JavaScript

This website requires the use of Javascript Explain This   to function correctly. Performance and usage will suffer if it remains disabled.
Liko Wapi Kanisa la Mungu Leo hii?
Photo of a CongregationNew York, Marekani Photo of a CongregationJamaika Photo of a CongregationPeru Photo of a CongregationIdaho, Marekani Photo of a CongregationIndia Photo of a CongregationUbelgiji Photo of a CongregationKenya Photo of a CongregationArkansas, Marekani Photo of a CongregationAfrika Kusini Photo of a CongregationUingereza Photo of a CongregationNigeria Photo of a CongregationOhio, Marekani

Yesu alisema, “Nitalijenga Kanisa Langu.†Kuna shirika moja linalofundisha ukweli wote wa Biblia, na limeitwa kuishi kwa “kila neno la Mungu.†Je, unajua namna ya kulipata? Kristo alisema lita:

  • Fundisha “yote†Aliyoagiza
  • Kuwa na washiriki walioitwa na kuwekwa wakfu kwa ile kweli
  • Kuwa “kundi dogoâ€
Habari za Mwandishi
Photo of David C. PackDavid C. Pack 

Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Mungu Rejeshwa, Mhariri-Mkuu wa Jarida la Ukweli Halisi, na sauti ya programu ya Ulimwengu Ujao, Daudi C. Pack amewafikia mamilioni wengi ulimwenguni na kweli za Biblia zilizo na nguvu sana—zisizojulikana karibu kwa wote. Ameandika vitabu na vijitabu 80, mwenyewe ameanzisha zaidi ya mikusanyiko 50, na alionekana kama mgeni kwenye Kituo cha Historia (The History Channel). Bwana Pack alihudhuria Chuo cha Mabalozi huko Pasedena, Kalifonia, aliingia katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu Mzima mwaka 1971, na yeye binafsi alifundishwa na mwanzilishi wake, Herbert W. Armstrong.

Pengine ungependa kusoma:

Kwa nini Unaishi?

na David C. Pack

KWA NINI unaishi—KWA NINI ulizaliwa? Maana ya maisha yako ni nini? Je uliwekwa Hapa kwa sababu? Unaweza kujua—lazima ujue!

KWA NINI ULIZALIWA? Je kuna sababu—maana—ya maisha yako? Je, Uwepo wako ni sehemu ya mpango wa Mungu?

Je, mwanadamu aliwekwa duniani na Muumba mwenye hekima-yote kama sehemu ya Kusudi kuu—MPANGO MKUU? Kujua jibu ni jambo la muhimu sana!

Fikiria kwa kitambo. Kipi chaweza kuwa muhimu zaidi kukielewa kuliko kusudi la maisha yako?

Wakanamungu hukataa kujua. Wale wasiokubali kwamba Mungu yuko kwa hakika hawawezi kukubali kwamba Ana Mpango Mkuu.

Wabeuzi hudhihaki juu ya uwezekano wa kujua. Wanaona mkanganyiko na kutokukubaliana kwa kiasi kikubwa juu ya swali hili na kuhitimisha kwamba kamwe haliwezi kujibika.

Wanasayansi hawawezi kugundua maarifa haya kwa njia ya uchunguzi wa kimaabara. Wanajimu, wanamikrobiolojia na wengine walio wakweli kuhusu hoja hukiri kwamba Mungu yupo, lakini hiki pekee yake hakiwezi kufunua Mpango Wake kwa ajili ya mwanadamu.

Wanafalsafa hawawezi kuutambua kwa njia ya kutafakari au mijadala. Majibu yanayofunuliwa kwa namna ya Mungu hayawezi kupatikana kwa karne za kutafakari maswali.

Waelimishaji hawawezi kufundisha kile ambacho wao wenyewe kamwe hawakufundishwa. Wale ambao tu hufundisha kutoka kwenye vitabu vilivyoandikwa na watu wengine hawezi kufundisha kile ambacho hakimo ndani ya vitabu hivyo.

Wanajimu hung’ara kwa ujanja na hila ambazo hazifunui chochote cha thamani. Je, kuna yeyote anayefikiri kwa makini kwamba “wafanya biashara†kama hawa (wale wanaouza ubashiri kama ufahamu wa kweli), wakidhaniwa huwasiliana na “wafu†na “ulimwengu wa roho†(kwa hakika roho za mapepo), wanashikilia maana ya maisha?

Wanateolojia hutoa nadharia zilizobuniwa-kibinadamu na bandia. Dini zote hudai kuwa na majibu kwa maswali ya maisha, lakini mawazo yao hufifia kama vibadala rahisi—ubunifu feki tupu—wakati ukweli wa kustaajabisha wa Mpango wa Mungu unapoeleweka kikamilifu.

Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila ya fununu kwamba kwa nini wako hapa. Wanaenda bila mwelekeo wowote, hawajali kuhusu majibu ya maswali makuu ya maisha—kwa nini maisha na kwa nini kifo? Wengine hufurahia kushiriki midahalo juu ya maana ya maisha, lakini kamwe hawafikii kwenye majibu sahihi. Wengi huhitimisha kwamba mwanadamu ni zaidi kidogo kupita uzao wa mageuko—upofu, ubahatishaji!

Matatizo Yasiyotatulika

Ulimwengu unashuhudia mlipuko wa maarifa katikati ya mateso, huzuni, kutoridhika na machafuko makuu sana. Kwa nini ongezeko la kuporomoka kwa maadili namna hii sambamba na maendeleo ya vitu ya kushangaza? Silaha za maangamizi sasa zinatishia kuendelea kuishi kwa mwanadamu.

Kwa nini? Na kutoka hapa tunaenda wapi?

Idadi na uzito wa matatizo yanayomkabili mwanadamu hayajawahi kamwe kuwa makubwa kama hivi—magonjwa, uchafuzi wa mazingira, umaskini, ujinga, mkanganyiko wa kidini, vita, ughaidi, uhalifu, ghasia, njaa, uovu, utumwa, unyanyasaji, mageuzi ya kisiasa na mengine mengi—kwa nini?

Matatizo ndani na kati ya mataifa hayajawahi kamwe kuleta mgawanyiko kati ya watu kama sasa—kwa nini?

Kadri muda unavyopita ndivyo matatizo zaidi huja, hayapungui—kwa nini?

Vile vile, matatizo yaliyopo kwa ujumla huendelea kuwa mabaya badala ya kuwa ahueni—kwa nini?

Kwa nini, kwenye kila geuko, mwanadamu ameboronga, vuruga na kushindwa vibaya katika harakati zote za kutatua matatizo yake ambayo kwa kweli ni makubwa?

Watu mmoja mmoja, hawajawahi kamwe kuonekana kutoweza zaidi kutatua na kuyashinda matatizo yao binafsi. Kama ilivyo kwa ulimwengu kwa ujumla, kadri muda unavyopita watu binafsi na familia wanaonekana kuzama katika bahari ya kuporomoka kwa maadili na katika kile kinachoonekana kuwa ugumu usiosemeka. Zaidi na zaidi wanaonekana kutokuwa na uwezo wa kuongoza maisha yao—kwa nini?

Wanadamu wamefanya ugunduzi mwingi wa kiteknolojia unaoshangaza, lakini hawawezi kutengeneza majibu ya matatizo yao. Wanadamu wamethibiti nguvu za kompyuta kuwasaidia kuchambua kiasi kikubwa cha habari, lakini watu hawawezi kutatua kwa usahihi matatizo yao binafsi. Wanasayansi wamegundua mengi kuhusu ukubwa, uzuri na usahihi wa ulimwengu, lakini hawawezi kugundua njia ya amani. Wanajimu wanaweza kutafuta na kuona galaksi mpya, nzuri kote ulimwenguni, lakini hawawezi kupata njia ya kuhifadhi uzuri na fahari ya dunia. Wanasayansi pia wamesambaratisha nguvu za atomu, lakini hawana uwezo wa kuainisha majibu kwa maswali makuu ya maisha. Wakufunzi wamewafundisha mamilioni jinsi ya kujipatia kipato, lakini si jinsi ya kuishi—kwa sababu wao wenyewe hawajui jinsi ya kuishi.

Pamoja na umahili wa ugunduzi wa mwanadamu ukiwa umetumika kutengeneza silaha za maangamizi, na kuleta mifumo ya ughaidi iliyo mibaya zaidi na zaidi kwa ulimwengu usio na uwezo wa kuishinda kwa mafanikio, ulimwengu uko katika machafuko ya kutisha.

Mwanahistoria wa mambo ya kiutawala anayejulikana sana Peggy Noonan anafupisha hali changamani, iliyovurugika ya historia ya mwanadamu namna hii: “Katika utepe mrefu wa historia, maisha yameendelea kutawaliwa na dosari na vurugu, yakijawa na njaa, vitisho, vita na magonjwa. Lazima tulifikiri tungekuwa na hali nzuri kwa sababu mwanadamu amekuwa bora. Lakini kwa hakika mwanadamu hawi “bora,†au siyo? Mwanadamu ni mwanadamu. Hulka ya mwanadamu ni hulka ya mwanadamu; utashi wa kuharibu unaenda sambamba na utashi wa kujenga na kutengeneza na kuboresha†(“Zama ya Amerika Isiyo na Uhakika,†Knight Ridder, 11/9/ 2001).

Nani angeweza kubisha?

Hivyo, kuna kitu hakiko sawa kabisa. Uwezo usio wa kawaida wa mwanadamu wa kuunda umemwacha hajakamilika—na umethibitika kuwa hautoshi kutatua matatizo yake. Nguvu na umahiri wa fikra zake zimeelekezwa zaidi kwenye kuharibu kuliko kwenye juhudi za uzalishaji katika upangaji na ubunifu.

CHANZO Kinachofunua

Mheshimiwa Winston Churchill, Waziri Mkuu mashuhuri wa iliyokuwa Uingereza Kuu, alitangaza, “Kuna kusudi linalotekelezwa hapa chini.†Alifahamu kwamba kwa namna fulani Mwenye Uwezo mkubwa kabisa alikuwa akitekeleza MPANGO usioonekana na unaoeleweka-kidogo-sana duniani.

Lakini mpango huo ni nini? Churchill hakujua.

Wengi wanatamani kujua kile ambacho Mungu anafanya “hapa chini,†lakini hawana wazo jinsi gani watajifunza ni kitu gani. Mwanadamu hajui aelekee wapi. Ubinadamu haujui Chanzo cha maelekezo ni kipi.

Muumbaji wa wanadamu aliwaletea Kitabu cha Maelekezo kwa kinaganaga chenye habari nyeti. Kinafafanua asili, usanifu na kusudi la uumbaji Wake mkubwa kuliko mwingine wowote. Kinatambulisha ufunguo uliofichwa—kipengele kinachokosekana—ili kufikia matumizi adilifu na sahihi ya fikra. Kinafafanua njia ya amani, furaha, wingi na mafanikio kwa wote.

Lakini Kitabu hiki kikuu cha Maelekezo kinapuuzwa karibu na wote, kinawakilishwa isivyo, kinaeleweka isivyo na kinakataliwa. Nazungumzia Neno la Mungu—BIBLIA TAKATIFU! Matokeo yake, matatizo, taabu na maovu ya ustaarabu yanaongezeka. Bila kuwa na suluhu inayoonekana, hali inazidi kuwa mbaya tu.

Simama na ufikiri! Tumia busara ya kawaida. Je Mungu angeweza kuumba maajabu Yake ya uhandisi—fikra zako—na kuzipeleka bila Kitabu cha Maelekezo kufafanua jinsi ya kuzitumia?

Hapana shaka! Kitabu hiki kisichothaminiwa na kinachoeleweka isivyo kipo. Tunahitaji kuchunguza “Kitabu hiki cha Mwongozo†ambacho kinafungua siri ya kwa nini unaishi. Kinakupatia matumaini—na suluhisho kwa matatizo ya mwanadamu. Kinafafanua ni kwa nini mwanadamu hawezi kutatua matatizo yake bila ya uingiliaji wa Mungu Ambaye anatekeleza Kusudi Lake. Kinafafanua maana ya maisha na kujibu swali la muhimu kuliko yote unalokabiliana nalo—kwa nini unaishi?

Mwanamageuko hawezi kujibu swali hili. Anaamini kwamba maisha yaliibuka kwa mamilioni ya miaka. Anaamini kwamba nadharia yake inafafanua uwepo wa mamilioni ya mimea na wanyama duniani, huku mwanadamu akiwa tu ni mnyama wa juu katika mlolongo wa matukio ya mageuko. Wanamageuko wanakataa uumbaji maalumu wa Muumbaji Mkuu na kwa hiyo hukataa Chanzo cha maarifa yaliyofunuliwa Aliyoyatuma kwa uumbaji Wake.

Watetezi wa nadharia ya mageuko hawawezi kufafanua uwezekano wa kustaajabisha wa mwanadamu, au kwa nini kamwe haujapatikana. Wala hawawezi kufafanua kwa nini mambo yanaendelea kuwa mabaya—huku ugeukaji ukifundisha kwamba mwanadamu anaibuka kuelekea daraja la juu.

Dini za ulimwengu zimeshindwa kabisa katika kutoa maana—au tumaini—kwa maisha. Dini hizi karibu zote kwa pamoja zimekubaliana na wanamageuko na hata ule unaodai kuwa Ukristo umekataa maelezo ya uumbaji katika kitabu cha Mwanzo kwa kiwango kikubwa kama hadithi za kubuni na “fasihi†za Kiyahudi. Lakini, wakati wakikataa Maandiko mengi yanayofafanua kusudi la maisha, wanadai kuamini aya chache zilizochaguliwa na kwa uongo kujipachika wenyewe jina la “Ukristoâ€!

Lakini Kitabu cha vitabu hutoa tumaini na maana. Huu hapa ni ukweli uliowekwa dhahiri kutoka kwenye Kitabu hiki cha Maelekezo.

Kilele cha Uumbaji wa Mungu

Mwanzo 1 inarekodi maelezo ya Uumbaji: “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi†(fu. 1). Haya ni maneno ya kwanza ya Biblia. Ni kauli iliyobeba kila kitu. Inajumuisha kila kitu na iko wazi, bila utata au nafasi ya kutilia shaka. Mungu anasema hiki ndicho Alichofanya.

Mnamo siku ya sita ya uumbaji, mwishoni mwa sura ya 1, Mungu alisema, “Na tufanye mtu kwa mfano Wetu, kwa sura Yetu†(fu. 26). Mwanadamu aliumbwa afanane, “aliumbwa wa jinsi†ya Mungu. Mwanadamu alikuwa hitimisho la mafanikio—kilele kikuu—cha Uumbaji wa Mungu. Hakuwa wa jinsi yoyote ya mnyama, bali aliumbwa katika “mfano na sura†ya Mungu. Hii inafunua tofauti kubwa baina ya wanadamu na kila jinsi ya mnyama.

Fungu la 25 linafunua kwamba wanyama walifanywa katika njia tofauti na kwamba kila mmoja alifanywa kwa “jinsi yake.†Angalia: “Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake...â€

Farasi wanafanana na farasi. Mbwa wanafanana na mbwa. Ng’ombe wanafanana na ng’ombe. Ndege wanafanana na ndege. Hakuna yeyote kati ya hawa—na hakuna kitu kingine chochote—kimefanywa na kutengenezwa katika sura na mfano wa Mungu. Ndivyo anavyosema Mungu, aliyevuvia maelezo haya katika Neno Lake!

Wanadamu siyo sehemu ya jinsi ya wanyama. Hawana mfano wa “mnyama wa nchi†awaye yote. Kama sehemu ya jinsi ya Mungu, mwanadamu aliumbwa ili kuingia katika uhusiano na Muumba wake ambao wanyama kamwe hawawezi kuufikia. Jambo hili litaelezewa baadaye.

Kufikia hapa, ni muhimu sana kufahamu kitu kuhusu NANI na NINI ni Mungu. Mwanzo 1 hufunua maarifa ya muhimu sana.

Fungu la kwanza linasema, “Hapo mwanzo MUNGU…†Musa alirekodi vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale katika lugha ya Kiebrania. Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “Mungu†ni Elohim. Neno hili ni la wingi katika umoja, kama timu, kundi, familia au kanisa.

Mungu ni Familia moja—wakati huu ikiwa imeundwa na Viumbe wawili.

Fungu la 26 lilisema, “Na tumfanye [zaidi ya mmoja] mtu kwa mfano WETU, kwa sura YETU.†Ni wazi kulikuwa na Nafsi zaidi ya moja katika uumbaji. Fungu hili linarekodi FAMILIA ya Mungu wakiongea na kuumba.

Mtume Yohana anakuza kile ambacho Musa alirekodi: “Hapo mwanzo kulikuwako Neno†(Yohana 1:1), na kisha akaendelea, “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.†Kama yuko Mmoja ambaye ALIKUWA Mungu, lakini pia alikuwa PAMOJA na Mungu, ni wazi kwamba Viumbe wawili—Nafsi mbili—wanaelezewa. Hii ndiyo sababu Kristo angeweza kuwa Mungu na pamoja na Mungu wakati huo huo.

Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “Neno†ni Logos. Lina maanisha “Msemaji.†Huyu ndiye alifanyika Kristo na ndiye Yule anayezungumza katika Mwanzo 2.

Yohana 1:14 linaendelea, “…Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu.†Kiumbe-Mungu pekee aliyefanyika mwili ili akae miongoni mwa wanadamu ni Yesu Kristo. Kumbuka, inasema kwamba Neno “alifanyika mwili.†Kristo hakuwa mwili mpaka alipokuja duniani ili kuwa Mwokozi wa wanadamu.

Kuanzia katika Mwanzo 2:4 kuna jina lingine lililotafsiriwa kama “Mungu,†YHVH. Linatafsiriwa vizuri zaidi “wa Milele†au “Aishiye-mileleâ€â€”Msemaji/Neno.

Fikra za Mwanadamu dhidi ya Silika ya Mnyama

Wanyama wana silika. Hakuna mwanamageuko aliyeweza kufafanua kwa usahihi kwa nini jambo hili liko hivi au jinsi gani hata linawezekana.

Kwa nini nyuki wanarudi kwenye mzinga wao siku baada ya siku, kizazi baada ya kizazi, wakitengeneza asali kwa njia ile ile waliyoitumia miaka 1,000 iliyopita, isipokuwa walisanifiwa kufanya hivyo?

Kwa nini wazaliwa wa ng’ombe na wa farasi husimama kitambo kidogo tu baada ya kuzaliwa? Ni kitu kilichopangiliwa ndani yao—kwa njia ya silika.

Kwa nini ndege wanajua kuruka kuelekea kusini, tena katika muda mwafaka? Kisha, ni jinsi gani wengi wanajua kurudi kwenye mti ule ule kila mwaka katika Amerika ya Kati au Amerika ya Kusini—na kisha huruka kurudi kaskazini, ndani ya ratiba? Silika!

Jinsi gani dubu wote “wanajua†kula chakula cha kutosha kuweza kustahimili ubumbwaaji kipindi chote cha majira ya baridi kali—na ni kwa jinsi gani dubu wote hata hujua kubumbwaa, isipokuwa kama hali hii imejengwa katika tabia zao za kisilika?

Kwa nini mbwa mwitu huwinda kwa njia ile ile—kwenye makundi—na hula vitu vile vile?

Kwa nini karibu kila ndege ana mtindo wake tofauti wa kutengeneza kiota?

Kuna wakati jaribio lilifanywa kwa ndege aina ya mnana. Vizazi vitano vilivyofuatana vilinyimwa vifaa vya kujengea viota. Kizazi cha tano kikapewa vifaa lakini kilikuwa hakijawahi kamwe kuona kiota. Papo hapo kiliendelea kutengeneza viota vilivyoonekana sawa kabisa kama viota vyote vya ndege mnana wengine.

Ingawa uwezo huu wa silika ni wa kushangaza kama ulivyo, hudumazwa na uwezo na nguvu za akili za mwanadamu. Wanadamu wana uwezo wa kupata maarifa. Wanaweza kufika mwezini na kuunda kompyuta zenye uwezo wa juu. Wanaweza kuchora ramani za nyumba zenye urefu wa viwanja sita vya mpira wa soka na kugundua siri za atomu. Wanyama hawana uwezo kama huo.

Watu hawapati kujua kila kitu wanachohitaji kukijua ili kuendesha maisha yao kwa mafanikio kisilika. Ni lazima wapate maarifa zaidi kadri wanavyoendelea kuwa watu wazima na kadri hali inavyowalazimu.

Maarifa yote huangukia katika makundi mawili: (1) maarifa ya asili juu ya jinsi ya kutenda kazi na maada [mata] na vitu vya asili, na (2) maarifa ya kiroho yaliyo muhimu kwa watu kuendeleza uhusiano binafsi na Mungu na wanadamu wenzao. Maarifa yote ni ama ya asili au ya roho.

Maarifa ya asili hupatikana kwa njia ya milango mitano ya fahamu—kuona, kusikia, kunusa, kugusa na kuonja. Watu wanaelewa kwamba ni lazima WAPATE maarifa fulani na kuongezea mengine katika maisha yao yote. Milango ya fahamu huwezesha jambo hili.

Aliumbwa Mpungufu

Mtunga Zaburi aliandika, “…kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha†(Zab. 139:14). Jambo hili ni kweli zaidi kuhusu ubongo wako—FIKRA za MWANADAMU! Lakini ni pungufu—na ndivyo ulivyo.

Mwanzo 1 inarekodi maelezo ya uumbaji wa mwanadamu KIMWILI. Adamu aliumbwa kwa namna kwamba alifanana—alionekana kama—Mungu katika umbile na sura kimwili. Japokuwa alikuwa mkamilifu kimwili, Adamu aliachwa mpungufu kwa namna ya roho. Kijenzi muhimu sana cha kiroho kilikuwa kinakosekana.

Angalia Mwanzo 2:7: “...Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.†Mwanadamu amefanywa kutokana na maada ya asili—nyama. Akiwa hajafanyizwa kwa Roho, kama Mungu, amefananishwa—fanyika—katika “sura na mfano†wa Mungu.

Adamu alikuwa wa mwili. Alivuta pumuzi, na alihitaji chakula na maji. Asingeweza kuishi bila mojawapo ya hivi.

Mungu alikusudia kuanza uumbaji Wake wa kiroho na Adamu. Mchakato huu kamwe haujawahi kuhusisha wanyama. Lakini kwanza tunalazimika kufahamu pointi inayohusiana.

Siyo Nafsi Isiyokufa

Watu wengi hawafahamu uhusiano baina ya watu na nafsi. Karibu kila mmoja amefundishwa na anadhani kwamba kila mtu huzaliwa na/na ana NAFSI ISIYOKUFA. Imani ya wengi ni kwamba, wakati wa kufa, nafsi za wenye dhambi huenda jahannamu milele, wakati waliookoka wanaenda mbinguni milele.

Je! hiki ndicho ambacho Biblia inasema?

Neno la Mungu linasema, “mshahara wa dhambi ni mauti†(Rum. 6:23), na kwamba “dhambi ni uasi wa sheria†(1 Yohana 3:4). Kisha Je! Biblia pia ingeweza kufundisha kwamba watu wana nafsi zisizokufa? Ni kweli inaongea juu ya “nafsi,†lakini kwa muktadha upi?

Kumbuka Mwanzo 2:7: “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.†Fungu hili halisemi kwamba watu wana nafsi, lakini kwamba wao ni nafsi. Adamu akawa nafsi—hakupewa nafsi.

Kisha, karibu mara ile, Mungu alimwonya Adamu, “Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika†(fu. 16-17). Mafungu haya yanapowekwa pamoja, yanafunua kwamba wanadamu ni nafsi, na kwamba nafsi zinaweza kufa!

Nabii Ezekieli anathibitisha agizo lililoko kwenye kitabu cha Mwanzo. Alivuviwa kuandika mara mbili, “roho [nafsi] ile itendayo dhambi ITAKUFA†(18:4, 20). Kifo ni kutokuwepo kwa maisha.

Hatimaye, angalia Mathayo 10:28: “Msiwaogope wauao mwili, wasiweze kuiua na roho [nafsi]; afadhali mwogopeni yule [Mungu] awezaye kuangamiza mwili na roho [nafsi] pia katika jahannamu.†Fahamu! Nafsi zinaweza kuharibiwa!

Lakini Yohana 4:24 inasema, “Mungu NI Roho.†Mungu amefanyika kwa Roho. Wanadamu wamefanyizwa kwa nyama. Kwa sababu Mungu ni Roho, Roho yake lazima itende kazi pamoja na roho nyingine ndani ya uumbaji Wake wa mwanadamu. Lakini siyo nafsi isiyokufa.

Hakuna “roho ya wanyama,†inayowapa uwezo wa kifikra, kwa kuwa Mungu ameweka mfumo ndani ya wanyama wa kutenda kwa mafanikio kila kitu wanachohitaji ndani ya mazingira yao kwa njia ya silika. Na wanadamu hawana nafsi isiyokufa. Lakini 1 Wakorintho 2:11-12 inafunua kwamba wana kile ambacho Mungu anakiita “roho ndani ya mwanadamu.†(Unaweza kusoma kijitabu chetu cha bure Kile Ambacho Sayansi Haitaweza Kugundua Juu Ya Fikra Zako ili kujifunza mengi zaidi kuhusu roho hii. Hapa imeelezewa kwa ufupi tu ili kukusaidia uelewe Mpango Mkuu wa Mungu.)

Wanadamu hupokea roho ya mwanadamu wakati mimba inapotungwa. Inawaruhusu, kupitia milango mitano ya fahamu, kupata na kuhifadhi maarifa kwa njia ambayo wanyama hawawezi. Roho ya mwanadamu siyo mwanadamu MWENYEWE—iko NDANI ya mwanadamu. Kuna tofauti kubwa! Roho hii haina uwezo wa fikra za kwake na kwa yenyewe. Vivyo hivyo ubongo.

Ubongo husikia kupitia masikio na huona kupitia macho. Roho ya mwanadamu haifanyi haya yenyewe na kwa namna yake. Ubongo hufanya kazi ya kufikiri—huku roho ikiupa uwezo wa akili. Kumbuka, roho iko ndani ya mwanadamu, ikiipatia milango mitano ya fahamu za kimwili uwezo wa kufanya kazi pamoja na ubongo kuchambua maarifa ya asili na kutambua maana yake. Roho huzitia nguvu fikra kuchakata taarifa zilizopokelewa kupitia milango mitano ya fahamu.

Uwepo wa roho hii unamruhusu Mungu, aliye Roho, aendeleze uumbaji wa kimwili kuingia kwenye milki ya kiroho. Baadhi ya vitu vingine lazima vieleweke kabla ya kuendelea na jinsi ambavyo Mungu anatenda kazi ndani ya fikra ambazo Amezitawala.

Uchaguzi Mkuu

Jinsi gani mwanadamu aliingia katika hali ya mkanganyiko, faraka na kutokukubaliana iliyoko duniani kote leo? Ilianza na uchaguzi mbaya kati ya miti miwili.

Zingatia maelekezo haya ya moja kwa moja kwa wazazi wetu wa kwanza: “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na MTI WA UZIMA katikati ya bustani, na MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA†(Mwa. 2:8-9).

Mungu alimwonya Adamu kwamba ulaji wa matunda ya mti wa pili ungeleta kifo: “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile: kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika†(Mwa. 2:17). Mungu alifafanua, “…kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi†(3:19).

Maelezo haya ya Bustani ya Edeni yanayojulikana sana lakini yanayoeleweka kidogo, ndiyo yanashikilia ufunguo. Ndani yake, Adamu na Hawa walifanya uchaguzi wa majaaliwa. Maelezo ya Mwanzo 3 yanarekodi hivi: “Basi nyoka [Shetani] alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu†(fu. 1).

Ulimwengu hauelewi juu ya ukweli wa kushangaza ambao unapita kila kitu kinachotokea juu ya sayari hii. Ufunuo 12:9 inasema, “Shetani, audanganyaye ulimwengu wote.†2 Wakorintho 4:4 inafunua kwamba yeye ni “mungu wa ulimwengu huu.†Fungu hili linamwonyesha ibilisi akiwa hodari, mjanja—mwerevu sana kiasi kwamba—ilimfanya afanikiwe sana katika kumtamanisha Hawa. (Soma vijitabu vyetu viwili Shetani Ni Nani? na Ulimwengu Matekani ili kujifunza juu ya roho huyu mkubwa aliyeanguka na ushawishi wake kwa ustaarabu.)

Tukiendelea na maelezo katika kitabu cha Mwanzo: “Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika HAMTAKUFA†(fu. 1-4).

Ibilisi alimdanganya Hawa. Alimwamini na akaweza kumfanya Adamu kuingia dhambini pamoja naye. Shetani aliwaambia, “Hakika hamtakufaâ€â€”kwa maneno mengine, “mna nafsi zisizokufa.†Tangu hapo amekuwa akiwadanganya wanadamu!

Shetani aliendelea, “kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo†(fu. 5-7).

Shetani akawafanya wakatae—WASIAMINI—onyo la Mungu katika Mwanzo 2:16-17. Udanganyifu wake uliwafanya watoto hawa wawili wakubwa waamini kwamba hawakuhitaji tena kumsikiliza Mzazi wao. Hulka ya mwanadamu ikaingia. Wakiwa wamefukuzwa kutoka bustanini, walilazimika kujitegemea wenyewe.

Shetani aliwaridhisha kwamba wangeweza kuwa “miungu†(neno la Kiebrania lililotumika hapa ni Elohim) akilenga kwenye fahari yao ya kibinadamu—ubatili wao. Aliwaridhisha kwamba fikra zao zilikuwa zimekamilika bila Mungu. Walimwamini na wakajitwalia wenyewe mamlaka ya Mungu ya kufasili jema na baya. Fikra zao kamilifu za kibinadamu zikaharibiwa na ubatili, uliowaingia na kuwafanya wajiinue.

Maelezo haya yanawakilisha uamuzi wa majaliwa. Mwanadamu alikuwa anakabiliwa na uamuzi mkubwa kati ya Njia ya Mungu, inayoenda kwenye UZIMA WA MILELE, au njia ya ibilisi, inayoenda kwenye KIFO!

Kumjaribu Mungu

Adamu na Hawa walichanganyikiwa kuhusu ama wamsikilize Shetani au Mungu. Hawakuweza kuwa na uhakika kama Mungu alikuwa anasema ukweli mpaka kwanza wamjaribu. Kusema kweli, Adamu na Hawa walifanya jaribio la kwanza la ulimwengu.

Akikataa maagizo ya Mungu yaliyofunuliwa, Adamu alitumia akili, uchunguzi, na majaribio ya kibinadamu. Akitumia fikra zake tu na akiongozwa na ibilisi, aliendelea mbele kula matunda ya “mti wa ujuzi wa mema na mabaya.†Alifikiri kuwa alijua zaidi kuliko Mungu. Alijichukulia mwenyewe haki ya kuamua kati ya kilicho sahihi (chema) na kisicho sahihi (kiovu). Alifikiri kwamba angeweza kutegemea fahamu zake mwenyewe za asili.

Kwa mantiki hii, uamuzi wa Adamu na Hawa kweli “ulifumbua macho yao†(Mwa. 3:7)—lakini si kwa mambo ya Mungu. Roho ya uasi ikawaingia kwa mara ya kwanza. Roho mbaya ya ushawishi wa Shetani iliziingia fikra zao kama kuonekana kwa “hulka ya mwanadamu†kwa mara ya kwanza. Hivi ndivyo vile macho yao “yalifumbuliwa.†(Ili kufahamu hii ilimaanisha nini soma kijitabu chetu Je Mungu Aliumba Hulka Ya Mwanadamu?)

Adamu na Hawa Watengwa

Kwa uamuzi huu, Adamu alijitenga kabisa yeye mwenyewe na wanadamu wote wasimfikie Mungu. Mti huu MWINGINE umekuwa ukiongoza namna ya kufikiri ya watu na mataifa tangia uamuzi wa majaliwa wa Adamu. Ni lazima tuelewe jambo hili linamaanisha nini kwetu. Kwa sababu alimkataa Mungu na Mti wa Uzima, Adamu alikataliwa na Mungu na kufukuzwa kutoka bustanini. Wanadamu walitupwa nje pamoja naye kwenye ulimwengu wa Shetani!

Uamuzi wa Adamu ulizuia fursa nyingine yoyote ya kupata maarifa ya kiroho. Hivyo, ufahamu wake ukakomea kwenye kile ambacho angeweza kujifunza kupitia milango mitano ya fahamu za asili—na ukamwacha wazi kupokea matangazo ya Shetani (Efe. 2:2). Hulka ya mwanadamu ikawa imezaliwa!

Kuchagua Mchanganyiko

Angalia kwamba mti mbaya uliwakilisha maarifa ambayo yalikuwa “mema na mabaya.†Mti haukuwa mbaya kabisa—ulikuwa na mchanganyiko wa maarifa mema na mabaya! Ndivyo ilivyo kwa serikali, falsafa, mifumo ya elimu, na dini na makanisa ya ulimwengu huu. Baadhi yana kiasi kidogo cha maarifa ya kweli (“memaâ€), yakiwa yamechanganyika na mengi ya uongo (“mabayaâ€).

Kwa miaka 6,000, Mungu amewaambia watumishi Wake kutochanganya ukweli na uongo. Alionya kwamba kula matunda ya mti mbaya kungepelekea kifo. Adamu hakumwamini Mungu, na alikufa—akatengwa na Mungu. Onyo ni lile lile kwetu!

Nilipokuwa nikijifunza ukweli kwa mara ya kwanza katika mwaka 1966, nilifundishwa kifanani ambacho sikuwahi kukifikiri kabla na sijakisahau tangu hapo: Fikiri juu ya keki tamu iliyochanganywa na kiasi kidogo cha sumu kama aseniki, sianidi au sumu kali ya kusisimua neva, ingawa haina kitu kingine bali viinilishe vizuri. Kuila keki hii kutasababisha kifo wakati wote.

Viinilishe vizuri visingeweza kuishinda sumu iliyofichwa ndani ya keki. Wanadamu walichagua keki iliyotiwa sumu na wamebaki wakiwa wametengwa na Mungu tangu hapo.

Mungu, siyo watu, huamua kati ya jema na baya! Watu wanaweza kuchagua AMA watatenda jema au baya—lakini kamwe SI kipi chema au kibaya! Shetani alimridhisha Adamu kwamba alitakiwa achukue uwezo wa kufanya uamuzi huu yeye mwenyewe.

Tangu wakati huo mwanadamu amekuwa akifanya majaribio yake ya “kisayansi.†Kama ilivyo kwa keki, matokeo yake bado ni yakufisha!

Sheria Kuu ya Sababu na Athari

Kila mmoja anaifahamu sheria ya nguvu ya uvutano. Wote wanafahamu kwamba kama wataivunja sheria hii, inaweza “kuwavunja.†Kama mtu kwa bahati mbaya atadondosha tofali kwenye mguu wake, matokeo yanaweza kuwa mifupa iliyovunjika. Kama mruka angani ataruka kutoka kwenye ndege, na mwavuli ukashindwa kufunguka, matokeo ni kifo cha hakika.

Ingawa wengi hawaitambui kamwe kanuni ya sababu na athari kama sheria ya kudumu inayotawala karibu kila tendo maishani, wana habari kwamba ni kanuni inayotenda kazi katika nyakati fulani.

Kila athari inaweza kufuatiliwa hadi kwenye sababu moja au zaidi. Mimba zisizotarajiwa au haramu, uhalifu, matumizi ya madawa ya kulevya, kufilisika na athari zingine maelfu zote zinaweza kuunganishwa kwenye sababu halisi.

Mithali 26:2 inafundisha, “…laana isiyo na sababu haimpigi mtu.†Fungu hili linaonyesha kwamba sababu huleta athari. Ni vitu vichache tu vilivyo matokeo ya bahati.

Kwa nini mwanadamu haoni sheria hii ikitenda kazi anapouangalia ulimwengu kwa ujumla? Kwa nini hakuna anayetafuta SABABU ya shida na maovu ya ulimwengu huu? Kwa nini waelimishaji hawafundishi kanuni hii kuu kuliko zote? Utazame ulimwengu. Unashangaa KWA NINI umejawa na shida, huzuni na kutoridhika? Hata ule unaodhaniwa kuwa Ukristo karibu umepuuzia kabisa uhusiano baina ya sababu na athari.

Sababu ya taabu za ulimwengu ilianzia katika Bustani ya Edeni. Rahisi kama inavyotamkika, jambo hili ni kweli. Ulimwengu unapuuza uamuzi uliofanywa na Adamu na Hawa. Hawakuchagua kula matunda ya Mti wa Uzima, badala yake wakachagua kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Je umejiuliza kungetokea nini kama watu wawili tu wangechagua Mti wa Uzima? Fikiria jinsi gani kufanya hivyo kungebadili ulimwengu wa leo. Kila kitu kingekuwa tofauti!

Kusingekuwa na majeshi, vita, kifo, uharibifu au uhamishaji wa watu. Kusingekuwa na ukosefu wa chakula au kusikia njaa kwa sababu kungekuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya kila mtu. Kusingekuwa na matabibu, kwa sababu kusingekuwa na maradhi. Hospitali na zahanati zisingekuwepo. Wala kusingekuwa na magereza, jela, majaji na majeshi ya polisi yaliyopo kwa ajili ya kuwaadhibu wavunja sheria.

Furaha kwa watu wote, wingi, ustawi, amani na umoja vingejaa ulimwenguni kote. Watu wote wangeelewana—majirani, familia, watu mmoja mmoja na mataifa. Unaweza kufikiria ulimwengu kama huo ungekuwaje?

Wakati Adamu na Hawa walipofanya uamuzi mbaya, ilituathiri wewe na mimi moja kwa moja. Uchaguzi mmoja mbaya—SABABU—ulileta ATHARI za huzuni isiyosemeka! Usiufanye mgumu urahisi wa rekodi ya Biblia.

Uamuzi wao ulikuwa ni kukataa SHERIA kamilifu ya Mungu (Rum. 7:12, 14) na utawala—SERIKALI Yake—kama mwongozo katika maisha yao, na wakajisalimisha kwa Shetani na njia yake ya dhambi. Kwa sababu ya dhambi, hawakuweza tena kuifikia mibaraka ya Mungu, uongozi, ulinzi au karama ya Roho Yake Takatifu, ambavyo vingekuja kwa kula matunda ya Mti wa Uzima.

Nia ya Mwili

Kuna sababu nyingine inayohusiana kwa nini kuvunja sheria ya sababu na athari imeuletea ulimwengu matatizo yasiyotatulika. Lazima tutambue UFUNGUO mwingine wa muhimu unaofafanua kwa nini ulimwengu uko katika hali yake ya sasa.

Tulijifunza mwanzoni kwamba hulka ya mwanadamu ilionekana wakati macho ya Adamu na Hawa “yalipofumbuliwa.†Paulo, katika waraka wake kwa Warumi, anatoa kauli ya kushangaza. Angalia: “Kwa kuwa ile nia ya mwili [ya asili] ni uadui juu ya Mungu: kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii†(8:7). Tafsiri zingine zinatumia usemi “ni adui wa Mungu†mahali pa “ni uadui juu ya Mungu.â€

Fungu hili linatoa ufahamu wa kushangaza katika utendaji wa kila mtu kimwili—“mwiliâ€â€”nia. Ikiwa imetengwa na Mungu, nia ya asili ni ADUI Yake—inamchukia. Fikiri! Je mtumishi yeyote au mwanateolojia alishawahi hata kukudokezea jambo hili, achilia mbali kulifafanua?

HAPANA! Viongozi wa kidini wa ulimwengu huu ama wanapuuza kabisa ufahamu huu au hawatambui madhara yake ya kutisha!

Nia ya asili haitaki (na hata INACHUKIA) kujisalimisha kwa Mungu na kutii sheria Yake. Ingawa watu wengi wanadai kwamba “wanampenda Mungu,†ukweli ni kwamba nia zao kiasili zinachukia njia Yake na zinakataa kumtii.

Sasa, hapa kuna sababu ya kwa nini wengi hawawezi na hawataigundua: “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?†(Yer. 17:9).

Kwa hakika hii ni kauli ya kuduwaza. Ifikirie kwa uangalifu. Juu ya tabia zote za hulka ya mwanadamu—ubatili, wivu, tamaa, uchoyo, husuda, kiburi, upumbavu, chuki, n.k.—Mungu anafunua kwamba udanganyifu unazipita zote.

Si ajabu Yeremia pia aliandika, “Ee Bwana, najua ya kuwa njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake; kuelekeza hatua zake si katika uwezo wa mwanadamu anayetembea†(10:23).

Hii ni kauli nyingine ya ajabu. Wanapokabiliwa na matatizo au uamuzi muhimu, kwa urahisi ni kwamba watu hawajui la kufanya. Wanapotewa na jinsi ya kushughulikia na namna ya kutatua changamoto, shida na matatizo katika maisha yao binafsi. Liweke jambo hili katika njia nyingine, hawajui namna ya kuelekeza hatua zao.

Jinsi gani basi wataweza kutatua matatizo makubwa na changamani zaidi yanayoughubika ustaarabu leo? Hawawezi. Suluhu zilizotokana na kufikiri kibinadamu wakati wote huzalisha matatizo zaidi. Tutajifunza kwa nini.

Sababu Sahihi ya Kiroho

Je! Yule aliyemuumba mwanadamu, Yule anayesema Yeye “ni pendo†(1 Yohana 4:8, 16), asingeweza basi kufafanua umuhimu mkubwa wa upendo ndani ya Mpango Wake? Je angeweza kupuuza kufafanua kanuni ya SABABU na ATHARI?

Kusema kwa upana, kuna njia mbili tofauti za maisha. Moja ni njia ya “KUTOAâ€â€”njia ya upendo na kuwajali wengine—Njia ya Mungu. Nyingine ni njia ya “KUPATAâ€â€”njia ya kujipenda na kujijali mwenyewe—njia ya ulimwengu huu. Upendo huvumilia, ni mkarimu na unajali. Hugawia, hushirikiana, hutumikia na husaidia. Kristo alifundisha kwamba “Ni heri KUTOA kuliko kupokea†(Matendo 20:35).

Njia ya upendo ni sheria kuu ya kiroho isiyoonekana ambayo inawahifadhi wanaoishika na kuwavunja wale wanaoivunja! Haibadiliki wala kuzuilika na inaunganisha katika kila nyanja na uhusiano katika maisha. Kama ilivyo sheria ya nguvu ya uvutano, huwezi kuiona, lakini unaweza kuona athari za kuivunja.

Ulimwengu huu umejengwa juu ya njia ya “kupata†badala ya njia ya “kutoa,†ambayo ni Njia ya Mungu! Wakati wote watu wanang’ang’ana “kupata†zaidi—kulimbikiza—kukusanya kwa ajili yao wenyewe katika maisha yao yote.

Kufanya hivi kunavunja Amri ya Kumi, ambayo inakataza kutamani. Angalia kile ambacho Mungu anasema juu ya watu Wake, na wa mataifa yote, katika unabii ulioelekezwa kwa watakaokuwa hai mwishoni mwa zama: “Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda kwa udanganyifu†(Jer. 6:13). Sura mbili baadaye, kuna kauli inayokaribia kufanana, isipokuwa kwamba Mungu pia anaonya juu ya adhabu ya kutisha Atakayoileta kwa sababu ya mwelekeo huu wa ulimwengu mzima.

Mungu alimtaka Adamu kula matunda ya Mti wa Uzima ili kwamba angeweza kufurahia mambo yote mazuri ya maisha. Ni lazima Mungu alikuwa amemfafanulia mambo haya, kwa kuwa alimwambia kwamba kuvunja amri Yake ya msingi kungesababisha kifo.

Kama Adamu angekula matunda ya Mti wa Uzima, angepokea Roho ya Mungu. Angejifunza njia ya UPENDO—njia ya “kutoaâ€â€”badala ya njia ya “kupata.â€

Upendo Wafasiliwa

Paulo aliandika, “…kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho [Takatifu] tuliyopewa sisi†(Rum. 5:5).

Sasa fasili ya upendo ya Biblia ni nini?

Yohana aliandika, “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu [hapa inakuja fasili], KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE; wala amri Zake si nzito†(1 Yohana 5:3). Bado, wengi sana wanaodai kuwa na upendo wanaamini kwamba amri NI nzito. Mungu anasema si nzito. Anaiita Sheria Yake “takatifu, ya haki, njema na ya-rohoni†(Rum. 7:12, 14).

Paulo anafafanua kwamba amri na sheria ni kitu kimoja [sawa]: “Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi PENDO NDILO UTIMILIFU WA SHERIA†(Rum. 13:10). Biblia inafasili dhahiri pendo kama “utimilifu wa sheria.†Kushika amri ni kutimiza sheria—na huku “HAKUMFANYII JIRANI NENO BAYAâ€

Biblia inaongea juu ya “Roho Takatifu, [ambayo] Mungu amewapa wale WANAOMTII†(Matendo 5:32). Wakristo wa kweli hutii Sheria ya Mungu ya rohoni. Yesu hakufundisha kamwe kwamba tunapaswa tu “kumwamini†ili kuokoka. Alipoulizwa ni kitu gani lazima mtu “afanye†ili kupata “uzima wa mileleâ€â€”KUOKOKA—Kristo hakusema, Wewe niamini Mimi tu.†Alisema, “Kama ukitaka kuingia katika uzima, “ZISHIKE AMRI†(Mat. 19:17).

Inawezekana kumtii Mungu. Ulimwengu hupingana na hili au haulijui kwa sababu watumishi wake na wanateolojia huwaambia haiwezekani, au kwamba Kristo alitii kwa ajili yao. Bado, “Pendo ni utimilifu wa SHERIA.†Warumi 8:6 inasema, “Kwa kuwa nia ya mwili [ya asili] [uadui kwa Sheria ya Mungu] ni mauti; bali nia ya roho ni UZIMA na AMANI.

Fahamu! “Dhambi ni uvunjaji wa SHERIA†(1 Yohana 3:4), na “Mshahara wa dhambi ni mauti†(Rum. 6:23). Kuna sababu kwa kila athari.

Adamu alikabiliwa na uamuzi wa kuamini na kukubali maarifa kutoka kwa Mungu. Aliahidiwa uzima wa milele bure. Kula matunda ya Mti wa Uzima kungemfanya Mungu atunge maisha mapya ndani yake—kwa njia ya Roho Takatifu. Kama angepokea Roho ya Mungu, angekuwa na uzima ukibubujika ndani yake. Angeishi njia ya “upendo,†ambayo huja kwa kupokea Roho Takatifu. Angekuwa ameijua njia ya amani, furaha, wingi na ustawi.

Adamu angepewa nafasi kukifikia kiasi kikubwa cha maarifa yaliyofunuliwa ambayo asingeweza kuyagundua yeye mwenyewe. Angekuwa amefundishwa tofauti kati ya maadili ya kweli na ya uongo. Angekuwa ameelewa mwanzo wa ulimwengu, pamoja na maarifa mengi ya kiroho yaliyo muhimu—ikiwa ni pamoja na kusudi la maisha yake. Asingehitaji kuendelea kufanya majaribio, kutoa nadharia na kubahatisha kuhusu kipi ni chema na kipi ni kibaya na kwa nini mambo yako vile yalivyo—ambavyo wakati wote vimeishia kukanganywa na utafiti wake.

Kamwe asingefanya jaribio kipumbavu ambalo liliishia na KIFO chake!

Aliumbwa Ili Apate Maarifa

Mungu aliwapa Adamu na Hawa “utawala†juu ya dunia (Mwa. 1:26). Hii ilimaanisha kwamba mwanadamu angeweza na angehitaji kujifunza na kutengeneza—kuzalisha—maarifa mengi sana kadri ambavyo angeitiisha sayari.

Mungu aliwasanifu wanadamu wenye akili ambazo zingeweza kuumba, kubuni, kufikiri, kuchunguza na kufanya majaribio. Kupitia uwezo huu wa kufikiri ulio ndani yake, maarifa ya asili yanaweza kuchakatwa. Jambo hili lilikuwa jema na sahihi, kadri ambavyo lingetumiwa katika mfumo ambao Mungu aliukusudia.

Tatizo la Adamu na Hawa lilikuwa kwamba walifikiri kila aina ya maarifa ya lazima kwa ajili ya wokovu wangeweza kuyapata wao wenyewe, kwa kufanya majaribio. Walipoenda-kombo tu kutoka kwa NJIA ambayo Mungu aliikusudia, hawakuwa na tumaini la kufikia kikomo-safari ambacho alikuwa amekikusudia kwa ajili yao—na wala mwanadamu, aliyefuata uchaguzi wao. Wakati uleule Adamu na Hawa walipokubali kauli isiyo sahihi kama MAHALI PAO PA KUANZIA—kwamba wanaweza kufikiri kila kitu wao wenyewe—mwisho wao ulikuwa kushindwa!

Mrundikano wa kiasi kikubwa cha maarifa, kwa kipindi cha zaidi ya miaka 6,000, hakujabadilisha—na kamwe hakutaweza kubadili—ukweli kwamba mwanadamu anauendea mwisho mbaya.

Maarifa Yaliyofunuliwa

Kila aina ya kifaa cha kisasa au cha kitaalamu huja na kitabu cha mwongozo [wa namna ya kukitumia]. Bila hicho, mmiliki angeona kwamba kifaa hakina matumizi yoyote. Hangeweza kujua namna ya kukitumia kwa usahihi. Wala hangeweza kukikarabati [ripea] au kukiweka katika hali nzuri wakati wote.

Kwa kurudia, Mungu alitoa Kitabu cha Mwongozo—Biblia—ambayo ina maarifa nyeti YALIYOFUNULIWA. Inafafanua jinsi ya kuishi, si tu jinsi ya kupata kipato. Inafafanua historia, unabii, maarifa muhimu ya mafundisho ya imani na maelfu ya pointi zingine na kanuni zinazotawala kila nyanja ya maisha.

Sasa fahamu. Biblia haikukusudiwa kubeba maarifa YOTE, ni yale tu yaliyo muhimu kwa ajili ya wokovu—maarifa ambayo mwanadamu hangeweza kuyagundua kwa akili za kibinadamu, ufanyaji wa majaribio, uchambuzi na uchunguzi. Biblia haikukusudiwa kumfundisha mwanadamu jinsi ya kusanifu maajabu ya uhandisi, darubini ambazo zinaweza kuchunguza pembezoni mwa ulimwengu au kompyuta ambazo zinaweza kukokotoa matrilioni ya mahesabu kwa sekunde.

Wanadamu walipewa uwezo wa kufikiri na kusanifu haya na mavumbuzi mengine mengi ya kitaalamu ambayo ni vigumu kuyaeleza. Elimu katika maarifa ya asili ni muhimu.

Hii hapa ndiyo sababu. Idadi kubwa ya watu duniani wanaishi katika umaskini mkubwa, magonjwa, uchafu, udhalili na ujinga. Wamekosa elimu iliyo ya msingi kabisa ambayo mataifa yaliyoendelea “yenye mali†yanaifurahia. Kwa hiyo, elimu ya msingi inaweza kupelekea uboreshaji wa hali ya nje ya maisha na maendeleo kwa ustaarabu.

Lakini kwa hakika miaka 6,000 ya shida, huzuni na kila aina ya uovu unaoweza kufikiriwa, mabaya na ole ambavyo mwanadamu amevipitia vinapaswa kuuambia ulimwengu kwamba ni lazima usikize kwa uangalifu Kitabu cha Mwongozo wa maarifa ya kiroho yaliyofunuliwa uliyoyapuuza. Bado, mwanadamu anaendelea kukataa UFUNUO WA KIROHO wa Mungu.

Hata hivyo, akiwa amekatwa kutoka mkondo na njia sahihi ya sababu na athari inayofahamika kwa namna ya kiroho na sheria ya Mungu iliyofunuliwa, mwanadamu bado ana nguvu za mwili, akili za kibinadamu, ambazo, kwa masikitiko, zimeelekea kwenye silaha za maangamizi na ughaidi, ukatili, utumwa, ugandamizaji, uchafuzi wa mazingira, jinai, mkanganyiko wa kidini na mengine mengi zaidi.

Hivyo, taabu na huzuni za mwanadamu huzidi kuwa ngumu na kuongezeka kila kukicha.

Lakini kumbuka, mchakato wa Mungu wa UUMBAJI WA KIROHO bado unaendelea. Haujakamilika!

Zao la Kazi ya Mikono ya Mungu

Hebu tuendelee kuchunguza picha kubwa ya KUSUDI la Mungu.

Wewe si wa kwanza kushughulishwa na Mpango mzima wa Mungu—au kushangaa kwa nini unaishi. Ayubu aliuliza swali hili hili: “Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena?†(14:14).

Mungu alimvuvia kujibu swali lake mwenyewe: “Mimi nitangoja siku zote za muda wangu ulioamuliwa, hata badiliko langu linifikilie. Wewe utaniita, nami nitakujibu; Utakuwa na tamaa kwa kazi ya mikono yako†(fu. 14-15).

Ayubu alikiri kwamba alikuwa “KAZI ya mikono ya Mungu.†Alijua Mungu “alitamani†kusudi fulani ambalo lilihusisha mchakato uliokuwa ukitenda kazi ndani yake. Alijua kwamba siku moja Mungu “atamwita†kutoka kaburini, na kwamba “atamjibu,†hivyo kutimiza kusudi lake.

Haya ni maarifa muhimu ambayo yangeweza kufunuliwa na Mungu pekee. Bila hivyo Ayubu asingeyajua.

Mungu yuko kazini ndani ya wale ambao Amewaita. Ana-unda, finyanga na kujenga tabia takatifu, ya haki ndani yao—tabia Yake hasa. Angalia: “Lakini sasa, Ee BWANA, wewe u Baba yetu; sisi tu UDONGO, nawe U MFINYANZI wetu; sisi sote tu KAZI YA MIKONO YAKO†(Isa. 64:8).

Cha kusikitisha, wengi hawatamruhusu Mungu kutenda kazi pamoja nao. Wanapinga KUSUDI Lake. Wanadhani wanajua vizuri kuliko Mungu aliyewaumba. Wengi wanakataa kuambiwa nini cha kufanya na kuwa udongo katika mikono ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa tatizo la Adamu.

Isaya pia aliandika, “Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie Yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au KAZI Yako, Hana [Mungu] mikono?†(45:9).

Watu wengi hawana habari kabisa kwamba Mungu anatenda kazi ndani ya wanadamu Aliowaita—au nini Anachokifanya wakati anapowaita. Tena, haya ni maarifa yaliyofunuliwa kiroho, yasiyoweza kufikiwa na wale ambao Mungu hajawaita kuelewa ukweli Wake (Yohana 6:44, 65; 17:17).

Mungu anatenda kazi sasa ndani ya fikira za wale wachache tu walio na Roho Yake Takatifu ndani yao (Matendo 2:38). Wanadamu hawazaliwi wakiwa na tabia ya Mungu. Na Mungu hawezi kuiingiza ndani yao mara moja kwa uwezo wa kiungu. Tabia ni lazima ikuzwe.

Mkristo halisi huongezeka katika ufahamu na “[hu]kua katika neema, na maarifa†(2 Pet. 3:18). Maisha yake yote huvumilia ili kushinda, kwa sababu yuko mafunzoni kwa ajili ya kusudi kuu. Wale walioitwa wanafahamu kwamba “…mwenye KUVUMILIA mpaka mwisho, ndiye ATAKAYEOKOKA†(Math. 24:13). Ili kufahamu mchakato huu, soma makala yetu ya bure “Unaweza Kushinda na Kuzuia Dhambiâ€.)

Kujifunza Biblia na kuomba kwa bidii ni sehemu ya ratiba ya Mkristo ya kila siku. Yule aliyeitwa ameipata “lulu ya thamani kuu†na amedhamiria kujenga TABIA YA KIROHO na HULKA ya Mungu. Ingawa hakuna lolote kati ya haya litamchumia wokovu, ni kiini cha tabia yake ambacho huamua thawabu yake.

Paulo alielewa jinsi Mungu anavyotenda kazi ndani ya Wakristo. Alitambua kwamba wokovu (Rum. 6:23), na hata imani ya kuupokea, ni karama za bure. Haziwezi kuchumwa. Lakini hii haimaanishi kwamba Mungu hatendi kazi sasa (akitaka matendo mema) ndani ya wanadamu, kadri ANAVYOZALIANA YEYE MWENYEWE.

Fikiria: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. MAANA TU KAZI YAKE, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende MATENDO MEMA, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili TUENENDE NAYO†(Efe. 2:8-10).

Je! Uliupata usemi ambao Paulo aliutumia—“tu kazi Yake� Kipi chaweza kuwa dhahiri? Mungu ana kusudi linalotenda kazi ndani ya kila mtu!

Fungu liliendelea kwa kusema kwamba Wakristo lazima “waenende†katika “matendo mema.†Wazo potofu la “kuamini tu katika Yesu†hupinga Kusudi Kuu la Mungu la kuwafinyanga watu kupitia KAZI YA MIKONO YAKE ya uangalifu, kama alivyo mfinyanzi na udongo.

Ingawa wokovu ni kwa “neema…kwa njia ya imani,†huhusisha matendo mema. Hii humaanisha kwamba wokovu ni mchakato na si kitu kinachotokea mara moja pale “unapotoa moyo wako kwa Yesu.â€

Angalia kitu gani kingine Paulo aliandika kuhusu mchakato huu unaoendelea ndani ya wale ambao Mungu anawaita: “na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae UTU MPYA, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli†(Efe. 4:23-24). 2 Wakorintho 5:17 huliweka jambo hili namna hii: “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya...â€

Wale ambao Mungu anatenda kazi pamoja nao ni VIUMBE VIPYA halisi!

Yule anayemtumikia Mungu huwa anaendelea kubadilishwa katika nia yake. Anasalimisha mapenzi yake mwenyewe na anatafuta kubadilishana na mapenzi ya Mungu katika mambo yote. Anatafuta kumpendeza Mungu—si nafsi yake mwenyewe!

Tumezaliwa Ili Tujenge Tabia

Kila mtu ambaye Mungu anamwita hupewa uchaguzi ule ule ambao Adamu na Hawa walikabiliana nao—kujisalimisha kwa Mungu na serikali Yake au kujisalimisha kwa Shetani na hulka yake.

Mungu ni Baba. Ana Mwana mmoja aliyefanyika kwa Roho, lakini baadaye atakuwa na wana wengi zaidi (Rum. 8:19). Anazaliana Mwenyewe kwa kujenga tabia Yake ndani ya wanadamu wanaojisalimisha, waliotwaliwa, waliotungwa kwa Roho. Kama vile baba wa kibinadamu wanavyotunga watoto wao kimwili, kadhalika Mungu hutunga watoto Wake kiroho.

Kama ilivyo kwa watoto kukua na kufanana na wazazi wao wa kimwili, kadhalika pia wana wa Mungu kwa utaratibu huchukua mfanano wa kiroho wa Mzazi wao, katika tabia takatifu, ya haki—“tabia ya uungu†(2 Pet. 1:4). Petro aliwaelezea Wakristo kama “washiriki wa TABIA YA UUNGUâ€â€”asili ya Mungu. Iko asili ya kimwili ya uumbaji, hulka ya mwanadamu na HULKA YA MUNGU. Mungu anaitengeneza upya, tabia ya mwanadamu ya kimwili iliyoharibika iwe TABIA YA KIROHO ya ajabu, tukufu, takatifu—TABIA Yake ya UUNGU!

Tabia ni kufahamu—kujua—kutofautisha jema na baya na kutenda lililo jema badala ya lililo baya! Mungu hufunua lililo jema, lakini ni kupitia kwa nguvu ya uhuru wa maamuzi, kuchagua KUTENDA lililo jema, ndivyo tabia ya haki inajengwa.

Tabia ni kuchagua njia iliyo sahihi kwa kujua, dhidi ya upinzani. Siyo ile njia rahisi. Ni kuogelea dhidi ya mkondo, badala ya kuserereka kizembe katika welekeo wake. Ni kujenga upendo, furaha, amani, uvumilivu, fadhili, utu wema, imani, upole, kiasi (kujizuia), hekima, maarifa, ufahamu na unyenyekevu. Jambo hili huchukua muda, kwa sababu tabia hujengwa kupitia uzoefu.

Wanyama hawajengi tabia yoyote kati ya hizi.

Mungu ana tabia kamilifu katika nyanja zote. Yeye ni pendo. Kumbuka, pendo ni utimilifu wa sheria (Rum. 13:10; 1 Yohana 5:3), ambao unahitaji mtu kujisalimisha kwa Mungu. Ni wa-kutoka, kushughulika kwa ajili ya wengine, kuwatanguliza—mbele ya matakwa binafsi.

Hulka ya Shetani ni ubinafsi, unaoingia na kujali tu na kile kilicho bora kwa ajili ya nafsi na namna ya kupata zaidi kwa ajili ya nafsi. Huu ndio mtazamo alioupenyeza ndani ya Adamu na Hawa pale walipokula matunda ya mti uliokatazwa.

Je! Unaona kwamba, ingawa Mungu alimuumba mwanadamu kimwili katika umbo na sura yake Mwenyewe, haiishii pale?

Uliumbwa ili uwe kama Mungu—kujenga tabia kamilifu, takatifu, ya haki. Mungu anazaliana Mwenyewe ndani ya wanadamu. Kama vile ulivyo mtoto wa wazazi, na huenda una watoto wako mwenyewe, Mungu ni Mzazi wako. Tena, kama vile unavyofanana na wazazi wako kimwili, na watoto wako wanafanana na wewe, Mungu anataka ufanane na Yeye—katika tabia ya kiroho! Katika maisha haya, Mungu huanza kuwatengeneza na kuwaunda upya kwa namna ya roho wale Anaowaita. Kusudi Lake ni kujenga asili Yake ndani yao.

Hivyo basi, Mungu anazaliana Mwenyewe ndani ya wale ambao wamepokea RohoYake Takatifu. Anaumba watoto ambao wataonekana na KUWA kama vile Yeye alivyo! Kujenga tabia ya Mungu hasa ndio sababu unaishi! Lakini yako zaidi ya kufahamu.

Mungu ametenga miaka 7,000—siku millennia saba—kutekeleza Mpango Wake “hapa chini.†Tunakaribia mwisho wa siku ya sita (miaka 6,000) aliyotengewa mwanadamu chini ya Shetani. Kristo atarejea hivi karibuni kusimamisha serikali ya Mungu na sheria kamilifu ya kiroho duniani. Shetani atafungwa (Ufu. 20:2) asiweze tena kuuvuta [kuushawishi] ulimwengu huu kwenye uovu na uasi dhidi ya maarifa ya Mungu yaliyofunuliwa.

Wachache watamkataa Mungu, wasikubali kumtii. Wataamini fikra zao za kibinadamu na kukataa kiunganishi kinachokosekana cha Roho ya Mungu, ambacho kingewaongoza kwenye uzima wa milele. Watakataa kujenga haki katika maisha yao na kuchagua kubaki wapungufu—wasiokamilika katika kusudi na tabia.

Lakini Haki ya Nani?

Ni muhimu mno—nyeti kabisa!—kufahamu kwamba Wakristo hukua tu wakiwa wameunganishwa kwa Kristo.

Mara nyingi Biblia inaongelea juu ya “Kristo ndani yetu†(Gal. 2:20; 4:19; Kol. 1:27; Efe.3:17; 2 Kor. 13:5). Sisi hatufanyi kazi za kujenga tabia. Yesu Kristo aliye kazini ndani yetu huzitenda. Elewa. Baba huongoza mchakato huu kadri kila mtu anavyobaki ameunganishwa na Yeye kwa njia ya Roho ya Kristo (na Mungu) ndani yake.

Liweke jambo hili wazi. Si kitu chochote, ambacho unafanya, wewe na kwa juhudi zako mwenyewe, ambacho huzalisha matendo ya haki. Warumi 10 inaonya dhidi ya wale wasiofahamu jukumu la Mungu katika kuijenga tabia, matendo mema na haki: “Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya MUNGU, na wakitaka kuithibitisha haki yao WENYEWE, hawakujitia chini ya haki ya Mungu†(fu. 3).

Ni kupoteza nguvu bure kujenga tabia yako mwenyewe, matendo yako mwenyewe ya haki. Hayakupi chochote kutoka kwa Mungu. Ukuaji wote wa kiroho unatoka Kwake! Lakini lazima ufanye sehemu yako katika kujisalimisha kwa Mungu.

Paulo aliandika, “Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni SHAMBA LA MUNGU, ni JENGO LA MUNGU†(1Kor. 3:9). Huu ni ufahamu wa kipekee. Mungu anajenga Familia. Yeye ni Mkulima. Wakristo wa kweli ni zao la “ukulima†Wake—“kazi ya mikono†Yake.

MUNGU, si mwanadamu yeyote, anajenga Kanisa Lake. Kristo alisema, katika Mathayo 16:18, “Nitalijenga Kanisa Langu.†Si ajabu Paulo aliandika, “ninyi ni jengo la Mungu.†Ndiyo, Mungu anajenga kitu maalumu ndani ya wale Anaowaita, sawa sawa kama Anavyojenga Kanisa Lake kwa ujumla.

Bila shaka, kila jengo imara lina msingi mzuri. Unalisaidia libaki imara. Katika 1 Wakorintho 3:11, Paulo anaongeza, “Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.†Maisha yako lazima yawe yamejengwa kwenye msingi imara, wa KRISTO wakati wote—na Yeye akitenda kazi ndani yako!

Lazima Uzaliwe “Mara ya Piliâ€

Wengi wanaodai kuwa Wakristo wanaamini kwamba “wamezaliwa mara ya pili†katika maisha haya. Kila wakati, wanaamini hili hufuata baada ya “kumpokea Yesu.†Hiki sicho kile Biblia inachofundisha.

Paulo alisema kwamba “…nyama na damu haziwezi KUURITHI ufalme wa Mungu; wala uharibifu KURITHI kutokuharibika. Angalieni, nawaambia ninyi siri†(1 Kor. 15:50-51). Hakika maarifa haya ni siri kwa wengi.

Mfululizo wa mafungu katika Yohana 3 kwa kawaida unaeleweka isivyo na watu wanaoamini kwamba wanaweza “kuzaliwa mara ya pili†katika maisha haya na “kuuona†ufalme wa Mungu, wakati wakiwa bado wamefanyizwa kwa nyama na damu.

Katika maelezo haya, Nikodemo alimuuliza Kristo, ambaye alijibu, “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu†(fu.3). Kisha, katika fungu la 6, Aliongeza, “Kilichozaliwa kwa mwili NI mwili; na kilichozaliwa kwa Roho NI roho.â€

Nyama na damu haziwezi kuuingia ufalme wa Mungu—lakini roho inaweza! Kwa sababu Kristo hakutaka kuacha mwanya wa kutoelewa isivyo, Aliifananisha roho na upepo. Kama ulivyo upepo, roho haionekani. Haiwezi kuonekana. Ni katika ufufuo tu Wakristo wote wa kweli wanabadilishwa kutoka nyama kuwa roho—KUZALIWA MARA YA PILI! (Ili kufahamu kwa undani kweli za mafundisho haya muhimu, soma kwa makini vijitabu vyetu “Kuzaliwa Mara Ya Pili†Kunamaanisha nini? na Ufalme Wa Mungu Ni Nini?).

Kile Utakachofanana Nacho

Kumbuka kwamba Mungu aliwaumba wanadamu katika “sura†na “mfano†Wake. Lakini mchakato huu hautakamilika hadi Ufufuo, wakati ambapo hatutakuwa tumefanyizwa tena kwa “nyama na damu.â€

Mungu alikuumba wewe ili uwe “kama†Yeye katika kila namna. Maisha mapya ya roho yanatungwa, kupitia Roho Takatifu inayoziingia fikra za kila mtoto Wake mpya anayeongoka. Kiinitete kidogo, kilichotungwa kwa roho kinakuja kuwepo. Acha nirudie: Kwa namna ile ile ambayo watoto hukua na kufanana na wazazi wao wa kimwili, vivyo hivyo watoto wa Mungu taratibu huchukua MFANANO WA KIROHO wa Mungu (Mzazi wao), katika asili na tabia, kama ilivyo katika sura na umbo (2 Pet. 1:4).

Maagano yote mawili la Kale na Jipya huweka jambo hili dhahiri kabisa! Wakati wengi wana wazo lisilo wazi kwamba Wakristo wanaweza kuwa “wana wa Mungu,†hakuna anayezingatia hili: “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe WANA WA MUNGU...Wapenzi, sasa tu WANA WA MUNGU, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, TUTAFANANA NAYE; kwa maana tutamwona kama Alivyo†(1 Yohana 3:1-2).

Kisha Yohana anaongeza, “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu†(fu. 9). Siku moja tutakuwa na mfanano halisi wa Kristo. Wakati huo, tutakuwa tumezaliwa kutokana na Mungu. Warumi 8:16 inasema kwamba tu “watoto†wa Mungu na warithi pamoja na Kristo.

Daudi aliielewa pointi hii miaka elfu moja kabla: “Bali mimi nitautazama uso wako katika haki: Nitashibishwa, NITAKAPOAMKA na SURA Yako†(Zab. 17:15).

Daudi na Yohana walifahamu kwamba, kama Ayubu, “wataamka†wakati wa ufufuo na kuonekana kama Mungu alivyo hasa, katika sura, umbo na tabia—na wakiwa wamefanyizwa kwa roho!

Hivyo basi—hebu nirudie hili—Mungu anazaliana Mwenyewe ndani ya wanadamu waliopokea Roho Yake. Anaumba watoto watakaoonekana na kuwa kama vile Yeye alivyo!

Paulo anakuza kile ambacho Yohana na Daudi walirejelea wakati waliposema kwamba Wakristo watakuwa “kama Yeyeâ€â€”na katika “mfano†Wake. Angalia: “Kwa maana sisi, wenyeji [uraia] wetu uko mbinguni; kutoka huko [Anakuja hapa] tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate KUFANANA NA MWILI WAKE WA UTUKUFU, kwa uweza ule ambao kwa huo Aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini Yake†(Filp. 3:20-21).

Haya ni maarifa yanayostaajabisha. Hakuna kinachoweza kulinganishwa nayo! Lakini hebu tulifanye jambo hili hata wazi zaidi.

Yafuatayo ni maelezo ya moja kwa moja ya Yesu Kristo, kama Alivyo sasa katika utukufu kamili. Yatafakari, ukitambua kuwa utafanana—na kuwa—kama Yeye: “Kichwa Chake na nywele Zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho Yake kama mwali wa moto; na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi. Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake†(Ufu. 1:14-16).

Kile ambacho maelezo haya ya kushangaza yanafunua kuhusu mustakabali wako siyo mawazo yangu. Ni kile ambacho Biblia yako inafunua! Hiki ndicho Paulo alimaanisha wakati alipoandika, “Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni†(1 Kor. 15:49). Japokuwa tumefanywa na tuko na umbo la Mungu kimwili sasa, baadaye tutakuwa Roho, na kuichukua “SURA yake Yeye aliye wa MBINGUNI.â€

Elewa hili. Roho ile ya Mungu iliyo ndani yetu itaturuhusu kuamka katika ufufuo. Angalia Warumi 8:11: “Lakini, ikiwa Roho yake Yeye aliyemfufua Yesu katika wafu inakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, KWA Roho Yake inayokaa ndani yenu†(pia 1 Kor. 15 na 1 Thes. 4:13-18). Kristo aliinuliwa (alifufuliwa) ili kurudi kwenye nafasi Yake kando ya Baba. Alikuwa ametimiza jukumu Lake la kuwa Mwokozi.

Sasa, elewa pointi hii! Ni Roho ile ile, inayokaa ndani yetu toka wakati wa kutungwa, itakayotufufua (wale wote waliotungwa na Mungu) kuungana na Mungu katika ufalme Wake.

Kama vile kitoto kipya-kilichotungwa kinavyokua ndani ya tumbo la mama yake, lazima pia Mkristo akue kabla hajatoka tumboni. Wakristo wanapaswa kukua katika kipindi cha maisha haya. Ili waweze kupewa nguvu za uungu na mamlaka, kama “warithi pamoja na Kristo†(Rum. 8:17) BAADAYE, ni lazima wafuzu, kupitia kujenga tabia ya Mungu iliyo takatifu, ya haki katika maisha yao SASA!

Mustakabali Wako Wa Kustaajabisha

Kitabu cha Waebrania kinafunua kusudi la Mungu la kustaajabisha kwa uwazi mwangavu kabisa. Muktadha unaanza katika Sura ya 1. Tazama picha ya kile ambacho mustakabali wako wa kustaajabisha unaweza kuwa ikifunguka.

Kwanza, elewa kwamba Mungu aliumba malaika ili wawe “roho watumikao†kuwasaidia “WARITHI wa wokovu†(fu. 14). Hili ndilo jukumu lao katika Mpango wa Mungu. Malaika hawajaahidiwa umemba katika Familia ya Mungu. Hii ndiyo sababu Shetani (kama malaika aliyeanguka) anachukia sana wazo kwamba mwanadamu mdogo, wa nyama anaweza kupokea kile ambacho yeye kamwe hakuahidiwa wala hawezi kukitimiza.

Paulo ananukuu sehemu mbili kutoka katika Zaburi: “Kwa maana Alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake Baba, Na yeye atakuwa Kwangu Mwana?†(Ebr. 1:5). (Waebrania 2:5 inaelezea dunia ikiwa chini ya “utawala wa malaika†sasa, lakini inaweka wazi kwamba malaika hawa hawatatawala juu ya “ulimwengu ujao.â€)

Mungu hajawahi kusema mambo haya kwa malaika yeyote!

Kisha Paulo ananukuu kutoka Zaburi nyingine, akifafanua kile ambacho kimekuwa Kusudi la Mungu wakati wote: “KITI Chako CHA ENZI, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya UFALME Wako ni fimbo ya adili...†(1:8). Fimbo ni bakora au mkongojo unaotumika kama nembo ya utawala au mamlaka—na katika ufalme Wake Mungu ndiye mwenye nguvu zote.

Hatimaye, Paulo analigeuza swali lile lile kuhusu malaika: “Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono Wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui Zako chini ya nyayo Zako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale WATAKAOURITHI wokovu?†(1:13-14).

Hii inaweka jukwaa kwa ajili ya kile ambacho lazima tukifahamu! Hebu tuelewe kabisa mustakabali wa kustaajabisha ambao Mungu ameandaa kwa ajili ya wale wanaomtumikia.

Mfululizo huu wa mafungu ya kushangaza unaendelea katika sura ya 2—na unajenga katika ufahamu na matokeo yake. Paulo ananukuu Zaburi 8:4-6. Hapo Daudi aliuliza swali kuu kuliko yote, “Mwanadamu ni nini hata umkumbuke?†(Ebr. 2:6). Kwa kuwa Mungu ni wa Milele, na anaketi juu ya ulimwengu wote na nguvu zote ziko chini ya utawala Wake, si ajabu Daudi aliuliza, na Paulo akarudia, swali hili.

Jibu la kushangaza liko katika fungu linalofuata: “Umemfanya [mwanadamu] mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za Mikono Yako.â€

Paulo anafafanua zaidi kwamba Mungu anapanga kutoa nguvu nyingi na mamlaka kwa Wana Wake: “Umeweka VITU VYOTE chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu VYOTE chini yake HAKUSAZA KITU kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona VITU VYOTE kutiwa chini yake†(fu. 8). Hili halijatokea bado—lakini litatokea hivi karibuni, wakati wa Kurudi kwa Kristo.

Mungu anaposema kwamba “vitu vyote†vitawekwa chini ya miguu ya mwanadamu, hiki ndicho Anachomaanisha. Ulimwengu mpana, pamoja na makwadrilioni ya nyota na trilioni moja ya galaksi, utawekwa chini ya mamlaka ya wanadamu waliozaliwa katika Familia ya Mungu. Kwa hakika, tafsiri ya Biblia ya Moffatt inalitafsiri neno la Kigiriki “vitu vyote†kama “ulimwengu.â€

Haya ni maarifa ya kuduwaza!—ya ajabu kupita maelezo! Tumia muda kuyaelewa hakika. Furahia kile kinachoweza kuwa mustakabali wako. Ndiyo sababu unaishi—yanafafanua kwa nini ulizaliwa!

Kabla ya kuendelea, zingatia fungu la kustaajabisha kuhusu kipengele kingine kinachohusiana na wokovu ambacho kinaeleweka kwa wachache. Tumeona kwamba Wakristo hakika wanangoja wokovu wa kustaajabisha. Lakini, uumbaji wote nao unangoja kwa shauku kuu kuonekana kwa hao wana wote wapya watakaoongezwa katika Familia ya Mungu.

Soma kwa uangalifu aya ifuatayo: “Kwa maana uumbaji unatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu; kwa maana uumbaji [vitu vyote katika ulimwengu unaojulikana] pia ulitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake Yeye aliyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa uumbaji wenyewe nao utawekwa huru kutoka katika utumwa wake wa uharibifu, na kupata uhuru wa utukufu wa WATOTO WA MUNGU. Twajua ya kuwa uumbaji wote [kila kitu] pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. Wala si huo tu; ila na sisi wenyewe [Wakristo] tulio na malimbuko ya Roho [WACHACHE wanaoitwa sasa], sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia [kuzaliwa] kufanywa WANA†(Rum. 8:19-23, RSV).

“Watoto wote wa Mungu†wa wakati ujao—WANA—watakuwa wakombozi wa uumbaji ambao sasa uko utumwani. Hii ni sehemu ya mwito wako. Dunia, mwezi na nyota vilivyojeruhiwa na kuharibiwa hivi karibuni vitafanywa upya na kurudishwa katika hali ya uzuri, umoja na utulivu chini ya uongozi wa Kristo na wototo wengine wa Mungu.

Wana Wengi

Sasa tunaweza kuendelea na maelezo yaliyo ya muhimu sana katika Waebrania 2: “ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu Aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. Kwa kuwa ilimpasa Yeye, ambaye kwa ajili Yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta WANA WENGI WAUFIKILIE UTUKUFU, kumkamilisha Kiongozi Mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso†(fu. 9-10).

Je! ulipata kile kilichosemwa? Unakielewa? Mafungu haya yana ahadi ya mustakabali wa kuduwaza uliopo kwa ajili ya wanadamu. Wale wanaoitwa katika zama hii watarithi “vitu vyote†na “kuvikwa utukufu na heshima†kwa njia ya dhabihu ya Yesu Kristo—“Kiongozi Mkuu wa wokovu wao.â€

Mafungu haya yanafunua uwezekano wa kustaajabisha uliokusudiwa kwa ajili ya Wakristo wote. Paulo anafunua kwamba, wakati Kristo atakaporudi, “WANA WENGI†wataufikilia “utukufu,†kupitia kwa kazi ya “Kiongozi Mkuu wa wokovu wetu†(Ebr. 2:10).

Biblia inafunua mwunganisho kati ya wana na warithi. Mrithi hajarithi bado kile kitakachomwangukia. Tunasoma, katika 1 Wakorintho 15:50, kwamba “TUTARITHI ufalme wa Mungu.†Lakini wale wanaoitwa sasa, katika wakati wa maisha haya, ni WARITHI—wana waliotungwa (hawajazaliwa bado). Paulo anafafanua zaidi, “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na WARITHI sawasawa na ahadi...Hivyo wewe si mtumwa tena bali u MWANA; na kama u mwana, basi, u MRITHI kwa Mungu kwa njia ya Kristo†(Gal. 3:29; 4:7).

Mungu atashiriki utawala juu ya uumbaji Wake wote pamoja na Wana Wake wote. Kristo ni wa kwanza tu miongoni mwa wengi. Angalia: “Maana wale Aliowajua tangu asili, Aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana Wake, ili Yeye awe MZALIWA WA KWANZA MIONGONI MWA NDUGU WENGI†(Rum. 8:29).

Kuzaliwa kwa mtoto wa kiume wa kwanza hakufungii kuzaliwa kwa watoto wengine wakiume (na wakike) kwa familia hiyo hiyo. Ninao watoto wawili wa kiume na mimi ni mtoto wa kwanza wa kiume pamoja na mdogo wangu wa kiume. Baba yangu alikuwa mtoto wa kiume wa pili, akiwa na kaka yake nakadhalika. Unaiona pointi.

Tukiendelea katika Waebrania 2, angalia kwamba Kristo “…haoni haya kuwaita ndugu zake [wale wana wengine wengi—sisi]†(fu. 11). Kwa hakika, Mkristo aliyetungwa ameitwa kwenye “utukufu†na kuwa mmoja wa “wana wengi.†Mateso ya Kristo na dhabihu vinamwezesha kuwa “Kiongozi Mkuu wa wokovu waoâ€â€”na anaweza kuwa wako.

Ni mustakabali wa ajabu kiasi gani kwa ajili ya wale ambao Yesu Kristo “anawaita…ndugu zake.†Angalia tena: “Maana yeye atakasaye [Kristo] na hao wanaotakaswa [Wakristo waliotungwa] wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu Zake†(fu. 11). Hakutakuwa na tofauti kati ya Kristo na ndugu Zake wadogo wakiume na wakike, isipokuwa kwamba atakuwa na mamlaka makubwa kiujumla ndani ya ufalme wa Mungu.

Wakristo “wametakaswa†(tengwa kando). Jinsi gani? Yohana alisema, “Uwatakase [Wakristo waliotungwa] kwa kweli Yako: NENO LAKO NDIYO KWELI†(Yohana 17:17. Kijitabu hiki kimekufundisha UKWELI kuhusu kwa nini unaishi!

Desturi na hadithi za wanadamu zilizohifadhiwa kwa upendo mkubwa, kuhusu maisha baada ya kifo, au kuhusu kitu kingine chochote, havina thamani. Ukweli wa Biblia ndiyo maarifa pekee yenye thamani ya kudumu. Wakristo, wakiwa wametoka nje ya ulimwengu uliodanganywa, na kukanganywa, wametengwa kando kutoka ulimwenguni kwa ile KWELI.

Ikiwa Kristo “haoni haya kuwaita wao (sisi) ndugu Zake,†basi sisi, wana wa Mungu waliotungwa, lazima tusione haya kuutetea ukweli wenyewe unaotutakasa—na ukweli wa injili (Fil. 1:17). Lazima “tukue†katika Kristo (Efe. 4:13) na kuyashika mafundisho ya kweli ya Mungu. Lazima TUFUZU kusimama kando ya Kristo juu ya “vitu vyote.â€

Je! Unakiona kilichoelezewa hapa? Lengo la Mkristo ni kuzaliwa katika UFALME WA MUNGU—kuwa kiumbe roho asiyepatikana na mauti atakayetawala chini ya Kristo. Kipi chaweza kuwa cha ajabu zaidi—cha UTUKUFU zaidi—kukitazamia?

Nafasi ya Mateso

Mapema, kijitabu hiki kiliongelea juu ya mateso ya kutisha, taabu na matatizo yasiyotatulika ya ulimwengu uliotengwa na Mungu. Rehema Zake zitafupisha hali hii hivi karibuni, na kuikomesha. Miaka 6,000 aliyotengewa mwanadamu chini ya Shetani itatimilika hivi karibuni, na wanadamu wote watafundishwa kwa nini walizaliwa.

Lakini kwa nini mateso ya kutisha kama hayo yamekuwa ni ya lazima—na kwa muda mrefu hivi? Yamesimamia kusudi gani katika Mpango Mkuu wa Mungu?

Zaidi! Tulisoma kwamba Kristo, kama “Kiongozi Mkuu wa wokovu wetu,†alifanywa “MKAMILIFU KWA NJIA YA MATESO.†Ni muhimu kufahamu kwa nini Kristo alipaswa kuteseka.

Waebrania 5:8-9 inafafanua kwa wazi: “Ingawa ni Mwana, ALIJIFUNZA KUTII kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtiiâ€

Ni fungu la muhimu kiasi gani kulielewa. Mateso huingiza mfumo wa kujifunza kwenye gia. Watu wanapoteseka, WANAJIFUNZA (Mhu. 7:14)! Wanapata uzoefu—wanajifunza masomo. Jambo hili ni nyeti kwenye mchakato wa kujenga tabia—ili kutimiza kusudi la kuwepo kwao!

Hata Kristo alijifunza kwa njia ya mateso. Jambo hili lilimwezesha “Kuongoza†wokovu wa wana wengi ambao Mungu atawaongeza kwenye Familia Yake.

Je! Unaweza kuelewa sasa kwa nini ulimwengu lazima uteseke? Je! Unaweza kufahamu sasa kwamba ni kupitia kwa njia ya uzoefu mgumu, wenye maumivu ndipo watu hatimaye watafahamu masomo mazito ya maisha?

Bila shaka, somo zito kuliko yote ambalo watu lazima watambue ni kwamba hawawezi kutimiza chochote—hawatafanikisha CHOCHOTE—bila Mungu. Wanahitaji mno MAARIFA YA KIROHO YALIYOFUNULIWA, ili waweze kupatana na Kusudi la Mungu la kustaajabisha la kuzaliana Mwenyewe!

Paulo aliwaandikia Wafilipi kwamba yeye (Paulo) alitaka kumjua Kristo “…na ushirika wa MATESO YAKE...ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu†(3:10-11). Hii ndiyo sababu aliwaambia Waefeso, “...kuwaangaza watu wote wajue habari za ushirika wa siri hiyo [ambayo inajumuisha hitaji la kuteseka ili kujifunza], ambayo tangu mwanzo wa ulimwengu ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote kwa Yesu Kristo; kwa kadiri ya KUSUDI la milele ALILOLIKUSUDIA katika Kristo Yesu Bwana wetu†(3:9, 11).

Mpango wa Mungu hakika ni siri kwa ulimwengu huu, lakini KUSUDI Lake halijabadilika tangu mwanzo wa ulimwengu.

Sasa unafahamu jinsi UNAVYOWEZA kuwa sehemu yake!

Kwa Nini Unaishi!

Aya zifuatazo ni jinsi ambavyo Herbert W. Armstrong alihitimisha kijitabu chake Kwa Nini Ulizaliwa? Vichwa vidogo ni vya kwake:

Sasa Fahamu Kwa Nini Ulizaliwa!

“Kusudi la maisha ni kwamba hakika Mungu anaumba upya jinsi Yake mwenyewe ndani yetu—akizaliana Mwenyewe kwa jinsi Yake—kwa kuwa, tunapoongoka halisi [kwa kweli], tunakuwa tumetungwa kama wana (hatujazaliwa bado) wa Mungu. Kisha kupitia kujifunza ufunuo wa Mungu katika Neno Lake, tukiishi kwa kila Neno Lake, tukiomba daima, kila siku tukipata uzoefu kwa majaribu na mitihani, tunakua kiroho zaidi na zaidi kama Mungu, mpaka, kufikia wakati wa ufufuo ghafla tutabadilishwa kutoka kufa hadi kutokufa—wenye kufanyizwa kwa Roho—hapo ndipo tutakuwa tumezaliwa na Mungu—tumezaliwa katika FAMILIA ya Mungu hakika!

“Kwa kuwa, kumbuka, neno ‘Mungu’ katika Mwanzo 1:1, linatujia kutoka neno la Kiebrania Elohim. Elohim maana yake ni MUNGU MMOJA—si miungu wengi. Lakini MUNGU huyo MMOJA ni FAMILIA ya Uungu—UFALME. Liko Kanisa la kweli moja tu—Kanisa moja, lakini washiriki wengi (1 Kor. 12:20).

“Ndivyo ilivyo kwa Mungu.

“Kama kielelezo, kuna ufalme wa madini, ufalme wa mimea, ufalme wa wanyama, ufalme wa wanadamu, katika ulimwengu huu wa vitu. Kwa namna ya roho, kuna ufalme wa malaika, na, juu ya wote, Ufalme wa Mungu. Mwanadamu wa nyama na damu—hawezi kuuingia Ufalme wa Mungu (Yohana 3:6; 1 Kor. 15:50), lakini yule aliyezaliwa na Mungu anaweza.

Uwezekano Wa Ajabu, Wa Kushangaza

“Je! unaelewa hakika? Kusudi la wewe kuwa hai ni kwamba hatimaye uzaliwe katika Ufalme wa Mungu, ambao ni FAMILIA takatifu ya Mungu.

“Wakati utakapoelewa kwa ukamilifu ukweli huu mkubwa, wa ajabu, fikra zako zitajawa na furaha na utukufu usio kifani. Unaleta maana mpya kwa maisha kwa namna ya ajabu ambayo kamwe hutaelewa vimo vya urefu kamili wa fahari yake.

“Bila shaka, inamaanisha, kukataa kabisa, kukana, vitu vyote vya hatari na njia ambazo kwa uongo zilionekana nzuri sana na zenye kuvutia kwenye ulimwengu huu.

“Lakini macho yako hatimaye yatafumbuliwa kwa udanganyifu mkuu—magamba yatadondoka kutoka uoni wako uliopofushwa—utaona maana ya maisha, kusudi lake kuu, kwa namna ambayo kamwe hukuwahi kuota kwamba ingeweza kuwa. Kuacha maovu ya ulimwengu huu, majaribu na mashimo—mitego na madanganyo yake ambavyo viling’aa na kisha vikaishia kwenye huzuni na mateso—inakuwa ni kuibuka kutoka katika giza nene kuingia kwenye fahari ya nuru ya kweli, na ya furaha na shangwe milele!

“Katika maneno ya 1 Petro 1:8, ‘utafurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye UTUKUFU’!â€

Pengine ungependa kusoma: