Angalizo kuhusu Sera ya Faragha & Haki ya Kunakili

Faragha yako ni muhimu kwetu. Kanisa la Mungu Rejeshwa (RCG) halitauza, kukodisha au kutoa habari zako binafsi kwa kampuni au shirika lolote la nje. Soma sera yetu kuhusu faragha.

Haki ya Kunakili © 2014 Kanisa la Mungu Rejeshwa (RCG). Haki Zote Zimehifadhiwa.

Kanisa la Mungu Rejeshwa (RCG) ni shirika lisilo la faida kulingana na Kifungu 501(c) (3) cha Katiba ya Marekani

Sera ya Faragha:

Faragha yako mtandaoni ni kigezo muhimu kwa tovuti zetu. Tamko hili la faragha linaweka wazi ni habari zipi tunazokusanya na kuzitumia katika rasilimali zetu za kimtandao.

Habari Tunazokusanya

Kanisa la Mungu Rejeshwa (rcg.org) na tovuti zake zingine (worldtocome.org na realtruth.org) hukusanya na kunyambulisha data za watumiaji wake. Kwa mfano: Idadi ya watumiaji, Viunganishi katika kutafuta habari, habari zinazotafutwa sana, na habari na huduma zinazotumika sana.

Watumiaji wanaojiandikisha katika mojawapo ya orodha ya kutumiwa ujumbe wanatakiwa kutoa baadhi au habari zote zifuatazo: (1) Jina, (2) anwani ya barua pepe, (3) nchi na (4) simbo ya posta. Maeneo mengine ya hiari au maswali yanayoshabihiana yanaweza kuulizwa. Habari hizi zote hutusaidia kutambua idadi sahihi ya watumiaji na kuboresha huduma tunazotoa.

Namna Tunavyokusanya Habari

Kuna njia mbalimbali kuhusu namna tunavyoruhusiwa kupata habari zako kwa kupitia mchakato huu:

Kujisajili katika Mtandao na Fomu: Watumiaji wanaweza kujisajili kwenye mojawapo ya orodha zetu za watu wanaotumiwa habari au kuomba vitabu kutoka kwenye tovuti zetu. Orodha hizi za habari pepe huwajulisha watumiaji maboresho mbalimbali na mabadiliko kwenye tovuti zetu au kusaidia ufanisi katika utekelezaji wa maombi ya vitabu.

Kuki: Kuki ni faili dogo la data linaloandikwa na tovuti kwenye kompyuta yako unapozitembelea. Mara nyingi huwa na habari kama UTAMBULISHO wa mtumiaji unaonukuu matumizi ili kupangilia uwekaji wa habari au kufuatilia kurasa zilizotembelewa. Tunatumia habari hizi ili kuboresha utembeleaji wa maeneo yetu, mfumo na utendaji kazi. Wakati wote uko huru kukataa “kuki” zetu kama kisakuzi chako kinaruhusu, lakini hii inaweza kuzuia baadhi ya maeneo ya utendaji kazi wa tovuti.

Anwani za IP: Tunakusanya habari za anwani za IP kwa makusudi ya mfumo wa kiutawala, kutolea taarifa za pamoja, na kuratibu matumizi ya huduma na nyenzo zetu. Kwa sababu tunakusanya na kutunza takwimu za kiujumla juu ya shughuli zako mtandaoni, habari hizi haziwezi kueleweka kibinafsi wakati wote. Hatuunganishi anwani ya IP na utambuzi wa mtu binafsi, labda kama kumetolewa ruhusa kabla au ikilazimika kushughulikia tatizo.

Namna Tunavyotumia na Kutoa Habari Zako

Rcg.org, worldtocome.org na realtruth.org hutumia habari zinazotolewa na watumiaji kwa hiari ili kuboresha uzoefu wao kwenye mtandao, iwe ni kutoa ubadilishanaji au vitu binafsi mahali husika au kuwezesha kuandaa fahirisi kwa wakati ujao kulingana na mapendeleo ya watumiaji.

Wakati mwingine, tunatumia taarifa zako binafsi zinazojulikana kukupatia taarifa wewe binafsi, kama vile, lakini haiishii hapo tu, vijarida mtandao na vitu vinavyotolewa kwa barua pepe.

Hatutatoa kwa umma habari yoyote tunayokusanya kutoka kwa watumiaji wa mtandao bila ukubali kwa maandishi uliotolewa kabla na mtumiaji isipokwa: (a) habari hiyo tayari inajulikana kwa umma, au (b) utoaji wa namna hiyo unatakiwa kisheria, agizo la mahakama, au unatakiwa na serikali nyingine au mamlaka ya kusimamia sheria.

Usalama

Kanisa la Mungu Rejeshwa (na rasilimali husika) hutumia viwango vya taratibu za usalama viwandani kulinda dhidi ya upotevu, matumizi yasiyo sahihi au mabadiliko yasiyoruhusiwa habari zote za kibinafsi zilizo chini ya uwezo wake zinazoweza kutambuliwa. Aina hii ya itifaki inajumuisha, kuta za moto, vificho, ulinzi kwa neno la siri na ulinzi halisi mahali pa kazi.

PAMOJA NA HATUA HIZI ZA KIUSALAMA, HATUWEZI KUKUHAKIKISHIA KWAMBA MAWASILIANO YAKO YOTE YA BINAFSI AU HABARI BINAFSI HAZITAWEZA KUTOLEWA AU KUFIKIWA KINYUME CHA SHERIA NA UPANDE WA TATU USIORUHUSIWA.

Sera ya Kujitoa

Mtumiaji anaweza kujitoa wakati wowote kutoka katika orodha za wanaotumiwa habari pepe. Tutatuma ujumbe wa kuthibitisha uamuzi wa kutaka kutoa data kwenye anwani ya barua pepe inayotumika sasa iliyosajiliwa kwa ajili ya mtumiaji huyo. Mtumiaji atatakiwa kujibu uthibitisho huo ndani ya siku tatu (3) za kazi. Pindi unapojibu, habari zako zinaondolewa kabisa kutoka kumbukumbu zetu. Kama ujumbe wa kuthibitisha hautapokewa, tutaendelea kumhifadhi msajiliwa na data zake husika.

Ukomo wa Uwezo Wetu

Wakati faragha yako ni ya muhimu sana kwetu, kwa sababu ya kuwepo sheria na mazingira ya marekebisho, hatuwezi kuhakikisha bila shaka kwamba mawasliano yako binafsi na habari zingine za kibinafsi zinazoweza kutambulika hazitaweza kutolewa kwa upande wa tatu. Kwa mfano, tunaweza kulazimishwa kutoa habari kwa serikali au upande wa tatu katika nyakati fulani, au upande wa tatu unaweza kuingilia kinyume cha sheria au kufikia upitishaji au mawasiliano binafsi. Vilevile, tunaweza (na unaturuhusu) kutoa habari yoyote juu yako kwa vyombo binafsi, kama vile vya usimamizi wa sheria au maafisa wengine wa serikali, na ikiwa, kwa busara yetu tutaamini ni lazima au inafaa kuchunguza au kushughulikia matatizo yanayoweza kutokea au maulizo.

Malalamiko ya Mtumiaji

Malalamiko ya mtumiaji kuhusu utunzaji wa faragha yapeleke kwenye Huduma za Tovuti.

14/01/15
AkSyFHyK

Vitabu Vingine