Jinsi Ufalme wa Mungu Utakavyokuja

Kisa Ambacho Hakijawahisimuliwa!

na David C. Pack

Mabilioni wanasubiri Kurudi kwa Yesu Kristo kusimamisha Ufalme wa Mungu. Lakini wachache wanajua jinsi gani Atafanya hivi. Jambo hili halitatokea namna ambavyo wengi wanatarajia. Kijitabu hiki kina kisa cha ajabu, ambacho-kamwe-hakijawahisimuliwa cha jinsi ambavyo Ufalme wa Mungu utakavyosimamishwa juu ya mataifa yote!

Fikiria ulimwengu wa leo! Maendeleo katika teknolojia na viwanda kamwe hayajawahi kuwa makubwa kama hivi. Kile ambacho kilikuwa riwaya za kisayansi sasa ni mambo halisi ya kila siku. Utajiri wa vitu umezidi kwa mamilioni ya watu katika ulimwengu wa Magharibi. Lakini vipi kuhusu nusu ya wanadamu—mabilioni!—ambao wana vichache au hawana kitu? Na vipi kuhusu kupungua kwa mwanadamu kwa haraka katika maadili, unyofu na TABIA—ambavyo zamani viliaminika kuwa nguzo za kila jamii? Je, mwanadamu anao uwezo, na je, viongozi wake kwa pamoja wana utashi wa kutatua changamoto kuu za ustaarabu—au nguvu kuu isiyoonekana lazima iingilie kati?

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusali, “Ufalme Wako uje!” Kitu kilichofuata Alichoagiza kilihusiana moja kwa moja: “Mapenzi Yako yatimizwe hapa duniani kama ilivyo mbinguni.” Mungu mwenye upendo ni lazima atume Ufalme Wake hivi KARIBUNI ili KUHITIMISHA jaribio la mwanadamu lililoshindwa la sivyo hakutakuwa na ulimwengu wa kuupokea!

Kurudi kwa Yesu Kristo—Kuja Kwake “Mara ya Pili”—ni kiini cha Ukristo. Mabilioni wanakungojea. Wenye kudhihaki wanakanusha. Lakini wale wanaojua kitu chochote cha Neno la Mungu wanajua Yesu anarudi. Kila kiashiria kinapendekeza kuwa Kuja Kwake hakuwezi kuwa mbali. Biblia inaongelea kwa upana juu ya jinsi ambavyo Yesu atasimamisha Ufalme wa Mungu, wakati mwingine ukiitwa Ufalme wa Mbinguni. Vitu vichache vingeweza kuwa vya muhimu zaidi. Yesu Mwenyewe alieleza kwa wazi jinsi Ufalme wa Mungu utakavyoanza—na siyo kile ambacho umejifunza. Kijitabu hiki kina maarifa ambayo kamwe hayakuwahi kufafanuliwa kabla! Na yanawakilisha sehemu ndogo tu ya uthibitisho wote wa Biblia katika Agano la Kale na Jipya juu ya jinsi Ufalme wa Mungu utakavyowasili katika namna ambayo hakuna yeyote anayesikia juu yake!

Ufalme wa Mungu utaleta njia Yake ya ajabu ya maisha kwa wale wanaoishi ndani yake, ambayo siku moja itahusisha ulimwengu wote. Lakini siyo pale unapoanza…

Fundisho Linalopendwa na Wengi

Imani inayoshikiliwa na wote ni kwamba Yesu Kristo atarudi Duniani katika Yerusalemu, na hii itafuatia miaka mitatu-na-nusu ya Dhiki Kuu—inayohusisha mihuri saba ya Ufunuo. Wanadamu wengi sana watakufa. Kisha mara hiyo atasimamisha serikali kuu ya ulimwengu. BIBLIA HAISEMI LOLOTE KATI YA HAYA! Ingawa haya yote yatatokea kwa wakati wake, na kwa kila namna yatakuwa mabaya zaidi kuliko mtu yeyote anavyofikiria, Neno la Mungu liko wazi kabisa kwamba Kurudi kwa Kristo kutakuja katika namna ambayo ni tofauti kabisa kuliko kile ambacho KILA MTU anatazamia!

Hakuna anayeuliza kwa nini swali la mwisho aliloulizwa Yesu na wanafunzi Wake lilikuwa: “Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” (Matendo 1:6). Bado walikuwa na majuma sita tu yaliyopita walipomsikia Kristo akifafanua kwa undani—ufafanuzi uliorekodiwa katika Mathayo (24), Marko (13) na Luka (21)—mambo yote ambayo hayana budi kutokea kabla ya Kurudi Kwake Yerusalemu, ikiashiria kipindi cha miaka kadhaa. Jinsi gani basi waliweza kuuliza swali hilo? Jinsi gani wanaonekana kusahau kwa haraka kila kitu Kristo alikuwa ameshawaambia?

Mitume walikuwa wamejua mambo mawili: (1) Ufalme wa Mungu kwanza ungeonekana katika sura ya kuurejesha kwa makabila 12 ya Israeli, siyo mara moja kama serikali ya ulimwengu. Pia walijua kwamba (2) “si kazi yenu [wao au sisi] kujua nyakati wala majira, Baba Aliyoyaweka katika mamlaka Yake mwenyewe” (Matendo 1:7). Ni lini hasa Yesu angeusimamisha Ufalme liliachwa kuwa fumbo—japokuwa alitoa viashiria vingi—lakini jinsi gani utakuja haikupaswa kuwa fumbo. Mitume walifahamu vyema asili ya Ufalme pale utakapoanza. Hili litakuja kuwa WAZI!

Aina Nyingi za” Ujio”

Hebu tujiulize swali la kushangaza, swali ambalo hakuna anayeonekana kulifikiria. Biblia inaelezea aina ngapi za kurudi kwa Kristo? Mafungu yanayotofautiana yanashikilia jibu la kushangaza. Nabii Haggai aliandika juu ya Kurudi kwa Yesu, “Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na Kinachotamaniwa na mataifa yote [muda mrefu ilijulikana kuwa ni Yesu Kristo] kitakuja…” (2:6-7). Watu wengi sana leo-hii wanatafuta na kutamania kurudi kwa Kristo. Japokuwa wengi wanaelewa kidogo sana juu ya kuwasili Kwake, wengi wa Wakristo wanakutamani, na sababu kuu ya kuutumaini kila siku zaidi ya siku iliyopita ni vile kumekuwa na kuporomoka kwa maadili katika ulimwengu mzima!

Tatizo hili hapa—na ni kubwa! Kitabu cha Ufunuo kinaongelea mwitikio tofauti sana kufuatia kuonekana kwa Yesu: “Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele…mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa…na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi” (11:15, 18). Picha ya mataifa yaliyokasirika haipatani na Haggai.

Aya hizi haziwezi kuwa zinarejelea wakati ule ule!

Wakiwa hawana maarifa ya Kristo kuja mara nyingi, wengi wanadai Anakuja na mara hiyo kuwafutilia mbali maadui Zake wote, akisimamisha Ufalme Wake. Ufunuo huonekana kusema hivyo, lakini fikiria 1 Wakorintho 15:25, ambayo inaonyesha kitu kingine tofauti kabisa, ikisema Kristo “sharti amiliki…, hata awaweke maadui Wake wote chini ya miguu Yake.” Wale ambao watapendekeza Anafika, anatawala kwa sehemu ya sekunde, kisha anawafutilia mbali maadui Zake wote, ni wazi wanapuuzia fungu hili, na mengine mengi.

Lakini tatizo linakuwa kubwa zaidi.

Mwandishi wa Injili Luka anarekodi maongezi ya kipekee kati ya Yesu na Mafarisayo: “Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu…ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza: wala hawatasema, Tazama, upo huku! au, kule! kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu” (17:20-21). “Ndani yenu” hutafsiriwa kwa usahihi zaidi “katikati yenu”—hivyo Kristo alimaanisha kwamba uwepo Wake tu unaweza kuashiria uwepo wa Ufalme. Alikuwa hasemi Ufalme wa Mungu ulikuwa ndani ya viongozi Aliowaita wanafiki, nyoka na wapumbavu! Mafarisayo walitaka maarifa ya ujio wa Ufalme kwa sababu walitegemea Masihi ambaye angewafagilia mbali Warumi na kusimamisha serikali ya ulimwengu—wao wenyewe wakiwa watawala wake! Ni wazi kwamba Yesu hakuwa na kitu kama hicho akilini Mwake. Angalia Ufalme ulipaswa kuwasili “bila kuuchunguza.” Maana ya Kigiriki ni “pasipo uchunguzi” au “uthibitisho wa kuona.” Kuona inahusiana na macho. Hivyo Kristo alisema Ufalme wa Mungu unawasili katika njia isiyoonekana.

Kuja huku kunatofautiana na kule kulikoelezwa katika Haggai na Ufunuo, ambako kwa wazi huyaelezea mataifa yote yanakutazamia—na KUKUNGOJA!—kuonekana kwa Kristo. Yesu hakuwa amechanganyikiwa juu ya kuja Kwake mwenyewe, na angehakikisha kuwa sisi pia hatuchanganyikiwi. Anafanya hili.

Elewa. Kurudi kwa Kristo kwa awali hakuhusiani na imani potofu ya Kiprotestanti kwamba Kristo “anawanyakua mbinguni” kwa siri watumishi Wake. Hakuna mahali Neno la Mungu linasema Yesu anawachukua Wakristo na kurudi nao mbinguni. (Mafungu mengi huthibitisha hili.) Utaona aya zilizo wazi zikionyesha Anausimamisha Ufalme wa Mungu Duniani, akitumia watumishi ambao wako hapa. Hili litakuja kuwa wazi.

Kurudi kwa Kristo “kusikoonekana”—ambako utaona kuwa ndiko kuja Kwake kunakofuatia—ni fokasi yetu. Hakuna Mkristo wa kweli anayetilia shaka kwamba Kristo anakuja. Lakini hakuna anayefafanua jinsi gani Atakuja—lini Atakuja (chini ya hali gani)—wapi Atakapowasili—kwa nini lazima aje—na nini atafanya kwanza. Kwa urahisi hawajui.

Picha Nyingine Isiyopatana

Ulimwengu uko katika machafuko ya kutisha leo hii—lakini kile tunachokiona kwa namna fulani ni utulivu ikilinganishwa na matukio ya kuoghofya ya Ufunuo, ambayo kwa muda mrefu yalidhaniwa kutangulia kuja kwa Kristo kunakofuata. Je, ni kweli kwamba Biblia inasema Kristo anarudi duniani wakati ulimwengu uko katika ukingo wa kuteketea kabisa?

Wengi wamekuja kuamini Amerika na Magharibi, na kwa hakika ulimwengu wote, vinatazamiwa kuingia kipindi cha ustawi mkubwa. Je, hii inapingana na hali ambazo Kristo alisema zitakuwepo wakati wa kuwasili Kwake—au, inaonyesha kwamba kuja Kwake kunaweza kuwa karibu zaidi? Ni lipi? Utaduwazwa katika maneno Yake yaliyo wazi.

Mathayo 24 huonyesha picha ivutiayo sana, ionekanayo kinyume. Baada ya Kristo kuwajulisha wanafunzi kwamba kila jiwe la hekalu “litatupwa chini,” waliuliza maswali matatu. Angalia: “Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja Kwako, na ya mwisho wa dunia?” (fu. 3). Bila shaka walimaanisha kuja Kwake Yerusalemu kwa sababu Alikuwa amemaliza kusema hili kabla (Math. 23:39) juu ya Kurudi Kwake pale.

Pata hiki. Wanafunzi walitaka kujua ni lini Kristo atarudi Yerusalemu! Lakini Kristo alienda mbele kuelezea kurudi Kwake kwa aina mbili kusikopatana kabisa—katika sura ile ile! Mwanzo wa sura unajibu swali lao, akitabiri vita vikali, njaa, magonjwa, matetemeko, dhiki kuu na ishara katika mbingu zinazotisha vyote vikielekea kwenye, “Kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu… ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi” (fu. 27, 30).

Elewa! Katika maelezo haya, Yesu harudi Yerusalemu mpaka majanga yaliyo katika kiwango kisichoelezeka yameipiga Dunia kwanza! Bila shaka hakuna chochote kinachofanana na haya hata kwa kiwango kidogo kinatokea sasa—ikimaanisha kurudi huku hakuwezi kuwa karibu. Vile vile angalia uwazi wa hali ya kurudi huku—ambayo huja “kwa kuichunguza.”

Sasa linganisha hiki na kile ambacho Yesu aliendelea kusema karibu na mwisho wa sura ile ile: “Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu…Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” (fu. 37-39, 44). Lakini tafakari kwa kina hili. Ulimwengu mzima kwa hakika “haufikirii” kwamba Yesu anakuja katika nyakati njema—kinyume cha vita, njaa, magonjwa, matetemeko, n.k.

Katikati ya kile kitakachoonekana kama kushamiri kwa uchumi wa ulimwengu, kuharibika kwa maadili kwa kiwango kikubwa pia kumetabiriwa. Hebu tusome Mwanzo 6 ili tuelewe wakati wa Nuhu. Huu ni wakati ambapo “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote” (fu. 5). Mafungu ya 11 hadi 13 yanaongeza maelezo kwa ukamilifu: “Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma. Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele Zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma.”

Kuvunjika kwa maadili kulikuwa kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba Mungu alidhamiria kuwafutilia mbali karibu wanadamu wote: “basi Nitawaharibu pamoja na dunia” (fu. 13). Mungu hata alisema kuwa Alijutia kumuumba mwanadamu BWANA Akaghairi kwa kuwa Amemfanya mwanadamu duniani, Akahuzunika moyo” (fu. 6). Bado Yesu alikuwa amesema kwamba wakati huo huo, hali za uchumi na maisha ya kawaida ya jamii—kula, kunywa, kuoa, n.k.”—vilikuwa vikiendelea kama kawaida.

Luka 17 inaongezea zaidi juu ya anguko la maadili katika ulimwengu mzima hivi leo. Inaanza kwa kurudia maelezo ya wakati wa Nuhu, kabla ya kuingiza kipindi kingine cha kibiblia: “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu [wakati wa Sodoma na Gomora], walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu” (fu. 26-30).

Kila mtu anayefahamu kitu chochote kuhusu Biblia anaelewa kwamba miji ya Sodoma na Gomora iliangamizwa kwa sababu ya ukengeufu katika mahusiano ya kimwili yaliyokuwa yameiteka jamii yote ya miji hii, na pia ilikuwa imesambaa kwenye “miji ya bondeni” kuizunguka kama ambavyo daima ukengeufu huo hufanya. Kwa hiyo ingawa maisha yalionekana kama kawaida katika Sodoma—na maelezo mengi zaidi yametolewa kuhusu kipindi hiki kuliko siku za Nuhu—hali ya tabia za watu iliporomoka kwa kiwango ambacho kilikuwa hakijashuhudiwa hapo kabla.

Hii hapa ndio pointi kuu kwa kusudi letu sasa. Kiuchumi, jamii hizi mbili zilikuwa zikifurahia nyakati za kawaida—nyakati za ustawi, ikijumuisha vyakula tele, ambayo ni kinyume cha njaa. Lakini nyakati hizi ghafla na kwa nguvu nyingi zilikatizwa na adhabu kutoka kwa Mungu. Katika mfano wa kisasa, Yesu Kristo anarudi na hii itafuatiwa na kutimia kwa unabii mwingi wa kutisha—unaotangulia kuja Kwake Yerusalemu.

Ifike mahali uelewe ukweli kwamba simulizi inayopendwa sana—kwamba mambo yatakuwa mabaya sana kabla ya Kristo kurudi Duniani—inapingana moja kwa moja na MANENO YA WAZI ya Yesu! Kuwasili kunakotangazwa na ongezeko la kitisho ambacho hakijawahi kushuhudiwa—ikimaanisha matukio mengi yenye kuonekana kwa kila mtu Duniani, ikijumuisha Kurudi kwa Kristo Yerusalemu—kama umeme ung’aavyo kutoka mashariki hadi magharibi—kwa namna yoyote hakuwezi kulinganishwa na kuwasili kwa kuja kusikotazamiwa kabisa “pasipo kuuchunguza” kunakotokea kwenye nyakati nzuri—nyakati za kujenga, kununua, kuuza, kula, kunywa, kuoa, n.k.

Sasa pointi kubwa. Haya yote yanakuambia wazi kwamba Kurudi kwa Kristo kuko KARIBU kuliko unavyofikiria na kile mamilioni ya wahubiri wanasema! Fikiria juu ya kile ambacho Yesu alisema na kama utamwamini, au watumishi waliokanganyikiwa.

Lakini ni kitu gani kingine ambacho Biblia inakisema kuhusu kuja huku? Utashangaa.

Ufalme Kama Punje ya Haradali

Kila mmoja anajua Yesu aliongea kwa mifano mara nyingi. Katika Mathayo 13 pekee, Alitoa mifano saba­­—mingi ni mifupi sana. Kila mmoja unaelezea sura ya Ufalme, kwa pamoja ikichora picha kamili. Mahali pa kuanzia ni fungu la 31: “Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake” (fu. 31-32). Punje ya haradali iliyokuwa ikifahamika na wale waliokuwa wakimsikiliza Yesu ilikuwa ni ndogo sana—ambayo ni vigumu sana kuiona. Hii ndiyo sababu Aliziita “ndogo [ikimaanisha ndogo sana katika umbile] kuliko mbegu zingine zote.” Ufalme wa Mungu unafanana na kitu kisichoonekana kwa macho unapowasili! Hakuna yeyote anayefokasi kwa hili. Hatimaye unakua na kuwa SERIKALI YA ULIMWENGU, ukiwa “mkubwa kuliko mboga zote”—“mti”—lakini hauanzi namna ile. Mfano huu kamwe hautajwi kwa sababu hakika hakuna anayeufahamu.

Hivyo hapawezi kuwa na shaka juu ya mwanzo mdogo wa Ufalme, mfano unaofuata unathibitisha hili: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia” (fu. 33). Neno la Kigiriki “sitiri” ni egkrupto, likimaanisha fichwa ndani. Fikiria juu ya neno la kisasa linalofanana na hilo—iliyofichwa. Yesu anasema—kwa kumaanisha—analeta UFALME ULIOFICHWA. Awali utakuwa umefichwa—awali umefichwa miongoni mwa mataifa!—lakini unapanuka kwa sababu chachu muda wote husambaa.

Yesu anafunua zaidi hili katika mfano wa tatu: “ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile” (fu. 44). “Sitiri” hapa imetokana na krupto, ikimaanisha “kuficha kwa kufunika.” Ujumbe wa Yesu kwa mara nyingine umewekwa wazi: Ufalme wa Mungu unaanza kidogo, uliofichwa na uliofunikwa. Ni lazima mtu atoke na kuutafuta!

Bado mfano mwingine unathibisha hili: “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri” (fu. 45). Zikiwa ni nadra kupatikana na za thamani kubwa, lulu za asili ni vigumu kupatikana. “Naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa [ilikuwa imefichwa na alilazimika kuitafuta], alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua” (fu. 45-46). Uliza: Je, mtu yeyote angelazimika kuutafuta Ufalme ambao ulikuwa juu ya Dunia yote toka kuanza kwake—ambalo ndilo fundisho maarufu? Kando na kuongezea nguvu mifano ya punje ya haradali na chachu, mifano ya hazina iliyositirika na lulu pia huongeza fokasi kwenye thamani ya kuuingia Ufalme.

Kabla ya kuingalia mifano mitatu iliyobaki ya Mathayo 13, tambua kwamba kila ufalme Duniani leo-hii una vitu vinne vya lazima: (1) Ardhi, mali au milki—bila kujali ukubwa au udogo wake. Lazima kuwe na mipaka halisi inayoonyesha ukubwa wa ufalme [saizi ya ufalme]. (2) Mtawala au mfalme anayeongoza serikali. (3) Watu—watawaliwa—wanaoishi katika milki inayotawaliwa. Na (4) mfumo wa sheria na kanuni pamoja na muundo msingi wa serikali.

Licha ya saizi yake, wakati ufalme kama punje ya haradali unapowasili, unakuwa na vitu vyote vinne. Ni Ufalme halisi.Usiufanye wa kiroho kama vile kanisa, au kitu “kilicho katika mioyo ya watu.”

Mifano Mitatu Zaidi

Mfano wa tano unaonyesha kupanuka kwa Ufalme wa Mungu kutoka mwanzo mdogo, vile vile kitu kingine ambacho hakuna anayeonekana kukiona: “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini...” (fu. 47). Juya linaanza likiwa tupu. Baada ya muda linajaa samaki wa “kila aina”—watu kutoka mataifa yote. Lakini siyo “samaki” wote wanastahili kuwepo: “hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia [au zama, wakati Kristo anahamia Yerusalemu]: malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki [angalia hii!], na kuwatupa katika tanuri [au oveni] ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno” (fu. 48-50). (Mwisho wa waovu haupatani na moto wa milele baada ya maisha. Kwa mengi zaidi juu ya hili, msomaji atahitaji kusoma kijitabu chetu Ukweli Kuhusu Ahera (The Truth About Hell).)

Achana na mtazamo wowote kwamba Ufalme wa Mungu unaanza na roho za kiungu tu. Mfano huu unaondoa udhanifu huo usio sahihi. Waovu wanaweza kuingia katika Ufalme na wakati fulani lazima waondolewe!

Bado mfano mwingine wa Mathayo 13 unaelezea ngano na magugu yenye sumu awali vikikua pamoja katika Ufalme wa Mbinguni. Ni wazi kwamba Ufalme hauko mbinguni. Kristo anaagiza kwamba magugu lazima yabaki pamoja na ngano mpaka mavuno—wakati Anapohamia Yerusalemu. Anafafanua kwamba, katika wakati huu, kama wakati juya linapovutwa pwani—baada ya Ufalme kama punje ya haradali kuwepo Duniani kwa muda fulani—malaika wanakusanya “kutoka katika ufalme” magugu na “kila kitu kichukizacho na kutenda uovu,” akirudia kwamba hawa wanaunguzwa katika tanuri [oveni].

Hivyo basi, awamu ya kwanza ya Ufalme ni kwamba, kadri inavyokua, aina mbaya ya watu wanaweza kuingia ndani yake. Kristo alisema hili mara mbili, akitumia vielelezo rahisi ili kwamba pointi isiweze kutoonekana. Fungu la 43 linaita mavuno wakati ambapo watakatifu katika Ufalme wa Baba yao “wanang’aa kama jua.” Kigiriki kinamaanisha “kung’aa kwa fahari.” Aya zingine zinaweka wazi ni katika kipindi hiki watakatifu wengine wengi zaidi, watu waliofuzu kwa utawala katika Ufalme wa Mungu, wanaungana na Kristo na idadi ndogo ya watawala wa awali (Luka 12:32) katika Yerusalemu mahali ambapo ataweka Ufalme Wake juu ya mataifa yote. Mpaka wakati huo utakuwa umechanua na kuwa mti mkubwa wa haradali ulioanza na punje ndogo.

Mfano wa kwanza kabisa katika Mathayo 13 bado unaleta mtazamo mwingine, ukionyesha wale ambao hatimaye wanafaulu kuingia katika Ufalme. Kristo aliongea juu ya mpanzi aliyekwenda kupanda mbegu, huku baadhi zikianguka katika udongo mzuri, zingine kwenye miamba, zingine kwenye miiba ambayo ilizisonga, na zingine zikianguka kando kando ya njia. Kama ilivyo kwa ngano na magugu, Kristo aliendelea kutafasiri mfano kwa faida yetu: “Basi ninyi sikilizeni [au eleweni] mfano wa mpanzi. Kila mtu alisikiapo neno la ufalme [utangazaji maalumu, wenye nguvu, utakaokuwa ukiendelea katika ulimwengu mzima ulioanza wakati Ufalme mdogo ulipofika], asielewe nalo, huja yule mwovu [Shetani], akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno [la Ufalme], akalipokea...kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa” (fu. 18-21).

Angalia pia kuwa dhiki na udhia vimeambatana na wanaokuwepo katika Ufalme! Bado thawabu itakuwa ya kustaajabisha. Hakuna yeyote anayesikia kwamba kitu kama hicho kinawezekana. Bado hali itakuwa ngumu sana kwa watakaokuwepo katika awamu fupi ya kwanza ya Ufalme—wakati fokasi ya Mungu ni katika kuwarejeshea Ufalme wale wanaoishi katika mataifa yaliyotokana na makabila 12 ya Israeli.

Kuendeleza mfano, “Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno [lile lile]; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai” (fu. 22).

Hili ndilo kundi la mwisho: “Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno [la Ufalme], na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini” (fu. 23). Hii ndiyo aina pekee ya wanaosikia ambao wanadumu—na hawa wanasitawi.

Mathayo 13 pekee inatosha kuelewa kwamba maelezo yote ya Ufalme yanayopendwa na wengi hayajakamilika kwa kiwango cha kutisha—na mara nyingi ni makosa matupu! Kuwa mwangalifu usije ukakataa au kuyafanya ya kiroho MAFUNDISHO YALIYO WAZI kuhusu jinsi Ufalme wa Mungu utakavyokuja kwa sababu rahisi tu kwamba hukuwahi kuyasikia kabla—kwa sababu hakuna mwingine anayeyafundisha. Mungu analo Kanisa Lake na hapa ndipo Anapofunua Kweli Yake.

Lakini yako mengi zaidi ya kujifunza.

Lile “Kundi Dogo”

Yesu alitumia istilahi ya kushangaza kuelezea kundi ambalo litakuwa watawala wa awali katika Ufalme Wake mdogo. Kama Ufalme wenyewe ulivyo, kundi hili halitakuwa kubwa kwa kuanzia. Katika Luka 12, Yesu aliwaagiza watumwa Wake “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme” (fu. 32). “Dogo” ni mikros kwa Kigiriki. Ni kundi-dogo ambalo linachukua ufalme mdogo—ina mantiki na ni rahisi kuelewa jinsi gani!

Mfano mwingine katika Luka 19 unamwelezea kabaila (Kristo) aliyekwenda nchi ya mbali (mbinguni) ili “ajipatie ufalme” (fu. 12). Mfano huu unabeba habari ya pekee sana kwa ajili ya kila Mkristo wa kweli. Unaelezea hukumu, utoaji wa hesabu, unaokuja mara hiyo kwa kundi la “watumwa” wakati wa kuwasili kwa Kristo akileta Ufalme Wake mdogo. Angalia: “...Aliporudi [kutoka mbinguni], Ameupata ufalme Wake, Aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili Ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake” (fu. 15). Baadhi ya watumwa walifaulu jaribio la Mungu, wengine walishindwa.

Kusoma maelezo yote kunafunua kwamba wale wanaofaulu wanawekwa juu ya miji Duniani (siyo Dunia yote kwanza) katika awamu ya kwanza ya Ufalme. Mungu amekuwa akitenda kazi na watu ulimwenguni kote, akiwaandaa kwa ajili ya nafasi za uongozi katika awamu ya kwanza ya Ufalme. Ni baada tu ya kutoa hesabu ya utendaji wa nyuma mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo (Rum. 14:10; 2 Kor. 5:10) ndipo hawa watumwa walioitwa kipekee na kufunzwa wataruhusiwa kutawala.

Mathayo 25 ina maelezo yanayoelekeana, ambamo baadhi wanaambiwa, “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako” (fu. 21). Ile “furaha ya Bwana” inahusisha kile ambacho ni awamu ya kwanza ya wokovu sambamba na kupokea sehemu katika kutawala kile ambacho kitakuwa ni Ufalme unaokua haraka—jukumu lililo na kusudi la kuwasaidia wengine waingie katika Ufalme wakati wa awamu yake fupi ya kwanza, ili kwamba pia wafuzu kutawala kitambo baadaye. Kila mmoja anayetamani kuja na kuwa chini ya Ufalme atapata fursa.

Kristo Kama Mfalme

Yesu Kristo, kama Mfalme wa Ufalme ulio kama punje ya haradali, Mwenyewe pia anaanza “kidogo” katika namna Anavyojifunua na katika eneo la awali la utawala Wake. Maelezo ya Kristo akipaa mbinguni yameshikilia kifungua macho ambacho hakuna yeyote anayekiona. Kumbuka swali la mitume: “Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” (Matendo 1:6). Baada ya jibu Lake inaongezea, “walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, Yeye alipokuwa akienda Zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe” (vs. 9-10). Wanaume hawa wawili, kwa hakika malaika, waliuliza, “...Mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Yesu huyu huyu [mtu, siyo Kiumbe Roho katika hali ya utukufu], aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona Akienda zake mbinguni” (fu. 11).

Usemi “Yesu huyu huyu” katika kumrejelea Yesu ni UFUNGUO muhimu sana. Kigiriki kwa hakika kinamaanisha “huyu huyu” Yesu, pamoja na neno la Kigiriki likiwa lile lile limerudiwa katika aya ya asili kwa ajili ya “huyu” na “huyu huyu.” Malaika walikuwa wakisisitiza kwamba Yesu atarudi katika mfanano wa umbile lile lile la kibinadamu Alilokuwa nalo Alipopaa.

Basi si ajabu kwamba mara nyingi Kristo ameitwa “Mwana wa Adam.” Hii ni kwa sababu Anakusudia kuendeleza (ya awali) umbile Lake la karne-ya-kwanza wakati atakaporudi. Hebu tuone uthibitisho zaidi.

Nabii Yeremia alimwelezea Kristo katika Ufalme Wake unaokua kwa jina lisilo la kawaida, wakati pia akimwita Mfalme wake: “Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki Mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku Zake [wakati fulani, lakini siyo mara ile] Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina Lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU” (23:5-6). Kwa Kiebrania “Chipukizi” ni kimea. Kama punje za haradali, vimea pia ni vidogo sana vinapoanza. Picha hii ya “kimea” haipatani kabisa na Yesu Kristo mwenye nguvu akirudi katika umbile lililotukuka.

Sura kumi baadaye Yeremia anaongeza zaidi, akithibitisha kitu nyeti kuhusu vimea: “Ni[ta]mchipushia Daudi Chipukizi la [kimea cha] haki; naye atafanya hukumu na haki...” (33:15). Kwa Kiebrania “chipushia” ni kitendo cha kuotesha. Mungu anasema, kwa hakika, atasababisha kimea kuchipuka. Tafakari uzito wa kile tunachoambiwa. Jukumu la Yesu litakua kutoka dogo kuwa kubwa.

Maelezo yote katika Yeremia yanafungamanisha “Chipukizi” kwa Mfalme Daudi. Angalia unabii mwingine kuhusu Kristo kutoka kwa malaika Gabriel kwenda kwa Mariamu: “Huyo [Kristo] atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba Yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na Ufalme Wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:32-33). Wakati wa kuja kama punje ya haradali, Kristo anaketi juu ya kiti cha enzi cha Mfalme Daudi baadaye atakalia kiti Chake mwenyewe katika Yerusalemu (wakati Daudi anapofufuka kupokea kiti kilichoachwa wazi alichokuwa amekalia Yesu).

Kutoka “Mahali Pake”

Ikithibitisha kwa nguvu Yeremia, Zakaria 6 pia inatoa picha ya ukuaji kuelekea utawala wa ulimwengu mzima. Fungu hili pengine ndilo lililo wazi sana miongoni mwa yale yanayoongelea juu ya Kristo kama Chipukizi: “Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, MTU [kwa mara nyingine, siyo Nafsi Roho katika umbile lenye utukufu] ambaye jina lake ni Chipukizi [kimea]; Naye atakua [chipuka] katika mahali Pake [mahali anapokaa mbali na Yerusalemu], naye Atalijenga hekalu la BWANA. Naam, yeye Atalijenga hekalu la BWANA; naye Atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti Chake cha enzi [wakati wa baadaye]; Naye Atakuwa kuhani katika kiti Chake cha enzi...” (fu. 12-13). Sehemu hii ya mwisho bila shaka inahusisha Kristo akitawala katika utukufu kutokea kwenye hekalu halisi ambalo litapaswa kuwa Yerusalemu.

Ile istilahi “mahali Pake” ni ya kushangaza—na kweli kabisa ni ya ajabu katika kile inachofunua. Ina maanisha “sehemu ya chini, iliyokandamizwa, chini, chini ya.” Hivyo Ufalme—na Kristo—wanaanza kutoka kile ambacho Mungu anakiita sehemu ya chini—sehemu iliyokandamizwa—chini­—ikimaanisha katika sehemu iliyofichwa na iliyo chini ya “anga” za falme za kibinadamu na mataifa. Hebu tujifunze kitu kingine.

Zakaria 6:12 inatoa picha ya Kristo akikua kutokea mahali pasipojulikana—“mahali Pake”—na hatimaye kujenga mahekalu mawili.

Nusu ya kwanza ya fungu inaelezea ujenzi wa Hekalu la kiroho, ambalo tutakuja kuona ni Kanisa. Hii inawiana sawia na Malaki 3:1, ambayo inaelezea Kristo akirudi Duniani kwenye Hekalu Lake. Angalia: “Angalieni, Namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbeleYangu; naye BWANA mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula; naam, yule Mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, Anakuja, asema BWANA wa majeshi.”

Hili haliwezi kuwa hekalu halisi katika Yerusalemu kwa sababu hakuna hekalu pale leo. Wayahudi hata hawamiliki Mlima wa Hekalu! Angalia kwamba Malaki anasema Kristo akija kwenye Hekalu Lake inamaanisha kwa watu wanaomtafuta na kumtamani.

Mtume Paulo alilifasili Hekalu hili kama Kanisa: “Hamjui ya kuwa ninyi [Kanisa—watu wa Mungu] mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho ya Mungu inakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi” (1 Kor. 3:16-17). (Pia ona 1 Wakorintho 6:19-20.) Hapa ni jinsi mtume Petro anavyowaelezea Wakristo wa kweli:

“Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai [ikimaanisha yanayoishi], mmejengwa mwe nyumba ya Roho, [u]kuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo” (1 Pet. 2:5). Ni mawe yanayoishi (binadamu) ambao kwa pamoja wanaunda “hekalu la Mungu” la kiroho.

Kristo anapanua zaidi idadi ya watu katika Hekalu hili la kiroho kupitia katika awamu ya kwanza ya Ufalme Wake, kipindi ambacho tutakuja kuona kinaitwa “Kazi ya Kustaajabisha na Kushangaza.

Mahali Ufalme Unakoanzia

Mahali ambapo Kristo anakusudiwa karibu na ulimwengu mzima kuelekea atakaporudi ni Yerusalemu. Lakini je, hiki ndicho Neno la Mungu linachosema? Bila shaka hatimaye Kristo atatawala kutokea pale—maandiko yasiyohesabika yanaonyesha hili—lakini je, hapo ndipo pale Ufalme Wake mdogo kama punje ya haradali unapoanzia? Je! Kuja Kwake katika karne ya kwanza kunatoa dokezo?

Angalia Mariamu aliishi katika "mji wa Galilaya, uitwao Nazareti" (Luka 1:26). Hapa ndipo Yesu alipotungwa mimba na mahali alipokulia baadaye—ulio kaskazini mwa Yerusalemu! Mbali kabisa na mji mashuhuri, Nazareti ulidharauliwa na wakazi wa Yerusalemu kama mji wa pembezoni usio na maendeleo. Baada ya Yesu kumwita Petro, kisha Akamwita Filipo aliyepeleka habari kwa Nathanaeli kwamba walikuwa wamemwona Kristo. Akiwa hajaridhishwa, Nathanaeli aliuliza, "Je! laweza jambo jema kutoka Nazareti?" (Yohana 1:46). Ni wazi kwamba kuja kwa Kristo katika karne ya kwanza kulikuwa ni kwenye sehemu isiyotegemewa. Kuwasili Kwake kuliwashangaza na kuwakanganya walio wengi: "Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?" (7:41). Miji yote ya Nazareti na Galilaya ilidharuliwa na wasomi wa siku za Yesu.

Kristo alianza huduma Yake mbali na Yerusalemu—mtindo ambao tutaona unadumu.

Nabii Mika anathibitisha zaidi Ufalme unahamia Yerusalemu: "Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme utamjilia binti Yerusalemu" (4:8) Haisemi Ufalme—Utawala wa Kristo mbali kabisa kabla ya matukio katika Ufunuo, wakati ambapo utasimama tena na kuendelea kwa miaka 1,000 zaidi—umejengwa Sayuni au unaanzia Sayuni. (Wala haisemi kwamba unawasili pale kutokea mbinguni.) Mika anasema "unakuja" pale, ikimaanisha awali ulikuwa mahali pengine. Kwa hakika ulikuwa—katika eneo linaloitwa "mahali Pake!"

Hebu tuangalie maelezo ya mwisho ya Chipukizi katika muktadha usio wa kawaida. Mpangilio ni vita kubwa inayoyatesa mataifa ya Israeli wa leo—na madhara ya kutisha juu ya Yerusalemu na kabila la Yuda: “Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani. Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini. Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu” (Isa. 3:25-4:1).

Aya nyingine nyingi za Biblia zinaongelea kwa kina vita ambayo Isaya anairejelea—mahali inakoanzia, jinsi inavyoenea, wale inaowaathiri, na ukali wake usiofikirika. Hili ni tukio tofauti kabisa linalotokea muda mrefu, mrefu kabla ya Harmagenia, lakini hili sio somo letu hapa. Wale wanaofikiri kwamba ulimwengu tayari uko vitani kati ya tamaduni zinazopingana si muda mrefu watagundua matukio ya leo kwa hakika SI KITU katika ulinganishi! Hali itaendelea kuwa mbaya sana na hatimaye kumeza mataifa yote ya Magharibi. Kile kinachokuja ni ng’ambo ya [kinapita] mafikirio. Hivyo wengi watakutwa bila kuwa na habari kabisa.

Isaya anaendelea, akionyesha kitu kingine kinachotokea sambamba na vita. Hebu tusome kile ambacho hakuna anayeona: “Siku hiyo [kwa wakati huu, wakati maangamizi ya vita yatakapokuwa yamekuwa makubwa] Chipukizi [chipukizi linalokua na kukomaa] la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi…mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka [kutoka kwenye vita]. Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu [wengi watakuwa wamekufa]; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza” (fu. 2-4). Hukumu ya moto inahusishwa, pamoja na tanuru tulilolisoma juu yake kabla. Soma Isaya 31:9.

Mpaka hapa Chipukizi na ule Ufalme—vikiwa vimekuwepo Duniani kwa muda—vinashamiri! Haya ni matokeo ya kile kilichotajwa kabla “Kazi ya Ajabu” itakayoongelewa zaidi hivi punde. Tunda linaitwa “jema” na “kupendeza”, ikimaanisha “pambo.” Kristo anaitwa “mwenye utukufu” na “mzuri,” hili la mwisho likimaanisha “katika mantiki ya umashuhuri; fahari (kama mwenye kuonekana)”—kufikia wakati huu Ufalme utakuwa umefikia kinyume cha ulio mdogo na uliofichwa! Unaonekana na ni mashuhuri! Mpaka hapa mamilioni mengi ya watu watakuwa wamekuja katika Ufalme. Jaribu kutengeneza haya yote—sehemu yoyote kati yake!—yapatane na maelezo yanayofahamika na wengi! Hakuna anayeyafundisha, bado ni ukweli wa Biblia yako UNAOONEKANA WAZI katika kurasa zake.

Isaya 59 inaleta mtazamo mwingine wa Kristo akija Yerusalemu—kwa mara nyingine, miaka mingi baada ya Ufalme Wake kuanza ukiwa mdogo: “Na Mkombozi atakuja Sayuni, kwao waachao maasi yao katika Yakobo, asema Bwana” (fu. 20). Kisha sura ya 60 inaanza, “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia [umekuzukia, siyo umekushukia] [kumbuka, kutoka mahali pa chini, chini ya na chini ya kuonekana]. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako” (fu. 1-2). Tafakari hili. Kama Yesu alianzia safari Yake kutokea mbinguni, Angeelezewa kama akishuka—siyo akizuka—juu ya Sayuni! Usilikose hili! Mafungu mengi yanathibitisha Yesu anakuja kutoka mbinguni kwa watu Wake. Lakini kwamba miaka kadhaa baadaye anakuja kwenye Mlima wa Mizeituni (Zak. 14:4) na muda mfupi baadaye Sayuni, ambao uko kando yake.

Mahali maalumu pa “Mahali” pa Kristo

Aya fulani zinathibitisha zaidi Kristo anahamia Sayuni, na hizi zinatoa fununu juu ya taifa lipi Atakuja kwalo. Unabii kwa ajili ya wakati wetu—siku za mwisho—ambazo karibu hakuna mtu anayeuongelea unapatikana katika Hesabu 24. Nabii Balaam alitabiri, “Siku za mwishoNyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi [Mtawala] itainuka katika Israeli [siyo Yuda]…Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini [huu ni Yerusalemu]” (fu. 14, 17, 19).

Akiitwa “Nyota” hapa, aya zingine zinamweleza Kristo kama “Jua la Haki” (Mal. 4:2), “Nyota ya Asubuhi (2 Pet. 1:19) na ile “Nyota yenye Kung’aa ya Asubuhi” (Ufu. 22:16). Analeta milki Yake—utawala Wake!—pale Yerusalemu na Yuda kutoka taifa lingine la Yakobo wa leo (Israeli). Hii haiwezi kuwa inarejelea tu ukoo wa kuzaliwa kwa Yesu kwa sababu Alizaliwa katika Yuda, na katika Uyahudi. Maandiko mengi yameongelewa katika kitabu changu kamili Amerika na Uingereza katika Unabii (America and Britain in Prophecy) kinaweka wazi tofauti baina ya Yuda na makabila mengine 11 ya Israeli. Kwa hakika, rejeleo la kwanza kwa “Wayahudi” katika Biblia linawaonyesha wakiwa vitani na Israeli (2 Wafalme 16:1-16)! Taifa la leo katika Mashariki ya Kati linaloitwa Israeli kwa hakika ni Yuda, huku mataifa ya kidemokrasia ya Magharibi yanayoongea Kiingereza yakitambulika kama wazao wa makabila mengine ya Israeli wa kale. Yesu Kristo anakuja kwa moja ya nchi hizi, SIYO Yuda!

Isaya 41 ina uthibitisho zaidi: “Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja” (fu. 25). “Kaskazini” humaanisha “fichwa, giza; ikitumika tu ya kaskazini.” Isaya anaendelea, bila kuacha shaka huyu ni Yesu Kristo: “Atawajilia maliwali kama akanyagaye matope [akisimamisha mamlaka Yake juu ya viongozi wote wa kidunia], na kama mfinyanzi afinyangaye udongo. Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na…nitampa [wakati huu] Yerusalemu mletaji wa habari njema” (fu. 25-27). Huu hapa ni unabii wa Yesu akiwa “anainuliwa”—fikiria “akikua”—chipuka kutoka—nchi ya kaskazini (taifa la Magharibi la Israeli ya leo) kuwashinda adui Zake.

Uingiliaji kati huu, ukiambatana na habari njema—injili ya kweli—ni lazima kabisa itolewe hasa kwa kuwa taabu kuu inaanza katika Yerusalemu siku ile ile Ufalme mdogo wa Kristo unapoanza na itaendelea kuwa mbaya mpaka Atakapowasili pale.

Jiji Linalokuja

Tuliona awali kwamba Ufalme umeundwa na vitu vinne—ardhi, mfalme, watawaliwa na sheria. Bila shaka, himaya itakuwa pia na muundo wa kiutawala. Je! Kristo anayajenga haya yote pale anapowasili—au Anakuja nao? Kumbuka Kabaila wa Luka 19 aliyekwenda kujipatia (kutoka mbinguni) Ufalme.

Hivyo Ufalme huu unakuja kutoka mbinguni. Hii inapatana na maelezo ya Matendo 1. Wanafunzi wale wale waliouliza juu ya Kurudi kwa Kristo wangekuwa wamemsikia akifafanua jambo hili kutoka Yohana 14: “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na Mimi. Nyumbani mwa Baba yangu [Kigiriki: Makazi au makao] mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia…” (fu. 1-2). Kristo anatuambia tuamini chochote anachokaribia kusema—bila kujali kwamba kinaweza kuwa ni kitu kisichoweza kuaminika namna gani! Akiendelea, “…Naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, NITAKUJA TENA niwakaribishe Kwangu; ili Nilipo Mimi, nanyi mwepo” (fu. 2-3). Huyu ni Yesu Kristo akija kwa watu Wake kutokea mbinguni, na si vinginevyo.

Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “mahali” ni topos, kutoka kwalo linapatikana neno topografia (mandhari). Neno pia linaweza kutafasiriwa “mahali au mtaa.” Kristo aliongea juu ya kuleta mahali palipoandaliwa tayari wakati Atakaporudi Duniani. Je! Kuna yeyote angetia shaka alikuwa anaongelea kuja Kwake kunakofuata?

Kristo analeta majumba kutoka mbinguni kwa ajili ya Ufalme Wake mdogo. Lakini watakaa wapi?

Ufunuo 22 inaonyesha picha ya jiji linalokuja. Kurudi kwa Kristo ndio muktadha: “Tazama, Naja upesi, na ujira Wangu u pamoja Nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo [hii ni namna ya kutoa hesabu au hukumu iliyoelezwa awali]. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia jijini kwa milango yake.”

Kinachofuata ni maelezo ya kipekee ya mpangilio wa jiji: “Huko nje wako mbwa [manabii wa uongo na watumishi], na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya”. (fu. 12-15). Aya hii inaunganishwa na Kristo akiwa mzao [Chipukizi] la ukoo wa Mfalme Daudi: “Mimi Yesu Nimemtuma malaika Wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota yenye Kung'aa ya Asubuhi” (fu. 16).

“Jiji” hili haliwezi kuwa Sayuni wala Yerusalemu. Hakuna manabii wa uongo, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na waongo wataruhusiwa mahali popote ng’ambo ya kuta za mipaka ya Sayuni—au popote katika Yuda, au kwa mantiki hiyo ulimwengu mzima—mara Kristo anaporudi Yerusalemu, Sayuni. Sura za mwisho za Zakaria zinaonyesha hili, hasa 13:1-3. Wala jiji hili haliwezi kuwa “Yerusalemu Mpya” unaosimamishwa wakati wa kuanza kwa utawala wa Kristo wa miaka 1,000 baadaye. Wale wote wanaompinga Mungu—kila mtu Duniani aliyepokea Alama ya Mnyama—atakuwa ameuawa kabla ya kuwasili kwa jiji hilo. Kwa hiyo aina ya watu hapo juu hawawezi kuwa “nje”—ikimaanisha nje yake. Fikiria tu shetani atakuwa amefungwa wakati huu. Hii inafanya isiwezekane kwamba pangeweza kuwepo hata mchawi mmoja mahali popote Duniani. Vivyo hivyo kwa manabii wa uongo na waabudu sanamu. Pia, kwa kuwa Shetani ndiye “baba wa mauaji na uongo” (Yohana 8:44), hakutakuwa na mauaji au kupenda uongo.

Ufunuo 21 yote na sura ya 22 fungu la 5, Yohana anarekodi ujumbe wa Kristo juu ya Yerusalemu Mpya wa ajabu ambao utakuja Duniani mwanzoni mwa utawala wa Millenia wa Kristo baadaye. Mwishoni mwa Ufunuo 22, Mungu anarejelea kwa ufupi tena Yerusalemu Mpya, akiuita “Mji Mtakatifu.” Usiikose tofauti muhimu!

“Kazi ya Ajabu na Kushangaza”

Wakati wa Ufalme ulio kama punje ya haradali, idadi kubwa sana watakuja kujua kweli hizi za Biblia ambapo Mungu, kupitia nabii Habakuki, anaiita “kazi ya Ajabu.” Angalia: “Angalieni, enyi mlio kati ya [mataifa], katazameni, kastaajabuni sana; kwa maana mimi natenda kazi siku zenu, ambayo hamtaiamini hata mkiambiwa” (1:5). Katika maandiko, “Kazi” inawakilisha watumishi wa Mungu wakifundisha na kuonya wale wote watakaosikia. Je! Utaamini ripoti ya utangulizi wa Kazi hii?

Nabii Isaya anasisitizia kwa nguvu kile ambacho Habakuki alitabiri: “kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na kushangaza [mwujiza]; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa (29:14).

Paulo pia alimnukuu Habakuki katika kitabu cha Matendo, akibadilisha kidogo: “Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii [Habakuki]. Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana” (13:40-41).

Hii ina maana lazima tutarajie Kazi kubwa mno, yenye kutikisa-Dunia kufungua Ufalme—moja ambayo itafika mbali sana itaduwaza akili—moja ambayo haiwezi kufahamika kikamilifu mpaka itakapoonekana—kwamba habari zake zinaposikika wengi hawataiamini! Kijitabu hiki si tu kwamba kinaitangaza kwako, bali kinaongeza kwamba inakuja hivi karibuni!

Unabii mwingine unaowiana, unaofahamika kidogo unadokeza juu ya muda itakayochukua Kazi ya Ajabu, ambayo hutendeka wakati wa awamu ya kwanza ya Ufalme. Danieli 9:27 inafafanua muda wa kuja kwa Kristo mara ya kwanza, lakini pia wa awamu ya awali ya Kurudi Kwake. Hebu tusome: “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu...”

Makala yetu kamili juu ya somo hili inaonyesha “juma” hili lilianza majira ya kupukutisha ya 27 BK—muda ule ule wakati huduma ya Kristo ilipoanza. Kristo—ambaye ni “sadaka na ile dhabihu” kwa ajili ya mwanadamu—aliuawa “kati”—katikati ya­—juma, linalowakilisha miaka saba ya kiunabii (Hesabu 14:34; Ezek. 4:6). Ni ufahamu wa kawaida kwamba huduma Yake ya kidunia ilidumu kwa miaka mitatu-na-nusu. Miaka mitatu-na-nusu zaidi ingetakiwa kumalizia “juma la kiunabii” linalokamilisha huduma ya Kristo. Huu unaonekana kuwa ndio muda wa awamu ya kwanza ya Kristo akirejesha Ufalme kwa Israeli wote.

Si-ajabu nabii Habakuki aliomba, “Ee Bwana, fufua Kazi Yako [Kristo] katikati ya miaka” (3:2). Kiebrania cha “katikati” humaanisha kati. Alikuwa akitoa unabii wazi juu ya “uamushaji” wa huduma ya Kristo katikati ya “juma” la miaka-saba lililoongelewa na Danieli (9:27). Miaka mitatu-na-nusu ya mwisho ya Kazi hii—huduma ya Kristo—bado haijatimizwa, na itatokea hivi karibuni!

Upotoshaji wa Ulimwengu Mzima Unaokuja

Kijitabu hiki hakingekamilika bila ya maonyo yanayotafakarisha sana. Wengi wanashangazwa kujifunza kwamba Biblia inamwita Shetani “mungu wa ulimwengu huu” (2 Kor. 4:4), ambaye kupitia historia “aliyadanganya mataifa” (Ufu. 20:3). Katika Mathayo 4, mwovu alidai kumiliki “falme zote za ulimwengu” (fu. 8)—ukweli ambao Kristo hakuupinga.

Shetani hutafuta kupotosha kila kitu. Angalia kile kinachotangulia Kurudi kwa Kristo. Akiongea juu ya “...kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele Zake” (2 Thes. 2:1), Paulo anarekodi, “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana siku hiyo haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu [unabii uliotimia katika karne ya 20]; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu” (fu. 3). Mtume Yohana alimwita mtu huyu “mpinga Kristo” (1 Yohana 2:18).

Hivyo mtu huyu anakuja kabla ya Kurudi kwa Kristo. Aya hiyo hiyo inaendelea kuonyesha chanzo—na kiwango—cha nguvu zake: “...ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo” (2 Thes. 2:9). Anakuja na NGUVU ZOTE za mwovu kiutendaji—kitu kinachofanana na kile Ayubu alikipitia, lakini kile ambacho ulimwengu kwa pamoja kamwe haujawahi hata kuanza kufikiria!

Mtu huyu atatamba juu ya ulimwengu wote wakati wa kuja kwake. Anadai kuwa Mungu: “...yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu” (fu. 4). Ueneaji wa mtu huyu (na mafungu mengi yanaonyesha kwamba kuna wanaume wengine wawili wanaofanyakazi sambamba naye na chini yake) unavuka ng’ambo ya Ukristo—yule “ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa” (fu. 4)—kila dini Duniani!

Nabii Habakuki, ambaye Paulo alimnukuu katika Waebrania 10 kuhusiana na mtu wa kuasi, anaongezea kwenye wasifu wa mtu huyu: “Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake. Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu” (Hab. 2:4-5). Huyu hapa ni mtu wa yule mwovu, lakini aliye na uwezo kama huo wa kustaajabisha kiasi kwamba mataifa yote ya ulimwengu yanatii utashi wake. Hakuna mtu anayeongea juu ya mtu huyu kwa sababu hakuna mmoja anayemfahamu au angeweza kuamini uwezo wake wa ajabu wa kuenea na nguvu atakayokuja nayo. Idadi kadhaa ya mafungu yanaweka wazi kwamba udanganyifu huu utakuwa wa muda mfupi. (Mafungu mengine ya msaada yanayohusiana ya kusoma ni pamoja na 2 Wakorintho 11:4; Habakuki 2 yote; 2 Timotheo 3 yote; Zakaria 11:15-17; Yakobo 5:1-6; Mathayo 7:15-23 na Luka 21:8, 35-36.)

Ufalme wa Kristo ulio kama punje ya haradali unaanza siku ile ile utawala wa mtu huyu unapokoma. Tukirudi kwenye 2 Wathesalonike, “...BWANA ata[mwua] kwa pumzi ya kinywa Chake, na ku[mwa]ngamiza kwa ufunuo wa Kuja Kwake” (2:8).

Kwa urahisi hivi. Mtu anayetumia nguvu kuu ya Kishetani atachukua utawala wa ulimwengu mzima kitambo kidogo kabla Kristo hajasimamisha Ufalme Wake. Ishara zote ni kwamba ujio wa mtu huyu ni hivi karibuni!

Picha Inayoeleweka Wazi

Muhtasari wa msingi. Kristo anakuja kwanza kwa watu Wake—Hekalu Lake—katika nyakati za mema, akileta Ufalme Wake “pasipo kuuchunguza.” Unaanza kwa namna ya kutoonekana kwa macho na uliofichwa! Pia awali unaongozwa na kundi dogo chini ya Kristo. Awali ataficha uwepo Wake kwa kuwa kama chipukizi. Kipindi cha awamu hii ya kwanza ya Ufalme itakuja adhabu ya kutisha kwa mataifa yaliyotoka kwa Yakobo, ambayo hatimaye itawafanya tayari kuupokea Ufalme wa Mungu. Ufalme utakuwa ukiongezeka katika idadi ya watawaliwa kabla Kristo hajahamishia Yerusalemu SERIKALI YA ULIMWENGU MZIMA iliyo tayari kupanuliwa sana. Kutokea pale atatawala mataifa yote pamoja na kundi kubwa la watakatifu Wake likitoka kwenye kile ambacho kitakuwa kundi kubwa zaidi wakati huo. Ni katika kipindi hiki ambapo atajenga Hekalu tukufu la Tatu juu ya Mlima Sayuni (Ezek. 40-48).

Kama umeshangaa, hata kushtushwa, kutokana na kweli rahisi ndani ya mifano ya Yesu, na unashangaa kwa nini kamwe hujaambiwa maana zake, tambua kwamba aliiunda ili kuwakanganya wale ambao Alikuwa hawaiti. Hiki hapa ndicho Kristo alichosema: “Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba...” (Math. 13:13-15). Walio wengi huchagua kufumba macho yao kwa ukweli wa Biblia. Mifano huwazuia wasifahamu kile ambacho hawataki kusikia.

Lakini UNAWEZA kufahamu! Akiongea zaidi juu ya sababu za mifano, Mathayo aliongeza, “Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno... akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu misingi ya ulimwengu” (13:34-35).

Umepokea maarifa ya thamani kubwa—yaliyositirika kutoka kwa ulimwengu. Siyo tamaduni zinazofahamika na wengi—hadithi zilizotungwa—za Ukristo wa leo, lakini maneno ya wazi ya Kristo—ambayo yanajulikana sasa katika wakati wetu. Mungu amekuwa akingojea kwa miaka maelfu kusimamisha Ufalme Wake katika Dunia ambayo inauhitaji sana. Lakini hautakuja kama mabilioni wanavyotegemea. Fikiri. Umesikia neno la Ufalme kabla haujaja. Kuna faida kubwa katika hili! Leo Kristo anaandaa timu iliyochaguliwa maalumu ya watawala waliofuzu kutawala chini Yake mbele ya kuwasili kwake.

Miaka elfu mbili iliyopita, Yesu Kristo alijenga Kanisa Lake—Kanisa la kweli—lile pekee Alilolijenga. Kanisa hili linaamini na kufundisha KWELI za Biblia—zote—siyo mawazo ya wanadamu—yoyote kati ya hayo! Watu wa Kanisa hili siku zote wamesimama katika UWAZI WA UHAKIKA wa kile ambacho Mungu anaahidi kwa ajili ya walio hai mwishoni—siyo matumaini ya uongo ya mavumbuzi ya wanadamu.

Sasa­—utang’ang’ania imani zilizoshikiliwa muda mrefu—au utashikilia UKWELI unaobadili-maisha?

171205
HGKWC

Vitabu Vingine