Karibu!

Karibu kwenye toleo letu la tovuti ya Kanisa la Mungu Rejeshwa (Restored Church of God) kwa lugha ya Kiswahili. Tafadhali tumia uhuru wako kusoma maandiko yetu. Kwa sasa tunatafsiri katika Kiswahili vitabu na makala tunavyovitoa katika toleo la tovuti yetu kwa lugha ya Kiingereza.

Ingawa huu ni mchakato mgumu na wa muda mrefu, kwa subira, utaendelea kuona toleo letu kwa lugha ya Kiswahili likikua sawa sawa na mfano wa mbegu ya haladari. Kwa wakati huu tutakuwa tunaongeza machapisho ambayo tayari yako kwenye lugha ya Kiingereza. Tunasonga mbele kwa haraka kadri inavyowezekana tukitumaini kwamba utapata majibu kwa maswali kutoka mada mbalimbali. Tunakushukuru kututembelea. Rudi mara kwa mara ili ujionee maendeleo ya tovuti ya Kiswahili!

Kitabu:

Uwezekano Wa Kustaajabisha Wa Mwanadamu

Jiandae kuduwazwa—kustaajabishwa amini usiamini! Ukweli wa ajabu umebaki mafichoni—umezuiliwa—usieleweke kwa wanadamu wote kwa miaka 2,000. Ulimwengu uliodanganywa umezuiliwa usielewe KIJENZI MUHIMU KINACHOKOSEKANA katika kumaliza matatizo ya mwanadamu. Wanasayansi, wanateolojia, waelimishaji na wanafalsafa wamebaki kuwa wajinga kuhusu ukweli wa kwa nini mwanadamu yupo. Na bado, UKWELI HUU WA KUSHANGAZA—MAARIFA HAYA YA AJABU—yamekuwepo wakati wote. Lakini walio wengi hawaelewi watafute wapi. Kristo alikuja kama MLETA HABARI akifunua matukio yajayo—akifafanua kabla HABARI NJEMA kwa ajili ya wanadamu wote. Hii ndiyo simulizi ya kushangaza ya injili ya kweli ambayo Aliileta—na jinsi inavyokuhusisha WEWE!


Injili Ya Kweli Ni Ipi?

Yesu na mitume walihubiri “injili”! Lakini ni kitu gani? Je, unajua? Je, ilikuwa ni injili ile ile ambayo Paulo alihubiri kwa watu wa Mataifa? Je, neno “injili” lina maana gani basi? Haya hapa ni majibu kutoka ndani ya Biblia yako!


Asili ya Kweli ya Krismasi

Krismasi ilianzia wapi? Kutoka kwenye Biblia au kwenye upagani? Ni nini hasa asili ya Baba Krismasi—mlimbo—mikrismasi—Mashada ya mholi—na desturi ya kupelekeana zawadi? Wengi wanajishughulisha juu ya “kumrudisha Kristo ndani ya Krismasi.” Je Aliwahi kuwa humo? Haya hapa ni majibu yanayoduwaza!


Asili ya Kweli ya Isita

Isita (Pasaka isiyokuwa ya Wayahudi) ni utamaduni wa ulimwengu mzima unaohusisha desturi ambazo watu wanaamini ni za Kikristo. Asili ya Kwaresima na ibada za maawio ya jua ni nini? Ni kwa jinsi gani sungura, mayai na maandazi ya moto yenye alama ya msalaba vilikuja kuhusishwa na Kufufuka kwa Kristo? Je, Isita imetajwa kwenye Biblia? Je, mitume na Kanisa la awali waliitunza? Majibu yatakushtua!


Liko Wapi Kanisa la Mungu?

Je! Kristo alijenga Kanisa moja, lililounganika, lenye utaratibu? Au Kanisa Lake limegawanyika? Alisema, “Nitalijenga KANISA LANGU”—si “makanisa,” “mashirika,” “vikundi,” “madhehebu” au “jamii za waumini.” Aliahidi kwamba “milango ya kuzimu haitalishinda.” Liko wapi na jinsi gani linatambulika? Ni-lipi na kwa nini ni hilo? Huhitaji kukanganyikiwa. Haya hapa ni majibu dhahiri!


Jinsi Dini Inavyokudanganya Kuhusu Mustakabali Wako wa Kustaajabisha

Ukweli wa injili—kusudi la Mungu la kustaajabisha kwa ajili ya mwanadamu—umefichwa. Hufafanua kwa nini ulizaliwa. Ni maarifa ya kushangaza! Yatakuacha umepigwa bumbuazi. Maarifa haya ya ajabu yamefunuliwa sasa—sambamba na njama ya kuyazuia!


Kwa nini Unaishi?

KWA NINI unaishi—KWA NINI ulizaliwa? Maana ya maisha yako ni nini? Je uliwekwa Hapa kwa sababu? Unaweza kujua—lazima ujue!


Nini Thawabu Yako Katika Maisha Yajayo?

Hakuna kitu kisichoeleweka zaidi kuliko wokovu. Kwa nini watu wengi wamechanganyikiwa—wamedanganyika—kuhusu kile watakachofanya baada ya maisha haya? Je, wokovu huja kwa neema au kwa njia ya matendo—na tofauti yake ni nini? Kwa namna gani—kwa vigezo vipi—watu hulipwa katika maisha yajayo? Kijitabu hiki cha muhimu sana kinaondoa mkanganyiko wote!


Shetani ni Nani?

Hivi shetani ni nani? Biblia humwita “mungu wa ulimwengu huu.” Lakini alitoka wapi? Je Mungu alimuumba kama alivyo? Je, yeye ni roho aliyeanguka? Haya hapa ni majibu kutoka katika Neno la Mungu!


Ufalme wa Mungu ni Nini?

UFALME WA MUNGU ni nini—na unaonekana lini? Je, uko mbinguni? Je, ni Himaya ya Uingereza? Je, ni kanisa la watu wote? Je, ni milenia? Je, “uko katika mioyo ya wanadamu” au tu “wema ulio ndani ya kila mtu”? Mamilioni wanaamini fikira hizi za watu wengi—lakini zote ni za uongo! Mchanganyiko na kutokukubaliana kusiko kwa lazima kunatawala. Huu hapa ni ufafanuzi wa Biblia uliowekwa wazi!


Jinsi Ufalme wa Mungu Utakavyokuja

Kisa Ambacho Hakijawahisimuliwa!

Mabilioni wanasubiri Kurudi kwa Yesu Kristo kusimamisha Ufalme wa Mungu. Lakini wachache wanajua jinsi gani Atafanya hivi. Jambo hili halitatokea namna ambavyo wengi wanatarajia. Kijitabu hiki kina kisa cha ajabu, ambacho-kamwe-hakijawahisimuliwa cha jinsi ambavyo Ufalme wa Mungu utakavyosimamishwa juu ya mataifa yote!


Hili Hapa Ndilo Kanisa la Mungu Rejeshwa

Wengi huuliza: Kanisa la Mungu Rejeshwa ni nini? Kwa hakika sisi ni Kanisa la namna ya peke yake—ambalo washiriki wake wamedhamiria kuiacha nuru yao iangaze katika ulimwengu unaohitaji sana nuru! Hii hapa ni historia mahsusi ya Kanisa lenye kuhamasishwa na imani ya kina, inayotokana na uelewa kwamba maisha halisi yenye furaha yanaweza kupatikana sasa—na kwamba ulimwengu wa kustaajabisha unakuja hivi karibuni!