo dhahiri ya Mungu.
Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “badili” linamaanisha “geuza, badilisha au idhinisha.” Neno lililotafsiriwa “majira” linamaanisha “matukio yaliyoamuliwa, majira au nyakati.” Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “sheria” linamaanisha “amri au sheria za Mungu.” Inapowekwa pamoja, sentensi hii inarejelea kwa mamlaka ambayo inajaribu “kugeuza matukio yaliyoamuliwa na majira ndani ya Sheria ya Mungu.” Bila shaka, Krismasi ni mfano mkuu wa jinsi gani jambo hili limefanyika. Maagizo ya Mungu yamebadilishwa na desturi za kidini za wanadamu.
Nukuu ifuatayo inafunua jinsi gani jambo hili limetokea. Pia inatoka katika Ensaiklopidia Britannika, chini ya “Ukristo”: “Hivyo, liturujia ya Ista imekuzwa sana katika Kanisa la Othodoksi Mashariki, na liturujia ya Krismasi imekuzwa sana katika Kanisa Katoliki la Rumi…Kalenda ya Kikristo ndiyo taasisi ya Kikristo iliyosambaa sana. Juma la siku saba na mdundo wa sikukuu za Kikristo zimekubaliwa hata katika nyingi ya nchi zisizo za Kikristo. Licha ya majaribio ya nguvu kuingiza juma la kazi linalobadilika, juma la siku saba pamoja na siku isiyo ya kazi Jumapili halikuweza kuondolewa hata katika nchi za Kikomunisti zenye mtazamo wa ukana Mungu. Hata katika jamii za kikana-Mungu na mashirika ulimwenguni kote, sikukuu za Kikristo zinafurahia umaarufu usiopingika kama siku zisizo za kazi…hasa Krismasi.”
Kiukweli, ni “wanasiasa wa kidini,” waliorejelewa hapo awali, ndio wamekuwa wakitafuta kulazimisha kalenda ya kisasa ya “Kikristo” juu ya ulimwengu usiofahamu. Ni viongozi hawa ambao “wameazimu kubadili majira na sheria.”
Nguvu Hatari ya Uongo
Moja ya majina ya Shetani ni Mharabu au Mwangamizi (Ufunuo 9:11). Nimrodi/Zohali [Satuni] /Moleki/Baali, kama Shetani, ndiye mungu moto anayeharibu na kurarua watoto wachanga. Yesu Kristo halisi kamwe hakuwa na kamwe hatakuwa katika Krismasi! Wala Hawezi kurudishwa mle ambamo kamwe hakuwemo. Lakini aliye “mungu wa ulimwengu huu,” Shetani (Kor. 4:4), wakati wote amekuwa katika Krismasi. Kwa kweli, anaonekana kuwa mwanzilishi wake!
Mungu wa Biblia anaamuru kwamba wale wanaomwabudu “lazima wamwabudu katika roho na katika kweli” (Yohana 4:23-24). Hii haiingiliani na uongo mkuu wa Krismasi na Baba Krismasi ambavyo watoto wote wanataka sana kuamini.
1 Timotheo 4:2 inaonya dhidi ya wale “wasemao uongo kwa unafiki, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe.” Wazazi wanaweza “kuchoma moto” watoto wao wenyewe, hadi kufikia pointi ya kuwaunguza, kwa udanganyifu na uongo wa Krismasi!
Hakuna “usalama katika wingi” katika ulimwengu huu kwa wale wanotunza Krismasi, kwa sababu Shetani, ambaye anaitwa “baba wa uongo” na “muuaji toka mwanzo” (Yohana 8:44), “ameudanganya ulimwengu wote” (Ufu. 12:9)! Rudi kwenye fungu hili na ulisome. Kisha tambua kwamba Krismasi bila shaka ni ushuhuda kwa udanganyifu huo mkuu.
Lakini Kristo analirejelea Kanisa lake kama “kundi dogo” (Luka 12:32). Mafungu mengine mengi yanaonyesha hili. Kanisa hili halina ile idadi kubwa ya aina za Ukristo zilizoanzishwa, zinazoheshimiwa za ulimwengu huu. Lakini linamtii Mungu!
“Yesu Mwingine”
Kuna tatizo lingine linaloenda pamoja na wazo la “kumrudisha Kristo katika Krismasi”—na ni kubwa! “Yesu” ambaye ni fokasi ya majira haya siyo yule Yesu Kristo wa kweli wa Biblia! (Kitabu chetu Yesu Kristo wa Kweli—Hajulikani kwa Ukristo kinafunua mengi zaidi juu ya mada hii.)
Wengi wamefundishwa kwamba yuko Yesu mmoja tu. Lakini Neno la Mungu linasema juu ya Yesu wa bandia, na huyu Kristo mbadala anatambulika katika historia. Uthibitsho? Mtume Paulo alionya dhidi ya “Yesu mwingine.”
Elewa nini kiko hatarini hapa!
Kwanza, fikiria utangulizi wote wa Paulo akiwa anaweka jukwaa kwa ajili ya onyo linalofuata: “Lakini nachelea; kama yule nyoka [Shetani] alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha wepesi [urahisi] ulio katika Kristo” (2 Kor. 11:3).
Sasa kwa onyo lenyewe katika fungu linalofuata: “Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye” (2 Kor. 11:4). Wakorintho walionekana “kuvumiliana na hili” bila upinzani mkubwa.
Paulo, chini ya uvuvio wa Yesu Kristo wa kweli wa Biblia, alivutwa kurekodi hatari kubwa ya kufuata “Yesu mwingine” bila kujua. Fikiria. Pengine wengi kamwe hawajawahi kufikiria wazo la Yesu wa uongo hata kwa kitambo—kwamba kuna kitu kama vile asiye sahihi, tofauti na “Kristo wa uongo” (Math. 24:23-24)—anaitwa “Yesu mwingine.” Huko nyuma, “Yesu” huyu hata aliharibu namna ya kufikiri ya Wakristo wa kweli. Yote haya yako dhahiri. Lakini “ujanja” wa jinsi hii unaweza kutokea, na jinsi ulivyotokea katika historia, ni kiudanganyifu sana—namna inayoshawishi sana—kiasi kwamba hata Wakristo wa kweli wanaweza kuteleza na kumwabudu huyu aliyeitwa Yesu bila kujua. Hiki ndicho kilikuwa kinatokea kwa Wakorintho.
Watu wanaweza kuabudu katika njia zinazowakilisha vitu ambavyo viko tofauti sana na kile wanachoamini kwa dhati au kukusudia. “Waumini” wa Biblia leo wanaweza kufikiri kwamba wanamwabudu Mwokozi wa kweli ili hali kwa hakika wanamwabudu mwokozi wa uongo—YESU MWINGINE! Ukristo wa mapokeo kwa ujumla wake kwa hakika unamwabudu Nimrodi/Zohali/Moleki/Baali. Msisitizo wa kisasa wa mama/mtoto “Mariamu/Yesu, ikijumuisha heshima kubwa ya kiibada kwa Mariamu inayofanywa na mamilioni, ni sambamba na Nimrodi na mama yake, Semiramisi, ambao hauwezi kukoswa.
Hii hapa ni pointi ya kile ambacho kimekuwa kikifafanuliwa. Wengi wanaongea juu ya “kumrudisha Kristo kwenye Krismasi.” Hii inasikika kila mwaka kutoka kwenye maelfu ya vibweta na mahali pengine. Lakini Kristo wa kweli kamwe hajawahi kuwa pale! Kama vile mtu hawezi kurudi ndani ya chumba ambacho kamwe hakuwahi kuingia, vivyo hivyo Kristo hawezi “kurudishwa” kwenye tukio ambalo kamwe hajawahi kuwemo, na ambalo kwa kweli Analichukia! (Tena, ona Marko 7:7.) Yule Yesu ambaye wahubiri na wanadini hawa wanaye kwenye fikira zao ni Kristo mwingine, mmoja mwenye injili nyingine, roho nyingine—roho ya Krismasi!—inayoleta mafundisho tofauti kabisa.
Je unaweza kuona muunganiko?
Unapaswa Ufanye Nini?
Hatimaye, hebu tuangalie kile ambacho Mungu aliwaambia watu Wake wanapaswa wafanye na namna ile wanavyopaswa kuwafundisha watoto wao.
Kumbuka Yeremia 7:31, mahali ambapo Mungu aliwalaani Israeli kwa ajili ya kuwachoma watoto wao katika bonde la Tofethi. Mafungu manane kabla (fu. 23-24), Mungu alikuwa ameweka dhahiri kile anachokitaka: “Lakini Naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti Yangu, Nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu Wangu: mkaende katika njia ile yote Nitakayowaamuru mpate kufanikiwa. Lakini hawakusikiliza…bali walikwenda…kwa ushupavu wa mioyo yao mibaya…”
Wanadamu hawataki kumtii Mungu (Rum. 8:7). Badala yake wanapenda kufuata “ushupavu wa mioyo yao”. Hawafahamu kwamba Mungu anataka maisha yao “yafanikiwe.” Anataka furaha, shangwe na mibaraka imiminike ndani ya maisha ya watu. Yote haya ni matokeo ya kumtii Yeye.
Mungu alimvuvia Musa kuwaonya wazazi juu ya wajibu mkuu ambao wanao katika nini na vipi wanavyofundisha watoto wao. Angalia maelekezo Yake katika Kumbukumbu la Torati 6:1, 6-7, 20-21, 25: “Na hii ndiyo sheria… alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki… Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo…Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N'nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu? Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu…Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.”
Mungu aliitoa Israeli kutoka Misri—kutoka utumwani—kutoka desturi za ulimwengu uliowazunguka na alifunua Sheria Yake kwao. Hataki watu Wake warudie mapokeo, desturi na njia ambazo ameshawaita kutoka kwake. (Kanisa ni moja tu linaloelewa na kufundisha kweli zote juu ya masomo haya. Ili-kujifunza zaidi, soma kitabu chetu “Liko Wapi Kanisa la Kweli? – na Historia Yake ya Ajabu!)
Wakati mapokeo yote yaliyofungamana, yaliyojawa na alama za kuabudu mungu wa zamani wa kipagani, aliyebuniwa na wanadamu, yanafundishwa, hii siyo kumwabudu Muumbaji wa kweli.
Hatujajua kwamba Krismasi ni ya Babeli
Yesu alisema mara mbili, katika Mathayo 7:16 na 20, kwamba “mtawatambua kwa matunda yao.” Kila kitu ambacho watu wanasema au kutenda, kizuri au kibaya, kina matunda. Matunda ya Krismasi yanatisha. Krismasi ni juu ya kupata kwa ajili ya nafsi—na biashara kabisa. Majira haya huupeleka mwaka mzima katika uzinzi, upweke, wivu, ulevi na kuendesha huku wamelewa, mabishano ya familia (na mabaya zaidi), na mrundikano wa madeni ambayo mara nyingi hudumu mpaka Machi. Tatizo hili ni kubwa kiasi kwamba makanisa yote huripoti kwamba mapato yao hushuka katika kipindi hiki wakati watu “wanapona” kutoka matumizi yao yote! Ni kejeli jinsi gani.
“Roho” Halisi ya “Krismasi”
Nabii Isaya alivuviwa kuandika, “Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu Wangu kosa lao” (58:1). Nimefanya hili. Sasa kwa vile umesoma UKWELI DHAHIRI kuhusu asili ya kweli ya Krismasi, utafanya nini?
Nukuu inayofuata inakuja kutoka kijitabu Ukweli Dhahiri Kuhusu Krismasi, na Herbert W. Armstrong. Inatoa muhtasari wa kijitabu ulichosoma:
“Krismasi imekuwa ni majira ya biashara. Inadhaminiwa, inawekwa hai, kwa kampeni nzito kabisa ya matangazo ya biashara ya rejareja ya mwaka. Unamwona ‘Baba Krismasi’ aliyebadilishwa katika maduka mengi. Matangazo hutuacha tumelaghaiwa [danganywa] na kudanganywa kuhusu ‘roho nzuri ya Krismasi.’ Magazeti, yanayouza matangazo, huchapisha tahariri za kuvutia zinazoinua na kusifu majira ya kipagani, na ‘roho’ yake. Watu waliodanganywa wametiwa kasumba, wengi wakichukizwa wanapoambiwa ukweli. Lakini ‘roho ya Krismasi’ inaumbwa kila mwaka, si kumwadhimisha Kristo, bali kuuza bidhaa! Kama ilivyo kwa ulaghai wote wa Shetani, inaonekana kama ‘malaika wa nuru,’ imefanywa ionekane njema. Mabilioni ya dola yanatumika katika shamrashamra hizi za biashara kila mwaka, wakati kusudi la Kristo likilazimika kuteseka! Ni sehemu ya mfumo wa kiuchumi wa Babeli!
“Tumedai kuwa mataifa ya Kikristo, lakini tuko ndani ya Babeli, kama unabii wa Biblia ulivyotangulia kusema, na hatujui! ‘Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake’—sasa karibu kuanguka—ni onyo la Ufunuo 18:4 [msisitizo wangu].
“Mwaka huu, badala ya biashara ya zawadi, kwa nini usiweke pesa hiyo kwenye Kazi ya Mungu?”